Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo anatumika vibaya sana aachane na uaskofu ateuliwe hata ukuu wa wilaya...
Kwa cheo cha Pengo ukuu wa wilaya, mkoa hata huo urais c chochote kwa Kardinal hata uraia wa Kardinal ni mataifa yote duniani mfano anaweza kuwa raia wa Tanzania lkn akawa mwakilishi wa papa popote duniani au kuwa kardinal wa Marekani wakati ni Mtanzania hata tu askofu wa kawaida hawezi linganishwa na wilaya au mkoa.
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake

Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Kweli unajua! Hongera, nadhani tumekuelewa.
 
Mwenye ile clip ya Gwajima kumhusu Askofu Pengo Tafadhali aipandishe hapa jukwaani
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.

Pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.

chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.

Pengo is hopeless. Hata yeye kauli yake si ya kanisa. Ni maoni binafsi.

TEC ndio chombo kikuu na rasmi cha kanisa hapa Tanzania.
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake

Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine

Na ndiyo maana yeye Pengo ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar, na Jimbo la Dar ndiyo Makao Makuu ya Ukatoliki, isitoshe unasema Kardinali kazi yake ni kupiga kura tu, unaweza kuwa Sawa lkn Kanisa Katoliki lina mambo mengi kumbuka Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania ni Papa -Roma na hakuna Mtanzania mwenye access na Papa zaidi ya Kardinali, wanakaa Meza moja na Papa Roma wanajadili, hivyo ana uwezo mkubwa zaidi kuliko hata Baraza la Maaskofu indirectly kwa maana yeye anawasiliana na Papa moja kwa moja, lkn Baraza Kuu la Maaskofu hawawezi kumuingia Papa kirahisi, hivyo nguvu anayo tena kubwa sana tu, kwanza kama Mkuu wa Jimbo la Dar pili kama Kardinali kwa maana ya access na Big Boss, Papa mwenyewe!
 
Pengo astaafu tu akapumzike .

Yuko kwenye hiyo nafasi tangu nipo shule ya msingi hadi Leo Nimekuwa MTU. Mzima
 
Mpakwa mafuta anapokwenda kinyume na maagizo ya mungu basi kuhani mkuu huagizwa na mungu kumtia mafuta mteule mpya na yule kaidi mungu humfutilia mbali hata kizazi chake...

Rejea daudi alivyopakwa mafuta kuchukua nafasi ya sauli.

kwa muktadha huo basi naomba tuamini mpakwa mafuta wa kale zama zake zishakwisha na sasa ni zama za mpakwa mafuta mpya....baba askofu niwemugizi.
. Kabisa! Pengo halijui analolitenda,naamini huo nao ni msimamo wake ila sio msimamo wa Kanisa Katoliki na Wakatoliki wengi tupo nyuma ya Askofu Niwemugizi kuitaka katiba mpya.
 
Wasalam, huyu askofu si ndo kati ya wale waliobeba pesa kwenye viroba, namshauri arudishe pesa za walipa kodi wa tanzania aache kujipendekeza kwa watawala
Usimshuhudie jirani au mtu yeyote uongo! Una uhakika na ulichokisema? Tubu uongo huu kabla ya kuingia kulala
 
Siyo kweli! Mimi ni Mkatoliki na sifuati kauli tu kwa vile imesemwa na papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo mpaka iwe na ushawishi kwangu kwamba haipingani na neno la Mungu na ina mchango chanya kwa imani ya Kanisa na imani yangu na pia ustawi wangu na wa familia yangu. Nje ya criteria hii, papa, askofu, padre, katekista au kiongozi wa jumuiya ndogondogo anajisumbua maana sitafuata neno lake. Hivyo, siyo kweli kwamba "Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao". Labda ungesema "baadhi ya Wakatoliki ni watiifu kwa viongozi wao" (maana hata wakiambiwa mambo yasiyo ya msingi wanatii).

Kwangu siyo hivyo - hata mahubiri ya padre nayachuja kama hayakidhi kiwango hata sisikilizi, natoka nje ili amalize au nakacha kabisa. Ninafuata imani yangu kwa uhuru na si kwa kumwogopa kiongozi wa kiroho maana hivi ndivyo nilivyoelelewa.
Tafuta ufafanuzi wa neno hili la kilatin ROMANA LOCUTA KAUTAFILITA.

Kisha ww ni mmoja unayepinga na kutoka nje waliowengi hubaki ndani bado hujajitafakari.
 
Sasa Kama Niwemgizi alitoa maoni binafsi sio ya kanisa kwa Nini wakati anayatoa alikuwa amevaa mavazi ya kiaskofu ikiwemo Pete na msalaba shingoni
Kama issue ni hivyo , askofu wa jimbo kuu katoliki DSM angetakiwa asubiri kauli hii itolewe na TEC kupitia kwa Rais wake au makamu au ingetolewa na Katibu wa TEC ili kuonesha kwamba kweli kauli ile haikuwa ya kanisa katoliki Tz. Lakini pia kama Askofu mkuu wa DSM anasema ule haukuwa msimamo wa kanisa jimbo la Rulenge basi Baraza la Walei Jimbo wangetakiwa kukanusha.

Hii ya askofu mkuu wa DSM kukanusha ile kauli inaweza kuendeleza mjadala kama Askofu Niwemugizi naye ataamua kumjibu (japo hawezi) kusema kuwa askofu wa kardinali nayo si msimamo wa kanisa Tz wala si msimamo wa kanisa jimbo kuu la DSM. Kama askofu Niwemugizi hakutoa msimamo wa jimbo lake tutaaminije kama kauli ya kardinali ni ya jimbo kuu la DSM?
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.

Pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.

chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.
Yaani huyu Mzee kwa kweli anachekesha sana. Alikuwa anampinga Kikwete kila jambo lakn sasa hivi eti anakanusha hata ukweli ulio wazi jamani hatari sana.
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.

Pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.

chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.
Pengo....Naona yale maharage alokula bado tu yanamsumbua!!!
 
Sioni tatizo kwa alichokisema Pengo. Askofu Niwemugizi ameongea msimamo wake binafsi kwa sababu tamko la Kanisa au ushauri wa kanisa Katoliki unatolewa baada ya TEC kujadiliana, jambo ambalo halikufanyika kabla ya tamko la Askofu Niwemugizi.

Alichokifanya Askofu Pengo ni kusisitiza kwamba tamko la Askofu Niwemugizi ni lake binafsi na siyo msimamo wa kanisa kama ambavyo Kadrinali Pengo mwenyewe ametoa msimamo wake binafsi kua Katiba sio kipaumbele kwa sasa.
Kanisa katoliki ni taasisi kwa hiyo tuache kulaumu ovyo.

Mnaompinga Pengo kwanza siyo wa katoliki nyie ni vijana wa Gwajima na tunajua mna vita na Pengo. Kanisa katoliki litaendelea kuimarika na Kadrinali Pengo ataendelea kupiga kazi kama hutaki hamia kwa wasabato au walokole, kwani shillingi ngapi aisee?
 
Pengo ni mtu asiyejulikana..! Zao la mfumo yule kama hamjui shauri yenu...!
 
Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu
Kwa nini Rais Ngalelemtwa asiende kupiga kura kuchagua papa aende Pengo?
Mnayumbisha watu ufahamu kwa kulazimisha matakwa yenu.
Muadhhama Kadinali Pengo ndio kiongozi mkuu wa kiroho wa kanisa Katoliki nchini Tanzania.
Papa hawezi kufanya mabadiliko ya maaskofu au uteuzi bila ya kushauriana na Pengo
Huyu sijui Rais wa maaskofu ni vyeo tu kurahishsa utawala na kazi za kiroho
 
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,

Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake

Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza

"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine
Asante
 
Mhashamu Askofu Kardinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa na askofu Niwemugizi kuwa katiba mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi sio msimamo wa kanisa kwa sababu kanisa lina taratibu zake za kuishauri serikali au kuzungumzia masuala ya jamii.

Pia amesema kwake yeye katiba ni kitu kije baadaye si cha haraka.

chanzo: gazeti la Mwananchi via facebook.
Laana inamwandama, yawezekana niya Rushwa
 
Back
Top Bottom