Elections 2010 Pengo: Msiwachague wanaogawa khanga na fulana

Elections 2010 Pengo: Msiwachague wanaogawa khanga na fulana

unajuwa kwanini huwa si replay post zako... "hazitoi nafasi kwa mtu wa pili kutoa maoni" mara nyingi unatoa conclusion mwenyewe!
acha nikujibu hii kwa mara ya kwanza PENGO hajataja chama flani... na hizo ndio busara za kiongozi!.. amewaachia waumini wachague kama ni CCM haya Kama ni CUF haya kama Chadema sawa! Pengo hatoi kauli za Jazba kama kakobe! ambaye ana command waumini wafanye hivi..!
njiwa kwani Kakobe alitaja chama gani.
 
ni wewe ulivyotafsiri anamsema kikwete!! .. sio waumini wake wote wametafsiri hivo
Mbona wewe unamtafsiri Kakobe kamsema Slaa waachie wengine nao rights za kutafsiri usizikumbatie peke yako. Kama wewe unatafsiri Kakobe kawaambia waumini wake wampigie Slaa wengine nao wanatafsiri Pengo kaisema CCM na Kikwete kwa vile ndiyo kinara wa kugawa khanga na fulana.
 
Viongozi wa juu wa kanisa katoliki mgombea wao alikuwa Salim Salim.Kikwete siyo kivile.Na hata Slaa pia hana baraka za hao wakulu.CUF ndiyo kabisaaa.Kwa CCM wanayemuamini kwa sasa ni Pinda na Magufuli.
 
I don't agree with you on the bold, nevertheless SAS is not on board so they have to chose at least the best among the present 7 candidates, they can't leave a vaccum.
 
Njiwa mbona akili yako finyu kweli kweli, ni Rais gani anayetoa rushwa na kutafuta urais kwa nguvu kama si kikwete? Kakobe hakumtaja mtu, anachosema uwezi ukasema rais hafai kwa sababu anaoa na kuacha! Tu wanadamu tumepungukiwa na utukufu wa Mungu, tunahitahi toba.

Nadhani mnamshambulia njiwa wangu bure! Yeye amepata ujumbe vizuri sana wa kutoka kwa Mwadhama Kardinali Pengo (huwa mnakosea cheo chake), lakini amekwenda mbele zaidi akampambanisha na Askofu Kakobe. Hajasema hajaona mada ameiona ila anafikiri ya Pengo imetulia, ile nyingine imekuwa ya jazba, naona ni sahihi. Sasa kwa kumshambulia mnataka kutoka ndani ya mada. Je Pengo alichosema si sahihi?
 
Viongozi wa juu wa kanisa katoliki mgombea wao alikuwa Salim Salim.Kikwete siyo kivile.Na hata Slaa pia hana baraka za hao wakulu.CUF ndiyo kabisaaa.Kwa CCM wanayemuamini kwa sasa ni Pinda na Magufuli.

Kiongozi Mkuu wa Katoliki Nchini amekwisha kusema bila kummumunya maneno kwamba kanisa halina mgombea! Sasa wewe hii umeipata tena wapi. Jamani tuachane na hisia!
 
I don't agree with you on the bold, nevertheless SAS is not on board so they have to chose at least the best among the present 7 candidates, they can't leave a vaccum.

Mkuu if you dont want to take it from me its ur right and that is what they call democracy anyway.Lakini nilitaka ku reveal hii kwenye public yenye maswali mengi yenye utata ooh sijui kuna mgombea katumwa na hilo kanisa,ooo kuna waraka na vitu kama hivyo,kwamba hakuna mgombea hata mmoja mwenye endorsement ya hao wakulu wa kanisa la roma.Ukibisha hao niliokutajia,basi subiri siku mmojawapo akija chukua fomu ya urais halafu utaona moto wake!
 
Nilichokuwa nakataa ni kuwa SAS ni chaguo la kanisa, hata hivyo kanisa haliwezi kutoka wazi wazi na kusema linamuunga mtu fulani litakuwa linaingilia uhuru wa wapiga kura na waumini wao, kazi ya kanisa ni kuainisha sifa gani wanataka mgombea awe nazo kama alivyofanya Kakobe na Pengo.
 
Kiongozi Mkuu wa Katoliki Nchini amekwisha kusema bila kummumunya maneno kwamba kanisa halina mgombea! Sasa wewe hii umeipata tena wapi. Jamani tuachane na hisia!

Mkuu kuna mwandishi mmoja 1995 wakati wa mchakato wa urais CCM aliwahi kumuuliza Nyerere:Vipi mzee mbona hueleweki,una mgombea wako nini?(sijanuu,lakini swali lilikuwa kama hivyo).Nyerere akamwambia,kuniuliza hili swali ni upumbavu,kwavile kila mtu ana mgombea wake na hata wewe una mgombea wako.
Kwahiyo ndiyo hivyo,hakuna asiyekuwa na mgombea.Na wakulu wote wenye ushawishi kwenye jamii,wana wagombea wao.Isipokuwa hili hawawezi kuliweka wazi katika jamii.Wakisimama majukwaani,watazunguka sana,lakini kama wewe ni insider au una insiders wako basi utayajua tu haya.
 
Nilichokuwa nakataa ni kuwa SAS ni chaguo la kanisa, hata hivyo kanisa haliwezi kutoka wazi wazi na kusema linamuunga mtu fulani litakuwa linaingilia uhuru wa wapiga kura na waumini wao, kazi ya kanisa ni kuainisha sifa gani wanataka mgombea awe nazo kama alivyofanya Kakobe na Pengo.

Watu wa nje hawawezi kupewa habari za uvunguni.Wewe kama utaamini ya majukwaani haya.Kuna mambo mengi sana yanaendelea chini kwa chini na kama huna access huko ndani basi utakuwa unaongea kama unavyoongea wewe hapa!
 
kwani TANESKO wanaingilia vipi?somo ni moja tu usichagua chama kinachogawa khanga na fulana na hiyo ni direct kuwa usimchague Kikwete na CCM..Simple!!!

Viongozi wa dini wamechoshwa na rushwa na ufisadi wa CCM, sasa wamekitosa, wanataka haki.
 
Viongozi bora wa dini Pengo na Kakobe - wote kuleni "thanks"
 
Sasa nashukuru Mungu kuwa wanajamii wameanza kuona ukweli juu JK

watu wanapewa Tshits, Khanga na kofia bure je hiyo si takrima? halafu anasema watu wamenunua kwa hela ya uchumi upi?????
Ni kweli kuwa Mramba kesi yake ni ndogo na kwa wale ambao hawajawahi kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya fisadi Mramba watajua kuwa serikali imefanya kazi kuwapeleka pale, ukweli ni kwamba kila shahidi anayekuja pale anapeleka lawama kwa Mgonya Agrey na mara ya mwisho nilipoenda walishatoa ushahidi ni 30 hivyo basi huyo jamaa kesi yake ni danganya toto ya JK

Chenge kesi yake ni ya ajabu sana na sijui kwa nini hawamuhukumu hadi sasa kwani alisababisha ajali na gari halikuwa na insurance na nyaraka nyingine zilikuwa feki sasa kwa nini hawamuhukumu sijui kwanini... Angalisho tu itakuwa ni ngumu kumuhukumu kwa kuwa ndiye mwanasheria wa dola ya CCM and serikali.... kama serikali ilikuwa na mikataba mibovu ni dhahiri kabisa kuwa lazima angewajibishwa kwa namna moja au nyingine.... ila kwa kulindana anapeta na JK anawapigia debe mbaya..

Hivi kwa kiongozi makini unaweza kwenda kwenye mkutano na kuwaambia watanzania kuwa huyu niliyemshitaki kesi yake ni ndogo tu... Jamani kuna kuna umakini hapo kweli???????

Angalia vijana wa chuo kikuu wengi wao walijiandikishia chuoni sasa wanaambiwa vyuo ni mpaka November ni SAUT ndiyo wameshafungua... Je hapo kuna umakini???? wewe una shahada kwa nini usipigie kura popote pale ulipo? kama kweli ni demokrasia????? Ni haki kweli??

Tuchague kiongozi kutokana na yale aliyoyafanya mema, yanayohusu familia yake wajameni hayo hayatuhusu kwani sisi ni wasafi kihivyo kwenye familia zetu.........

Tufanya mabadiliko na tuache woga nasema tena na tena Tanzania si lazima CCM iongoze milelel hata Nyerere alisema hayo... CCM siyo Mungu wa Tanzania. Na kama ni hiyo Amani ipo tu siku zote tu Hatuwezi kuwa na vita.. Hivi chanzo cha vita ni nini Njaa na Umaskini.
 
Tafakari ujumbe wa Pengo na uchukue atua

Nimeutafakari ujumbe wa pengo,kwa bahati mbaya au nzuri nina tofautiana naye sana. Natofautiana naye si kwa maudhui ya kile alichokisema bali kwa dhamira ya yale aliyoyasema. Sio pengo tu, viongozi wote wa dini kwa ujumla wamekuwa wanatuchanganya. Mfano ni viongozi hao wa dini wanajua wazi kuwa katiba yetu ina utata na hakuna haki. Ni wangapi wamewahi kusema kuhusu hilo. Viongozi wetu wa dini wanajua kuwa mfumo wa uchaguzi una matatizo hasa katika haki[level field] ni wangapi wamesema kuhusu hilo. Unapowaambia waumini wachague kiongozi safi bila kuchukua khanga huku ukijua kuwa kuna wizi wa kura na hukemei, hii ni nini kama si woga au unafiki.
Viongozi wa dini wanajua wazi kuwa haki haitendeki, wakulima wanaponyan'ganywa ardhi yao na kigogo mmoja tu, wangapi wameongelea hilo!
Viongozi wa dini wanajua kuwa kuna wizi wa kodi za wananchi na kikundi kidogo cha watu, mbona hawajakemea hadharani licha ya kuongea kwa mafumbo. Viongozi hao hao wanaona jinsi akina mama na watoto wanavyoteseka huko vijijini ili hali kodi zao zina nunua mashangingi, mbona wamekaa kimya. Ni hao hao kwa kutumia dini zao wanaingiza magari bila kulipia kodi na kuyauza, je ujasiri wa kuwakemea wagawa khanga wanaupata wapi.
Kiongozi Askofu mmoja aliwahi kumwalika Rais mmoja mstaafu na kuwaambia wananchi rais huyo ni msafi amefanya mengi juu ya uchumi. Kiongozi huyo anazijua tuhuma za wizi ambazo zipo wazi dhidi ya kiongozi huyo, lakini kwa kutaka milioni 5 za mchango akamsafisha mbele ya waumini wake. Sasa kiongozi huyu ataniambia niache kuchukua khanga kwa kumumini kwa lipi. Ninakemea vikali tabia za kuchukua khanga na kofia au 20,000 kuuza kura, lakini dhamira yangu lazima iambatane na matendo. Hawa viongozi hawana hilo.
Taifa lilipogubikwa na kashfa za wizi wa hali ya juu, viongozi wa dini zote walikaa kimya na kuwaachia akina ''Kubenea'', sasa leo wanatambua umuhimu wa viongozi wasio wala rushwa, swali ni je walifanya nini kutetea haki za mamilioni ya watanzania yaliyotafunwa kwa kupitia mikataba feki kama richmond,? au labda wizi wa kalamu ni dhambi ndogo kuliko kuvunja banda la kuku!
Nina jumuisha kwa kusema, alichosema Kadinali Pengo ni sahihi kabisa, lakini yeye na viongozi wa dini zote na madhehebu yote hawajasimamaia yale wanayoyajua, ni vipi leo watufundishe kile wasichoweza kukisimamia.? Ningewaomba wakae kimya watuachie mapambano ya khanga, kofia na bahasha za 20,000 sisi wapiga mayowe kwasababu tunaamini mayowe yetu yatasikika kwa mungu na wadhalimu wanaotutia umasikini siku zao zinakarabia, inaweza isiwe leo au kesho lakini tunaona pambazuko la matumaini mema.
Nitamsiiliza Dr Slaa kwasababu yeye amethubutu kusimama si mara moja au mbili kukemea maovu kwa dhamira yake,kwahiyo akiniambia anaichukia rushwa ninamwelewa zaidi kuliko yule anayenishawishi niichukie rushwa huku akiwabeba wala rushwa kwa namna flani ilimradi tu mambo yake au yao yaende vizuri.
 
Sasa mhashamu askofu si ni bora ungesema kwa kifupi tuu,kuwa msiwachague akina Kikwete na wenzake,ili watu wapate kuelewa vizuri!!!
 
Sasa mhashamu askofu si ni bora ungesema kwa kifupi tuu,kuwa msiwachague akina Kikwete na wenzake,ili watu wapate kuelewa vizuri!!!
Ndiyo maana yake unataka hadi ataje jina.
 
61681_116933228364861_108449092546608_126852_5607954_n.jpg
 
Mkuu kuna mwandishi mmoja 1995 wakati wa mchakato wa urais CCM aliwahi kumuuliza Nyerere:Vipi mzee mbona hueleweki,una mgombea wako nini?(sijanuu,lakini swali lilikuwa kama hivyo).Nyerere akamwambia,kuniuliza hili swali ni upumbavu,kwavile kila mtu ana mgombea wake na hata wewe una mgombea wako.
Kwahiyo ndiyo hivyo,hakuna asiyekuwa na mgombea.Na wakulu wote wenye ushawishi kwenye jamii,wana wagombea wao.Isipokuwa hili hawawezi kuliweka wazi katika jamii.Wakisimama majukwaani,watazunguka sana,lakini kama wewe ni insider au una insiders wako basi utayajua tu haya.

Mkuu, Nakubaliana na wewe juu ya hili mia kwa mia. Na kwa ili kuweza kujua kila kundi na viongozi wenye ushawishi katika jamii wana wagombea wake subiri jinsi siku ya uchaguzi inavyokaribia ndio viongozi hao watakavyo weza kutupa maono na kuwalengesha wapiga kura juu ya mgombea wanayemtaka kwa kutoa ishara kwa wafuasi wao ili wasifanye makosa. Na tuzidi kufuta subira kwani kila kitu kwa sasa ni kinakwenda na strategy na timing tu. Na tuendelee kuvuta pumzi.
 
Heko Pengo kwa kuweka mambo sawa. Kilaini alipotosha wengi aliposema Kikwete alikuwa chaguo la Mungu!
 
Back
Top Bottom