Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

tatizo braza niko huwa unaongea baada ya kupiga nyagi

Mkuu kama huelewi issue zinazoendelea nikusaidiaje uelewe iliyopo mezani. Gwajima alisema kiongozi wetu kawasaliti ktk kikao, sasa kiongozi huyo huyo kaja mkana tena mkazi mwenzie ktk nyumba yao. Na huyo mkuu kakosea tena zaidi .

Kasema wana utaratibu wa kuwasilisha maoni kwa serikali bila kusema pia nyumba yake ina utaratibu wa kusuluhisha tofauti za wakazi wake za ndani. Kamwanika mwenzie hadharani huku wanakaa nyumba moja. Eti sio msimamo wa nyumba yao, kwani kuwaanika wenzio ni msimamo wa nyumba yao?
 
huhitaji kusema kuwa huna chama.
Unashauri mbinu gani labda?
Girl..stay calm..take your way.we take our way
Vipi unaamini kwa siasa za Chadema za sasa zina ushawishi wowote zaidi ya kuonewa huruma.?
 
huhitaji kusema kuwa huna chama.
Unashauri mbinu gani labda?
Girl..stay calm..take your way.we take our way
Vipi unaamini kwa siasa za Chadema za sasa zina ushawishi wowote zaidi ya kuonewa huruma.?
 
chadema haifungamani na dhehebu lolote.
waulize hao maaskofu yale matamko dhidi ya serikali ya kikwete yamepata kigugumizi gani kwa utawala huu?
 
Wakuu natanguliza salamu .

Maelekezo makuu ya Mungu kwa wanadamu ni kuishi katika kweli iliyojaa haki tupu , kutenda mema na kukataa maovu , hivyo tunategemea kiongozi yeyote wa dini ya kweli aishi na atende kama Mungu alivyoelekeza .

Kardinali Pengo anatenda kinyume na Maagizo haya ya Mungu , ni wazi ameamua kujipambanua kuukumbatia unafiki , Amejipachika usemaji wa Kanisa kinyume cha utaratibu .

Ni vema sasa Kwa kulinda heshima yake lililojiwekea miaka mingi , kanisa Katoliki linapaswa KUMTIMUA kardinali Pengo ili akaendeleze harakati zake za kupinga katiba mpya ndani ya chama chake cha ccm .

Naomba kuwasilisha .
Naunga mkono HOJA
 
mimi ni mkatoliki, ilishangaza kuona kanisa katoliki halikulaani kushambuliwa kwa tundu lissu

Vijana mashabiki Wa Chadema na Demokrasia maji Taka.

Majuzi huko bongo kulikuwa na mjadala wa uhuru Wa mitandao ya Jamii ,mada Nzuri na ya kuvutia. Uzuri Wa mjadala ni pale pro and cons zinapojadiliwa kwa usawa ,hoja na ustaarabu WA kimantiki ili kupata compromise ya what’s really positive for the betterment of this given Society.

Given Society in this instance ni Tanzania. In general mitandao ya kijamii kama yenyewe ilivyo haina shida. Na experience yangu kwa kupitia humu Nimeona uhuru Wa kutoa maoni upo. Ingawa kikubwa nilichoona. Wengi humaanisha hakuna uhuru Wa maoni kwanza kimkumbo mkumbo tu na Zaidi sana wanamaanisha uhuru Wa „Kupinga tu na kutukana tu ,na kutumia Lugha yeyote“bila kujali heshima na utu Wa mwingine regardless of chama Au itikadi yake. Bahati mbaya hata Viongozi waliotoa mada hawajazingatia this given Society na hali yake.

Tumekuwa tukidhani kuwa hoja lazima iwe against the government and Sio inayotuhusu kutokana na uelewa wetu. Ndo mana hapa Jamii F. Matusi. Kashfa ndo hoja of the day. Mtu anatafuta namna yoyote aingize hoja ili kusema ujinga na fustrations zake ambazo angeweza kuzitatua binafsi au kwa msaada Wa wanaomzunguka.

Demokrasia ndo neno linalozungumziwa karibu kila Siku. Na nilichogundua Vijana wengi hata hawaelewi maana ya neno lenyewe. Kwao Demokrasia ni jambo La kufanya na Serikali tu. Na Hasa ruksa ya kutukanana na kusingiziana habari. Neno Uhuru Sio licence. Uhuru unakuwa na Rights na obligations kadiri ya hali yako kama mwanadamu. Kama mtanzania na kama baba. Mtoto mama. Mwanafunzi mwalimu. Kiongozi. Nk. (Maadili ya given Society).

Jamii F sasa inajipambanua kama Mahali penye Vijana Au wazee („watoto“) Wa chama pendwa cha Humu CDM. Wamekuwa hawaheshimu maoni ya wengine. (Demokrasia) wamekuwa searchers and seekers of negativity.JF imekuwa Sio Mahali Pa pro and cons in search for a solution bali kupinga bila tafakari ya wenyewe binafsi. You want Demokrasia lakini we wenyewe Mtu akienda kinyume Lugha huja matusi na kibaraka.

Vijana „Watoto“ ukiamua kupigania kitu pigania si kile tu mbele ya PUA yako bali global and Metaphysikal —the truth not only logically. Jitunze kuheshimu hoja na uelewa Wa wengine. Jifunze kutumia Lugha inayokutambzlisha wewe .kwamba hata Leo Id yako ikifumuka Wazi heshima yako na utu na msimamo utatambulika.

Lema alimtaja Muro ,na Muro akamtaja Lema. Ona sasa Vijana Wa Demokrasia wanapotokea. Kelele. Matusi kashfa. And then wanasema Demokrasia Mkasome kwanza Nendenni mkajitambue na rudisheni Hela manazopewa kuwa wapingaji mpaka uhalisia Wa wazazi wenu. Then come and demand Demokrasia. Leo kuwa Mbunge eti Sio muhimu kukaa na kufanya Kazi jimboni. Ohhhh kweli Demokrasia inachu
 
Uchaguzi wa 2010 Kanisa lilishiriki kikamilifu kuwashawishi waumini wake, kutoa waraka wa aina ya viongozi wanaohitajika, kutoa elimu ya uraia na haki zao kwa waumini wao.

Ni wakati huo Chadema ilikuwa inaungwa mkono na jamii kubwa hasa wasomi na vijana.

Ni wakati huo Watanzania wengi walijitolea kuitetea Chadema kwa jasho na Damu....

Ilifika wakati ikawa ni aibu kwa Mtanzania hasa wa mjini kujitambulisha yeye ni ccm.

Iwe kwenye mkusanyiko au vyombo vya usafiri ukitetea ccm jamii yote inageuka kukuangalia wewe ni mtu wa aina gani...

Hii yote ilichangia na ushawishi wa Kanisa....

Uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 uliweka rekodi kwenye siasa za upinzani Tanzania hasa Chadema, Chadema walichukua vijiji vingi sana hata kule ambako hakukutarajiwa walishinda.

Hii yote ilitokana na Mbegu iliyopandwa kwenye uchaguzi wa 2010.

Kosa kubwa mlilofanya ni kumkabidhi Lowasa chama, wenye akili walikaa pembeni na wengine kumuunga mkono Magufuli....wasomi wengi walikaa pembeni, watetezi walikata tamaa. chama kikabaki kutembelea kivuli cha 2010.

Kosa kubwa zaidi mnalolifanya ni kulishambulia Kanisa na viongozi wake, hili ndio kosa litakalowapoteza zaidi kwenye siasa za ushindani.

Dunia yote inatambua uwezo na nguvu ya ushawishi wa Kanisa, hivyo kujaribu kupambana na kanisa ni sawa na kunywa chai kwa mluzi....
Mawazo ya Pengo yasiwe mawazo ya waumini wa kanisa katoliki Mimi hata Leo nimekuwa kanisani mapadri wengi hawapendezwi ya yanayoendelea nchini kwa mafundisho yao hasa wanashangaa matamshi ya pengo na wanamkosoa bahati ni kuwa sio kila kanisa lina mwandishi wa habari..

Vile vile waumini wakatoliki wanajitambua sio bendera fuata upepo

Pengo ni wa kukemewa na masilahi yake binafsi juu ya utawala uliopo madarakani.
 
Kabisaa
Huyu mzee anatufedhehesha sana wakatoliki (Roman Catholic - TC)

Najisikia aibu kuwa na kiongozi mnafiki level hii

Hafai kwakweli hafai
Wewe sikia aibu kwa sababu hujui taratibu za matamko ya kisiasa yanayotolewa na kanisa katoliki. Kama Kadinali Pengo anatumika na CCM sasa unasemaje kuhusu kauli ya Balozi wa Vatican nchini Tanzania ambae ametoa maoni kama ya Cardinal Pengo kuhusu sakata hili? Wewe hamia tu dhehebu la UKAWA huko kwa wakatoliki hakukufai.
 
Ni vema sasa Kwa kulinda heshima yake lililojiwekea miaka mingi , kanisa Katoliki linapaswa KUMTIMUA kardinali Pengo ili akaendeleze harakati zake za kupinga katiba mpya ndani ya chama chake cha ccm .

Mara nyingi nimekupa like zangu kwa michango yako thabiti ila hu leo naona umekosea. Je, waijua kanisa katoliki?? Je, waijua sakramenti ya upadrisho? Basi, usiotee juu ya mti wa mwembe ukaanguka ukavunjika.
Pengo ni Kardinali, aweza chaguliwa kuwa Papa. Hivyo, kusema ati atimuliwe! Unashangaza sana. Hivi wajua kuwa siku si nyingi atakuwa anasema moja kwa moja na Muumba wako akiwa hai?? Upako alio nao haulinganishwi na yeyote Tz hii.
 
Haya ni mawazo yako. kwa upande wangu Pengo amejidhalilisha sana kupinga uwepo wa katiba mpya. na huwezi kusema suala la katiba si la wananchi wakati hao hao wananchi ndio waliotoa maoni ya namna wanavyotaka nchi yao itawaliwe. Katiba na maendeleo huwezi kuvitenganisha
Nakubaliana nawe kuhusu hilo kwenye maandishi mekundu. Na hakuna Ibara au Kifungu chochote kinachohusu haki na uhuru kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja au kundi, cha Katiba iliyopo kilichobadilishwa kwenye Katiba inayopendekezwa. Kama vipo, nitajie.
 
Hapo kuhusu Gwajima ni uwongo mkubwa. Pengo hajawahi mshitaki Gwajima.

Pia kumbuka maelezo ya Pengo yalikuwa kwamba anafafanua kuwa kauli ya Niwemugizi siyo ya kanisa kwani tayari ulikuwa na hiyo argument iliyohitaji ufafanuzi
Pengo ni msemaji au Rais wa TEC?
 
Kikatoliki Papa ndiyo Mkuu wa Kanisa Katoliki aliyeteuliwa na Mungu, hakuna njia nyingine hapo!
Mimi mkatoliki ila hii kauli huwa inanipa ukakasi kidogo! Ni kweli Papa anateuliwa na Mungu!? Kiaje?
 
Kwani hayo si ni maoni tu? Au pengo ndiyo kanisa? Lini kanisa katoliki lilimtuma akatangaze msimamo wake? Pengo ni askofu wa Dsm, period.
 
Unajua ccm imejaribu sana kuwadanganya watu duni kama wewe kwamba PENGO ni kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Tanzania , Jambo ambalo si kweli hata chembe .
 
Back
Top Bottom