Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Nimesikitishwa sana na kauli zako za kipuuzi, zilizo jaa unafiki, tumekusikia sana ukijipambanua kuwa wewe si muumini wa mabadiliko, tuambie upande wako ni UPI.
Mtoto mwenye hekima kamwe hawezi kumuita mzazi wake mnafiki na mpuuzi
Ungelikuwa Mkatoliki, tena mshika dini 'mkatoliki hai', usingelimtukana na kumkejeli kiongozi wako
 
Mtoto mwenye hekima kamwe hawezi kumuita mzazi wake mnafi na mpuuzi
Ungelikuwa Mkatoliki, tena mshika dini 'mkatoliki hai', usingeli mtukana na kumkejeli kiongozi wako
Hivi Paulo alipowaandikia wakristo wa Galatia "Enyi wagalatia msio na akili ni nani aliyewaloga" hakuwa na adabu kwa Wakristo wenzake wa Galatia?
 
Pengo yuko sahihi hata uingereza kipaumbele chao sio katiba na hawajawahi kuwa na katiba na hawatarijii kuwa na katiba. kipaumbele ni kero halisia za raia wake kutatuliwa. Askofu pengo yuko sahihi asilimia 100
Sasa hapani london
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Kwa Mungu mwenda wazimu na timamu na takataka na masikini na tajiri yeye hana kubagua wote watu wake!siku ya mwisho hautaulizwa wewe ulikuwa nani duniani ama ulikuwa na cheo gani bali utahukumiwa kutokana na matendo yako, kile kibaba ulichowapimia wenzako ndicho nawe utapimiwa hicho hicho hautazidishiwa wala hautapunguziwa
 
Kama huu ndio mwisho wa Pengo hakika halitendei haki kanisa
 
Pia Pengo sio msemaji wa kanisa katoliki Tanzania bali baraza la maaskofu ndio lenye kuweza kusema kupitia kaatibu wake au Rais wa baraza.

Pili kila askofu anayo mamlaka ya kutoa msimamo wa jimbo analosimamia bila kuingiliwa na Pengo.
Je hiyo mamlaka ya kumkosoa huyo askofu ameipata wapi.

Lakini pia hoja ya askofu Niwemugizi sioni kama inakinzana na kanisa na unaweza kuwa msimammo wa waumini wa jimbo lake na pia unaweza kuwa msimaamo wake binafsi. Na wala hakusema ndio msimamo wa kanisa kardinali Pengo ametoka wapi kumjibu?

Mojawapo ya sifa ya kanisa katoliki ni kusema kweli pasipo kificho ama unafiki.

Mhashamu Kardinali Pengo umekengeuka kwa hili
Halafu wanakataza nisiongeze mke wa pili!
 
Huyu mzee naye ni miongoni mwa wazee wanaozeeka vibaya kabisa. Viongozi wa namna hii wananipa uvivu wa kwenda kanisani.

Siku zote hizo mambo yanatuendea ovyo amekaa kimya, nilitarajia kiongozi wetu mkuu akiibuka hadi atatoa msimamo wa maana hadi kanisa litasifiwa, anakuja na ujinga ambao unashusha hata heshima ya kanisa kabisa.

Unawezaje kuona katiba si kipaumbele wakati ubovu wa katiba ndio unatuweka hapa tulipo hadi sasa..?
 
Wewe huna tofauti na Gwajima
Hapa kuna hoja tatu za kujadili, chagua moja uijadili.

Hoja ya kwanza ni Askofu Pengo kasema kauli ya Askofu Niwemugizi si ya Kanisa Katoliki. Ni wapi Niwemugizi alisema kwamba Kauli yake ni kauli ya Kanisa na jee kama Pengo anadai kauli ya Niwemugizi si ya Kanisa jee na kauli yake pia ni ya Kanisa Katoliki?

Hoja ya Pili ni kweli kuwa kila wanachokisema viongozi wa Kanisha Katoliki ni lazima kiheshimiwe? Kama ni hivyo jee kati ya Kauli ya Askofu Niwemugizi na ya Askofu Pengo ni ipi kauli inayotakiwa iheshimiwe na waumini wa kikatoliki?

Hoja ya tatu ni kwa nini Askofu Pengo ni mwepesi wa kupingana na Maaskofu wenzake Maaskofu hao wanapoielekeza serikali? Jee Askofu Pengo ni maalum tu kuisemea serikali inaposhambuliwa na Maaskofu wenzake wa kikatoliki?
 
Hawa ndio viongozi wanaosababisha waumini wayumbeyumbe na kuishia kukimbia kanisa. Kwahiyo yeye anasema kama nani hapo? Shame!
Ni kweli kabisa hyu jamaa kwanza katudharau waumini Wa jimbo LA Rulenge Ngara ila kawadhalilisha zaidi waumini wengine Tanzania kusema kwamba msimamo Wa niwemugizi Ni msimamo Wa jumbo lake huko Ni kuligawa kabisa huyu muhuni anafaa kukemewa!!
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Acha kuita watu takataka
 
Duuh...kweli hali si hali..
Mtoa mada ana haki ya kusema anachoona kinafaa kwa mtizamo wake....

Hoja yake kubwa nahis ni jinsi ambavyo Pengo kajitokeza kujibu hoja ya Askofu mwenzake kwa nguvu wakati kuna mambo ambayo kwa mujibu wa mtoa mada kanisa linapaswa kuyasema waziwazi....na limekua kimya....
Kanisa linapaswa kukumea maovu bila kupepesa macho hata kama litawachukiza baadhi ya watu, serikali etc...

Kwa wafuatiaji wa historia ya kanisa katoliki wanafahamu kabisa kwamba kuna makosa mengi ambayo Mapapa walifanya...na pia kuna misimamo ya kanisa ambayo alisababisha mpasuko mkubwa lkn kanisa halikua na budi kuonyesha msimamo..mfano kutokea kwa kanisa la Anglican...kwa wanaofuatialia historia ya kanisa wataelewa...

Hivyo bac Pengo asisubir mpaka watu waongee ndo ajibu....yeye na kanisa walipaswa kujua kabisa kwamba labda waumini wao wanataka kujua msimamo wa kanisa kuhusu katiba mpya, hali ya kisiasa etc....hivyo wanapaswa kuwa wawazi..wakinyamaza watu watatafuta misimamo sehemu nyingine
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?

Kwani papa kitu gani kuna papa samaki Acha kua mtumwa wa Dini
 
....Acha ujuha, tunazungumzia katiba ya nchi kwa watanzania 50 mill, hivi unajua watanzania walioko kwenye vyama ni wachache kuliko wasio na vyama? Mkiwa majukwaani mnahubiri utaifa na uzalendo, huku vichochoroni mnakomaa na chama chenu cha makanikia.
Acha ukilaza vyama ndivyo vinavyo mteua mtu kutokana na katiba na taratibu zao chama kikiwa na vilaza kama wewe watateua mgombea Kilaza atakae badilisha katiba kwa maslahi yake na chama chake. Tuanze kurekebisha katiba za vyama kisha tutapata mtu ataetuunga mkono wa kizalendo kurekebisha katiba tuliyo nayo. Umesikia wewe Kilaza?
 
Saint Mery's ni shule za madhebu ya kilokole na siyo shule za kanisa katoliki.
 
Back
Top Bottom