Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

Thanks Lege, ila waandishi wengi mwisho huwa unawasumbua sana jinsi ya kuimaliza
 
Kiukweli Mwisho Sijaupenda Wahusika Hawa Mtunzi hakuwatendea Haki
Anita na Anna

Pia Mtunz kamshusha hadhi alokuwa nayo Mathew kwani uzembe wake wa kutokukiweka Kirusi ktk Sehemu Salama ndo uloleta Maangamivu ingependeza kama angefanikiwa kukitia Mikononi kuliko kazi yote na Damu ya Noah kumwagika pasina faida ilhali Mwaulaya alifanikiwa kutunza kirus leo Mathew kashindwa kukipata

Pia Kiujumla Mtunz kaonesha kuchoka Labda sababu ya Urefu wa Riwaya ama kutaka kuingia Sokoni lakini Kwa Ujumla Wahusika kawauwa kwa Mara moja na kutuaminisha hivyo ilhali akiicha Jamii kwenye Taharuki

Binafs nimekosa Raha kabisa

Amejaribu kuonyesha tamaa ya utajiri inavyo shawishi watu kuwaambia WASALITI.
Hata hivyo Bado mtunzi ana Akiba nyingi za wahusika ambao anaweza Bado kuwatumia.
 
Huku mwishoni mtunzi ametetereka kidogo, kazi kubwa aliofanya Mathew na wenzake haikupaswa kuishia kwa kirusi kusambaa, Tena katika nchi yao wenyewe
Yap..nguvu, akili na rasilimali nyingi vimetumika lengo likiwa ni kuzuia maafa ya kirusi.....kile kirusi kilitakiwa kilindwe haswaaaaa....
Au kungekuwa na njia ya kukiharibu bila kuleta maafa.....kukiacha kisambae kisa peniela ana kinga mhhh just thinking tho........
 
Asante Sana kwa hii story mkuu... Lakini huku mwisho hapana Kwa kweli, hata kama sisi wasomaji tuna expectations of zetu ambazo ni tofauti na mtunzi Kuna ulazima wa ku base kwenye reality... Mwisho wa story sijamuona Mathew yule niliyemuona kwenye season ya 1-4,hakukuwa na ulazima wa yeye kuwa na Peniela ila kwa parts nyingine story ni nzuri Sana.... Anitha I will revenge your cruel death my girl, RIP.
 
Mkuu wangu LEGE shukrani sana sana kwa kumaliza riwaya hii.Hakika tumekusumbua sana lakini hujawahi kutujibu kwa jazba ulituchukulia kama watu walio na njaaa kali.BIG up LEGE.Tunategemea sasa utuletee Wimbo wa Gaidi utakapopata nafasi. Kwa niaba yangu mwenyewe natoa shukrani sana sana mkuu.Uwe na roho hiyo hiyo na utazidi kuwa maarufu humu JF😀😀😀
 
Kwa manbo aliyoyafanya Peniella ya usaliti hakustahili kuwa mke wa Mathew nilitegemea Anna apone ndio awe mke wa Mathew maana alirisk maisha yake sana kuiba kirusi cha Aby mikononi mwa baba yake..Anna alijitoa mhanga nashangaa hajaongelewa tena wakati alikuwa mahututi na mtu wa maana sana kwa Mathew.Peniella amezoea kugawa papuchi popote pale atakspotaka kitu hivyo Mathew maisha yake yatakuwa magumu unless Peniella aokoke awe mtumishi wa Mungu
 
Duu! Hatimaye imeandika
THE END. Nimeburudika sana na season 1 mpaka 4 zilikuwa zimeshiba kwa ubora wa hali ya juu sana ila kidogo season 5 imepungua ladha. Yani sukari ya season 5 iko kwa mbaaali sana. Lakini yote kwa yote mtunzi yuko vizuri sana tofauti na yule jamaa wa kubonyeza button na kupakapaka mate kule JLW.
Ubarikiwe sana LEGE kwa kufanikisha kuturejesha enzi zile riwaya zikiwa riwaya kweli hadi umenikumbusha dude kali la MSAKO WA HAYAWANI.
 
SEHEM YA 43 NA........................

bila mafanikio hadi leo hii nilipofanikiwa.Mathew n
ataka tu
nikwambie kwamba mimi na wanangu tulichukuliwa na
kuletwa Marekani na tuliambiwa kwamba umefariki dun
ia
kuna watu wamekuua na kwamba hata sisi tulikuwa
tunatafutwa tuuawe.Nililia sana na nilijilaumu sana
kwa nini
ukachagua kuifanya kazi ile ya upelelezi? Baada ya
kufika
Marekani tulianza maisha mapya na baada ya miaka mi
tatu
nikapata bwana nikaolewa nikijua kwamba umekufa.Kwa
sasa mimi na wanangu tuna uraia wa Marekani na toka
nilipoondoka Tanzania sijawahi kurejea kwani John
aliniambia kwamba sitakiwi kuonekana tena Tanzania
kwani
siku nikitia mguu wangu ndio utakuwa mwisho wangu.K
wa
sasa nina watoto wawili kwa huyo mume wangu mpya na
tunaishi kwa furaha.Nimebadili jina naitwa Martha.
Wanao
wote wazima na wanaendelea vyema na maisha yao ila
maisha yao yamebadilika ghafla baada ya kugundua kw
amba
baba yao yu hai.Jambo hili limewastua sana .Tumewat
afutia
mtaalamu wa saikolojia ambaye anaendelea kuwasaidia
wakubaliane na hiki kilichotokea.Watakapokuwa tayar
i
watakuja kuonana nawe but for now they are not read
y
yet.Mathew sitaki kuchukua muda wako mwingi ila nap
enda
kukwambia kitu kimoja kuwa kazi yako uliyochagua ku
ifanya
ndiyo iliyofanya hadi mambo haya yakatokea.Ndiyo
iliyotutenganisha.Mara nyingi nilikuwa nikikusisiti
za uachane
na kazi hiyo lakini hukutaka kunisikia hadi yalipo
tokea haya
yaliyotokea.Ninachotaka kukushauri ni kwamba umepat
a
mke mzuri sana na nina hakika ameirudisha furaha ya
ko
tena.Peniela ni mwanamke mrembo na dunia nzima
inamuheshimu nakuomba ,muheshimu ,mtunze na
usimuumize kama mimi kwa sababu ya kazi hiyo
uifanyayo.Ukitaka maisha yako yawe na furaha achana
kabisa
na hiyo kazi unayoifanya.Huwezi kuwa na maisha ya k
awaida
yenye furaha na amani ukiwa katika kazi hiyo.Nawata
kia
maisha mema yenye furaha na amani na mpatapo nafasi
mjapo hapa Marekani msiache kuja kututembelea.Ahsan
te
sana Mathew na fungate jema.” Akamaliza Zita na kuk
ata
simu.Mathew na Peniela wakaangaliana
“ Ni mipango ya Mungu mimi na wewe kuwa
pamoja.Yote yaliyotokea yametokea ili mimi na wewe
tukutane.Let’s enjoy life my angel” akasema Mathew
na
kumbusu Peniela wakainuka na kuingia majini kuogele
a.
TAMATI


UKITAKA KUJIPATIA RIWAYA/STORY YA KIJASUSI NA YAKUSISIMUA YA WIMBO WA GAIDI. KUTOKA KWA MTUNZI WAKO MAHILI NA BINGWA WA RIWAYA ZA TAHARUKI HUSSEIN ISSA TUWA .KITABU KINAACHIWA WIKI HII

0655428085 WAHI NA UPATE COPY YAKO MAPEMAA .KAMA UJUAVYO VITABU VYA TUWA HUWA VINAGOMBEWA KAMA NJUGU.
Shurani kiongozi[emoji4]
 
Hakika hatukupoteza muda ktk kuisoma hadithi hii,Tumejifunza baadhi ya mambo na tumeburudika sana! Asante LEGE...
 
Hivi zile hela alizowekewa rais kwenye zile account mbili za kingine atazichukua Nani?maana raisi amekufa na aliyeziweka amekufa pia nina uhakika Dr kigomba hawezi kuzichukua hizo pesa maana yupo gerezani..........Ana alikuwa mahututi alikufa au alibaki hai? Anita alizikwa bila ndugu zake kujua ......vip maisha ya edimud na mke wake huko marekani hawakumtafuta kwa nn kawasaliti......Nani alifata kuwa raisi baada ya rais kufa ikiwa wote waliokuwa wamepangwa kungombea walikufa ......
Natamani kuwe na part tu .....but lazima season 5 ibadilishwe ndiyo inawezekana kupatikana ..........

Hongera mwandishi ......LEGE big up brother msalimie mwandishi
 
Back
Top Bottom