Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Ombi langu kwa Papa Francis aruhusu haraka mapadri kuoa.
Angalau nao wapunguze stress ili wawaze sambamba na sisi waumini wao .maana duuhh
 
Usikariri! Nani aliyekudanganya kuwa UK haina katiba? UK does not have a codified constitution. Hiyo haina maana kuwa haina katiba. Katiba yao imeundwa na Acts of Parliament, Court Judgments na Conventions.
Unaruka ruka Kama chura aliyeangukia kikaangoni kifupi ulitakiwa useme uingereza haina katiba ila inatawaliwa na sheria zilizopitishwa na bunge zinazogusa kila eneo
 
Usikariri! Nani aliyekudanganya kuwa UK haina katiba? UK does not have a codified constitution. Hiyo haina maana kuwa haina katiba. Katiba yao imeundwa na Acts of Parliament, Court Judgments na Conventions.
Nielimishe mkuu hapo huwa sielewi kitu wanaposema UK hawana katiba
 
Nani anamjua Nimewemugizi bhana? Pengo ndo kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania, ndio maana wakatoliki kote Tanzania humuombea Pengo katika sala zao baada ya pope, huyu jamaa ndo anatoa report ya maaskofu wote Tanzania kwa pope juu ya mienendo yao na ku propose nani amrithi hapo baadae ,kwa hiyo pengo ni mkubwa wao.
Wewe Mungu akurehemu tu, Pengo ni askofu wa jimbo la Dar es salaam, mamlaka yake inaishia kiluvya ukivuka tu daraja kuingia kibaha Pengo hana mamlaka napo.

Maaskofu wote wa majimbo ya Tanzania wana hadhi sawa na hakuna mkubwa zaidi ya mwenzake.

Makao makuu kuwepo Dar haimaanishi Pengo ni mkuu wa maaskofu wote hakuna kitu kama hicho kwenye system ya kanisa katoliki.

Wanaomumbea Pengo ni makanisa ya jimbo la Dar es salaam ambako yeye ndio kiongozi wao na siyo sehemu nyingine acha kupotosha kitu usichokijuwa.

Mwakilishi wa Papa Tanzania ni balozi wa Vatican na siyo huyo Askofu Pengo.

Akili za kijinga kama hizi ndio zimemfanya Makonda ajione yeye ni zaidi ya wakuu wa mikoa mingine, huu ni upumbavu mtupu.
 
Kila mtu anajua ile kauli ya Askofu Niwemugizi haikuwa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC); bali ni ya askofu mmoja ambaye naye anajua fika kuwa kauli aliyoitoa ni ya kichungaji na inaungwa mkono na wenzake walio wengi. Hata Kadinali Pengo analijua hili na hakuwa na haja ya kulitolea ufafanuzi. Kwamba Kadinali Pengo ameamua kufafanua jambo lisilohitaji ufafanuzi kuna maana moja tu: amemuombwa kufanya hivyo!
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Acha kua mbumbumbu wewe uingereza inayo katiba sema katiba yao haijaandikwa ni unwritten constituion
 
Wewe Mungu akurehemu tu, Pengo ni askofu wa jimbo la Dar es salaam, mamlaka yake inaishia kiluvya ukivuka tu daraja kuingia kibaha Pengo hana mamlaka napo.

Maaskofu wote wa majimbo ya Tanzania wana hadhi sawa na hakuna mkubwa zaidi ya mwenzake.

Makao makuu kuwepo Dar haimaanishi Pengo ni mkuu wa maaskofu wote hakuna kitu kama hicho kwenye system ya kanisa katoliki.

Wanaomumbea Pengo ni makanisa ya jimbo la Dar es salaam ambako yeye ndio kiongozi wao na siyo sehemu nyingine acha kupotosha kitu usichokijuwa.

Mwakilishi wa Papa Tanzania ni balozi wa Vatican na siyo huyo Askofu Pengo.

Akili za kijinga kama hizi ndio zimemfanya Makonda ajione yeye ni zaidi ya wakuu wa mikoa mingine, huu ni upumbavu mtupu.

Pengo ni archbishop maana yake ni chief or high level leader , na hukaa makao makuu tu, hivyo St peter la dar sio tu jimbo la Dar es salaam bali ni makao makuu ya kanisa katoliki Tanzania, mtu anae kaa makao makuu ndo kiongozi mkuu wa kanisa ila kanisa analosalisha kama mtume.

Ndio maana hata niwemuguzi akifikia hatua ya kuwa archibishop atatoka huko aliko aje Dar akisubili pengo kuresign au kufariki yeye arithi, ndio maana hata pengo mwenyewe baada ya Rugambwa kuona hali yake sio nzuri aliteuliwa kuwa archibishop, maana yake alikuwa normal BISHOP kama wengine, na baada ya rugambwa kuresign ndo akamrithi na kuwa cardinal, kutomtambua pengo kama kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania sio sahihi.

Labda twende tukaangalie details za archinishop, bishop & cardinal yana maana gani, pengine wakatoliki waje watueleze kwa undani zaidi.
 
Pengo ni archbishop maana yake ni chief or high level leader , na hukaa makao makuu tu, hivyo St peter la dar sio tu jimbo la Dar es salaam bali ni makao makuu ya kanisa katoliki Tanzania, mtu anae kaa makao makuu ndo kiongozi mkuu wa kanisa ila kanisa analosalisha kama mtume . Ndio maana hata niwemuguzi akifikia hatua ya kuwa archibishop atatoka huko aliko aje Dar akisubili pengo kuresign au kufariki yeye arithi, ndio maana hata pengo mwenyewe baada ya Rugambwa kuona hali yake sio nzuri aliteuliwa kuwa archibishop, maana yake alikuwa normal BISHOP kama wengine, na baada ya rugambwa kuresign ndo akamrithi na kuwa cardinal, kutomtambua pengo kama kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania sio sahihi. Labda twende tukaangalie details za archinishop, bishop & cardinal yana maana gani, pengine wakatoliki waje watueleze kwa undani zaidi.

Acha ku profess ignorance mbele za watu. Tanzania kuna majimbo makuu 5, sio Dar peke yake, Arusha, Dodoma, Songea, Mwanza. Ukuhani ndani ya kanisa una daraja tatu yaani ushemasi, upadre na uaskofu. Hayo mengine ni taratibu tu za kiutawala.
 
esitena tetena,

Mimi ni muumini mwaminifu wa Kanisa Katoliki. lakini kwa hili siwezi kumuunga mkono kadinali Pengo hata kidogo.Kwa hali halisi ya watanzania ilivyo sasa, suluhisho pekee ya kututoa hapa tulipo ni kuruhusu ule mchakato wa katiba ya tume ya Jaji Warioba uendelee tena bila kuchakachuliwa kwa maana ya ile rasimu ya kwanza aliyoafiki JK kabla ya kuja kuchakachuliwa na bunge la Samwel Sitta.

Huyu mzee Pengo nilikosa imani naye tangu pale alipowageuka maaskofu wenzake wote kwenye msimamo wa kanisa katoliki kuhusu katiba mpya wakati wa mchakato wa mwanzo.

Huyu mzee hajui mateso wanayoyapata waumini wake na watanzania kwa ujumla juu ya mapungufu makubwa yaliyopo kwenye katiba inayotumika sasa kwa kumpa mtu mmoja mamlaka makubwa kiasi cha kuweza kuamua mustakali wa maisha ya watu zaidi ya milioni 55 kwa namna anavyojisikia yeye mwenyewe bila kubanwa na mtu au kitu chochote.... kweli?!! not fair kwa kweli
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake


Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Sasa mbona huyu ana sauti kubwa?
 
Mkuu raisi wa baraza la maaskofu ni wa Iringa, Ngalalekumtwa alichukua kutoka kwa huyo wa Mwanza Dr. Ruweichi na msaidizi ni Niwemugizi wa jimbo la Rulenge kama sijakosea!
kumbe yule msaidizi ana sauti, sasa huyu kwa nini anamkanusha mwenye sauti kubwa?
 
Pengo kasema ukweli kuwa si msimamo wa kanisa .. Basi kwanini misimamo awamu hii hamna?
kwani aliyesema atalihamasisha kanisa kuhusu mchakato wa katiba ni kanisa gani?
 
Back
Top Bottom