Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Hii ni kunyutrolise mambo
 
ni kweli
 
Acha ku profess ignorance mbele za watu. Tanzania kuna majimbo makuu 5, sio Dar peke yake, Arusha, Dodoma, Songea, Mwanza. Ukuhani ndani ya kanisa una daraja tatu yaani ushemasi, upadre na uaskofu. Hayo mengine ni taratibu tu za kiutawala.

Nimekuelewa mkuu, swali langu ni moja tu, je mkuu wa kanisa katoliki Tanzania ni nani? tuache mambo ya nani msemaji wa kanisa katoliki kwani hata serikali ya ina Rais na inamsemaji mkuu wa serikali, je msemaji mkuu wa serikali anaweza kuwa mkuu wa serikali? najua system ya serikali na ya kanisa ni inaweza ikawa tofauti au ikashabiliana kwa aina moja, au kanisa katoliki Tanzania halina kiongozi mkuu?

Mfano nimejaribu kutafuta head of catholic church in Uganda nikampata kama ilivyo hapa chini kwenye link, nikatafuka Kenya nikaona pia wanasema somebody njue, je Tanzania hakuna?, tuachane na mambo ya madaraja wengine hatujui, tunachotaka kujua ni kimoja tu je kuna kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania au hakuna?
bpy3ciz/index.htmlBishop Odama is new head of Catholic Church in Uganda
 
ukweli mtupu pasina shaka
 

Kama hulifahamu kanisa takatifu na mfumo wake wa kiuongozi ni heri ukae kimya kuliko kupotosha.

Mfumo wa Kanisa katoliki umegawanyika Kutoka Duniani down to Archdioceses(Majimbo Makuu) yanayoongozwa na Maaskofu Wakuu then Dioceses(Majimbo) yanayoongozwa na Maaskofu wa Jimbo.

Hivyo basi hakuna mfumo wa Kanisa Katoliki katika mipaka ya Kinchi na mdio maana hata Majimbo hayafuati mifumo ya Mikoa ya Kiserikali/Kijiografia.Hivyo basi eneo kua Jimbo Kuu haimaanishi ndio makao makuu ya KK katika nchi.

Askofu Pengo ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam lenye majimbo madogo kama Moro,Tanga n.k.

Kuna majimbo 34 Tanzania,Kati ya hayo matano ni Majimbo Makuu-Arusha,Mwanza,Dodoma,Tabora na Dar es Salaam na haya yote yana Maaskofu wakuu na wanakua na Nguvu katika Jimbo kuu lake tu na kua askofu mkuu haimaanishi ww ndio mkuu wa Maaskofu katika nchi.

Kwa mantiki ya ulichokiandika kua Askofu mkuu ndio kua mkuu wa kanisa nchini,basi utamaanisha Tanzania ina Wakuu wa KK watano maana wote ni Maaskofu wakuu.
Nadhani nimesaidia kuondoa huo utata.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 

Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania na Duniani ni Papa. Hakuna Askofu mwingne zaidi ya Askofu Mkuu wa Roma yaani Papa anaekua mkuu wa Kanisa katika Nchi yoyote au bala lolote.

Kutoka Papa inafuata level ya Jimbo na Mkuu wa Jimbo ni Askofu mahalia.

Hakuna Cheo cha Mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania ila Duniani kote kuna mabaraza ya Maaskofu wa Kila nchi au eneo fulani na huchagua Marais wao ili kupata uongozi unaowaunganisha lakini haimaanishi kua uyo Rais ndio mkuu wa Kanisa bado mamlaka yanabaki kwa Askofu wa Jimbo mahalia.

Shida inayosumbua wengi ni kutaka kuchukua mfumo wa kiutawala wa Dini/Madhehebu mengne kuulazimisha ufiti katika Kanisa Katoliki.

Waandishi wa Habari mara nyingi wamepotoka na kuandika habari fake kwa kuchanganya haya mambo.Hata iyo habari ya Uganda ni matokeo ya kuchanganya huku.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kwa Watanzania wenye upeo wa kufikiri KATIBA MPYA ilitakiwa ipewe kipau mbele na Awamu ya 5. Tulitumia hela nyingi sana kwenye Tume ya Warioba na Bunge la Katiba sasa kazi yote iliyofanyika ina maana haikuwa na tija? Kwa hiyo tulichezea rasilimali zetu wenyewe? Basi Rais awawajibishe wote waliohusika kwenye ule mchakato!

Ile Rasimu ya Warioba ingepitishwa na Bunge la Katiba tungejenga Tanzania ya Viwanda katika muda mfupi sana maana kila mhusika angefanyia kazi nafasi yake ipasavyo.

Katiba mpya ingefanya kila kiongozi awe wa siasa au wa kiserikali kuwajibika ipasavyo na akizembea tu anaondolewa kisheria!
 

Katika Kanisa Katoliki hakuna cheo cha mkuu wa kanisa wa nchi. Waandishi makanjanja ndio wanaopotosha na kuandika hivyo. Hapa Tanzania kwa vile tunaye Kardinali watu hudhani kuwa ndio mkuu wa kanisa. Vp kwa zile nchi ambazo zina makardinali Zaidi ya mmoja?

Kila Askofu wa Jimbo ni mkuu katika Jimbo lake. Huyo Pengo hawezi kwenda Rulenge bila ruhusa ya Askofu Niwemugizi and vice versa. Kila Askofu anawajibika moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu. Na hapa Baba Mt sio mtu bali ni ofisi.....kuna idara Vatican inahusika na Maaskofu......na kwa nchi za kwetu "nchi za misioni" mambo yetu yote yanashughulikiwa na idara inaitwa propaganda fide.

Ukisikia Jimbo limepewa hadhi ya Jimbo Kuu basi Askofu wake ataitwa Askofu Mkuu na yale majimbo yaliyo chini yake suffragan diocese yanamwangalia huyu Askofu Mkuu kama muunganishi wao....sio mkubwa wao.

Maaskofu wa nchi wameruhusiwa kuunda mabaraza ndizo hizo episcopal conferences.... na maaskofu huchagua yeyote kati yao kuwa Rais wa hilo baraza.... Niwemugizi amewahi kuwa Rais wa Baraza.....Pengo hajawahi kuwa Rais wa Baraza. Hiki ni chombo tu cha kulisemea kanisa mahalia - a particular church. Kwa sbb wakati mwingine kuna mahitaji maalumu ya kanisa mahalia. Mfano. Sheria ya Kanisa Katoliki kuhusu ndoa ni miaka 16 kwa mwanaume na 14 kwa mwanamke.....Sasa hapa Tanzania sharia za nchi ni kinyume na sharia ya kanisa...basi kanisa katoliki la Tanzania - hilo baraza linaomba kwa hapa Tanzania tufuate utaratibu wa nchi yetu!!!!!! What if mkatoliki wa TZ akiwa nje ya TZ akafunga ndoa akiwa na miaka 16 mwanaume ndoa yake itatambuliwa na kanisa katoliki TZ au la? nakuachia assignment.
 
Mungu akupe maisha marefu Polycarp Cardinal Pengo.
 
Pengo hana mamlaka ya kuwasemea maaskofu wengine. Anayo mamlaka ya kulisemea jumbo la Dar es Salaam.
 
Mzee Pengo sina imani kama unachosema ni kwa utashi wako, nadhani unajitoa tuu ufaham ukijua kabisa unachofanya. Hata mie nakuunga mkono kuwa kauli ya yule askofu ni maoni yke binafsi, ni kweli kabisa, ila je; ni kweli wewe hujui umuhimu kupata katiba inayofuata matakwa ya wananchi !? Ni kweli katiba haina umuhim !? Noooo, sina imani kama huo ndio utashi wako.

Naomba ujue sisi wananchi ambao wewe pia unatuongoza tunahitaji katiba kwa maslahi ya wananchi na kwa dira imara ya taifa kwa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Wewe!!! Kwanini umeamua kupotosha kiasi hiki...??? Ili iweje..? Umetumwa au ni akili zako zimekutuma kuandika haya.. ???
 
Wengi unamaanisha nini?unadhani kila mtu ni kama wewe?
Wengi amemaanisha wale walioshiriki kutoa mawazo yao kwa tume ya warioba ambayo ilileta matokeo ya ile rasimu II. Maoni yaliyoleta ile rasimu ndio maoni ya watanzania wengi, sasa wapi hujamwelewa ? Kama hukumwelewa ni vema usingeandika llte.

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Pengo na balozi wa papa hawajakosea.hata yy kasema mtazamo wake binafsi.sio kanisa.kutoa matamko ya jimbo yana utaratibu wake.

Hata kwa jimbo la dsm bado halijatoa msimamo ila aliesema ni pengo.sio jimbo kuu la dsm.

Pia kupitia baraza kuu la maaskofu napo kuna utaratibu wake ambao maaskofu wote wanaketi na kuamua hivyo hata askofu wa iringa ambaye ni rais bado kuna mashart kadhaa huo ndio ukweli kabisa.

Wananchi wanahitaji katiba mpya ila kwa kiwango gani hapo ni utafiti,kanisa linapenda kuona huduma zinatolewa vema
 

Nimekuelewa vizuri, ateast hata wengine walio nje ya mfumo catholic tunaweza elewa, niko na swali lingine, mfano ukiangalia katika archibishops or bishops wengi, majina yao mengi yanaanza na Rev francis,or Rev Musa, lakini ikifika kwa cardinal wanaanza na His eminence makanga etc, pengine haiwezi ikawa ni unification figure within the Catholic Church and society?.
 
Asiyejitambua huyu! Kauli ile ni msimamo wa Watanzania tulio wengi. Unazidi kupoteza mvuto kwenye jamii ya Watanzania kwa kutokemea maovu ya dikteta uchwara.
mkuu upo sahihi kabisa, japo pia Askofu hakusema ule ni msimamo wa Kanisa, vivyo hivyo aliyosema Pengo nayo siyo msimamo wa kanisa. Ila kiongozi asiyeweza kukemea uovu huyo hafai, sijaisikia sauti ya Pengo juu ya shambulio la Lissu, ni ajabu.
 
ASANTE[emoji122] [emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…