Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Hapo kuhusu Gwajima ni uwongo mkubwa. Pengo hajawahi mshitaki Gwajima.

Pia kumbuka maelezo ya Pengo yalikuwa kwamba anafafanua kuwa kauli ya Niwemugizi siyo ya kanisa kwani tayari ulikuwa na hiyo argument iliyohitaji ufafanuzi
Kwa hiyo kauli ya Pengo ndio kauli ya kanisa ??!!
 
Nyie wakosa adabu wa chadema huko mnakokwenda msidhani mnakijenga chama bali ni kuendelea kkiuwa.
Hawa viongozi wetu wa kiimani wakiongea waacheni wajibizane wao kwa wao kwani ndio wanaojua nini kanisa lapaswa kutenda.
Pia wewe kusoma sunday scchool kusikufanye ukawa umeujua uRoman Catholic kuliko Kadinali Pengo. Mnaelekea kutengeneza wakatoliki chadema na wakatoliki wazalendo wa Tanzania. Komeni kumshambulia huyu mzee humu mitandaoni. Mjue kuwa si wote watakao vumilia kuona mkidhalilisha humu. Alivyojengwa kiimani mzee huyu watu wengi wamemfanya kuwa kiigizo bora kwao. Sasa wewe mkosa adabu ukianza kumshambulia tena si rika lako kwa kweli inaumiza sana. Chunga sana kama wazazi wako hawakukufunza kuheshimu wakubwa dunia itakufunza. Kumbuka si kila vita hupiganwa.
 


Hakuna kitu unajua, ikitaka kuulewa Ukatoli, angalia mfumo wa Tanzania au Monarchy kamaUingereza ndiyo utaelewa, Papa ni Kiongozi wa Kisiasa, Roma ni Dola, kuna Bunge, Mahakama na Serikali ambazo zote ziko chini ya Papa na maamuzi yake anachaguza aidha ashirikishe Serikali (Bunge, Mahakama na Serikali) au aamue mwenyewe, ndiyo maana Tanzania kuna Ubalozi wa Vatikani, unafikiri Balozi wa Vatikani Tanzania anamuwakilisha nani?!

Ndiyo maana Ulaya kulikuwa na Mapinduzi yaliyoanzishwa na Martin Luther (Martin Luther original na siyo yule msanii wa USA) ambaye ndiye muanzilishi wa Uprotestani/Ulutheri Duniani, kufanikisha hilo kulitokea Vita kubwa Duniani ambayo ilijulikana kama thirty years war ambapo Mamilioni ya Watu walipoteza maisha, na Vita ilikuwa ni Kidini/Kisiasa ambapo Ukatoliki vs Ulutheri!
 


Msaliti kwako, lkn kwa Wakatoliki ni Mtumishi Mungu na kauli yake ni kauli ya Mungu kwani ana roho Mtakatifu ndani yake!
 
MUNGU alikwambia lini kwamba amemteua Papa Ndani ya kanisa katoliki au umejitungia


Wakatoliki ndivyo wanavyoamini na ndiyo maana anaitwa Baba Mtakatifu, unafikiri ni kwa nini wanamuita Mtakatifu?
 
Ni swala la mtazamo tu, kwako ni kauli ya ukakasi kwa wengine ni kauli ya Mungu kwani Kardinali ni mtumishi wa Mungu ambaye ameteuliwa na Mungu kuwa Kardinali wa Kanisa Katoliki hivyo sauti yake ni sauti ya Mungu kwa wafuasi wa Kanisa Katoliki!
Uoni wako hafifu!!
Ndicho nachoweza kusema
 
Papa nini wewe mammalia ? umesahau papa Francis aliachia ngazi sasa nani mkubwa kati yake na huyu kijakazi wa CCM?


Kijakazi kwako lkn kwa Wakatoliki Tanzania Kardinali ni Mtumishi Mungu, mimi Bibi yangu anashinda Kanisani, anasikiliza Redio Maria siyo tbc,itv au sijui star bali Redio Maria au Tumaini tu na kesho Kardinali akimwambia Wakatoliki tuipigie kura CCM hatouliza wala kujadiliana na mtu atafwata tu, na ninakuhakikishia Wakatoliki kama Bibi yangu wako idadi ya kutosha tu!
 
Sio ameolewa kwenye jimbo na Papa yeye huidhinisha tu ila wanaoteua jina ni baraza
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Halafu upuuzi mwingine anaoufanya ni kutaka kauli yake ndio isimame kwa niaba ya wakatoliki wote.

Heshima anayopewa Baba Askofu Pengo ni kubwa sana lakini lazima mtu atambue nguvu ya kiti chake, na mahusiano chanya kati ya kanisa na serikali, tangu siku ya kwanza kabisa mwaka 1961 desemba.

Kama mtu amepata akili miaka ya juzi juzi tu halafu hana tabia ya kuyachimba mambo kwa undani atakachokifanya na kuangalia siasa za sasa na kuishi kuwa na hitimisho jepesi sana.
 
Kinachotia shaka enzi za kikwete kabisa hili lilikua mbele kukosoa lkn Tangu alipoingia mkatoriki du! Kimyaaaaaaaaa totolo.
Hivi nini kimelisibu wajameni?????
Hata wakati wa Kikwete huyu bwana Pengo mambo yake ni haya haya ya kuwakana wenzie!! Wakati wa bunge la katiba alilikana waraka wa baraza la maaskofu Tz. Ni TABIA yake anatumika na Magogoni kutuliza upepo.
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Kwan kukaa na papa ndo nn....papa naye c binadam km wewe ..Nyie ndo wale mnaoweza hata kujidhalilisha utu wenu kisa umaarufu wa MTU.. C bora hata ungesema Ibrahim anaeketi mbimgun kwa Mungu
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Kwani Papa Mungu?
Au amehakikishiwa kwenda mbinguni sababu ana namba ya simu ya PAPA?
 
Saint Mery's ni shule za madhebu ya kilokole na siyo shule za kanisa katoliki.
Zipo seminary nyingi za kikatoliki zinaitwa st Mary.. mf ile ya hapo mbalizi mbeya inaitwa st mary mbalizi... kuna moja iko hapo pwani inaitwa st. Mary's pia au maarufu kama Visiga seminary
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…