Uchaguzi wa 2010 Kanisa lilishiriki kikamilifu kuwashawishi waumini wake, kutoa waraka wa aina ya viongozi wanaohitajika, kutoa elimu ya uraia na haki zao kwa waumini wao.
Ni wakati huo Chadema ilikuwa inaungwa mkono na jamii kubwa hasa wasomi na vijana.
Ni wakati huo Watanzania wengi walijitolea kuitetea Chadema kwa jasho na Damu....
Ilifika wakati ikawa ni aibu kwa Mtanzania hasa wa mjini kujitambulisha yeye ni ccm.
Iwe kwenye mkusanyiko au vyombo vya usafiri ukitetea ccm jamii yote inageuka kukuangalia wewe ni mtu wa aina gani...
Hii yote ilichangia na ushawishi wa Kanisa....
Uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 uliweka rekodi kwenye siasa za upinzani Tanzania hasa Chadema, Chadema walichukua vijiji vingi sana hata kule ambako hakukutarajiwa walishinda.
Hii yote ilitokana na Mbegu iliyopandwa kwenye uchaguzi wa 2010.
Kosa kubwa mlilofanya ni kumkabidhi Lowasa chama, wenye akili walikaa pembeni na wengine kumuunga mkono Magufuli....wasomi wengi walikaa pembeni, watetezi walikata tamaa. chama kikabaki kutembelea kivuli cha 2010.
Kosa kubwa zaidi mnalolifanya ni kulishambulia Kanisa na viongozi wake, hili ndio kosa litakalowapoteza zaidi kwenye siasa za ushindani.
Dunia yote inatambua uwezo na nguvu ya ushawishi wa Kanisa, hivyo kujaribu kupambana na kanisa ni sawa na kunywa chai kwa mluzi....