Luno G
JF-Expert Member
- Sep 22, 2012
- 2,549
- 1,849
Niliisoma pia ila arosto ikawa kali nikaipotezea ndio naanza upya maana sikumbuki niliishia wapiHii story mwaka 2016 sikuimailiza
Wiki 3 zilizopita nikaiona nikaianza upya mpk Leo ndio naimaliza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niliisoma pia ila arosto ikawa kali nikaipotezea ndio naanza upya maana sikumbuki niliishia wapiHii story mwaka 2016 sikuimailiza
Wiki 3 zilizopita nikaiona nikaianza upya mpk Leo ndio naimaliza
[emoji95][emoji95]PENIELA
SEASON 1
SEHEMU YA 24
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Hatukuwa tumetegemea shambulio kama lile lililotokea kwa kitendo cha kufumba na kufumbua kwa hiyo tulijikuta tukipoteza kikosi kizima na ni mimi peke yangu niliyefanikiwa kutoka salama.Mpaka leo ninaamini nilifanikiwa kutoka katika shambulio lile kwa maongozi ya Mungu tu. Kila mara picha ya shambulio lile ikinijia mwili wote husisimka.Siwafichi ndugu zangu ni miaka kadhaa imepita sasa lakini mpaka leo hii nikikumbuka kilichotokea usiku ule huwa ninaogopa sana.Ni picha ambayo ni ngumu hata kuielezea” Akanyamaza kidogo na kuinama halafu akasema
“ Nilipofanikiwa kutoka salama eneo lile nilikimbia moja kwa moja hadi nyumbani kwangu lakini nikakutana na kitu cha ajabu ambacho mpaka leo hii picha yake haiwezi kunitoka kichwani.Nyumba yangu ilikuwa ikiteketea kwa moto.Familia yangu yote ilikuwa imeteketea katika moto ule mkubwa” Mathew akashindwa kuvumilia akainama na kuangusha chozi
ENDELEA……………………………………..
Nilichanganyikiwa baada ya kuona nyumba yangu ikiteketea kwa moto.Nilitamani hata kujitupa ndani ya moto ule ili nami niteketee pia pamoja na familia yangu.Mara walitokea watu wawili ambao sielewi walitokea wapi ambao nilidhani walikuwa ni miongoni mwa majirani zangu,wakaniingiza katika gari na kuniwekea bastora kichwani wakinitaka nisifurukute bali nifuate kila watakachonielekeza.Kwa wakati huo nilikuwa kama mtu niliyechanganyikiwa na sikuwa nikiogopa chochote,nilianza kupambana nao na walipoona nimewashinda wakaamua kunitupa nje na kukimbia huku nikiwa nimejeruhiwa kwa risasi begani.” Mathew akavua shati na kuwaonyesha akina Anitha kovu mahala alikopigwa risasi
“ Nilikimbia na kujificha chini ya daraja,nikampigia simu mkurugenzi na kumfahamisha kilichotokea.Dr Wilbert Augustino mkurugenzi wa idara ya ujasusi aliyekuwapo wakati ule alifika mara moja mahala nilipokuwa nimejificha na kunichukua akanipeleka katika nyumba fulani kubwa.Akawapigia simu rafiki zake wawili madaktari wakafika na kunitoa risasi ile niliyopigwa begani.Nilijaribu sana kumuuliza mkurugenzi kama anafahamu chochote kuhusiana na shambulio lile lakini alinieleza kwamba hafahamu chochote.Aliniambia niendelee kukaa katika nyumba ile wakati wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio lile la kustusha.” Mathew akainama na kuzama katika mawazo .Alikuwa amekumbuka mbali sana.
“ Kwa takribani siku kumi na nne “ akaendelea Mathew
“ Niliendelea kukaa ndani ya ile nyumba kubwa na nzuri ambayo haikuwa ikikaliwa na mtu mwingine yeyote zaidi yangu.Daktari alifika kila siku na kunitibu jereha.Mkurugenzi pia hakukosa hata siku moja kufika na kuniletea mahitaji mbali mbali ikiwemo chakula.Bado mkurugenzi aliendelea kunisihi nisijaribu kutoka nje kwani hali ya huko haikuwa bado nzuri kwa upande wangu.Alinieleza kwamba nilikuwa natafutwa sana lakini hakunieleza ni akina nani waliokuwa wakinitafuta.Hiki kilikuwa ni kipindi kigumu mno katika maisha yangu.Nililia mno kila siku nikiiililia familia yangu niliyoipenda kupita kitu chochote.Ilifika mahala sikutamani hata kuendelea kuishi kwani sikuona faida ya kuishi bila ya familia yangu iliyoteketezwa kikatili.” Mathew akainama kwa uchungu akikumbuka familia yake halafu akaendelea.
“ Siku moja mkurugenzi alikuja na kunikabidhi nyaraka za kusafiria na kunitaka niondoke nchini haraka sana kwa ajili ya usalama wangu kwani tayari nimekwisha julikana mahala ninakojificha.Niliondoka usiku huo kama mkimbizi nikielekea nchini japan.Tayari mkurugenzi alikuwa amekwisha suka mipango yote na nikafanikiwa kuingia nchini Japan kwa jina la Adrian Kusema nikiwa kama mtafiti wa kilimo ninayekwenda kufanya utafiti wa zao la mpunga.Mwenyeji wangu alikuwa ni mtu mmoja niliyemfahamu kwa jina moja tu la Yamazuka ambaye tayari alikwisha wasiliana na mkurugenzi wangu .Nilipelekwa katika kijiji kimoja cha wakulima wa mpunga ambako nilianza kujifunza kuhusu kilimo cha mpunga.Niliishi katika kijiji kile kwa muda wa miaka mitatu.Nilijifunza maisha ya ukulima.Watu wale walikuwa wakalimu sana.Walinifundisha mambo mengi .Yalikuwa ni maisha mazuri na niliyapenda.Nilijitahidi sana kuyazoea maisha yangu mapya na kuyasahau maisha yangu ya nyuma lakini pamoja na jitihada zote za kutaka kuyasahau maisha ya nyuma,bado picha ya usiku ule iliendelea kunitesa kila uchao.Kila nikifumba macho nilikuwa nikiwaona wenzangu namna walivyokuwa wakiuawa na mbaya zaidi ni ule moto mkubwa niliouona ukiiteketeza familia yangu.Nilishindwa kuiondoa kumbu kumbu ile kichwani kwangu hivyo kunilazimu kuondoka nchini japan nikaelekea Marekani ambako nilikutana na rafiki yangu mmoja aitwaye Jerry Washington ambaye anafanya kazi katika shrikika la ujasusi la marekani C.I.A.Huyu ndiye aliyenisaidia kufahamu kila kitu kuhusiana na kilichotokea siku ile usiku na hata mauaji ya familia yangu.” Mathew akainuka na kuchukua mvinyo akanywa kidogo na kuendelea
”Nchi ya Marekani kwa sasa ndiyo inayoongoza kwa uwekezaji mkubwa sana hapa Tanzania na katika eneo lote la afrika mashariki .Wamewekeza mabilioni ya dola katika sekta ya mafuta na gesi.Kwa sasa wanajenga kituo kikubwa kabisa cha mazoezi ya kijeshi cha wanamaji katika bahari kuu eneo la maji ya Tanzania.Hiki ni kituo kikubwa kabisa kuwahi kujengwa barani afrika.Kutokana na uwekezaji huu mkubwa ,serikali ya Marekani imelazimika kutafuta namna ambayo itayalinda maslahi yake katika eneo hili la ukanda wa afrika mashariki na ndipo walipounda kikosi kiitwacho Team SC41.Kikosi hiki kipo nchini Tanzania na kinaendeshwa kwa usiri mkubwa mno kiasi kwamba si rahisi kufahamu kama kuna kikosi kama hiki hapa nchini.Hata serikali ya Tanzania haifahamu chochote kuhusiana na uwepo wa kikosi hiki ndani ya ardhi yake.Team SC41 ni kikosi kidogo lakini hatari sana na kilichosheheni watu wenye uwezo mkubwa waliopata mafunzo ya hali ya juu nchini Marekani.Kikosi hiki kina uwezo wa kupata taarifa za kila kinachoendelea kila siku serikalini na lengo likiwa kuhakikisha maslahi ya marekani yanalindwa kwani uwekezaji huu mkubwa katika mafuta na gesi unauinua sana uchumi wa Marekani” Akanyamaza kidogo halau akaendelea
“ Makachero wa marekani walikuwa wakimfuatilia Faizat kwa siri toka alipotoka nchini Oman na kuzisoma nyendo zake.Hawakuwa na haraka ya kumkamata japokuwa uwezo huo walikuwa nao.Sisi hatukulifahamu hilo na ndiyo maana baada tu ya kupata taarifa za kuwepo kwa Faizat hapa nchini tulianza mara moja mikakati ya kumkamata bila kuishirikisha serikali ya marekani.Taarifa za mpango wetu ziliwafikia team SC41 hivyo wakawa wamejiandaa kutukabili ili tusiweze kufanikisha mpango wetu wa kumkamata Faizat.Hatukujua kilichokuwa kikiendelea hivyo wakatushambulia na lengo lao likiwa ni kuua kikosi chote kilichokwenda kumkamata Faizat. Hawakutaka siri ivuje kuhusiana kuonekana kwa Faizat hapa nchini.Ni mimi peke yangu niliyefanikiwa kutoka hai katika shambulio lile kwa hiyo ilikuwa lazima wanipate .Waliiteketeza nyumba na familia yangu wakiamini kwamba kwa kufanya vile watakuwa wamenichanganya kwa hiyo itakuwa rahisi kwao kunipata.Namshukuru sana mkurugenzi wangu Dr Wilbert Augustino ambaye alinisaidia nikatoroka nchini vinginevyo nisingekuwa hai mpaka muda huu.Kwa bahati mbaya Dr Wilbert naye alifariki dunia katika ajali tata.Hii yote ikiwa ni kazi ya Team SC41 .Mungu amrehemu sana Yule mzee” akasema Mathew na kunywa mvinyo kidogo halafu akaendelea.
“ Nikiwa nchini Marekani ,nilianza kufanya uchunguzi wa kina ili kujaribu kukifahamu kikindi hiki cha Team SC41 lakini juhudi zangu hazikufanikiwa kwa sababu kikundi hiki kinaendeshwa kwa usiri mkubwa mno na ni watu wachache hata ndani ya Pentagon wanaofahamu uwepo wa kikundi hiki hapa nchini kwa hiyo ni vigumu sana kuzipata taarifa zake.Kingine kikubwa nilichofanikiwa kukifahamu ni kwamba hapa nchini kikundi hicho kinaongozwa na mtu aitwaye John Mwaulaya Albert.Baada ya kukosa taarifa zake za kina niliamua kuachana nao na kujitahidi kuyasahau maisha yangu ya awali na ndipo nilipoanza kufanya kazi za kujtegemea.Kwa hiyo ndugu zangu naomba mtambue kwamba Team SC41 ni kikundi chenye nguvu lakini hatari sana.Ni watu wenye mafunzo na uwezo wa hali ya juu mno.” Akasema Mathew.Anitha na Noah walikuwa kimya kabisa wakisikiliza.
“ Kuna mawasli ambayo tunatakiwa tujiulize.Kwanza ni je Peniela ana mahusiano gani na kikundi hiki? Watu wale walioingia ndani mwa Penny walitoka na kuelekea moja kwa moja hospitali alikolazwa John Mwaulaya.Je wana mahusiano naye au wanamuwinda? Lakini je wanamuwinda kwa kitu gani hasa? Kama Peniela ana mahusiano yoyote na Team SC41 basi she is a very very dangerous woman.Na kama kweli ni Team SC41 basi nina hakika kabisa kwamba hata Edson aliuawa na watu hawa na kama ni hivyo basi lazima kuna sababu kubwa na ya msingi iliyopelekea kufanyika kwa mauaji hayo kwani team SC41 huwa inashughulika na masuala mazito yenye maslahi na nchi ya Marekani tu.Tuna kazi kubwa ya kufanya mbele yetu.I can say this is a victory or death.We have to get prepared for a big war” akasema Mathew.Anitha na Noah walikuwa kimya kana kwamba wamemwagiwa maji.Anitha akamtazama Mathew na kuvuta pumzi ndefu akasema
“ I’m scared.Real scared but I have to fight”
“ Me too.Hii ni mara yangu ya kwanza kuisikia Team SC41 “ akasema Noah.
“ Ndugu zangu naomba nisiwafiche hata mimi ninaogopa sana nikiwafikiria Team SC41.Tukio la siku ile usiku halitaweza katu kufutika kichwani kwangu.These people have got no souls.They are monsters.Lakini pamoja na hofu hiyo tuliyonayo sote lazima tupambane nao.Najua ni jambo la hatari kubwa sana kwani unapogusa Team SC41 unagusa taifa lenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi duniani kwa hiyo hawako tayari siri zao zijulikane na kuvuruga uhusiano mzuri ilionao na nchi za afrika mashariki na ndiyo maana nikawaambia kwamba this is a victory or death..” Akasema Mathew.Noah akafuta jasho usoni na kusema
“ Mathew sisi tuko tayari kuingia katika mapambano na Team SC41 ,lakini kuna swali ninajiuliza .Je tunatafuta nini kwa Team SC41.Is this about revenge ?
“ Hata mimi nakubaliana na mawazo yako Noah.Lazima tunapoingia katika mapambano na hawa jamaa tufahamu tunapambana kwa ajili ya kitu gani.” akasema Anitha
Mathew akacheka kidogo na kusema
“ Mapambano haya si kwa ajili ya kulipiza . Msingi mkuu tunaoenda nao ni mauaji ya Edson.Tunatafuta nani alimuua na kwanini.Kadiri uchunguzi wetu unavyoendelea mambo mengi yanazidi kujitokeza likiwamo na hili la Team SC41 na mengine mengi ambayo yatajitokeza mbeleni,lakini naomba tusipoteze msingi mkuu wa kazi yetu yaani kuchunguza kifo cha Edson.Ndani ya mauaji ya edson kutaibuka mambo mengi mazito ndani yake.Kwa hiyo tutachunguza endapo kuna mahusiano yoyote kati ya Peniela na Team SC41,tutachunguza endapo Team SC41 walihusika katika mauaji ya Edson na kama walihusika basi tufahamu ni kwa nini.Endapo tutagundua kwamba Team SC41 walihusika katika mauaji ya Edson basi mapambano yetu na wao yataanzia hapo.” Akasema Mathew
“ Nimekuelewa Mathew lakini nina wazo moja, kwa nini basi tusianze kwanza kumchunguza Peniela na kufahamu uhusiano wake na Team SC41? Hii inaweza ikaturahishia kazi sana” Noah akauliza
“ Not yet Noah.Suala hili ni kubwa na tutalichimba hadi mzizi wake kwa hiyo suala la kumchunguza Peniela lina wakati wake.Kwa sasa tuelekeze nguvu katika suala la kesho.Tuna kazi ngumu sana kesho” akasema Mathew na majadiliano yakaendelea kuhusiana na kazi kubwa waliyokuwa nayo kesho.
*********************
Ni asubuhi nyingine tena,nchi ikiwa inaendelea na maombolezo kufuatiwa msiba mzto wa Dr Flora Johakim mke wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Bado hakukuwa na taarifa rasmi zilizotolewa kuhusiana na nini kilichosababisha kifo chake cha ghafla.Salamu za rambi rambi zilimiminika toka kila pembe ya dunia,watu mbali mbali wakimpa pole Dr Joshua rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Jaji Elibariki akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katika pilika pilika nyingi siku hii akastushwa na mlio wa simu .Akaitoa na kutazama mpigaji,alikuwa ni Peniela
“ Peniela !!...” akastuka kidogo.Hakuwa ametegemea kama angepigiwa simu na Penny
“Hallo Penny” akasema Jaji Elibariki baada ya kupokea simu ile
“ Jaji Pole sana kwa matatizo yaliyokupata.Nimestushwa sana na msiba wa mama mkwe wako” akasema Penny
“ Ahsante sana Penny.Ni mapenzi ya Mungu,yeye ndiye mwenye kutoa na kutwaa.Vipi unaendeleaje?
“ Ninaendelea vizuri Jaji Elibariki.” Akasema Penny
“ Nimekutafuta kwa siku kadhaa hukuwa ukipatikana kabisa.Nilipatwa na wasi wasi mkubwa kwamba pengine umepatwa na matatizo”
“ Naomba unisamehe sana Jaji Elibariki,nilipatwa na safari ya ghafla ikanilazimu kuondoka bila hata kuaga.”
“ Ok nashukuru kama umerudi salama.Siku nyingine usifanye hivyo.Unatupa wasi wasi sana sisi ambao tunajali usalama wako”
“ Ndiyo Jaji Elibariki.Siku nyingine sintofanya hivyo” akasema Penny halafu kikapita kimya kifupi
“ Jaji Elibariki samahani kwa kukusumbua mida hii lakini nimekupigia simu nina tatizo kidogo na ninahitaji msaada wako”
“ Una tatizo gani Penny?
“ Sintoweza kukueleza katika simu.Unaweza kupata muda sasa hivi tukaonana nikueleze?
“ Uko wapi mida hii? Akauliza Jaji Elibariki
“ kwa sasa niko nyumbani kwangu” akajibu Penny
Jaji Elibariki akafikiri kidogo na kusema
“ Ok ninapafahamu nyumbani kwako nitafika muda si mrefu.” Akasema Jaji Elibariki na kukata simu
“ Penny ana matatizo gani? akajiuliza jaji Elibariki akiwa bado amesimama katika maua
“ Yawezekana akawa na tatizo kubwa ngoja nikamuone” akawaza na bila kuaga mtu yeyote akaingia katika gari lake na kuondoka
“ Nina hakika lazima atakuwa na tatizo kubwa sana ambalo si rahisi kuelezeka simuni.Lazima nikamsikie ana tatizo gani kwani tayari nimekwisha jitolea kwa hali na mali kumsaidia ,kumlinda na kila anayetaka kumdhuru.Peniela tayari amekwisha niingia katika mishipa ya damu .Toka nilipokutana naye kwa chakula cha usiku,kichwa changu hakitulii,kila mara namfikiria yeye “ akawaza .
Penny alikuwa amejilaza kitandani wakati akiongea na jaji Elibariki
“ Mwili wote unaniuma kwa gwaride alilonichezesha Jason jana usiku.Dah ! Jason kweli ni kidume wa shoka.Mziki wake si mdogo.Anajua kuicheza ngoma na hachoki ana mapafu kama ya farasi.” Akawaza Penny halafu akainuka na kwenda kuchukua glasi ya maji ya matunda
“ Kwa kweli jana Jason amenikuna kiswa sawa na kunifikisha ninapopataka.Ni bahati mbaya sana kwamba siwezi kuwa na kijana huyu katika maisha yangu ingawa ninatamani sana kama angekuwa ni mume wangu nikaishi naye mpaka kifo kitutengenishe.Lakini haiwezekani kwa sababu tayari nimekwisha yaharibu maisha yangu na hayawezi kuwa sawa tena.Sintoweza kupata furaha kamwe..” akawaza Penny na kwenda sebuleni akajilaza sofani
Kengele ya getini ndiyo iliyomstua Penny toka katika kijiusingizi kilichoanza kumpitia.Akainuka na kwenda getini.Alikuwa ni Jaji Elibariki
“ Hallo jaji Elibariki.Karibu sana” akasema Penny na kumkaribisha ndani Elibariki kwa furaha
“ Karibu ndani Jaji Elibariki” Penny akamkaribisha sebuleni
“ Penny just call me Elibariki or Eli.Hayo mambo ya Jaji tuyaache mahakamani.” Akasema Jaji Elibariki na kumfanya Penny atabasamu
“ Ok Eli” akasema Penny huku akicheka kidogo
“ Eli unatumia kinywaji gani? akauliza Penny
“ Naomba mvinyo kidogo kama upo.” Akasema Jaji Elibariki.Penny akamtazama na kutabasamu akaenda na kuchukua chupa ya mvinyo akamminia Elibariki katika glasi
“ Pole sana Jaji Elibariki kwa matatizo yaliyowapata.Dr Flora alifariki kwa ugonjwa gani?
“ Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi iliyotolewa lakini kwa muda mrefu sasa Dr Flora alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na ninaamini hicho ndicho kilichomuua”
“ Pole sana Eli”
“ Nimekwisha poa Penny.Vipi wewe unaendeleaje ?
“ Ninaendelea vizuri sana Eli.Vipi wewe unaendeleaje?
“ Ninaendelea vizuri pia.Wasi wasi wangu ulikuwa ni juu ya usalama wako”
“ Nashukuru sana Eli kwa kunijali.” Akasema Penny na kimya kifupi kikapita
“ Nimestuka sana uliponiambia kwamba una tatizo nikaona nikimbie mara moja nije nikuone.Una tatizo gani Penny? Akauliza Jaji Elibariki
“ Eli nina tatizo ambalo nataka nikueleze lakini kwanza unaonekana umechoka sana.Unaonekana hukupata usingizi wa kutosha usiku.Hii ni hatari kwako Jaji Elibariki kuendesha gari katika hali hii.You need some rest” akasema penny
“ Ni kweli nimechoka Penny.Mambo yalikuwa mengi sana msibani.”
“ Ok Jaji Elibariki,naomba kwanza kabla ya kurejea msibani upate wakati wa kupumzika walau kidogo hapa kwangu .”
“Penny nikitoka hapa nitaelekea moja kwa moja nyumbani kupumzika.”
“ Hapana Elibariki.Huwezi kuendesha gari ukiwa katika hali hii ya uchovu. Utapumzika hapa na utakapoamka utakuwa tayari kuendelea na majukumu mengine.Naomba usiogope Jaji Elibariki.Hapa ni sehemu salama” akasema Penny.Jaji Elibariki hakujibu kitu akatabasamu
“ Kabla ya kupumzika,twende nikupeleke ukaoge kwanza ili uondoe uchovu.Ninayafahamu mambo ya msiba yanavyokuwa,hutapata hata wasaa wa kujimwagia maji”
“ Kweli kabisa Penny.Mambo ya msibani ni mengi mno” akasema jaji Elibariki.Penny akainuka na kumuongoza hadi chumbani kwake akamfungulia bafu ili Jaji Elibariki aweze kujimwagia maji.
“ Dah ! Kweli Penny anajua kuchunguza watu.Ni kweli nimechoka sana na ninahitaji mapumziko.Toka jana sijapata wasaa wa kupumzika.” Akawaza Jaji Elibariki huku akivua nguo akijiandaa kujimwagia maji
“ Penny anataka kunieleza nini? Ana tatizo gani? akajiuliza
“ Sikuwahi hata mara moja kuingia katika nyumba ya Penny.Ni kubwa na nzuri.Dah ! Penny ni mzuri jamani.Ukimuangalia tu hadi unapatwa na msisimko “ akawaza Jaji Elibariki na mara mlango wa bafuni ukafunguliwa.Jaji Elibariki alipatwa na mstuko wa mwaka.Hakuamini kile alichokuwa akikiona.Macho yalimtoka pima.
“ P…pe..Pee..” akataka kusema lakini maneno hayakutoka
Mlangoni alikuwa amesimama Peniela akiwa na tabasamu usoni huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………………………
Ngoma inogileSeason 1
SEHEMU YA 34
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Osmund alionekana kuwa na hofu kubwa sana.Kila alipojaribu kupiga simu kwa vijana wake waliokuwa katika mapambano na watu waliokuwa wamekwenda kumkomboa mke wa Dr Michael.Alimuhitaji sana Dr Michael kwa ajili ya kumfanyia upasuaji John Mwaulaya.Hali ya John iliendelea kuwa mbaya na alihitajika daktari kwa haraka na daktari pekee ambaye walimtegemea ni Dr Michael.Aliishika tena simu yake na kupiga
“ hallow bosi” ikasema sauti ya upande wa pili
“ Victor ni kitu gani kinaendelea huko? Kwa nini hampokei simu?
“ Bosi,hali huku ni mbaya sana.Wale jamaa ni hatari sana.Wamefanikiwa kumchukua Yule mwanamke na wameondoka.Watu wetu sita wameuawa lakini na sisi tumefanikiwa kumuua mmoja wao”
Osmund alihisi miguu ikimuisha nguvu akakaa juu ya msingi.
ENDELEA……………………
“ Whats happening to me? Nimeshika tu uongozi ndiyo mambo yote haya yanaanza kutokea.Ugonjwa wa John Mwaulaya,na hawa watu wanaoanza kutufuatilia” Akajiuliza Osmund akiwa amekaa juu ya jiwe.
“ Lakini watu hawa ni akina nani? Wanatafuta nini kwetu? Wametumwa na nani? Kwanini walikuwa wakimfuatilia John?.Wamefahamuje mahala alipokuwa amefichwa mke wa Dr Michael? Osmund akaendelea kujiuliza maswali mfululizo bila kupata jibu
“ Nina wasi wasi kuna watu kati yetu wanaotoa taarifa zetu.Si rahisi kwa mtu wa kawaida kufahamu mahala tulipokuwa tumemficha mke wa Dr Michael.Inabidi tufanye uchunguzi haraka sana ili tubaini kama kuna yeyote ambaye atakuwa akitoa habari zetu na kuwapa hawa jamaa .Nina hakika lazima kuna mtu ambaye anatoa habari zetu na ndiyo maana hawa jamaa wamekuwa wakifahamu kila tunachokifanya.Nitafanya uchunguzi na kama nikifanikiwa kumpata ninaapa nitatoa somo kwa wengine.” Akawaza Osmund halafu akakumbuka kwamba hakuwa ameikata simu akaiweka tena sikioni
“ Hallow Victor ! akaita
“ Hallow bosi,wale jamaa wameondoka na tunasubiri maelekezo yako”
“ Ondokeni sehemu hiyo haraka sana muda wowote polisi wanaweza wakafika.Hakikisheni hakuna mtu yeyote anayebaki hapo hapo.Hakikisheni miili ya watu wote inarejea hapa.Mtu wao aliyeuawa muacheni hapo hapo lakini kata kidole gumba chakulia ili tuweze kumfahamu ni nani.Chukueni pia simu yake na chochote mnaachoona kinaweza kutusaidia.Nawahitaji hapa haraka sana” akasema Osmund na kukata simu.
“ Ninaanza kuwa na wasiwasi sana na Peniela.Nyendo zake zinanitia shaka sana na nina mashaka labda yeye anaweza akawa ndiye anaye toa taarifa zetu kwa wale watu. Nyendo zake sizielewi kabisa.Siku hizi havai tena kile kifaa cha mawasiliano ambacho kinatuwezesha sisi kuwasiliana naye kwa urahisi kila wakati ambacho ni salama zaidi kuliko kutumia simu.Kuna kila sababu ya kuanza kumchunguza Peniela na kuzifahamu nyendo zake.Tunatakiwa kufahamu anafanya nini,anashirikiana na watu gani na tunaweza kugundua kitu.Nina hakika kabisa kwamba tukimchunguza Pennykuna kitu tutakigundua.Nimekuwa na mashaka naye sana” Akawaza Osmund wakati akipanda ngazi kwa kasi kuelekea chumbani kwa John Mwaulaya.Alifungua mlango na kumfuata John kitandani
“ John……John..”akaita.John mwaulaya akafumbua macho
“ Unajisikiaje hivi sasa?
‘ I’m weak, I’m very weak Ossy.” Akasema John Mwaulaya kwa sauti ndogo.Roho ikamuuma sana Osmund kumuonaJohn Mwaulaya akiwa katika hali ile.Akaenda kuegemea kabati
“ Nitafanya nini kuhusiana na John? Nitamtibu vipi? Hali yake inazidikuwa mbaya.Hapa hakuna namna zaidi ya kuwasiliana na makao makuu niwape taarifa hii kwamba tumeshindwa kumtibu John ili waweze kuona namna ya kumsaidia.Daktari tuliyekuwa tukimtegemea ni Dr Michael pekee lakini naye kwa hivi sasa hatutaweza kumpata tena” Osmund akatoka nje akaingia katika chumba kimoja kilichokuwa na kompyuta kadhaa akawakuta vijana wawili.
“ Stanley wataarifu watu wote tukutane hapo chini haraka sana.Kuna jambo zito la kuwafahamisha” akasema Osmund na kutoka akaelekea chini mahala alikoelekeza wakutane
“ Kwa mara ya kwanza ninahisi mambo kutaka kunishinda.I don’t know what I’m going to do.” Akawaza wakati akishuka ngazi.Mara tu baada ya kupata mwito ule toka kwa Stanley watu wote waliokuwepo pale katika nyumba ya John wakakusanyika chini.
“ Ndugu zangu,nimewaita hapa kwa dharura kuna mambo makubwa matatu ambayo nataka kuwaeleza.Jambo la kwanza ni kuhusiana na afya ya mkuu wetu.Kama sote tunavyofahamu kiongozi wetu anaumwa sana na hali yake inazidi kuwa mbaya.Jitihada za kumfanyia upasuaji ili kuokoa maisha yake zinaonekana kugonga mwamba kwani daktari tuliyekuwa tukimtegemea kwa ajili ya upasuaji huo hatutaweza kumpata tena.Kwa sasa ninajaribu kuwasiliana na makao makuu ili tuone namna tunavyoweza kuokoa maisha ya John.Nimeona niwaeleze kuhusu hili kwa sababu kwa hatua aliyofikia hivi sasa anything can happen so we have to be prepared.” Akanyamaza akameza mate na kuendelea
“ Jambo la pili ninalotaka kuwaeleza ni kwamba kuna watu wanatufuatilia.Bado sijafahamu wana tafuta nini kwetu lakini watu hawa wanaonekana ni watu hatari na wanafahamu kila tunachokifanya.Inaonekana kati yetu kuna mtu anayetoa taarifa zetu kwa hawa jamaa.Ninatoa onyo kwamba kwa yeyote atakayebainika kufanya jambo kama hilo adhabu yake ni kali sana.Kila mmoja wakati akijiunga na Team SC41 aliapa kwamba hatatoa siri za aina yoyote lakini inaonekana kuna mtu au watu waliokiuka kiapo chao na kuanza kutoa siri.Uchunguzi mkali unaendelea ili kwanza kuwafahamu wale watu wanaotufuatilia ni akina nani na vile vile kumfahamu mtu anayetoa taarifa zetu kwa wale jamaa.” Akanyamaza tena akawaangalia watu wake na kuendelea
“ Jambo la tatu ninalotaka kuwaeleza ni kwamba usiku huu yametokea makabiliano kati ya watu wetu na hawa jamaa niliwaeleza kwamba wanatufuatilia na katika mapambano hayo tumewapoteza vijana wetu sita na tumefanikiwa kumuua mmoja wao.Hili ni pigo kubwa kuwahi kutokea katika team SC41 .Ninaahidi kwamba tutawasaka watu hawa na kuwapata wote .Usiku huu tutawazika watu wetu ili kesho tuamkie jambo moja tu.Kuwasaka wavamizi hawa.Miili italetwa hapa na tuatwaaga wenzetu na usiku huu tutawazika” akasema Osmund. Halafu akareja katika chumba walichokuwamo wale vijana wawili na kumuita Stanley nje
“ Stanley wewe ni kijana ambaye ninakuamini sana na sina shaka nawe hata kidogo.Kuna kazi ambayo ninahitaji unisaidie kuifanya.”
“kazi gani mkuu? akauliza Stanley
“ Nadhani umefuatilia niliichokuwa nawaeleza wenzako kule chini.Kuna watu wanatufuatilia na wanapata taarifa zetu.Hili ni jambo hatari sana kwetu na kwa serikali ya Marekani na Tanzania kwa maana hiyo basi ninataka ufanye kazi moja ya muhimu sana.Ninataka umchunguze mtu mmoja mmoja katika Team SC41 ,angalia mawasiliano yao katika siku hii ya leo hii ili tuone kama kuna yeyote anayetoa taarifa zetu kwa watu hawa.Jambo hili sitaki mtu mwingine yeyote alifahamu.This is between us .Can you do that for me? Akauliza Osmund
“ Ndiyo ninaweza kufanya hivyo ingawa inaweza kuchukua muda kidogo lakini nitafanya hivyo.Lakini ninaweza kufanya hivyo kwa kutumia vifaa vilivyopo kule makao makuu .”
“ Ok Stanley go, do it”akasema Osmund na kurejea tena katika chumba cha John mwaulaya.Akamfuata palekitandani
“John…”akaita na John akafumbua macho
“ John,nasikitika upasuaji wako hautaweza kufanyika.Daktari tuliyemtegemea hatutaweza kumpata tena.kwa hivi sasa ninawasiliana na makao yetu makuu ili kuona uwezekano wa kukuhamisha na kukupeleka nje ya nchi kwa matibabu ”akasema Osmund kwa masikitiko.John akamfanyia ishara kwamba akipandishe kitanda.Osmund akabonyeza kitufe ukutani na kitanda kikainuka upande wa juu,na kumuwezesha John kukaa
“ Osmund,listen to me my boy.Tafadhali usiwasiliane na makao makuu.Muda wangu umefika and please dont do anything. Its my time to go on rest now”akasema John
“ No John! Don’t give up.Tunafanya kila linalowezekana ili uweze kupona.Ninakwenda kuongea na makao yetu makuu ili tuone uwezekano wa kupata ndege na ukakimbizwa mara moja Marekani kwa matibabu”
“ Osmund tafadhali usisumbuke kijana wangu.You have done enough.Stop wasting your time.”
‘ John ninakuomba usikate tamaa.Tutakushughulikia na utapona”
John akamtazama Osmund na kumwambia
“ Ossy tafadhali naomba uniache mwenyewe.I need to be alone now”akasema John.Osmund akamtazama halafu akatoka kwa kasi .John Mwaulaya akafumba macho na kuendelea kukumbuka
Mambo yaliyotokea usiku ule .Picha ya mtoto mdogo akiwa amelala katika kiti cha nyuma ya gari ikamjia na kwa mbali akatabasamu
“ She was so cute.I didn’t even know her name that night.” akasema kwa sauti ndogo
27 April 1986
Bado mvua kubwa iliendelea kunyesha.John alikuwa amembeba yule mtoto mdogo ambaye tayari alikuwa amelala.
“ You’ll be safe little angel.You’ll be fine.I’ll do everything I can to make sure that you are safe” akawaza John
“ Bosi tunaelekea wapi? Akauliza mmoja wa vijana wake.John hakujibu kitu akachukua simu yake na kuzitafuta namba fulani za simu akapiga.
“ Hallow Martha.” Akasema John baada ya simu yake kupokelewa
“Hallow John” ikasema sauti ya mwanadada aliyeonekana kujawa na usingizi.
“ Samahni nimekuamsha usiku huu”akasema John
“ Bila samahani John.Una tatizo gani?
“ I need to see you”
“ Now? Akauliza Martha
“ yes.Now” akajibu
“ Uko wapi mida hii?
“ Niko barabarani katika hii njia inayoelekea Mkuse Lodge”
“ Ok,naomba unisubiri pale Eusebio night club, nitafika pale muda si mrefu” akasema Martha na kukata simu.John akamuelekeza dereva aliyekuwa akiendesha gari lile mahala walikokuwa wakielekea.Walifika Eusebio Night club na kuegesha gari,bado mvua kubwa iliendelea kunyesha.Baada ya dakika kama kumi na tano hivi ikatokea gari moja ndogo .John akaitambua gari ile.Akachukua koti la mvua na kumfunika yule mtoto akashuka na kuwaamuru vijana wake waendelee na safari ,yeye akaenda hadi katika lile gari ,akafunguliwa mlango na kuingia
“ John..whats going on? akauliza Martha .John hakujibu kitu akalitoa lile koti la mvua na kumstua Martha baada ya kukiona kitoto kidogo.
‘John !!..akasema Martha kwa mshangao
“ What are you doing with this baby? Akauliza
“ Usiulize maswali mengi sana Martha.Mtoto huyu anahitaji sehemu salama na ya siri.Nahitaji msaada wako katika hili” akasema John.Martha akamtazama yule mtoto mdogo akamshika usoni halafu akawasha gari
“ Mama yangu mdogo rafiki yake anayemiliki kituo cha kulelea watoto yatima.Ngoja niwasiliane naye anipe namba zake za simu nimpigie.” Akasema Martha na kusimamisha gari pembeni ya barabara akachukua simu yake na kumpigia mama yake mdogo wakaongea kwa dakika kama tatu akampatia namba za huyo rafiki yake mwenye kituo cha kulelea yatima.Baada ya kuongea na mama yake mdogo,Martha akampigia simu yule mama mwenye kituo cha kulelea watoto yatima akamtaarifu kwamba anahitaji kuongea naye.Ilikuwa ngumu kidogo kwa mama yule kukubali ombi la Martha hadi alipomtajia jina kwamba ameelekezwa na mama yake mdogo ndipo alipokubali kwani ni rafiki yake mkubwa.Alimuelekeza mahala aliko na bila kupoteza wakati wakachoma mafuta kuelekea huko.
Bi Bernadetha Usuwo mmiliki wa kituo kile cha kulelea watoto yatima akawapokea na kutaka kufahamu shida iliyowapeleka kwake usiku ule.John akamdanganya kwamba mtoto yule aliyekuwa amemshika amezaa na mwanamke mmoja ambaye amekuwa ni mlevi na anakesha katika kumbi za usiku akifanya biashara za kujiuza.Aliendelea kudanganya kwamba alipigiwa simu na majirani wa mwanamke huyo ambao walimtaka aokoe maisha ya mwanae kwa kwenda kumchukua na ndipo alipoamua kwenda kumchukua mwanae na kumleta pale ili aweze kupatiwa uangalizi makini.
“ Ouh Jamani kwa nini wasichana wa siku hizi wamekuwa hivi? Unawezaje kumfanyia mambo kama hayo malaika kama huyu? Mtoto huyu bado mdogo tayari anaanza kuruka ruka katika starehe ! Mwanamke mwenye vitendo kama hivyo hafai kabisa kuachiwa mtoto amlee.Umefanya jambo la maana sana kumchukua mwanao.Hapa atalelewa na kupata malezi anayostahili” akasema Bi Bernadetha
“ Ninashukuru sana mama kwa msaada wako huu mkubwa.Pamoja na hayo kuna jambo lingine ambalo ninataka unisaidie”akasema John
“ Jambo gani hilo?
“ Nataka mtoto huyu alelewe kwa siri.Sitaki watu wafahamu kwamba ni mwanangu na wala sitaki mtoto huyu anijue mimi kama baba yake na wala asifahamu kama ana mama.Nitakulipa fedha nyingi kama utanisaidia katika hilo.”
“ kwa nini unataka iwe hivyo John?
“ Ni kwa ajili ya usalama wa mtoto.Yeyote atakayekuuliza kuhusiana na mtoto huyu sema kwamba aliletwa kutokea huko Singida au sehemu nyingine yeyote mbali kabisa na Dar es salaam.Tafadhali mama nakuomba sana unisaidie katika hilo” akaomba John
“ Hii ni ajabu sana.Kwa nini mtoto asifahamu kuhusu wazazi wake ni akina nani?
“ Mama Bernadetha ni vigumu kukuelewesha kwa sasa lakini naomba unisaidie sana katika hilo.Mimi nitagharamia gharama zote za matunzo na malezi yake na atapata kila kitu kinachotakiwa isipokuwa tu hataniona.Nitakuwa karibu nawe ili kuhakikisha anakua katika malezi mazuri na ninakuahidi ataishi maisha ya raha mustarehe kuliko hata mtoto wa rais lakini kitu kimoja tu atakikosa ambacho ni wazazi.” akasema John..Bi Benrnadetha alijaribu kufikiri kuhusu suala lile lakini kiasi kikubwa cha pesa alichoahidiwa na John kikamfanya akubali kufanya vile anavyotaka John
“ Jina lake nani huyu malkia? Akauliza Bi Bernadetha.John na Martha wakaangaliana.Hakuna aliyekuwa akilfahamu jina la yule mtoto.Mara John akajikuta akitamka
“ Peniela.Her name is Peniela”akatamka John.
********
“ Ahsante Mungu kwa kuturejesha nyumbani salama” akasema Dr Michael baada ya kuwasili nyumbani kwa Mathew.Gari lilisimama lakini hakuna aliyetaka kushuka.Wote walionekana kuwa katika hali ya kutoamini kama ni kweli wamerejea salama.Anitha ambaye naye alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kupoteza mawasiliano na akina Mathew ilipoanza kusikika milio ya risasi mfululizo alikuwa amesimama katika kibaraza akiwa na Jaji Elibariki.Wote walishangazwa kuona sekunde zinasonga mbele na hakuna mtu yeyote aliyeshuka mle garini.Kwa wasi wasi mwingi wakalisogelea lile gari .Ilikuwa vigumu kujua nani alikuwamo ndani kutokana na vioo vyeusi vya gari lile.Jaji Elibariki akagonga katika kioo cha mbele upande wa dereva.Taratibu mlango ukafunguliwa akashuka Mathew akiwa ameloa damu.
“ Ouh my God ! Mathew..”akasema Jaji Elibariki.Anitha alistuka sana akamfuata Mathew
“ Pole sana Mathew. ?akauliza Anitha huku machozi yakimlenga.Mathew alitaka kuongea kitu lakini alihisimaumivu makali. Mlango mwingine ukafunguliwa akashuka Noah naye akiwa katika hali kama aliyokuwa nayo Mathew.Alikuwa amechafuka kwa damu.
“Ouh Mungu wangu ! Noah..” akasema Anitha na kwenda kumkumbatia na kumsaidia kusimama vizuri kwani alionekana kushindwa kusimama.Jaji Elibariki akafika mara moja na kumtegemeza akampeleka ndani.Katika mlango wa kati kati akashuka Dr Michael akifuatiwa na mke wake.
“ Dr Michael !! akasema Anitha na kumkumbatia kwa nguvu
“ Ahsante Anitha.Ahsante sana kwa kila kitu.Umetuokoa ” akasema Dr Michael.Mke wa Dr Michael bado aliendelea kumwaga machozi.Mume wake akamkumbatia na kumtuliza akimuhakikishia kwamba anyamaze kulia kwani tayari alikuwa huru.
Mathew alikuwa ameegemea gari lililokuwa na matundu mengi ya risasi.Anitha akamsogelea
“ Pole sana Mathew.Nashindwa kuelezea wasi wasi niliokuwa nao baada ya kuanza kusikia milio ya risasi na ghafla mkapotea.Sijawahi kuogopa kama leo hii.” Akasema halafu akanyamaza kidogo na kuuliza.
“ Where is A…….” kabla hajamaliza kusema alichotaka kukisema Mathew akamkatisha
“ We lost him….”
Anitha akainama.
Dr Michael akamfuata Anitha na kumuomba ampeleke mke wake ndani halafu akamfuata Mathew
“Mathew ,nina mambo mengi ambayo ninataka kuyasema kwako na timu yako lakini kwa sasa nataka niseme maneno mawili tu ahsante sana.Uliniahidi kunirejeshea mke wangu na umefanya hivyo.Mmepambana kufa na kupona ,mmetukinga kwa risasi mimi na mke wangu na mkajeruhiwa kwa risasi ambazo zilipaswa kutupata sisi na mmeturejesha salama.Ninyi ni mashujaa ambao nchi ya Tanzania imejaaliwa kuwapata.Nchi hii inapaswa kujivunia watu kama ninyi.Papo hapo nawapa pole sana kwa kumpoteza Dr Adolf.Naomba nikiri nimekuwa nikiyatazama matukio kama yale katika filamu na leo nimeshuhudia kwa macho yangu namna watu wanavyobadilishana risasi.Nimeogopa sana.Picha ile haitaweza kamwe kufutika kichwani kwangu.” Akasema Dr Michael huku michirizi ya machozi ikionekana mashavuni pake.
“ Dr Michael ahsante nawe pia kwa ushirikiano wako.Sote tumepambana mpaka tukatoka salama.Katika mapigano kama yale mtu mmoja au timu nzima kufa ni kitu cha kawaida sana” akasema Mathew
“ Mathew jeraha linatoa damu nyingi,tafadhali naomba tuingie ndani ili niweze kuwatibu majeraha haya”akasema Dr Michael halafu Jaji Elibariki akamshika mkono Mathew na kumsaidia kutembea kuelekea ndani.
Ndani ya jumba hili la Mathew kulikuwa na chumba maalum cha matibabu.Aliifahamu vyema kazi yake kwamba imezungukwa na hatari muda wote hivyo akatenga chumba maalum kwa ajili ya matibabu pale anapokuwa ameumia.
“ Mathew umejiandaa sana.Hapa una kila kitu kinachohitajika.Hii ni kama hospitali ndogo”akasema Dr Michael wakati akiviweka sawa vifaa kwa ajili ya kumtibu Mathew aliyepigwa risasi mkono wa kushoto.Mathew akalala kitandani na Dr Michael akaanza kumuhudumia akianzia na jeraha la risasi katika mkono wa kushoto.
“ Una bahati sana Mathew.Risasi ile haikupiga mfupa.Imepita pembeni kidogo.Ingepiga mfupa ingekuwa ni hatari zaidi”akasemaDr Michael wakati akiendelea kulitibu jeraha la Mathew.Baada ya kumaliza kulitibu jeraha la Mathew akaendelea pia kumtibu Noah ambaye alikuwa amepigwa risasi ya paja.Wakati Dr Michael akiendelea kumtibu Noah,Mathew alikuwa sebuleni na Anitha na jaji Elibariki ambao walitaka kufahamu kila kitu kilichotokea katika kumkomboa mke wa Dr Michael.
“ Sikuwa nimetegemea kama mapambano yale yangekuwa makubwa kiasi kile.” Akasema Mathew
“ Maelekezo uliyokuwa ukitupatia yalitufikisha katika kanisa lililokuwa likiendelea kujengwa.Tuliwakuta watu wanne waliokuwa wakimlinda mke wa Dr Michael ambao tulipambana nao na kuwamaliza wote na tukafanikiwa kumuokoa mateka.Ghafla wakati tukijiandaa kuondoka,ziliwasili gari tatu na tukajikuta tumezingirwa.Hapo mapambano yakaibuka upya.Inavyoonekana kuna wenzao waliwapa taarifa kwamba tumevamia na ndiyo maana wakaja kwa kasi namna ile.Mapambano ya kujiokoa yalikuwa makali sana .Watu wale walikuja wakiwa wamejipanga vizuri sana wakiwa na silaha kali.“ akasema Mathew
“ Nakumbuka mara ya mwisho ulinitaarifu kwamba tayari mateka mko naye na mnajiandaa kurudi lakini ghafla nikasikia milio ya risasi nadhani ni hapo ndipo wale jamaa walipowazingira.Mawasiliano yalikata ghafla na sikuweza kuwapata tena.”akasema Anitha
“ Eneo lote lilikuwa giza kwa hiyo yalikuwa ni mapambano makali sana.Wale jamaa walikuwa na kifaa kilichokuwa kikifuatilia masafa tuliyokuwa tukitumia kwa hiyo ilikuwa rahisi kwao kuweza kufahamu mahala tulipokuwa tumejificha na hivyo kutuelekezea mashambulizi hivyo tukalazimika kuvitupa.” Akasema Mathew.
“ Tulipambana sana na tukafanikiwa kupata upenyo wa kukimbia. Wakati tukiingia katika gari kuna mtu mmoja alivurumisha risasi ambazo zilitakiwa kumpata Dr Michael lakini anali Adolf akalazimika kumkinga na risasi zile zikampata na kumuua pale pale.Tulishindwa namna ya kuondoka naye kwa namna risasi zilivyokuwa zikivurumishwa kwetu.” Akasema Mathew
“ Watu hawa ni akina nani?akauliza jaji Elibariki kwa uoga
“ Team SC41 “ akasema Mathew
“ Team SC41? Elibariki akauliza kwa mshangao
“ Ni nani haoTeam SC41? akauliza Elibariki
“ Ni habari ndefu sana nitakueleza baadae kwa sasa bado kuna kazi ya muhimu sana ambayo tunatakiwa kuikamilisha.” Akasema Mathew na kuinuka akamfuata Dr Michael ambaye alikuwa akimalizia kumtibu Noah Jeraha la risasi katika paja lake.
“ Dr Michael tayari nimeitimiza ahadi yako na sasa ni zamu yako kumalizia ile kazi yetu” akasema Mathew.Dr Michael akamgeukia na kumtazama akatabasamu
“ Mathew nilidhani utahitaji muda zaidi wa kupumzika baada ya tuko lile la usiku wa leo na isitoshe jeraha lako lilikuwa linavuja damu nyingi .”akasema Dr Michael
“ Dr Michael,sisi tuko vitani na tunapokuwa vitani tunapambana hadi dakika ya mwisho bila kuchoka,we fight like devils.We never give up.Majeraha ni kitu cha kawaida katika mapambano kama haya kwa hiyo usitishike na jeraha kama hili.Kazi ile lazima imalizike usiku wa leo.”akasema Mathew.Dr Michael akamfunga Noah bandeji halafu akamchoma sindano halafu akamuomba Mathew wasaidiane kumpeleka chumbani kupumzika.Noah aliachwa chumbani akipumzika ,Mathew na Dr Michael wakaelekea sebuleni.
“ Dr Michael kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa wale jamaa wataendelea kukufuatilia kwa karibu sana.Sikushauri uchunguzi wa zile sampuli ukaufanyie pale hospitalini kwako.Hakuna sehemu ambako tunaweza kwenda usiku huu ukafanya uchunguzi huo? Tunahitaji majibu kabla ya jua kuchomoza “ Akasema Mathew.Dr Michael akafikiri kidogo na kusema
“Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Dr Robert yeye anamiliki hospitali yake binafsi.Ana maabara kubwa pale na ninaweza kwenda na kuzifanyia uchunguzi sampuli zile tulizonazo”
“ Vizuri sana Dr Michael.Anitha msaidie Dr Michael awasiliane na rafiki yake kwani simu yake haitakiwi kutumika.Team SC 41 lazima watakuwa wakifuatilia ili wafahamu mahala alipo.” akasemaMathew na kuelekea chumbani kwake.Akaegemea kabati lake kubwa na kuyafuta machozi.Picha ya Kanali adolf akimiminiwa risasi ilimjia akilini na kumuumiza sana.
“I’m so sorry Adolf.Umekufa kishujaa “ akasema Mathew halafu akachukua baadhi ya vifaa vyake na kuwafuata akina Anitha
“ Mathew tayari nimekwisha wasiliana na Dr Robert na ameniambia hakuna tatizo naweza kwenda kuitumia maabara ya hospitali yake.” Akasema Dr Michael.
“ Ok Good.Elibariki wewe utabaki hapa pamoja na Noah na familia ya Dr Michael.Sisi tunaenda kuzifanyia uchunguzi sampuli tulizochukua ili kubaini chanzo cha kifo cha Dr Flora.Tutakaporejea tutakuwa tayari na jibu lenye uhakika nini kilimuua” akasema Mathew na kumfuata Noah.
“Noah endelea kupumzika ,tunakwenda kutafuta majibu ya zile sampuli.Elibariki na familia ya Dr Michael watabaki hapa.Protect them.Anitha tunaondoka naye yeye ndiye atakayetuendesha kwani mkono wangu bado una maumivu makali sana.” akasema Mathew kisha akaongozana na Dr Michael,na Anitha wakaingia garini wakaondoka
“ Nilifahamu toka mapema team SC41 ni watu hatari sana.Kwa mara nyingine tena leo hii nimenusurika toka katika mikono yao.Nitapambana nao.safari hii sintaogopa wala kukata tamaa lazima nihakikishe nimepambana nao na kulipa kisasi cha familia yangu na wenzangu walioteketezwa kikatili.Tukio la leo ni salamu kwao kwamba watu wanaopambana nao kwa sasa si wa kawaida.” Akawaza Mathew wakiwa garini
“ kwa sasa tunahamia kwa Peniela.Kwa sasa inabidi tuanze kumchunguza Peniela.Katika hili itabidi kuwatumia akina Elibariki.Tunatakiwa kuzifuatilia nyendo zake.Siku ile wale watu wa Team SC41 walitokea kwake ndipo wakaelekea hospitali kwa John Mwaulaya.Ninashawishika kuamini kwamba yawezekana kabisa Peniela akawa na mahusiano naTeam SC41.Endapo tutagundua kwamba Penny ana mahusiano na Team SC41 basi nitawaunganisha katika kifo cha Edson.Baada ya hapo tutaanza kuitafuta sababu ya kumuua.Kama ni kweli TeamSC41 walihusika katika mauaji ya Edson it’ll be for something big.very big”akawaza Mathew
TEAM SC41 WANAPATA PIGO LAKWANZA LA KUULIWA KWA VIJANA WAO .WATACHUKUA HATUA GANI? JOHN MWAULAYA NAYE ANAENDELEA KUIKUMBUKA HISTORIA YA PENIELA TOKA UTOTO WAKE HADI HIVI LEO,NI MAMBO GANI YAMO KATIKA HISTORIA YA PENIELA? TUKUTANE TENA KATIKA SEHEMU IJAYO………
HtrSEHEMU YA 35
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Nilifahamu toka mapema team SC41 ni watu hatari sana.Kwa mara nyingine tena leo hii nimenusurika toka katika mikono yao.Nitapambana nao.safari hii sintaogopa wala kukata tamaa lazima nihakikishe nimepambana nao na kulipa kisasi cha familia yangu na wenzangu walioteketezwa kikatili.Tukio la leo ni salamu kwao kwamba watu wanaopambana nao kwa sasa si wa kawaida.” Akawaza Mathew wakiwa garini
“ kwa sasa tunahamia kwa Peniela.Kwa sasa inabidi tuanze kumchunguza Peniela.Katika hili itabidi kuwatumia akina Elibariki.Tunatakiwa kuzifuatilia nyendo zake.Siku ile wale watu wa Team SC41 walitokea kwake ndipo wakaelekea hospitali kwa John Mwaulaya.Ninashawishika kuamini kwamba yawezekana kabisa Peniela akawa na mahusiano naTeam SC41.Endapo tutagundua kwamba Penny ana mahusiano na Team SC41 basi nitawaunganisha katika kifo cha Edson.Baada ya hapo tutaanza kuitafuta sababu ya kumuua.Kama ni kweli TeamSC41 walihusika katika mauaji ya Edson it’ll be for something big.very big”akawaza Mathew
ENDELEA……………………
Waliwasili katika hospitali inayomilikiwa na Dr Robert.Kwa kutumia simu ya Mathew Dr Michael akamfahamisha Dr Robert kwamba tayari wamekwishafika ,akawafuata katika maegesho halafu akawachukua na kuwaongoza hadi ndani ya hospitali.Mathew na Anitha wakaombwa wakae katika viti vilivyokuwa katika sehemu ya kupumzikia wakati Dr Michael na mwenzake wakiendelea kuzifanyia uchunguzi sampuli toka kwa mwili wa Dr Flora .Kabla hawajaanza kazi Dr Robert akamuuliza Dr Michael
“ Michael,kuna tatizo gani? Kwa nini jambo hili lifanyike usiku na haliwezi kusubiri hadi kesho? Akauliza Dr Robert
“ Dr Robert kuna sampuli ninazotakiwa kuzichunguza usiku huu na siwezi kusubiri hadi kesho.” Akasema Dr Michael.Robert akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akauliza
“ Niambie Michael, nini kimetokea? Macho yako yanaonyesha kabisa kwamba kuna tatizo Fulani.Na hawa watu ulioongozana nao ni akina nani?
“ Robert wewe ni rafiki yangu mkubwa na siwezi kukuficha kitu lakini naomba nitakachokueleza kiwe ni kati yetu wawili.”
“ Niambie Michael kitu gani kimetokea?
“ Mke wangu alitekwa nyara na watu wasiojulikana ambao walitaka kunilazimisha nimfanyie upasuaji mgonjwa wao waliyemtorosha toka hospitali.Vijana hao nilioongozana nao ndio waliopambana hadi wakafanikiwa kumuokoa mke wangu toka katika mikono ya watekaji.Mwenzao mmoja alifariki dunia katika mapambano hayo kwa hiyo unapowaona hapo wako katika majonzi makubwa lakini bado hawakati tamaa wanaendelea na mapambano.Kuhusu kilichonileta hapa usiku huu ni kwamba mke wa rais alifariki ghafla na mpaka sasa sababu ya kifo chake haijajulikana na imetolewa amri ya kutochunguza chanzo cha kifo chake.Vijana hawa wanataka kuufahamu ukweli wa kilekilichomuua mke wa rais .Tulifika katika hospitali ulikohifadhiwa mwili wa mke wa rais kwa dhumuni la kuufanyia uchunguzi kwa siri lakini wakati tukiendelea na kazi hiyo wakapokea taarifa kwamba tumegundulika tunaufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora.Ilitulazimu kuacha kila tulichokuwa tunakifanya na kukimbia.Kabla ya kutoka nilichukua sampuli kadhaa kwa ajili ya kuendelea kuzifanyia uchunguzi.Kwa hiyo niko hapa na wale vijana ili kuufahamu ukweli wa nini kilimuua mke wa rais” akasema Dr Michael.
“ Michael umejiingiza katika matatizo makubwa na vyombo vya dola.Kwa nini ulikubali kufanya kitu cha hatari kama hiki? Unafikiri ikijulikana kwamba ulishiriki katika jambo kama hili utakuwa salama? Akauliza Dr Robert
“ Robert nililazimika kukubali kufanya hivi kwa sababu waliahidi kunisaidia kumpata mke wangu na wamefanya hivyo kwa hiyo na mimi nalazimika kutimiza ahadi yangu.Lazima niwasaidie kufahamu chanzo cha kifo cha mke wa rais.Kuhusu usalama wangu usijali kuhusu hilo tayari nina mpango mzuri baada ya kumaliza kazi hii” akasema Michael.Robert akamtazama kwa muda kidogo na kusema
“ Sawa Michael mimi nitakusaidia kufanya uchunguzi huo lakini tafadhali kuwa makini sana,na sitaki ijulikane kwamba hospitali yangu imehusika kwa namna yoyote ile na jambo hili.Je unaweza ukanihakikishia hilo?akauliza Robert
“Ndiyo Robert.Nakuhakikishia kuhusu hilo”akasema Michael.Robert akavaa koti tayari kwa kuanza kazi
“ Katika uchunguzi mliokwisha ufanya mligundua chochote?
“ Tuligundua kwamba mishipa ya damu ilipasuka ishara kwamba kulikuwa na mgandamizo mkubwa wa damu,tunachotaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha hali hiyo kutokea?.Hapa nina sampuli kadhaa ambazo tunatakiwa tuzifanyie uchunguzi na tutapata jibu.”akasema Dr Michael na mara moja shughuli ya uchunguzi ikaanza.
“ Mathew whats next? Akauliza Anitha wakiwa katika sehemu ya kupumzikia.
“ Baada ya kupata majibu ya nini kilimuua Dr Flora ,tutaendelea na kazi yetu ya msingi yaani kuchunguza kuhusu kifo cha Edson.Kazi hii ya kuchunguza kiini cha kifo cha Dr Flora imeingia tu kwa dharura na haikuwa katika mpangilio wetu wa kazi.Kuanzia kesho tutaelekeza nguvu katika kuchunguza kama Team SC41 walihusika katika kifo cha Edson.Tutaupata ukweli wa jambo hilo kwa kumchuguza Peniela.Tukifahamu mahusano yake na Team SC41 basi itatuwia rahisi sisi kufahamu kama walihusika katika mauaji ya Edson na kwa nini.” Akasema Mathew
“ Kuna zile kamera mbili ulizozitega nyumbani kwa penny zinaweza kutusaidia sana kufahamu nyendo zake”akasema Anitha
“Kweli Anitha.Kamera zile zitatusaidia sana kufahamu kila kinachoendelea nyumbani kwa Penny lakini hata hivyo tutawatumia rafiki zake wa karibu,Jason na Elibariki katika kupata taarifa tunazozihitaji”akasema Mathew
*******
Miili ya vijana sita waliouawa katika mapambano na akina Mathew ikawasili katika makazi ya John Mwaulaya ambako vijana wote walikuwa wamekusanyika.Gari lile ilimokuwamo ile miili ilikuwa imechafuka kwa damu.Osmund alitaarifiwa kuwasili kwa miili ile akashuka kwa kasi na kwenda kushuhudia.Alipandwa na hasira zilizochangayika na mstuko baada ya kuzishuhudia maiti zile namna zilivyochakazwa kwa risasi.
“ Whoever did this must be in our hands by sunset tomorrow “akawaza .
“ Lakini ni nani huyu ambaye anaweza kuwa amefanya kitu kama hiki? Nani huyu ambaye anathubutu kucheza na team SC41 na kuua vijana wetu sita? Hii haijawahi kutokea kuanzia kuanzishwa kwake.Lazima tuwatafute watu hawa na tuwafahamu ni akina nani.” Akaendelea kuwaza Osmund akiwa amesimama kandoni mwa gari lililobeba miili.Mara akastuliwa na sauti ya Victor
“ Bosi, kile kidole ulichoniambia nikichukue hiki hapa.”akasema Victor na kumkabidhi kidole gumba cha mkono wa kulia ambacho kilikuwa ndani ya kifuko kidogo cha nailoni
“ Poleni sana Victor” akasema Osmund
“ Ahsante sana bosi.Yalikuwa ni mapambano makali .Ilikuwa ni kama vita” akasemaVictor
“ Watu hawa ni akina nani?
“ Ni vigumu kusema ni akina nani lakini ninaweza kusema kwamba watu wale ni wapiganaji hasa wenye ujuzi na uzoefu wa hali ya juu.Wanatumia vifaa vya hali ya juu vya mawasiliano.They are professionals.Hata yule mwenzao tuliyemuua alikufa wakata kiwakinga wenzake wasishambuliwe na risasi ” akasema Victor
“ Tukimfahamu huyu mwenzao ni nani basi tutaweza kuwafahamu watu hao ni akina nani”akasema Osmund
“ Kitu kingine,nimeahirisha mazishi ya vijana wetu niliyokuwa nimepanga tuyafanye usiku wa leo.Vijana wetu wamekufa kishujaa na tutawazika kwa heshima zote.Kuanzia kesho tutaanza kuwazika mmoja mmoja katika makaburi tofauti tofauti.Kesho asubuhi shughulikia suala hilo.Kila kitu kuhusu jambo hilo ninakuachia wewe,hakikisha mpaka kesho saa tatu asubuhi kila kitu kuhusiana na maziko ya vijana wetu kiwe kimekamilika na kuanzia saa tano tuanze kuwazika mmoja mmoja”akasema Osmund
“ Sawa bosi ninalishughulikia suala hilo.” Akasema Victor na mara simu ya Osmund ikaita akaipokea na kuiweka sikioni
“ Hallow Joseph” akasema
“ Bosi ,Edwin Mackson yupo katika laini anakusubiri”akasema Joseph
“ Ok Joseph ninakuja sasa hivi”akajibu Osmund na kukata simu
“ Victor tutaendelea na maongezi baadae lakini kwa sasa hakikisha kila aliyeumia anapatiwa matibabu na wanapewa mapumziko katika zahanati yetu kule makao makuu. Hakikisha kila kitu kimekwenda sawa,nina mambo mengi ya kufanya siku ya leo”akasema Osmund na kuondoka kwa kasi kuelekea juu ghorofani hadi katika chumba cha mikutano ya ana kwa ana kilichokuwa na runinga nne kubwa ukutani..Kwa kutumia remote control akawasha runinga namba mbili.
“ Hallow Edwin”akasema Osmund
“ Osmund .Habari za Tanzania?
“habari za huku si njema sana”
“ Kuna tatizo gani?
‘ tatizo la kwanza ni kuhusiana na ugonjwa wa John mwaulaya.Anaumwasana.Tulitegemea kumfanyia upasuaji lakini daktari tuliyemtegemea kufanya upasuaji huo hataweza tena kupatikana.Hali yake inazidi kuzorota kila dakika na kama asipofanyiwa upasuaji wa haraka tunaweza tukampoteza.” Akasema Osmund
“ Osmund,tulipokukabidhi nafasi kubwa kama hii ya kuongoza kikosi chenye nguvu kama hiki tulitegemea kwamba una uwezo wa kushughulikia masuala madogo madogo kama haya.Suala kama hili si suala la kutaka maelekezo toka makao makuu.Unatakiwa kuomba msaada wa makao makuu kama kuna jambo kubwa na zito lakini katika masuala kama haya ya ugonjwa tumewapa uhuru huko huko wa kufanya kila linalowezekana kutafuta matibabu..Umenielewa Osmund ? akasema Edwin.
“ Nimekuelewa Edwin lakini John Mwaulaya anahitaji kutibiwa.Huyu ni mtu mkubwa katika Team SC41.Suala la ugonjwa wake si la kulichukulia kirahisi rahisi namna hiyo” akasema Osmund huku akionyesha wazi kukakasirishwa na matamshi ya Edwin
“ Ni kweli John ni mtu mwenye wadhifa mkubwa katika Team SC41 lakini tunaweza tu kutoa msaada endapo utatuhakikishia kwamba mmeshindwa kabisa kumtibu.”
“ Edwin mpaka kufikia hatua hii ya kukupigia simu na kukuomba msaada ni wazi tumeshindwa”akasema Osmund
“ Sawa Osmund ,tutamtuma Dr Marcus burke atafika huko ndani ya siku mbili zijazo kuangalia ukubwa wa tatizo la John halafu atashauri nini cha kufanya”
“ Ahsante sana Edwin kwa kulipa uzito suala hili.Kuna suala lingine vile vile. “
“ suala lipi tena?
“ Kuna tatizo limetokea usiku wa leo”
“tatizo gani?
“ Kuna vijana wetu sita wameuawa katika shambulizi .”
“Mbona sikuelewi Osmund,wameuawa vipi? Nani kawaua? Akauliza Edwin
“ Bado hatufahamu ni nani lakini tumegundua kuna watu ambao wamekuwa wakitufuatilia.”
“ Umechukua hatua gani mpaka hivi sasa za kuwafahamu watu hao ni akina nani na wanataka nini? Akauliza Edwin
“Bado hatujawafahamu watu hao ni akina nani na wanataka nini toka kwetu lakini tutalishughulikia suala hilo kuanzia kesho.kwa hivi sasa ninashughulikia kwanza kuihifadhi miili ya vijana waliopoteza maisha na baada ya kukamilisha shughuli za mazishi yao kesho tutaanza rasmi kuwasaka na kuwafahamu watu hao ni nani na wanataka nini.”
“ Osmund lipe uzito mkubwa suala hili kwani ni suala zito sana.lazima tuwafahmu watu hawa ni akina nani na wametufahamu vipi na nini wanatafuta toka kwetu.Team SC41 ni kikosi kinachofanya kazi zake kwa siri kubwa kiasi kwamba hata ndani ya serikali ya marekani ni watu wachache wanaofahamu uwepo wake kwa hiyo kwa watu hao kuanza kutufuatilia ina maana kwamba tayari wanatufahamu sisi ni akina nani.Kujulikana kwa Team SC41 na kazi zetu kutahatarisha kwa kiasi kikubwa maslahi ya marekani katika afrika mashariki .Pamoja na kumtuma Dr Marcus Burke kuja kuangalia afya ya John,ataambatana vilevilena timu ya watu watatu ambao watakuja kusaidiana nanyi katika kuwabaini watu hawa ni akina nani.Nataka ndani ya kipindi kifupi tuwe tumewafahamu na kuchukua hatua zipaswazo.Nitaongea nawe tena kesho saa saba mchana kwa saa za Afrika mashariki ili kufahamu namna mnavyoendelea na kama mmekwisha wafahamu watu hao” akasema Edwin na kutoka katika laini..
“ Afadhali aje daktari toka Marekani kuja kuangalia afya ya John.Lazima apatiwe matibabu anayostahili.Hakuna sababnu ya kuendelea kusumbuka wakati kuna uwezekano mkubwa wa kumpeleka Marekani au nchi nyingine yoyote na akatibiwa ” Akawaza Osmund wakati akipanda ngazi kuelekea chumbani kwa John.Moyo wake ulifarijika sana baada ya kuhakikishiwa ujio wa Dr Burke.Aliufungua mlango wa chumba cha John na kumuomba daktari aliyekuwa akimuhudumia atoke nje .
“ Kuna nini Ossy?akauliza John kwa sauti ya chini
“ John nimeongea na makao makuu,wameahidi kumtuma daktari haraka iwezekanavyo.Ndani ya siku mbili hizi Dr Marcus Burke atakuwa amewasili kuja kuangalia afya yako na kutoa ushauri wa nii kifanyike” akasema Osmund.Pamoja na kuwa dhaifu lakini aliposikia jina la Marcus Burke John akastuka sana.Akamfanyia ishara Osmund asogee karibu
“ Umesema Dr Marcus Burke?
“ Ndiyo John.Anakuja Dr marcus Burke kuja kuangalia afya yako”
“ No Ossy.Dont let him.” Akasema John Mwaulaya
Osmund akamtazama kwa mshangao
“ Do you know him? Akauliza
“ yes I know him” akajibu John
“ John unaumwa na Dr Marcus anakuja kuangalia afya yako na kutoa ushauri nini kifanyike.Unatakiwa ufanyiwe upasuaji wa haraka ili kuokoa maisha yako“ akasema Osmund.John akaushika mkono wa Osmund na kusema
“ Osmund listen to me my boy.Ninamfahamu Dr Burke.He’s coming for one reason only”
“ One reason? Osmund akashangaa.
“ Yes.He’s coming to kill me.Please don’t let him.I need to die a natural death” akasema John na kuzidi kumshangaza Osmund
“ John nashindwa kukuelewa una maanisha nini.Dr Marcus anakuja kuangalia afya yako na si kukuua” akasema Osmund
“ Osmund please listen to what I’m telling you.Nilikataa kwenda kutibiwa marekani kwa sababu nilifahamu lazima wataniua.”
“ kwa nini wakuue John?
“ Kuna siri nzito ambayo hauifahamu kwa hiyo tafadhali usimruhusu Dr Burke kuja kuniangalia.Ninajua sina maisha marefu sana lakini ninataka nife kifo cha kawaida.”
“ John ni siri gani hiyo ambayo ingepelekea uuawe endapo ungeenda kutibiwa marekani?
“ Siwezi kukwambia Ossy.Ni siri ambayo nitakwenda nayo kaburini.” Akasema John.
“ John unataka nikusaidie na wakati huo huo unanificha siri uliyonayo.Tafadhali niambie na nitakusaidia”
“ Hapana Osmund siwezi kukwambia.Lifanyie kazi hilo nililokueleza .You can go now I need to be alone.”akasema John.Osmund akamtazama na kuondoka .
“Nitakufa hivi karibuni.Sifahamu kama ninaweza kusamehewa kwa mambo niliyoyatenda hapa duniani.Nimefanya mambo mengi mabaya lakini kuna jambo moja tu linalonipa faraja hata kama nikifa muda huu nitakufa huku nikitabasamu.I didn’t kill an Innocent child.I didn’t kill Peniela” akawaza John na kumbu kumbu zikamrudisha May 30 1990
30 May 1990
Gari la kifahari linafunga breki katika maegesho ya shule ya kimataifa ya watoto wadogo.John Mwaulaya anashuka ndani ya gari lile huku akivuta sigara .Kwa mbali akasikia kelele za watoto wakicheza.Akachukua simu na kumpigia mtu aliyekuwa akimtafuta.Baada ya dakika tano akatokea Bi Bernadetha mlezi wa kituo cha yatima anakoishi Peniela
“hallo mama Bernadetha.Habari za siku?
“ habari nzuri sana John.Pole na safari”
“ahsante sana mama nimekwisha poa.NashukuruMungu nimerejea salama.Peniela anaendeleaje?
“ Peniela anaendelea vizuri sana na zawadi zote ambazo umekuwa ukimtumia kutoka Marekani amezipata na anafurahi sana.John unamjali sana mwanao .Kwa nini lakini hutaki akuone wala akujue?
“ Mama Bernadetha,kama nilivyokwambia siku ninamkabidhi kwako ,sihitaji Peniela anifahamu kwa sasa.Hii ni kwa ajili ya usalama wake .Yuko wapi mida hii?nahitaji kumuona”akasema John.Bi Bernadetha akamchukua John na kumpeleka katika ofisi ya mkuu wa shule ile na kumtambulisha kama mfadhili wa Peniela.Waalimu walifurahi sana kumfahamu John na kumpongeza kwa namna alivyojitolea kumsomesha peniela katika shule ile ya gharama kubwa.Wote walimsifu Peniela kwamba ni mtoto mwenye bidii sana ya kujifunza.John akaomba akaonyeshwe mahala alipo Penny,akaongozana na mwali mmoja pamoja na bi Benrnadetha hadi katika uwanja wa michezo,kulikokuwa na michezo mbali mbali.Peniela alikuwa amejumuika na watoto wenzake wakicheza na kuruka kwa furaha.John alihisi furaha ya ajabu baada ya kumuona Peniela.
“She’so cute.Ni mtoto mzuri na mrembo.Nitahakikisha kwa kila nitakavyoweza anakuwa na maisha yenye kujaa furaha kubwa” akawaza John huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu .Alitamani akae pale kwa siku nzima ili aendelee kumuangalia peniela .
“ Natamani kama ningekuwa na mke ningemchukua Peniela niishi naye.Kwa mara ya kwanza natamani na mimi kuitwa baba lakini kazi hii hainiruhusu kuwa na familia.Anyway nitaendelea kumtunza Peniela kwa siri .”akawaza John halafu akaondoka na kurejea garini.Akafungua albamu lililojaa picha za Peniela ambazo alikuwa akitumiwa na Bi Bernadetha wakati akiwa kikazi nchini marekani
“ You are such a cute baby.I’ll take a good care of you Penny.You’ll never see me but I’ll always take very good care of you.”akasema John.
********
“ Mathew ..mathew..” akaita Anitha na kumstua Mathew toka katika usingizi uliokuwa umempitia. Aliitazama saa yake ilipata saa kumi na dakika kumi na tatu.Mbele yake walikuwa wamesimama Anitha,Dr Michael na Dr Robert.
“ Pole sana Mathew” akasema Dr Michael huku akitabasamu
“ Sorry nilipitiwa na usingizi kidogo “
“ Usijali Mathew,ni kutokana na zile dawa nilizokupa.Zina nguvu sana “akasema Dr Michael
“Nini kinaendelea Dr Michael? Akauliza Mathew
“ Tumemaliza kuzifanyia uchunguzi zile sampuli ingawa imetuchukua muda mrefu”
“Good.tayari mna majibu?
“Ndiyo Mathew,tayari tuna kila kitu” akajibu Dr Michael na kuketi kitini.
“ Mathew kilichosababisha kifo cha mke wa rais ni sumu iitwayo Spinolin .Tumekuta chembe chembe za sumu hii katika sampuli ya ini tuliyochukua.Sumu hii inapatikana katika dawa iitwayo Encozynes ambayo hutumiwa na watu wenye shinikizo la damu.Matumizi ya dawa hii mgonjwa hutumia mara moja kila baada ya mwezi mmoja tena kwa kiwango kidogo kwa sababu endapo ikitumiwa kwa kiwango kikubwa ina madhara makubwa na husababisha kifo kwa mgonjwa.Inaonekana mke wa rais alichomwa kiwango kikubwa cha dawa hii na hivyo kusababisha kifo chake.Nina mashaka na mtu aliyemchoma dawa hii kama alikuwa akifahamu madhara yake au alidhamiria kufanya alichokifanya.Inatakiwa kuchunguza ni nani aliyemchoma sindano hiyo kama ni daktari wake au ni mtu mwingine ili kufahamu dhamira yake ilikuwa nini .” akasema Dr Michael na kumkabidhi Mathew bahasha iliyokuwa na majibu ya vipimo walivyovifanya
“ Ahsante sana Dr Michael.Nashukuru sana kwa msaada wako.”akasema Mathew akasimama.Akapeana mkono na Dr Robert wakaagana wakaingia garini na kuondoka
“ Dr Flora alichomwa sindano iliyokuwa na kiwango kikubwa cha dawa tofauti na inavyotakiwa.Hapa inaonyesha wazi kwamba aliyemchoma alidhamiria kumuua.Naikataa hoja ya kwamba mchomaji hakuwa na ufahamu kuhusu madhara ya dawa ile.Ni nani basi aliyemchoma sindano ile na kwa nini? Hilo ndilo swali ambalo tunatakiwa kujiuliza kwa sasa.Tukimfahamu ni nani aliyemchoma Dr Flora sindano ile tutakitegua kitendawili hiki.” Akawaza Mathew wakiwa garini wakirejea nyumbani
“ Mathew ! akaita Dr Michael
“ Nimeikamilisha kazi yangu.Nadhani hatudaiani tena” akasema .Mathew akatabasamu kidogo na kujibu
“ Ahsante sana Dr Michael kwa msaada huu mkubwa.Pole sana kwa misukosuko mikubwa iliyokupata katika siku ya leo.Ninatumai ni mara yako ya kwanza kupitia misukosuko mikubwa kama hii.Ninashukuru kwamba baada ya misuko suko kumalizika nyote mu salama.Wewe na familia yako yote mko salama salimini.Hatuna deni tena mimi na wewe lakini ninachoweza kukushauri ni kwamba usifikirie kwenda nyumbani kwako wala kazini katika kipindi cha wiki moja au mbili mpaka hapo tutakapohakikisha kumekuwa salama.Wale jamaa wataendelea kukutafuta bila kuchoka hadi wahakikishe wamekutia mikononi.Kama hutajali naomba wewe na familia yako muendelee kukaa pale kwangu hadi hapo tutakapohakikisha kwamba hali ya usalama imeboreka.” Akasema Mathew.Dr Michael akatabasamu na kusema
“ Mathew nakiri kwamba kwa mara ya kwanza uliponifuata pale ofisini kwangu na kunielekezea bastora nilikuchukia mno.Nilikuona ni mtu mbaya sana na kwa hasira nilizokuwa nazo nilitamani hata nitafute kitu nikupige nacho nikuue kabisa.Lakini baada ya kukaa nawe kwa saa kadhaa nikagundua kwamba uko tofauti na nilivyokuwa nakufikiria.Wewe ni mmoja wa mashujaa wa taifa hili.Wewe ni kijana mwenye roho nzuri na huruma.Sina shaka yoyote kuhusu kukaa pale kwako ambako ni sehemu salama sana kwangu na kwa familia yangu kwa sasa lakini baada ya matukio ya leo tayari nimekwisha fanya maamuzi.Ninaondoka hapa nchini.”
“Unakwenda wapi?
“Mwezihuu nilikuwa namalizia mkataba wangu wa miaka mitano na hospitali ile ninayofanya kazi .Tayari nimekwisha pata kazi nyingine nchini Philipines katika jiji la manila.Ninataka kuelekea huko.Sitaki kuendelea kupoteza muda tena hapa.Kwa maana hiyo basi kuna jambo moja ambalo nitataka unisaidie.”
“Hizo ni habarinzuri.Umefanya maamuzi mazuri na familia yako itaendela kuwa salama.Ni kitu gani ambacho unataka nikusaidie?akauliza Mathew
“ Ninahitaji unisaidie kupata ndege .Kwa sasa mimi na familia yangu hatuwezi kutoka na kuanza kuzunguka kutafuta ndege.Naomba unisaidie kuifanya kazi hiyo.Nataka ndege ya kunitoa hapa na kunifikisha afrika ya kusini na kutokea pale nitakuwa salama. “ akasema Dr Michael
“ usijali kuhusu hilo Dr Michael ,tukifika nyumbani Anitha ataingia mtandaoni na kuangalia kama anaweza akapata ndege ya kukufikisha Afrika ya kusini na pale unaweza ukawa salama kutafuta ndege ya kuelekea kokote unakotaka”akasema Mathew
“Nitashukuru sana Mathew.”akasema Dr Michael na safari ikaendelea
Saa kumi na moja na dakika ishirini na saba wakawasili nyumbani kwa Mathew.Ni Noah peke yake ambaye hakuwa amelala licha ya kuwa na maumivu makali ya mguu.
“ Poleni sana.”akasema Noah
“Ahsante Noah.Elibariki yuko wapi? Akauliza Mathew,Noah akamfahamisha kwamba yuko chumbani amelala,akamfuata akamuamsha
“ Mathew !!..akasema jaji Elibariki kwa uchovu uliochanganyika na maumivu ya kidonda alichokuwa nacho kichwani mahala alijkopigwa chupa na Jason.Akaitazama saa yake ilikuwa ni saa kumi na mbili kasoro za asubuhi.
“Its morning.!! Akasema
“ yah ! Kumekucha.”
‘ Kuna taarifa gani ?akauliza Elibariki
“ Ile kazi yako imekamilika.”
“ Thank you Lord ! akasema
“Ripoti ya uchunguzi hii hapa.kwa ufupi tu ni kwamba Dr Flora alichomwa dawa iitwayo Encozynes yenye kiambata kijulikanacho kama Spinolin.Dawa hii hutumiwa na watu wenye matatizo ya shinikizo la damu lakini ni kwa kiwango kidogo sana.Mgonjwa akipewa dawa hii kupita kiwango chake basi husababisha kifo ndani ya muda mfupi kutegemea na kiwango alichopewa.Kwa hiyo tunatakiwa tuchunguze ni nani aliyemchoma dawa hiyo na kwa nini alimchoma.Tukimpata mtu aliyemchoma tutakitegua kitendawili hiki”akasema mathew
“ Kwa maana hiyo kuna kila dalili zinazoonyesha kwamba Dr Flora aliuawa kwa kuchomwa kwa makusudi sindano ile .Na hii ni sababu kumekuwa na jitihada kubwa za kutaka kuzuia uchunguzi wa kifo cha Dr Flora usifanyike kwa sababu waliogopa itabainika kwamba aliuawa.” Akasema Jaji Elibariki
TAYARI MATHEW ANA MAJIBU YA KILICHOMUUA MKE WA RAIS,NINI KITAFUATA? KWA NINI JOHN MWAULAYA ANAMUOGOPA DR MARCUS BURKE? TUKUTANE TENA KATIKA SEHEMU YA MWISHO YA SEASON ONE YA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA…..………………
“
InabambaSEASON 2
SEHEMU YA 3
ILIPOISHIA SEHEMUILIYOPITA
Sauti za watu wakijadiliana jambo zilisikika katika chumba cha kulia chakula.Hakutaka kupoteza muda akaufungua mlango ule kwa kasi na kujitoma ndani.Kitendo kile kiliwastua sana wazee wale waliokuwemo mle ndani.Kufumba na kufumbua bila hata kutamka neneo moja John akaanza kuifanya kazi iliyompeleka mle,aliwamiminia risasi wazee wale ,Seneta Joe Burke na DrElisante wakaanguka chini hawakuwa na uhai tena,Risasi nyingi zilizotoka katika bastora mbili za John zilizokuwa na viwambo vya sauti ziliwasambaratisha na kuwaharibu vibaya.Bila kupoteza hata sekunde moja John akakusanya makaratasi yote yaliyokuwapo pale mezani,akayapakia katika sanduku dogo akaenda chumbani na kuchukua kompyuta ndogo ya seneta Burke pamoja na kila kitu ambacho alikiona kinafaa kuchukuliwa halafu akaufunga mlango na kurejea katika chumba kile alichoacha mavazi yake akavua zile nguo za wahudumu wa hoteli akaziweka katika sanduku dogo na kuondoka.
“That’s how I killed seneta Burke.Baada ya miaka mingi kupita mwanae anakuja kulipiza kisasi,he’s coming to kill me”
Akawaza John Mwaulaya
ENDELEA…………………………….
Arnold alimtazama Mathew machoni na kugundua kwamba hakuwa akihitaji masihara.Aliogopa sana.
“Brother unanipeleka wapi? Kama una shida ya pesa tafadhali naomba uniambie” akasema Arnold huku akitetemeka na uso wake tayari ulikwisha loa jasho
“ Drive !..akasema Mathew kwa ukali.Mita kama mia tano toka waliache jengo lile Mathew akafanya kitu kimoja ambacho Arnold hakuwa amekitegemea.Kwa kasi ya ajabu alimpiga pigo moja kichwani kwa kitako cha bastora na Arnold akapoteza fahamu.Mathew akaudaka usikani wa gari na kulizuia gari lisiyumbe na taratibu akaliongoza gari hadi pembeni ya barabara akalisimamisha .Hakuna aliyeweza kuona kilichokuwa kinatendeka ndani ya ile gari kutokana na kuwa na vioo vyeusi.Anitha aliyekuwa analifuatilia gari lile kwa nyuma naye alisimamisha piki piki na kujiweka tayari kwa chochote ambacho kingejitokeza
Kwa haraka Mathew akachukua waya na kumfunga Arnold mikono na miguu halafu akamrushia katika kiti cha nyuma akaukalia usukani na kuliwasha gari akaendelea na safari
“Huyu jamaa ni nani?Mbona haonekanai kama nimtu hatari? Mbona hana silaha yoyote? Akajiuliza Mathew
“ Tutapata majibu muda si mrefu” akawaza Mathew na safari ikaendelea hadi nyumbani kwake.Wakamtoa Arnold na kumuingiza katika chumba kilichokuwa na kitanda cha chuma.Wakamlaza juu ya kile kitanda
“Huyu jamaa haonekani kama ni mtaalamu wa mambo haya.Nimempekua na hana silaha yoyote.Katika mkoba wake kuna vitu vya kawaida tu pamoja na ile tablet aliyopewa na wale jamaa kule City centre”akasema Mathew
“ Hata mimi ninahisi hivyo .Haonekani kama ni mtu anayefahamu chochote.Lakini lazima tumfahamu ni nani na nini lengo la kumfuatilia Eva.”akasema Anitha
“ Inawezekana akawa anatumiwa na watu Fulani.Anatakiwa ahojiwe na aseme kila kitu” akasema Noah.
Mathew akatoka mle chumbani na baada ya muda akarejea kiwa ameshika kitu Fulani mkononi mithili ya dawa,akakifungua na kukiweka katika pua za Arnold na baada ya sekunde kadhaa Arnold akapiga chafya mfululizo.Akafumbua macho na kujikuta ndani ya chumba akiwa amelazwa kitandani na kufungwa mikono.Akaangaza huku nahuku na kumbu kumu za nini kilichotokea zikamjia
“ Mmenileta wapi? Ninyi ni akina nani? Mnataka nini kwangu? Kama mnahitaji fedha niambeni m,mnataka kiasi gani niwapatie? Akasema Arnold huku machozi yakimtoka
“ Relax Arnold.Hatutakufanya kitu chochote kibaya .Kuna mambo tunayohitaji kuyafahamutoka kwako na baada ya hapo tutakuachia uendelee na shughuli zako lakini endapo utashindwa kutupatia kile tunachokihitaji basi itatulazimu kutumia nguvu ”
“ Tafadhali naombeni mnifungue ninasikia maumivu.Nitawapa kila mnachokihitaji lakini mniachie huru.Mimi si mtu mbaya .” Akasema Arnold.Mathew akatazamana na Anitha na kumpa ishara amfungue mikono
“ Arnold kuna kitu kimoja tu tunachokihitaji toka kwako”
“Kitu gani ? Pesa? Gari ? Chukueni chochote lakini mniache mzima” akasema Arnold
“ Hatuna shida na pesa Arnold.Tunahitaji utuambie ukweli.Kuna vijana Fulani wanne ambao mmoja wao ulikutana naye pale City center na akakupa kifaa chenye muundo kama tablet walikuwa wakimfuatilia dada mmoja anaitwa Eva.Vijana wale walitega kifaa Fulani katika gari la Eva ambacho hutuma taarifa katika ile tablet.Tunataka kufahamu ni kwa nini mnamfuatilia Eva? Kwa nini mnataka kujua mizunguko yote ya Eva? Ukitupa majibu ya kuridhisha basi tutakuachia huru uende zako lakini endapo utatudanganya ni wazi itatulazimu tutumie nguvu.Ninakushauri usitufanye tufike huko .Utapata maumivu makali sana ambayo hujawahi kuyapata toka uzaliwe” akasema Mathew
“ Jamani naombeni msitumie nguvu.Nitawaeleza chochote mnachokitaka” akasema Arnold
“ Kusema ukweli mimi simfahamu huyo msichana Eva na wala sijawahi kumuona.” Akasema Arnold
“ Tafadhali Arnold usitulazimishe tutumie nguvu .Sipendi tufike huko .Tueleze ukweli kwa nini mnamfuatilia Eva?
“ Nawaelezeni ukweli ndugu zangu,huyo Eva simfahamu na wala sijawahi kumuona.Ninaomba mniamini ndugu zangu.Mimi ni mtaalamu wa program za kompyuta na nina ofisi yangu katika jengo lile mlikonikuta.Ninachofahamu mimi kuhusu huyu msichana unayemuita Eva ni kwamba wiki iliyopita walikuja watu Fulani wawili ofisini kwangu na kuniomba niwafanyie kazi yao fulani na wakaahidi kunilipa pesa nyingi kama nikiifanya wanavyotaka.Waliniambia kwamba wanahitaji niwatengenezee program ya kompyuta kwa ajili ya kumfuatilia mtu Fulani bila ya yeye kufahamu kama anafuatiliwa.Waliahidi kunipa shilingi million kumi na mbili endapo ningefanikisha kazi hiyo ambayo ilionekana ni ya muhimu sana kwao.Sijawahi kuifanya kazi yenye malipo makubwa kama hii kwa hiyo nilishawishika kukubali kufanya kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kuifanya .Nilitengeneza program ambayo ingeweza kuonyesha mizunguko yote ya mtu huyo waliyemtaka.Baada ya kuikamilisha program hiyo kilichofuata ilikuwa ni kukiweka kifaa hicho katika gari la mlengwa.Ili kuifanyakazi hiyo ilinilazimu kuwakodisha wale vijana mliwaona kule City centre kwaniwao ni wazoefu wa mambo kama hayo.Walifanikiwa kukiweka kifaa kile katika gari la Eva na programu yetu ikafanya kazi vizuri jinsi inavyotakiwa.Hicho ndicho ninachokifahamu .Huyo Eva simjui na wala sijawahi kumuona.” akasema Arnold
“ Baada ya kuikamilisha kazi uliyopewa nini kitafuata? Akauliza Anitha
“ Kinachofuata baada ya hapo ni kuwakabidhi kazi yao na wao kunipatia malipo yangu yaliyobaki.”
“Hao jamaa walikupa sababu ya kwanini wanataka kumfuatilia Eva? Akauliza Noah
“ Hapana hawakunieleza chochote kuhusiana na sababu ya kumfuatilia huyo mtu.” Akasema Arnold
“ saa ngapi utaonana nao ili uwakabidhi kazi yao?
“Tumepanga tukutane leo saa moja jioni.Wamesemawatanipgia simu kunipa maelekezo ya mahala kwa kukutana” akasema Arnold
“ Ok vizuri.sasa utaendelea kukaa hapa hadi jioni na tutakwenda sote katika hayo makabidhiano na halafu tutakuacha uende zako.Sisi hatuna shida na wewe hata kidogo.Sisi shida yetu ni hao jamaa waliokupa hiyo kazi” akasema Mathew
“ Tafadhalini jamani nimekwisha waeleza kila kitu mlichokuwa mnataka ,niachieni basi niende zangu” akasema Arnold
“ Usijali Arnold,tutakuachia uende zako ,lakini hadihapo tutakapohakikisha kwamba makabidhiano yamefanyika” akasema Mathew halafu wakaufunga mlangowa kile chumba wakatoka wakaingia katika chumba cha kupangia kazi .
“Wakati tunasubiri kuonana na Elibariki ili kuliweka sawa suala la Peniela,limeibuka suala hili la watu hawa wanomfuatilia Eva na hatuwezi kuliacha.Eva ni rafiki yangu mkubwa na wa miaka mingi na ni mtu ambaye nina hakika anaweza akawa ni wa msaada mkubwa sana kwetu .Ametusaidia katika kulifanikisha suala lile la kuipata ripoti ya kifo cha Dr Flora.Bila yeye tusingeweza kumpata kanali Adolf.Kwa hiyo wakati tunamsubiri Elibariki naombeni mnisaidie kuwabaini watu hawa ni akina nani na nini wanakitafuta kwa Eva? Nina imani kuna kitu tunaweza kukigundua hapa” akasema Mathew
“ Mathew ! akaita Noah
“ Wewe ni rafiki yangu mkubwa na ni kwa msaada wako nimefika hapa nilipo.Umenitoa mbali sana.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Umetuita hapa ili tukusaidie kazi ya kutafuta nani muuaji wa Edson, Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda sielewi ni kazi gani iliyotuleta kwani kila siku kazi zinabadilika na hatuelewi kazi ya msingi ni ipi.Jana tumefanya kazi isiyotuhusu na ilibaki kidogo tungepoteza maisha.Leo tena imeibuka kazi nyigine mpya.Mathew tumeyaweka maisha yetu rehani kwa ajili ya kukusaidia ,tuko hapa kwa ajili ya kusaidiana nawe kama ulivyotuomba lakini naomba utuweke wazi ,tunakusaidia kufanya kazi ipi? Akauliza Noah
“Noah !!...akasema Anitha
“ No ! Anitha,Noah ana haki ya kuuliza .Ni kweli niliwaiteni kwa ajili ya kunisaidia kufanya uchunguzi wa suala la Edson lakini kadiri tunavyoendelea na uchunguziwetu mambo mengine zaidi yanaibuka .Ni sawa na unapotafuta madini.Ili uyafikie utakutana na vizingiti vingi kama mawe n.k lakini kwa vile nia yako nikupata madini basi itakulazimu kuyaweka pembeni ili upate njia ya kukufikisha yalipo madini.Hilo ndilo linalotutokea sisi.Tunafanya uchunguzi wa kifo cha Edson tufahamu ni nani alimuua na kwa nini,lakini ndani ya uchunguzi huo yanaibuka mambo mengine mfano Team SC41.Hatuwezi kuacha kuchunguza kila kitu kinachoibuka mbele yetu ambacho tunahisi kinaweza kuwa na mahusiano na kifo cha Edson.Suala lililojitokeza jana na hili la leo ni mambo ambayo nisingeweza kukataa kuyafanya.Elibariki ndiye aliyetupa kazi hii ya kuchunguza kuhusu kifo cha Edson na ndiye anayetulipa kwa hiyo alipokuja na kazi nyingine nakuomba tumsaidie ili kuwa ngumu kukataa.Hata hivyo tumefanikiwa kugundua jambo kubwa sana kuhusiana na kifo cha Dr Flora mke wa rais.Leo hii Eva naye amepatwa na matatizo.Eva ni rafikiyangu wa siku nyingi na amekuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa kwangu.Ni yeye aliyetusaidia tukampata kanali Adolf jana na mkumbuke pia kwamba tulikuwa na makubaliano kwamba atanisaida kumpata kanali adolf lakini naye ana kazi yake ambayo anahitaji msaada na niliahidi kumsaidia.Leo hii amenipigia simu na kuniomba tena msaada kuna watu waliokuwa wakimfuatilia toka alipotoka nyumbani kwake.Ilikuwa vigumu sana kwangu kukataa kumsaidia .Kwa kujibu swali lako Noah ni kwamba bado hatujatoka nje ya kazi yetu ya msingi.Bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na kifo cha Edson lakini hatuwezi kuachana na mambo madogo madogo yanayojitokeza wakati wa uchunguzi huo”akasema Mathew
“ Ninakuelewa Mathew .lakini je ni lini basi tutamaliza kazi hii kama tukiendelea na mpango huu wa kuifanya kila kazi inayojitokeza mbele yetu ? Akauliza Noah
“Noah Please stop that !!..akasema Anitha ambaye alionekana kukerwa na maswali yale ya Noah.
“ I’m sorry Anitha but I need to know .Jana almanusura nipoteze uhai wangu kwa hiyo nahitaji kufahamu kuhusu mpangilio maalum wa kazi tunazozifanya.”akasema Noah
“Usihofu Noah.Kazi itaendelea hata kama hautakuwepo.Inavyoonekana hauko tayari kuendelea na kazi hii.Endapo unahitaji kuondoka uko huru kufanya hivyo.Simzuii mtu yeyote kuondoka.Nina watu wengi ambao wanaweza wakanisaidia katika kazi hii lakini niliona ninyi ni chaguo langu la kwanza ndiyo maana nikawaita.Kwa hiyo kama kuna yeyote kati yenu ambaye hajisikii kuendelea kuifanya kazi hii anaweza akaondoka” akasema Mathew
“ Please Mathew don’t say that.You know I’m always with you.Tumefanya kazi nyingi pamoja na tumepitia hatari nyingi sana kuliko hata hizi za sasa.kwa hiyo siwezi katu kukuacha .Noah kama unajisikia kutaka kuondoka you can just leave!! Akasema Anitha
“Jamani naomba msinielewe vibaya .Sina maana ya kwamba ninataka kuondoka.Siwezi kuondoka na kuwaacha kwani hii ni kazi yetu sote.Samahani kama niliwakera kwa maneno yangu .Tusipoteze muda tuendelee na kazi.”akasema Noah
“Kabla hatujaendelea na kazi nahitaji kufahamu who is with me ? akauliza Mathew
“ I’m with you Mathew” akasema Anitha
“ Me too “ akasema Noah
“ Ok good.Nawashukuruni sana .Saa moja jioniya leo Arnold anakwendda kuonana na watu waliompa kazi na kuwakabidhi kile kifaa ambacho kazi yake ni kuonyesha mienendo yote ya Eva.Katika tablet ile kuna ramaniyote ya jiji la Dar es salaam kwa hiyo kila sehemu aliko Eva ataonekana.Kitu cha kufanya Anitha utaichukua tablet hii na kuiwekea programu nyingine ya siri ya kutuwezesha sisi kuifuatilia.Arnold atakabidhiana nao na baada ya hapo sisi tunatakiwa kuwafuatilia watu hao na kuwafahamu ni akina nani na nini lengo lao kwa Eva.Can you do that Anitha?akauliza Mathew
“Yes I can.Ni kazi ndogo sana hiyo kwangu”akasema Anitha
“Ok thank you.Do it” akasema Mathew na kutoka akaelekea chumbani kwake na kumpigia simu Eva
“ Halow Mathew” akasema Eva baada ya kupokea simu
“ Eva unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri Mathew.Nipe habari.Mmegundua nini kuhusu wale jamaa?
“ wale jamaa hawakuwa na hatari yoyote,walipewa kazi ya kukiweka kifaa kile cha kukufuatilia katika gari lako na kazi yao ikaisha.Tumempata mtu aliyetengeneza program ile na amedai kwamba alipewa kazi hiyo na watu wawili ambao waliahidi kumlipa pesa nyngi.Kwa namna Programu hiyo ilivyotengezwa ni kwamba kifaa kile kilichowekwa katika gari lako hutuma taarifa katika kifaa kingine muundo wa tablet ambacho kina ramani nzima ya jiji la Dar es salaam na hivyo kila sehemu utakayokwenda utaonekana .”
“ watu hao ni akina nani? Na kwa nni watumie gharama kubwa hivyo kunichunguza? Mathew nimeanza kuingiwa na woga .Inaonekana maisha yangu yako hatarini.Inaoenekana hawa jamaa ni watu wanaonifahamu sana”
“Bado hatujawafahamu watu hawa ni akina nani lakini hautapita usiku wa leo kabla ya kuwafahamu ni akina nani.Mpaka wakati huo tutakapolifahamu lengo lao ni nini nakushauri chukua tahadhari kubwa”
“ Ahsante Mathew kwa msaada wako mkubwa.Ninahamu sana ya kuwafahamu watu hawa ni akina nani na kwa nini wanamfuatilia”
“ Usijali Eva.Nitafanya kila linalowezekana ili kuwafahamu watu haoi” akasemaMathew na wakati huo huo ikaingia simu ya jaji Elibariki.Akamuomba Eva akate simu ili aweze kuipokea
“ Hallow Elibariki “akasema Mathew
“ Mathew utanisamehe nilishindwa kufika hapo nyumbani mchana kuna tatizo lilitokea.Mke wangu alipoteza fahamu ghafla na kukimbizwa hospitalini.Lakini mazingira ya kupoteza kwake fahamu yananipa shaka sana”
“ Ilikuaje hadi akapoteza fahamu? Akauliza Mathew
“ Wakati shughuli ya kuuaga mwili wa Dr Flora zikiendelea katika viwanja vya ukombozi,mke wangu alifuatwa na mtu Fulani na kumwambia kwamba anahitajika katika gari la wagonjwa na alipoelekea huko alijikuta akipoteza fahamu na kukimbizwa hospitali.Mathew mazingira ya tukio hilo yanatia shaka sana”
“ Ni kweli Mathew,mazingira hayo yanatia shaka sana .Ninachokuomba kwa sasa chukua tahadhari kubwa.Watu waliomuua Dr Flora ni watu toka ndani ya ikulu na watafanya kila njia kuhakikisha kwamba hawajulikani.Yeyote yule ambaye ataonekana kuwa ni hatari kwao watamshughulikia kwa namna wanavyojua wao kwa hiyo mpe tahadhari mke wako awe makini sana kwa wakati huu.Elibariki tutaliongea vizuri zaidi suala hili jioni naomba ujitahidi usikose kuna jambo la muhimu sana la kuongea kuhusiana na Peniela”
“ Peniela? !..Jaji Elibariki akastuka
“ Kuna nini kuhusu Peniela?
“ Kuna jambo la muhimu sana la kujadili kuhusu Peniela”
“ Ok Mathew nitafika baadae lakini endapo nitashindwa kufika basi tutaonana kesho jioni au kesho kutwa kwa sababu kesho tutakwenda kumzika Dr Flora kijini kwao alikozaliwa na tutarejea jioni na endapo hatutaonana hiyo jioni basi tutaonana kesho kutwa asubuhi”
“ sawa Elibariki.Tutaonana utakapopata nafasi” akasema Mathew na kukata simu
“ Kuna kitu gani kinachoendelea pale ikulu ? Dr Flora ameuawa na nina uhakika mkubwa waliofanya jambo hili wako ndani ya ikulu.Nguvu kubwa imetumika kutaka kuzuia sababu ya kifo cha Dr Flora isijulikane lakini tumefanikiwa kujua nini kilimuua.Kuna kitu gani kinachoendelea ikulu? Lazima liko jambo kubwa hapa linalotakiwa kuchunguzwa.Kwa vile suala hili liko tayari mikononi mwa rais basi nina hakika litashughulikiwa ipasavyo.Kazi yangu mimi ilikuwa ni kuchunguza na kuwapa majibu” akawaza Mathew na kuelekea katika chumba cha kulia chakula .Alihisi njaa.Noah aliyekuwa amebaki nyumbani alikwisha andaa chakula
“ Watu hawa wanaomfuatilia Eva ni akina nani? Nafahamu Eva ana fanya kazi kwa siri katika idara ya usalama wa taifa.lazima kuna wau watakuwa wanataka kumchunguza.Hizi kazi niza hatari sana.Siku zote unaishi kama ndege.” Akawaza Mathew na mara Anitha na Noah wakaingia kujumuika naye pale mezani
“Anitha umefikia wapi kuhusu ile program ?
“ Ninaendelea na hiyo kazi .Lakini huyu jamaa Arnold anaonekana ni mtu anayeifahamu sana kompyuta .Nimeangalia namna alivyoitengeneza ile program dah ! yuko vizuri sana” akasema Anitha
“ Nimezungumza na Elibariki kwamba atajitahidi kufika jioni ya leo ili tuweze kuongea naye kuhusu lile suala la Peniela.Yeye ndiye tutakayemtumia katika kumchunguza Peniela.Peniela lazima kuna kitu anakifahamu kuhusiana na kifo cha Edson na Team SC41.Ili tuufahamu ukweli yatubidi tumfanyie uchunguzi mkubwa sana na nina hakika yeye ndiye atakayetuongoza kwenye ukweli ”akasema Mathew
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
Na kwako piaWAKUU NIWATAKIE USIKU MWEMA
FayaaaSEASON 2
SEHEMU YA 30
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ hallow peniela”akasema Captain Amos akimpa mkono Peniela.
“ naitwa Amos mimi ndiye ambaye nimekuwa nikiwasiliana nawe katika simu” akasema Captain Amos
“ Nafurahi sana kukufahamu Amos” akasema peniela
“ Ninaitwa dr Kigomba.Mimi na Amos ni marafiki wakubwa” akasema Dr Kigomba.
“ Nafurahi kukufahamu dr Kigomba .Nadhani ninyi nyote hatujawahi kuonana “ akasema peniela
“ Hapana hatujawahi kuonana na hata mawasiliano yako nilipata taabu sana kuyapata” akasema captain Amos.
“ Ok vizuri.Uliniambia kwamba unashida kubwa na mimi.Ni shida gani hiyo?akauliza Peniela bila kuchelewa.Hakutaka kupoteza muda
“ Peniela nimekuita tukutane hapa lakini si mimi mwenye shida.Huyu mwenzangu ndiye mwenye shida na wewe.kwa maana hiyo basi nitawaacha ninyi peke yenu muweze kuongea na akueleze ana shida gani” akasema Captain Amos na kuinuka akatoka nje akawaacha mle chumbani Dr Kigomba na Peniela.
ENDELEA…………………
Kimya kikatawala mle chumbani walimobaki Dr Kigomba na Peniela.Uzuri wa peniela ulimchanganya sana Dr Kigomba na kumfanya ababaike namna ya kumuanza.Hakuwahi kukutana ana kwa ana na peniela na hakufikiri kama anaweza kuwa ni mwanamke mzuri kiasi hiki.
“ Amos alikuwa sahihi Peniela ni binti mwenye uzuri usio wa kawaida.Sikuwahi kukutana naye ana kwa ana na kuushuhudia uzuri wake.Ana uzuri ambao siwezi kuuelezea.Siwezi kukubali kumkosa mrembo huyu,lazima nimpate.Nashukuru Dr Joshua kwa kunipa jukumu la kumchunguza Peniela kwa amenikutanisha na malaika.” Akawaza Dr Kigomba .Peniela naye alikuwa ametulia akiwa na glasi yake ya wine akinywa taratibu akimsubri Dr Kigomba aanzishe maongezi.
“ Nimegundua Kigomba tayari ameanza kuniogopa.Nimeiona sura yake namna anavyohangaika kutaka kunianza.Hii ni dalili nzuri kwangu kwamba kazi yangu itakuwa rahisi sana.Ngoja nimsubiri aanzishe maongezi “ akawaza Peniela akiendelea kunywa wine taratibu sana.Dr Kigomba akakohoa kidogo na kurekebisha tai yake akasema
“ maisha yanakwendaje Peniela?
“ maisha yanakwenda vizuri sana.Kila kitu kinakwenda vizuri na ninamshukuru Mungu”
“ Vizuri sana.kazi zinakwendaje?
“ Kazi nzuri tu.Ninaendelea vizuri.Vipi kwa upande wako kazi zinakwendaje? Unafanya kazi hospitali gani? Akauliza Peniela na kumfanya Dr Kigomba acheke kidogo
“ Peniela mimi si daktari wa kutibu magonjwa bali ni daktari wa ssheria.Kuhusu kazi yangu mimi ni katibu wa rais “
“ Wow ! “ Peniela akajifanya kushangaa sana
“ Kumbe niko na mtu mkubwa hapa bila kuelewa.Katibu wa rais ni mtu mzito.Nimefurahi sana kukutana nawe Dr Kigomba”
“ Hata mimi nimefurahi sana kukutana nawe peniela.” Akasema Dr Kigomba
“ Amos naye anafanya kazi gani?
“ Amos naye pia anafanya kazi ikulu kama daktari wa familia ya rais.”
“ Ouh ! Kumbe leo nina bahati sana ya kukutana na watu wazito .”akasema Peniela huku akiachia tabasamu kubwa.Baada ya kimya kifupi Dr Kigomba ambaye alikwisha anza kumzoea peniela akauliza
“ Peniela unajishughulisha na nini sasa hivi baada ya matatatizo yako kumalizika?
“ Unazungumzia yale matatizo ya kesi ? akauliza peniela
“ Ndiyo.Tena naomba nichukue nafasi hii kukupa pole kwa matatizo yale”
“ Ahsante sana Dr Kigomba nimekwisha poa.Ninamshukuru Mungu kesi ilimalizika salama ,mahakama haikunikuta na hatia na ikaniachia huru.Baada ya kesi kumalizika nimerejea tena katika maisha ya kawaida na nimekutana na changamoto nyingi za kimaisha mfano kabla ya kwenda gerezani nilikuwa na maduka makubwa mawili ya nguo na….” kabla hajaendelea dr Kigomba akaingilia kati
“ Niliyafahamu maduka yako,mke wangu alikuwa anapenda sana kununua nguo toka katika maduka yako”
“ ouh kumbe ulikuwa ukiyafahamu maduka yangu.Kwa hiyo baada ya kesi kumalizika nimekuta maduka yangu yamefilisika ,biashara zangu karibu zote zilikufa kutokana na watu kutokuwa waaminifu kwani wengi waliamini kwamba ningefungwa maisha gerezani au kuhumumiwa kifo.Hivi sasa ninajipanga upya ili niweze kuzifufua tena biashara zangu zote” akasema Peniela
“ Pole sana Peniela.Wanadamu hawana wema hata kidogo.lakini usijali kuhusu hilo.Kwa vile sasa uko huru kila kitu kitarejea kama kilivyokuwa awali na hata zaidi ya awali.watu wa kukusapoti na kukushika mkono tupo na mimi nitakuwa mmoja wao katika kuchangia maendeleo yako.Watu waliofanya kitendo kile cha kukusingizia kesi walifanya kitendo kibaya sana lakini serikali ipo na siku moja watabainika tu”akasema Dr Kigomba
“ Mwanaharamu huyu angejua kama ninamfahamu zaidi ya anavyojifahamu wala asingethubutu kuongea upuuzi wake huu mbele yangu.Natamani hata nimvamie nimng’oe pua yake” akawaza Peniela halafu akauliza
“ Dr Kigomba ulisema kwamba una shida na mimi.Ni shida gani hiyo? Akauliza Peniela kwani hakutaka kuendelea kusimuliana hadithi za maisha
“ Uhhm..ni kweli peniela nilikuwa nahitaji sana kukuona na sikujua ningekupata vipi ndiyo maana nikamuomba Amos anisaidie niweze kukupata kwani yeye anafahamiana na watu wengi na angeweza kupata mawasiliano yako.Nashukuru sana hukupuuza wito wake na umekuja kunisikiliza na inaonyesha ni namna gani ulivyo mstaarabu na mwenye adabu”akasema Dr Kigomba
“ Siku zote sina tabia ya dharau na Amos aliniomba kiustaarabu sana nije nionane nanyi na nikaona ni vyema nikavunja ratiba zangu na kuja kukusikiliza” akasema Peniela.Dr Kigomba akafikiri kidogo na kusema
“ peniela nimekuita hapa kwa jambo moja kubwa.”
“ Ndiyo nakusikia Dr Kigomba” akasema peniela huku akimkazia macho
“ Uuhm… Peniela kilichonifanya nitake kukutana nawe usiku huu hapa ni kwamba nimevutiwa nawe,na ninataka mimi nawe tuwe marafiki.kwa ufupi ninahitaji kuwa na uhusiano na wewe.Umenivutia sana Peniela na nimeshindwa kuvumilia kwa hiyo nimekuita hapa ili kukueleza jambo hilo.Ninakupenda sana Peniela na ninataka uwe mpenzi wangu”akasema Dr Kigomba.Peniela akanywa wine kidogo halafu akamtazama Dr Kigomba na kutabasamu
“ Kigomba I can see you have a wedding ring” akasema Peniela huku akicheka kidogo.Dr Kigomba akatabasamu kidogo na kusema
“ To be honest I have a wife and kids and..”
“ kama una mke na watoto unahangaika nini Dr Kigomba? Akauliza Peniela
“ Unajua katika ndoa huwezi ukapata kila kitu unachokihitaji kwa hiyo kama huwezi kupata kitu unachokihitaji basi unaruhusiwa kutoka kwenda kutafuta nje.Ninahitaji mapenzi motomoto ninahitaji vitu vingi ambavyo mke wangu hawezi kunifanyia.Siwezi kuelezea sana jambo hili lakini naomba tu ufahamu kwamba ninakuhitaji sana Peniela.Nitakupatia kila kitu unachokihitaji katika maisha yako.If you need a house,a car au kitu chochote kile nieleze nitakupatia.” Akasema dr Kigomba
“ Dr Kigomba kwa nini unataka kumfanyia hivyo mke wako? Kwa nini unataka kumsaliti na kuvunja kiapo chenu cha ndoa? Akauliza Peniela
“ Ouh Peniela ,naomba tusijadili kuhusu mambo hayo na tujadili kuhusu mimi na wewe.Peniela ninakuhitaji sana uwe mpenzi wangu na nitakufanyia kila kitu unachokihitaji katika katika maisha yako.”
“ Dr Kigomba nashind………….” Akataka kusema peniela lakini Dr Kigomba akamuwahi
“ Peniela kwani una mchumba? Akauliza Dr Kigomba
“ hapana sina mchumba kwa sasa.Mpenzi wangu niliyekuwa naye alikuwa ni edson na akauawa.baada yake sina tena mchumba” akasema Peniela
“ kama ni hivyo kwa nini basi usinipe nafasi hiyo Peniela ? Nipe nafasi ya kukutunza,kukuenzi na kuyafuta majeraha yote ya nyuma uliyoyapata.Ninastahili kabisa nafasi hiyo Peniela.Tafadhali naomba usininyime nafasi hii ya kukuonyesha upendo ”akasema Dr Kigomba
“ Sina muda mrefu wa kuzungushana na huyu paka shume ambaye hata kutongoza hajui,ngoja nimkubalie tu ili niokoe muda kwani natakiwa kuonana na akina Elibariki usiku huu” akawaza Peniela
“ Dr Kigomba umeniweka katika wakati mgumu sana kiasi kwamba ninashindwa kusema hapana kwa ombi lako.Hata hivyo kwa hali niliyo nayo hivi sasa baada ya kuyamaliza yale matatizo ,ninahitaji sana msaada.Ninahitaji sana mtu ambaye anaweza akanikwamua hapa nilipo na kuniwezesha kusimama tena.kwa kuwa umeonyesha kutaka kunisaidia ili niweze kurejea katika maisha yangu ya kawaida basi mimi sina namna nyingine zaidi ya kuridhia ombi lako.Nitakuwa mpenzi wako na nitakutimizia kile ulichokikosa kwa mkeo lakini naomba unihakikishie kwamba hautaniingiza katika matatizo mengine na mkeo wala familia yako.Sihitaji tena matatizo yoyote yale” akasema Peniela.Dr kigomba akainuka na kumfuata peniela pale sofani alikokuwa amekaa.Alikuwa na furaha ya ajabu,furaha ya ushindi wa kumpata kimwana yule ambaye uzuri wake uliyafanya mapigo ya moyo wake yaende mbio.
“ Peniela ahsante sana kwa kunikubalia ombi langu,Huwezi kujua ni furaha kiasi gani niliyonayo moyoni mwangu kwa kunikubalia kuwa mpenzi wako.Ninajiona ni mwanaume mwenye bahati sana kukupata mwanamke mrembo kama wewe.Nakuahidi kwamba sintakuletea matatizo yoyote yale na badala yake nitafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha bora zaidi kuliko yale ya awali .Nitakufanyia mambo makubwa ambayo hukuwahi kuyafikiria,I’ll make you a queen.Peniela sisiti kufanya jambo lolote lile kwa ajili yako na usisite kuniambia chochote kile unachokihitaji na nitakufanyia.Ila kuna jambo nataka unihakkishie”
“ Jambo gani Dr Kigomba?
“Ninataka unihakikishie kwamba ni kweli hauna mahusiano na mwanaume mwingine yeyote yule? Kama unaye naomba uniambie ili nijue kwamba nina ingia katika mahusiano na mtu ambaye ana mahusiano na mwanaume mwingine.Mimi pia ni mume wa mtu na nimekuweka wazi kuhusu suala hili na hata pete ya ndoa hii hapa sijaitoa kwa hiyo naomba na wewe uwe wazi kwangu kama kuna mtu ana mahusiano na wewe hata kama ni mume wa mtu nitaelewa.”akasema Dr Kigomba
“ Dr kigomba kwa nini unasisitiza kutaka kufahamu jambo hilo la mahusiano ? Nimekwisha kwambia kwamba sina mahusiano na mtu yeyote yule.Au huniamini?” Akasema peniela
“peniela usinielwe vibaya kusisitiza kulifahamu jambo hili kwa sababu unajua tunaingia katika mahusiano kwa hiyo lazima tufahamiane vizuri.Nitahitaji kuja nyumbani kwako mara kwa mara kwa hiyo sihitaji kukusabishia matatizo ya aina yoyote ile kama una mpenzi wako nahata mimi sihitaji kujisababishia matatizo yoyote.Kwa hiyo ninataka unithibitishie kwamba ni kweli hauna mchumba na uko peke yako”
“Niko peke yangu.Thats all I can say” akasemaPeniela
“ Nashukuru kwa kunihakikishia hilo” akasema Dr Kigomba huku akiendelea kumuangalia Peniela kwa matamanio.Peniela akaligundua hilo naye akajilegeza .Dr Kigomba akamsogelea karibu zaidi
“ Peniela unataka nikufanyie kitu gani? Akauliza kwa sauti ya taratibu halafu akaupitisha mkono wake shingoni mwa Peniela ambaye hakuonyesha kustuka wala kuuondoa.Kigomba akafurahi sana moyoni kwani alichokuwa akikitaka sasa anakaribia kukipata
“ Tell me Peniela unahitaji kitu gani nikufanyie? Akauliza Dr Kigomba na kuusogeza mdomo wake karibu na mdomo wa Peniela.Taratibu Peniela akauinua mkono wake na kuupeleka maeneo nyeti ya Dr Kigomba na kusababisha mvurugano eneo hilo.
“ I want this.I miss this so much”akasema Peniela kwa sauti laini huku akiishika ikulu na kumfanya Dr Kigomba azidi kuchanganyikiwa.Peniela hakutaka kupoteza muda akaanza manjonjo yake .Dr Kigomba naye hakutaka kubaki nyuma naye akaaka kuonyesha umahiri wake katika sekta hii naye akaanza manjonjo yake.Baada ya dakika kumi hali ikazidi kuwa mbaya Dr Kigomba akamuinua peniela na kumpeleka kitandani na bila kuchelewa mchaka mchaka ukaanza.Ulikuwa ni mtanange mkali kwani kila mmoja akitaka kumuonyesha mwenzake ujuzi wake.Mpaka wanamaliza mzunguko mmoja Dr Kigomba alikuwa hoi akihema kwa kasi.Mchaka mchaka aliokimbizwa na peniela haukuwa mdogo.
“ peniela nimekuvulia kofia.Sijawahi kukutana na mjuzi kama wewe katika haya mambo.Nilikuwa sahihi kukutaka mtu kama wewe kwani ndiye unayenifaa.Umenionyesha vitu adimu ambavyo sijawahi kuonyeshwa.Ahsante sana peniela .Sema chochote ukitakacho nami nitakusikiliza na kukitekeleza” akasema Dr Kigomba huku jasho likiendelea kumtiririka.Peniela akatabasamu
“ Nilijua tu,lazima atachanganyikiwa .Mpaka hapa nadhani kazi yangu imekamilika.Nimeuvaa uhusika vizuri na tayari Kigomba ameingia mfukoni.” Akawaza peniela huku akimuangalia Kigomba na kutabasamu
“ Kigomba hata mimi ninashukuru sana kwa raha ulizonipa .Umenipeleka mbio sana.Ngoma hii unajua kuicheza vizuri.”akasema Peniela
“ peniela I’m serious,niambie chochote unachokitaka nikufanyie ili niwe na uhakika kwamba nitakuwa nawe siku zote.Hata ukisema nimuache mke wangu kwa ajili ya kuwa nawe niko tayari” akasema dr Kigomba.Peniela hakujibu kitu akatabasamu
“ Say something Peniela.Neno lako ni amri kwangu” akasema Kigomba
“ Kigomba ninachokihitaji toka kwako ni hiki ulichonifanyia leo.Hicho ndicho ninachokihitaji zaidi kwani ndicho nilichokikosa zaidi’ akasema peniela na Kigomba akamvuta kwake akamkumbatia na kumbusu.
“ Peniela nitakufanyia mambo makubwa sana.naomba uniamini’ akasema Dr Kigomba
“ Ninakuamini Dr Kigomba.Nisigeweza kuuachia mwili wangu kama sikuamini.”akasema Peniela.
“Ahsante sana peniela kwa kuniamini.Usiku wa leo umekuwa ni wa kipekee sana kwangu.”
“ Hata mimi pia usiku huu umekuwa mzuri na umenikutanisha na mtu mkubwa sana katika nchi hii.Nafurahi kukutana nawe.Nadhani sasa baada ya kufahamiana na kuufungua ukurasa wetu mpya basi niruhusu niondoke na tutapanga tena siku na mahali pa kukutana.”
“ peniela kwa nini tusilale leo hapa hapa hotelini? Bado nina hamu sana na wewe’
“ Hapana Dr Kgomba kwa leo haitawezekana kwa sababu sikuwa nimejiandaa kwa kuja kulala.Nina hakika hata wewe pia hukuwa umejiandaa kama leo hii utakuja kulala hapa kwani hukujua kama ningeweza kukukubalia ombi lako.Go back to your wife.Tutapanga siku nyingine ya kukutana na tutakesha usiku mzima nikikuonyesha vitu ambavyo hujawahi kuviona.Next time nataka tukutane kwangu na utakuwa wangu kwa usiku mzima” akasema peniela
“ Natamani sana siku hiyo ifike haraka peniela”akasema Dr Kigomba
“ Vipi kuhusu kesho unaweza kupata nafasi ?
“ Siwezi kukosa nafasi kwa ajili yako Peniela.Niko tayari kuahirisha kila kitu kwa sababau yako”
‘ basi usijali jiandae kwa usiku wa kesho.I’ll be yours for the whole night” Akasema peniela na kumbusu Dr Kigomba halafu akainuka na kwenda kuvaa nguo zake na kisha akamuaga Dr Kigomba akaondoka.
“ Dr Kigomba amechanganyikiwa kabisa mzee wa watu hadi ananitamkia kwamba yuko tayari kumuacha mkewe kwa ajili yangu.Hivi mimi nina kitu gani ambacho kila mwanaume ninayetembea naye ananing’ang’ania na hataki tena kuachana na mimi? akajiuliza Peniela akiwasha gari lake na kuondoka pale hotelini
“ Yawezekana labda kuna kitu nimebarikiwa nacho kinachowachanganya sana hawa wanaume.Hata hivyo ninashukuru mpango wangu umekwenda vizuri sana kama nilivyokuwa nataka.Dr Joshua ,Dr Kigomba wote katika mifuko yangu kwa hiyo kilichobaki hapa ni kuimaliza kazi yangu.Lakini kabla ya yote natakiwa usiku huu nikaonane na Elibariki na Jason.Ngoja kwanza nimpigie simu Mathew” akawaza Peniela na kuchukua simu akampigia Mathew
“ hallow Peniela,habari yako?
“ habari nzuri Mathew.”
“Peniela uko wapi mbona hutokei? Mathew na Jason wanakusubiri mpaka wamekata tamaa kwamba hutakuja tena” akasema Mathew
“ Niko njiani ninakuja nilikuwa na udhuru kidogo.Are they ok? Akauliza Peniela
“ Una maanisha nini kwa swali hilo Peniela? Akauliza Mathew
“ Nina maanisha hawana matatizo yoyote,je wanaongea ?
“ Hawana tatizo lolote na wanaongea vizuri.Ni marafiki wakubwa hawa “ akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.Niko njiani ninakuja naomba mnisuburi” akasema peniela na kukata simu
“ Ahsnate Mungu kwa Elbariki na jason kupatana.Sasa mipango yangu itakwenda vizuri kama ninavyotaka.Elibariki na Jason ninawahitaji sana katika jambo hili.Halafu kuna kitu nimekuwa nikijiuliza sana bila kupata jibu huyu Mathew ni nani ? Anafanya kazi gani? Kwa nini Elibariki na Jason wanamuheshimu sana ? Nitamuuliza Elibariki anifahamishe kuhusiana Mathew pengine naye anaweza akawa ni mtu wa msaada kwangu katika jambo hili” akawaza Penny
“ natamani sana kujua kama John anaendeleaje lakini kwa namna akivyoniudhi sitaki hata kumsikia.Ngoja kwanza nimalize suala hili la operesheni 26B halafu nitaangalia pengine ninaweza kumsaidia na pengin…………….” Peniela akastuliwa mawazoni na mlio wa simu yake.Alikuwa ni captain amos
“ Halow Amos” akasema Perniela baada ya kupokea simu
“ Peniela good Job.Kigomba amenipigia simu na kunieleza namna alivyochanganyikiwa kwako.Amekiri kwamba hata ile kazi aliyopewa na Dr Joshua ya kukuchunguza haitaki tena yeye anachotaka ni kuwa na wewe tu.Huu ni wakati wetu Peniela wa kuimaliza operesheni 26 B.Endelea kumchanganya Kigomba na nitakuwa nikikufahamisha kila kinachoendelea.” Akasema Captain Amos
“ Usijali Amos.Kigomba tayari nimemuweka mfukoni na ninachosubiri ni kuikamilisha tu operesheni yetu.” akasema Peniela
“ Nitakufahamisha pindi rais atakapomkabidhi Dr Kigomba ule mzigo” akasema Amos na kukata simu.Akaelekea moja kwa moja nyumbani kwake akaoga na kubadili mavazi halafu akaelekea nyumbani kwa Mathew
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………..
AsanteSEASON 2
SEHEMU YA 32
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mtaona hapa kwamba Elibariki ni mtu sahihi kwa sababu kwanza hana kundi lolote katika chama na pili hana kashfa yoyote,na vile vile kitendo atakachokuwa amekifanya cha kufichua maovu ya Dr Joshua kitamuweka katika nafasi nzuri kuchaguliwa kwani kumg’oa rais madarakani si kitu chepesi.Sifa nyingine Elibariki bado kijana na ana nguvu za kutosha kwa hiyo atapata uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa vijana.Ndugu zangu chama kinahitaji mageuzi makubwa na mageuzi haya yataanzia kwa kumuweka madarakani rais kijana kama Elibariki.Najua kila mmoja wenu akilitafakari suala hili kwa makini sana atakiona kile ninachomaanisha.” Akasema Mzee Deus na kikao kikaendelea hadi usiku mwingi na kisha wakatawanyika kwa makubaliano ya kukutana tena siku nyingine kulijadili kwa upana wake suala lile alilolipendekeza mzee Deus.
ENDELEA……………….
Peniela aliwasili nyumbani kwa Mathew,mlinzi akampigia sImu Mathew na kumfahamisha kwamba peniela amewasili akamruhusu amfungulie geti aingie ndani.
“ Its hard to do this but I hve to.lazima niwaeleze ukweli akina Elibariki.Bila kufanya hivyo sintaweza kabisa kujitoa katika team SC41 na maisha yangu hayataweza kamwe kubadilika” akawaza Peniela na kushuka garini akaelekea mlangoni akabonyeza kengele .Katika chumba cha kazi kilichokuwa na mitambo na luninga kubwa tatu ukutani,Mathew na Anitha walikuwa walimkagua Peniela kupitia katika kifaa kilichofungwa pale mlangoniili kukagua kama ana silaha amakitu chochote kinachoweza kuwa kinarusha mawasiliano na kuyapeleka sehemu nyingine.
“ She’s clean” akasema Anitha baada ya kuridhika kwamba Peniela hakuwa na silaha walakitu chochote cha kurusha mawasilianokupeleka sehemu nyingine. Mathew akatoka na kwenda mlangoni kumlaki Peniela
“ karibu Peniela” akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew. Samahani kwa kuwasumbua usiku huu” akasema Peniela
“ usijali P eniela ,unakaribishwa muda wote.katika nyumba hii watu hawalali “ akasema Mathew na kumkaribisha Peniela sebuleni walikokuwa wamekaa jaji Elibariki na Jason.Mtu wa kwanza kusalimiana naye alikuwa ni jaji Elibariki ambaye alimfuata na kumbusu halafu akamsalimu na Jason kwa kumpa mkono kisha akaketi kitini
“ Samahani sana kwa kuwaweka hadi mida hii.Nilikuwa na shughuli moja ya muhimu sana iliyonichelewesha ” akasema Peniela
“Usijali Peniela,hata kama ungekuja asubuhi lazima tungekusubiri tu” akasema jaji Elibariki na wote wakacheka.
“ Ok.Mmeshindaje toka muda ule nilipowaacha? Are you ok now? Akauliza Peniela ambaye uso na sauti yake vilionyesha kwamba hakuwa akihitaji mzaha wowote
“ We’re good.Tuko sawa.Tumeongea na tumeyamaliza yale mambo” akasema Jason
“ Good..I’m so happy for that.You are real men” akasema Peniela na mara akatokea Anitha wakasalimiana.
“ Peniela unatumia kinywaji gani? Akauliza Anitha
“ Ahsante sana Anitha,naomba kama una whsky yoyote tafadhali” akasema Peniela Anitha akaenda kumletea mvinyo ,akanywa funda kubwa.Watu wote pale sebuleni walikuwa kimya wakisubiri kusikia Peniela anataka kuwaambia kitu gani
“ Ninashukuru kwamba ninyi nyote mko hapa .Nilikuwa nawahitaji sana nyote muwepo ili tuongee jambo moja muhimu sana” akaanzisha mazungumzo Peniela bila kupoteza wakati
“ Kwanza kabisa ninakushukuru Mathew kwa kunikaribisha hapa kwako .Ninashukuru vile vile kwa kuendelea kuhakikisha usalama wa Elibariki”akanyamaza na kunywa funda moja la mvinyo
“ Nina mambo mengi sana ambayo ningependa kuwaeleza usiku huu lakini kutokana na muda nitawaeleza mambo mawili au matatu makubwa ya muhimu kwa sasa.” Akanyamaza tena akawaangalia akina Mathew kisha akaendelea
“ Nadhani nyote mnafahamu kuhusiana na kesi ya mauaji iliyokuwa ikinikabili.Ninawashukuru sana Jason wakili wangu na jaji Elibariki kwa kunipigania na hatimaye nikawa huru.Baada ya kesi ile kumalizika jaji Elibariki na Jason walitaka kwenda ndani zaidi kulichimba suala lile na kumfahamu muuaji.Leo hii naomba niwaeleze ukweli kwamba sikutaka jambo lile lifanyike kwani tayari nilikuwa nikimfahamu muuaji.”akasema Peniela na wote mle ndani wakastushwa na kauli ile isipokuwa Mathew
“ Ulifahamu aliyemuua Edfson? Akauliza Jason
“ ndiyo nilifahamu mtu aliyemuua Edson na sikutaka kufumbua mdomo wangu kusema .Niliogopa ningeuawa kwani ni mtu mzito na mwenye nguvu” akasema Peniela
“ Who is that? Akauliza Jason.Peniela akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Ni mheshimiwa rais”
Kimya kifupi kikapita mle ndani na baada ya sekunde kadhaa akasema
“ Ulijuaje kama rais ndiye aliyemuua Edson? Akauliza jaji Elibariki
“ Nimekuja hapa kuwaelezeni ukweli wa kila kitu kwa hiyo msihofu nitawaeleza kila kitu kilivyo.”akasema na kukaa kimya kidogo akaendelea
“ Kabla sijaingia katika mahusiano ya kimapenzi na Edson ,tayari alikuwa katika mahusiano na mtoto wa rais aitwaye Anna na wakati huo mimi nilikuwa na mahusiano ya siri na mheshimiwa rais” akasema Peniela.Uso wa jaji Elibariki ukabadilika.Hakuwa ametegemea kusikia jambo kama lile.
“ Unasema ulikuwa na mahusiano na nani? Akauliza jaji Elibariki
“ Tafadhali usihamaki Elibariki utafahamu kila kitu hatua kwa hatua.Usikuhuu ni usiku utakaojaa ukwelimtupu wa kila jambo.Nilikuwa katika mahusiano na rais Dr Joshua na mpaka sasa bado niko katika mahusiano naye “
“ Shetan…..” jaji Elibariki alipandwana hasira za ghafla akainuka na kutaka kumfuata Peniela lakini Mathew akawahikumdaka akamzuia
“ Elibariki please calm down.Msikilize kwanza Peniela anataka kutueleza jambo gani.Tafadhali naomba usihamaki “akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.Nafahamu umekasirika kwa sababu unanipenda,lakini naomba utulie na usikie kila kitu ninachotaka kuwaeleza” akasema Peniela
“ Endelea peniela” akasema Mathew
“ Wakati nikiwa katika mahusiano na mheshimiwa rais, siku moja alinialika katika sherehe moja kubwa iliyokuwa ikifanyika ikulu .Katika sherehe hiyo ndipo nilipokutana na Edson na urafiki wetu ukaanzia hapo na baadae tukawa wapenzi.Dr Joshau aligundua kuhusu mahusiano yangu na Edson na alikasirika sana na kupanga mpango ule wa kumuua Edson na mimi nikabebeshwa mzigo ule wa kesi, lengo lake likiwa ni kuniangamiza kabisa.Japo nilimfahamu muuaji lakini sikuthubutu kufumbua mdomo wangu kusema chochote kwa sababu endapo ningethubutu kufanya hivyo basi ningeuawa mara moja ”akasema Peniela na kukaa kimya kidogo huku Elibariki akiendelea kumuangalia kwa macho makali ya hasira
“ Ilitokeaje wewe na rais mkaingia katika mahusiano ya kimapenzi? akauliza Anitha
“ Ni hadithi ndefu kidogo ila nitawaeleza hilo baadae lakini kwa sasa naomba mniruhusu niwaeleze kile nilichokusudia kuwaeleza usiku huu ” akasema Peniela akawaangalia watu wote mle sebuleni na wote walikuwa kimya wakimtazama,akaendelea .
“ baada ya kesi ile iliyokuwa ikinikabili kumalizika na mahakama kuniachia huru,Jaji Elibariki na Jason waliamua kuanzisha uchunguzi ili kulichimba zaidi suala lile na kufahamu nani aliyemuua Edson kwani wote waliamini mimi si muuaji.Niliogopa kwa wao kujiingiza katika suala hili kwani Endapo wangelichimba jambo hili kwa ndani wangeweza kugundua kwamba rais ana mkono wake katika mauaji yale na wangekuwa katika hatari kubwa kwani ninamfahamu vizuri Dr Joshua .Elibariina Jason ni watu wangu wa karibu na wa muhimu sana.Wote wana nafasi kubwa sana ndani ya moyo wangu na katika maisha yangu kwa ujumla kwa hiyo sikuwa tayari kuwaona wakiingia katika matatizo makubwa na kuhatarisha maisha yao.Niliogopa kuwaeleza ukweli wa jambo hilo na kwa hiyo nikatafuta njia ya kuweza kuwavuruga wasiendelee na mpango wao na nikaamua kuwagombanisha.Wenyewe wanafahamu kitu kilichotokea na wakavurugana..Mtanisamehe sana Elibariki na Jason kwa nilichokifanya hadi mkagombana ,lakinisikuwa na njia nyingine ya kuweza kuwazuia msiendelee na mpango ule wa kulichimba kiundani suala la lile la mauaji ya Edson.” Akasema peniela .Elibariki alimuangalia Peniela kwa jicho kali.
“ Sikuwahi kuhisi kama Peniela anaweza kuwa namna hii.Dah ! ama kweli umdhaniaye siye,ndiye.Nilikuwa tayari kufanya kila linalowezekana iliniwe naye lakinikmbenilikuwa najiingiza katika mdomo wa joka kubwa bila kujua.Nilidanganywa na uzir wake wa nje lakini kumbe ndani hana hata chembe ya ubinadamu.Siku ile Jason aliponipiga na chupa kichwani ningeweza hata kupoteza maisha kumbe yote ilisababishwa na Peniela.”akawaza jaji Elibariki akiendela kumuangalia Peniela kwa chuki
“ Ulimuuliza Dr Joshua sababu ya kumuua Edson? Akauliza Mathew
“ Nilimuuliza na akaniambia kwamba alifikia maamuzi yake kutokana na mimi kumsaliti kwa kuanzisha mahusiano na Edson kwa hiyo alitaka wote wakose na mimi nikaozee gerezani na ndiyo maana nikabebeshwa mzigo wa ile kesi kubwa” akasema Peniela.Mathew akamtazama na kusema
“ Alikudanganya”
“ alinidanganya? Peniela akashangaa
“ Ndiyo.dr Joshua alikudanganya kuhusu sabau ya kumuua Edson”
“ Unajuaje kama alinidanganya? Akauliza Peniela
“Tayari tunafahamu kila kitu kuhusiana na kifo cha Edson na ninisababuya yeye kuuawa.”
“ You know? Peniela akazidi kushanga
“ How do you know? Who are you Mathew? Akauliza Peniela
“ Nadhani Elibariki ndiye anayeweza kukueleza kila kitu kuhusiana na mimi.Elibariki please tell Peniela everything’ akasema Mathew.Jaji Elibariki akamtazama Peniela na kusema
“ Kutokana na mambo mengi yasiyo ya kawaida niliyoyaona wakati wa usikilizwaji wa kesi iliyokuwa ikikukabili ,niliazimia kwamba lazima nilifanyie uchunguzi wa kina suala hili na nifahamu ukweli wake.Nilimshirikisha Jason wazo langu na kwa pamoja tukakubaliana kulifanyia uchunguzi suala hili.kwa kuwa sisi wawili hatuna ujuzi wowote wa kufanya mambo haya ya uchunguzi na sikutaka kulichunguza jambo hili kwa kutumia jeshi la polisi nililazimika kutafuta mtu ambaye ana ujuzi na uzoefu wa kutosha wa mambo haya na ndipo nilipomfuata Mathew na kumuomba msaada wake katika jambo hili.Mathew ni mzoefu wa siku nyingi katika kazi hizi,amekwisha fanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa na kwa sasa anafanya kazi zake binafsi” akasema jaji Elibariki na kuendelea
“ Mathew aliwaita wenzake wamsaidie kuifanya kazi hii na mmoja wao ni huyu hapa Anitha na Noah aliyepoteza maisha wakati akiniokoa katika lile shambulio . Kitendo cha Peniela kunivuruga mimi na Jason kwa kutugombanisha hakikuathiri chochote kuhusu mpango wetu wa kulichunguza sualahili ,kwahio Mathew na wenzakewaliendelea na uchunguzi wao.Ni hayo tu ninayoweza kusema kuhusiana na Mathew na kuhusu namna walivyochunguza atakueleza yeye mwenyewe” akasema Elibariki akionekana kuishiwa kabisa maneno ya kusema
“ Peniela nadhani sasa umenifahamu mimi ni nani na kazi yangu ni nini.” Akasema Mathew na Peniela akatingisha kichwa kukubaliana naye,Mathew akaendelea
“ Tumelichungza suala hili na tumegundua kwamba Edson aliuawa kwa amri ya rais lakini kilichopeleka auawe si kwa sababu ya wewe kuingia katika mahusiano naye bali ni kwa sababu nyingine kabisa.Tumegundua kwamba Edson alikuwa akishirikiana na watu Fulani ambao walimtumia katika kuiba nyaraka za siri Ikulu.Nyaraka hizo walipanga waziuze kwa mabilioni ya fedha.Kwa bahati mbaya yeye na watu wote aliokuwa akishirikiana nao wote wamekwisha fariki kwa sababu ya nyaraka hizo na kwa bahati nzuri nyaraka hizo tumezipata na kwa sasa tunazifanyia uchunguzi wa kina kuzifahamu zinahusianana na nini kwani zimeandikwa kwa lugha ya kisayansi na sisi hatuelewi ni kitu gani kilichoandikwamo.Nadhani sasa umeelewa sababu iliyopelekea kifocha Edson.” Akasema Mathew.Peniela alionekana kustushwa sana na taarifa ile.
“ sikuwa nikilifahamu jambohilohilo .Niliaminimanenoaliyoniambia Dr Joshua .Nashukuru kwa kunifahamisha ukweli.’ akasema Peniela.
“ Dr Joshua asingeweza kukueleza ukweli kwa sababu inaonekana nyaraka hizo zina kitu kikubwa sana ndani yake na ndiyo maana wote waliozishika wamepoteza maisha.” akasema Elibariki
Peniela akainama chini akaonekana kujawa na mawazo
“ Ilikuaje hadi ukaanzisha mahusiano na mheshimiwa rais?akauliza Mathew
“ Ni hadithi ndefu kidogo lakini nitawaeleza ukweli wa kila kitu kinachoendelea kwani nina hakika hata ninyi mpaka mmefikia hatua ya kufahamu kuhusiana na jambo hili basi mtakuwa mmekwisha fahamu mambo mengi”akasema Peniela.Akakaa kimyakidogona kuendelea
“ Mimi ni Team SC41.Sina hakika kama mnafahamu au mmekwisha sikia kuhusu Team SC41 “ akasema Peniela na kuzidi kuwachanga Elibariki na Jason ambao hawakuwa wakifahamu chochote kuhusiana na Team SC41.
“ we already know what team SC41 is” akasema Mathew
“ You know? Peniela akashangaa
“ Peniela we don’t know anthything.Kama Mathew anafahamu kuhusu hiyo team unayoisema ni yeye mwenyewe lakini sisi hatufahamu chochote kuhusianana hiyo team ” akasema jaji Elibariki
“ I’m sorry guys ,sikuwahi kuwaeleza chochote kwamba katika uchunguzi wetu tuligundua uwapo wa team SC41 lakini hakukuwa na ulazima wa kuwaeleza kwa sababu kikundi hiki hakikuhusika na kifo cha Edson ”akasema Mathew
“ Ulipaswa kutuweka wazi kuhusu kila kitu Elibariki. Kwa hiyo team SC41 ni akina nani? shughuli zao ni nini? Akauliza Elibariki.
“ Team SC41 ni kikundi cha siri kinachofanya kazi zake kwa siri hapa nchini na katika ukanda wa afrika mashariki.Kikundi hiki kilianzishwa kwa siri na serikali ya marekani kwa ajili ya kulinda maslahi yake katika ukanda huu wa afrika ya mashariki.Kazi kubwa ya kikundi hiki ni kuhakikisha kwamba maslahi ya Marekani yanalindwa na yanakuwa salama.Serikali ya Marekani imefanya uwekezaji mkubwa katika eneo la afrika mashariki kwa hiyo wameweka kikundi hiki makusudi ili kiwe ni kama jicho la kuhakikisha kwamba hakuna hatari yoyote katika uwekezaji wao.Team SC41 imekita mizizi yake ndani ya serikali na wanafahamu kila kinachoendelea ndani ya serikali na endapo kuna mpango wowote wa kuhujumu maslahi ya marekani basi watafahamu mara moja.Mimi ni mmoja wao japokuwa kazi yangu mimi ni tofauti na wengine.Kazi yangu mimi ni kutafuta taarifa Fulani toka kwa mtu.Endapo kuna mtu ambaye team SC41 wanahitaji kitu Fulani toka kwake basi hunitumia mimi.Hujenga mahusiano na mtu huyo na kisha huhakikisha kwamba nimekipata kitu hicho au taarifa hiyo inayotakiwa.” akasema Peniela
“ Kuingia katika mahusiano na Dr Joshua ulikuwa ni mpango wa team yako au ulipenda mwenyewe? Ama kuna kitu ulikuwa unakitafuta? Akauliza jaji Elibariki ambaye alionekana kuwa mkali sana.
“ Ulikuwa ni mpango wa TeamSC41 wala haikuwa ni kwa mapenzi yangu.Kuna kitu walikuwa wanakihitaji toka kwake na ndiyo maana wakanitumia mimikuanzishamahusiano naye” Akasema Peniela
“ Ni kitu gani mnachokitafuta kwa Dr Joshua? Akauliza Mathew
“ Package E21” akajibu Peniela
“ Package E 21?.Ni kitu gani hicho? Akauliza Mathew
“ Hata mimi sifahamu ni kitu gani na hakuna aliyewahi kunieleza package hiyo ina nini lakini inaonekana ni kitu chenye thamani kubwa kwa sababu Package hiyo inafichwa ikulu na hata hapo ikulu kwenyewe anayefahamu mahala ilipo ni rais peke yake .Dr Joshua anataka kuiuza package hiyo kwa matrilioniya fedha.Dr Flora mke wa rais aligundua kuhusu jambo analotaka kulifanya mume wake na alijitajhidi sana kumsihi mume wake asiiuze package hiyo lakini bila mafanikio na ndipo alipoamua kuwaeleza wanae kile anachotaka kukifanya baba yao na mchana wa siku ambayo alipanga kuonana na wanae jioni ili awaeleze anachokifanya baba yao akafariki dunia.Aliuawa ili asiweze kutoa siri”
“ What ?! Dr Flora aliuawa kwa sababu ya hiyo Package? Akashangaa jaji Elibariki.
“ Ndiyo.Dr Flora aliuawa ili asiweze kutoa siri hiyo.”akasema Peniela.Kila mtu alikuwa kimya pale sebuleni.
“ Una uhakika gani kwamba Dr Flora aliuawa ili asiweze kutoa siri? Akauliza Mathew
“ katika biashara ya package hiyo Dr Joshua anashirikiana na watu wengine wawili.Katibu wake Dr Kigomba na daktari wa familia ya rais anaitwa Captain Amos.Hawa ndio wanaofahamu kila kitu kuhusianana biashara nzima ya package hiyo.Captain Amos naye yuko team SC41 na ndiye anayetupa taarifa zote kuhusiana na kila kinachoendelea ikulu.Captain Amos ndiye aliyemchoma sindano ya sumu Dr Flora kwa amri ya rais.” Akasema Peniela
“Mawazo yangu yalikuwa sawa kabisa kwamba Dr Flora aliuawa.Nilitegemea tu kwamba lazima kifo chake kitakuwa kimesbabishwa na jambo kubwa na kama anavyosema Peniela nikwamba aligundua kuhusiana na hiyo package anayotaka kuiuza Dr Joshua na ndipo alipouawa.Package hiyoni ya nini? Inamahusiano yoyote na hizi nyaraka alizoziiba Edson? Mhh! Mambo haya yanazidi kuwa magumu.” Akawaza Mathew.
Jaji Elibariki alikuwa ameinama amekishika kichwa chake
“ Ouh Mungu wangu ! akasema Elibariki halafu akainua kichwa akasema
“Mathew tulikuwa sahihi kabisa kuhisi kwamba Dr Joshua atakuwa akihusika na kifo cha mkewe na ndiyo maana nguvu kubwa ikatumika kuhakikisha sababu ya kifo cha Dr flora haijulikani.Kumbe tulipompelekea ile taarifa yetu ya uchunguzi iliyobainishakwamba dr Flora aliuawa kwa sumu tulikuwa tunajipalia makaa ”akasema Elibariki na kumstua peniela
“ Mlifahamu kilichomuua Dr Flora? Akauliza Peniela
“Ndiyo tulifahamu kila kitu.”akasema Mathew
“ Badaa ya kifo cha Dr Flora ilitolewa taarifa kwamba mwili wake usifanyiwe uchunguzi wowote kubainisababuya kifo chake na badala yake ikatolewasababu ya jumla kwamba kilichomuua ni shinikizo la damu. Mke wa Elibariki aliingiwa na hofu kuhusu kifocha mama yake namazingira kilivyotokea hivyo akamuomba mume wake amsaidie kuweza kuufahamu ukweli.Elibariki likuja kwangu akaniomba nimsaidie kufanya uchunguzi wa kubaini kilichomuua Dr Florana nusura tungepoteze maisha yetu wakati wa kufanya uchunguzi huo lakini mwishowe tuliubaini ukweli .Tuligundua hadi aina ya sumu iliyomuua Dr Flora .Baada ya hapo Elibariki alimpelekea mheshmwia rais majibu yale ili ayafanyie kazi bila ya kufahamu kwamba ni yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya yale mauaji”akasema Mathew
“I’m impressed with you guys.Namna mnavyofanya kazi zenu mmenifurahisha sana” akasema Peniela
“ Baada ya Dr Joshua kugundua kwamba tayari Elibariki amegundua kilichosababisha kifo cha dr Flora aliamuru auawe na ndipo lilipopangwa lile shambulio ambalo alinusurika kuuawa”akasemaMathew.Jaji Elibariki naye akasema
“ Katika shambulio lile alitokea mwanamke mmoja na kunichukua toka eneo la tukio na akanikabidhi kwako.Mpaka leo sijamfahamu mwanamke yule ni nani na kwa nini aliniokoa.Hakutak……”kabla Elibariihajaendelea Penielaakaingilia kati
“That’s Jessica.Naye ni team SC41.Alipewa maagizo ya kukuokoa na Amos .”akasema Peniela.
“ Dah ! nimechoka kwa kweli.Hawa team SC41 wako kila mahala ,but why they saved me? Akauliza Elibariki.Kabla Peniela hajajibu kitu Mathew akauliza
“ John mwaulaya anaendeleaje?
Swalilile lilimstua mno Peniela.Hakuwa ametegemea kama Mathew anamfahamu John
“ Umesema John mwaulaya? Akauliza peniela
“ Ndiyo.John Mwaulaya.is he ok? Akauliza Mathew
“ Do you know him?
“ yes I know him” akasema Mathew
“ John mwaulaya ni nani? Akauliza jaji elibariki
“ Ni kiongozi wa team SC41”akajibu mathew
“ Unafahamiana na kiongozi wa team SC41? akauliza Elibariki kwa mshangao
“ Ndiyo ninamfahamu.Japokuwa si marafiki lakini mimi na yeye tun historia .Nitawaeleza siku nyingine ninamfahamuje John mwaulaya lakini usiku huu ni usiku wa peniela ,ametueleza mambo makubwa kabisa na kutufunulia mambo mengi mazito.Peniela endelea kutueleza kile ulichokusudia kutueleza” akasema Mathew,Penielaakaendelea
“ baada ya kunusurika katika ajali ile ,Elbariki alikuja nyumbani kwangu kwani aliamini ni sehemu salama.Ni kweli ni sehemu salama na alikuwa salama hadi pale Jason alipokwenda kutoa taarifa polisi kwamba Elibariki yuko kwangu.Taarifa zile zilimfikia Amos naye akamtaarifu kiongozi wangu John mwaulaya aliyeamuru Jason akamatwe na aeleze kwa nini alitoa taarifa zile kwa jeshi la polisi.Alikuwa na wasi wasi kwamba yawezekana Jason akawa anafahamu mambo mengi kuhusu team SC41.Walimteka Jason na kumtesa na ndipo alipopata nafasi ya kunipigia simu na kunifahamisha kwamba ametekwa.Nilichukizwa mno na kitendo kile cha kuwateka na kuwatesa watu wangu wa karibu na hiyo ndiyo sababu niko hapa nikiwaeleza haya yote niliyowaeleza ambayo sikupaswa kuwaelezakitendo kile na hii ndiyo sababu niko hapa kwenu mida hii nikiwaeleza haya yote niliyowaeleza na nikihitaji msaada wenu.” akasema Peniela akaak kimya kidogona kusema tena
“ I need your help guys”
“Our help? Akauliza Mathew
“ yes. Your help.”
“ Unahitaji msaada gani? Akauliza Mathew
“ To take down Team SC41”
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
PamojaPENIELA SEASON 3
SEHEMUYA 16
ILIPOISHA SEHEMUILIYOPITA
“ Nitakuwa nikikufahamisha kila kitu kuhusiana na kinachoendelea lakini kuna jambo nitaomba ulifanyie uchunguzi.Ninataka unisaidie kufanya utafiti Rosema Mkozumi yuko wapi ? Idara yenu ya usalama wa taifa mnazo nyenzo za kuweza kupata taarifa mapema sana kwa hiyo nisaidie kufahamu mahala aliko Rosemary .Can you do that for me? Akauliza Vincent
“ Niachie suala hilo nitalifanyia kazi .Nitafuatilia ofisini ili nione kama kuna taarifa zozote zimepatikana kuhusu mahala alipo Rose.” akasema Jesica
“ Ahsante sana Jesica.Lifanyie kazi sualahlo kwani nina wasiwasi sana na kutoweka huku kwa kutatanisha kwa Rose .Yule ni mtu anayetufahamu sana sisi na anayafahamumamboyetu mengi kamasisi tunavyoyafahamu yak wake “: akasema Vincent akaagana na Jesica.
“ Sasa kidogo ninaweza kuvuta pumzi baada ya kuwa na uhakika Amos ametoweka.Huyu alikuwa ni mtu muhimu mno kwa Deus na ndiye alikuwa anamtegemea sana katika mpango wake.Kwa sasa mipango yake haitaweza kufanikiwa tena na ni nafasi yetu kumuandaa mtu wetu ambaye atatusaidia sana endapoatashika madaraka “ akawaza Vincent.
ENDELEA……………………
Mathew akaingIa chumbani kwake akalifungua kabati ambao huhifadhi baadhiya vifaa vyake mbalimbaLi.Akachukua sanduku moja la kijani pamoja na vifaa kadhaa akatoka mle chumbani na kuelekea katika chumba alimolazwa Rosemary Mkozumi.Akakinyonga kitasa na kuingia ndani.Rosemary alipomuona akainuka na kukaa kitandani.Alikuwa na hasira kali sana “ Who are you? Kwan in umeniweka humu? Nani kakutuma ufanye hivi? Akauliza kwa ukali Rosemary.Mathew hakumjibu kitu akaviweka vifaa vyake mezani akavuta kiti na kuketi akamtazama Rosemary kwa sekudne kadhaa kisha akasema
“ Hello Rosemary! “ Sina haja ya salamu yako.Tafadhali kijana naomba usijitafutie matatizo zaidi.Mpaka sasa tayari umekwishajiingiza katika matatizo makubwa.Umemuua Henry na kama vile haitoshi umeniteka na kunifungia humu chumbani.Unadiriki kumteka nyara mke wa rais? Umelipwa shilingi ngapikijana wangu hata ukakubali kujihatarisha namna hii? Tafadhali naomba uniachie huru haraka sana na nitaangalia namna ya kukusamehe na kukusaidia kukutoa katika janga hili ulilojitumbukiza bila kujua....” akasema Rosemar y Mkozumi kwa sauti ya juu .Mathew akamtazama kwa makini na kusema
“ Rosemary Mkozumi just relax…”
“ Kijana naomba tafadhali usiendelee na upuuzi wako unaotaka kuufanya.Nani lakini kakutuma unifanyie hivi? Unashirikiana na akina nani? Hao waliokutuma wamekuingiza katika tanuru la moto na wewe kwa tamaa zako ukakubali kuingia na kuungua .Ninakuonya kwa ara nyingine kijana tafadhali naomba unifungue haraka sana miguu yangu inaumia” akasema Rosemary.
“ Rosemary tafadhali naomba uniskilize kwa makinisanana sihitaji mzaha hata kidogo” Akasema Mathew.
“ Ninaitwa Mathew,ni mchunguzi wa kujitegemea.Nimewahi kufanya kazi katika idara ya usalama wa taifa Tanzania idara ya kupambana na kuzuia ugaidi na baadae nikaacha kazi hiyo na kuanza kufaya kazi zangu binafsi za kiuchunguzi.Mwezi wa pili mwaka jana kijana mmoja aitwaye Edson aliyekuwa akifanya kazi katika idara ya mawasiliano ikulu aliuawa na watu wasiojulikana lakinikesi hiyo ya mauaji ikamuangukia mpenzi wake aliyeitwa Peniela.Mahakama ilimuachia huru Peniela baada ya kuridhika kwamba hakuw ana hatia na hakumuua Edson kama ilivyodaiwa.Nilikabidhiwa jukumu la kumtafuta muuaji halisi wa Edson .Katika uchunguzi wangu niligundua kwamba Edson alishiriki katika uibwaji wa nyaraka nyeti sana toka ikulu.Niligundua kwamba ili kulifanikisah jambo lile Edson hakuwa peke yake alikuwa akishirikiana na watu wawili Mzee Kitwana na Mzee Matiku ambao kwa sasa wote ni marehemu.Nyaraka hizo zilizoibwa zilikuw ana kanuni za kutengeneza kirusi hatari sana ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa sana kwa binadamu.Nimelichimba suala hilikwa undani zaidi na kugundua kwamba mtu aliyetaka kuzinunua karatasi hizo anaitwa Habib Soud raia wa Saudi Arabia .Habib anatajwa kuvifadhili vikundi kadhaa vya kigaidi nahivyo kunifanya niamini kwamba yawezekanaalizihitaji karatasizile kwa ajili ya kutengeneza kirusi kile ili wakitumie kwa mambo ya kigaidi.Sikuishia hapo nilimchunguza Habib na kugundua kwamba amekuwa na mawasiliano nawe ya mara kwa mara .Nimegundua pia kwamba wewe ndiye uliyeratibu na kufanikisha mpango mzima wa kuibwa kwa karatasi hizo ikulu kwa kumtumia Edson na baadaya kuzipata karatasi hizo uliwazunguka washirika wako na kuwamaliza ili ubaki na karatasihizo na pesa yote itokanayo na mauzo ya karatasi hizo uipate peke yako.Ili kuendelea kuuficha uhusika wako katika suala hili kumbu umbu za mawasilianokatiyako na washirika wako wakuu katika suala hili yaani mzee Kitwana na matiku zilifutwa kabisa .” Akasema Mathew na uso wa Rosemary ukabadilika .Mathew akaendelea.
“ Kwa bahati mbaya pamoja na kuwaua washirika wako lakinihukufanikiwa kuzipata nyarakazile kwani ziifichwa na mmoja wa washirika wako.baadaya kuona jambo lile limeshindikana hukukata tamaa ukaingia tena katika biashara nyingine namtu mmoja anaitwa samir Asaad.Umekuwa ukiwasiliana na Samir na katika mojawapo ya barua pepeuliyomtumia Samir umemuhakikishia kwamba muda si mrefu toka sasa utafanikiwa kuupata mzigo anaoutaka kwani una mawasiliano ya karibu na mtu wa karibu na rais .Baadae tukagundua kwamba mtu uliyemtaja kuwa karibu na rais ambaye umekuwa na mawasiliano naye ni Captain Amos ambaye ni daktariwa familia ya rais.Tulimpata Captain Amos na wakati tukimfanyia mahojiano ,alitokea mtu na kumpiga risasi akamuua na hili lilifanyika makusudi ili Captain Amos asiweze kutoa siri.” Mathew akanyamaza akamtazama Rose ambaye matone ya jasho yalionekana usoni pake.
“ Amos is dead?! Akauliza Rosemary kwa msahngao mkubwa
“ yes ..he’s dead” akasema Mathew.Rose akainamisha kichwa kwa masikitiko
“ Rosemary kuna mambo mengi ambayo ninyafahamu kuhusu wewe namtandaowako nasitaki kpoteza muda kuyaongelea hapa.Ninachokihitaji toka kwako nikunipatiamajibu sahihiya kila nitakachokuuliza kaini kama hutanipa ushrikiano wa kutosha na kuniletea jeuri sahau kabisa kutoka hapa ukiwa hai.” Akasema Mathew na kunyamaza kidogo halafu akasema
“Kitu cha kwanza ninachotaka toka kwako nataka kufahamu ,ukiacha wale washirika wako walikwisha fariki,nani mwingine ambaye umeshirikiana naye katika kuziiba karatasi zile ikulu? akaulizia Mathew .Rosemary Mkozumi akasonya na kubetua midomo kwa dharau akasema
“ You go to hell,wewe na huyo aliyekutuma!! .Mathew akamuangalia na kusema
“ Rose ninakukumbusha kwa mara nyingine kwamba hapa ulipo ni nusu ya jehanamu kwa hiyo nataka unijibu kiufasaha kila nitakachokuuliza na kitakachokuokoa ukaweza kutoka humu ndani ni ukweli..Tell me the truth and you’ll get out of here alive..Ninarudia tena nilichokuuliza mwanzo,nina kila ushahidi kuthibitisha kwamba ulihusika katika kuratibu mpango wa kuziiba karatasi zile ikulu.Ninataka kufahamu ni akina nani wengine ulioshirikiana nao kulifanikisha jambo hili ukiacha wale ambao wamekwisha fariki? Akauliza Mathew.
“ You go to hell you witch..nakuhurumia sana wewe kijana kwa nini unakubali kutumiwa kirahisi namna hiyo ? tafadhali achana na huu upuuzi unaoufanya.Mwambie aliyekutuma kwamba hawezi kupambana na Rosemary..” akasema Rosemary kwa dharau
“ Hakuna mtu aliyenituma bali ninafanya kazi hii kwa niabaya serikaliya jamhuri ya muungano wa Tanzania na si mtu binafsi kama unavyodhani..” akasema Mathew.Rose akacheka kwa dharau na kusema “ Serikali !! Unafahamu serikali ni nani? Poor boy hujui hata unachokiongea.Tafadhali naomba unifungue niondoke zangu na nitakusamehe,lakini ukiendelea kunishikilia hapa kwako kwa dakika kumi zijazo ninakuapia kijana sintakusamehe hata kidogo.”akasema Rosemary
“ Vitisho vyako havitaweza kukusaidia hata kidogo Rose.Nakuonya kwa mara ya mwisho kwamba utatoka humu ndani ukiwa salama endapo utanipa majibu ya kile ninachokitaka.Ukileta jeuri ninakuapia Rose hautatoka humu ndani salama.” Akasema Mathew na Rose akaukunja uso wake
“ Kijana kwa nini unakuwa mgumu kunielewa? Kwa nini unaendelea kuhatarisha maisha yako na kujiweka katika matatizo makubwa? Ninakwambiwa kwamba ndani ya muda mfupi ujao utajutia hiki unachokifanya .Sintokusamehe kabisa na wala usidhani kwamba h iyo serikali unayodai unafanya kazi kwa niabayake watakusaida kitu .Iam the government! ….Akasema kwa ukali Rose. Mathew akainuka na kumsogelea karibu. “ Rose ninafahamu kwamba unalengo la kugombea urais na kwa sasa mimi ndiye nitakayeamua kama jambo hilo litafanikiwa ama vipi.Endapo sintaridhika na majibu yako ndoto hiyo kubwa haitatimia kamwe.Nita…” Ghafla Mathew akastuka baada ya kutemewa mate usoni
“ I’ve told you go to hell you black devil !! akasema kwa ukali Rosemary.Mathew akamtazama Rosemary kwa hasira na kusema
“ umefanya kosa kubwa sana.Ni bora ungekutana na mtoa roho kuliko mimi.Sasa kwa kuwa umekataa kunijibu kwa hiari yako na umeonyesha kiburi ,nitakulazimisha kunijbu kwa nguvu” akasema Mathew na kuchukua ndoo ya maji akammwagia Rosemary na kumloanisha chapa chapa
“ Are you crazy?!!.I swear I’ll never forgive you for this ”akafoka Rose.Mathew akalifungua lile sanduku halafu akatoa vifaa kadhaa akaviweka mezani.Akachukukua vyuma Fulani viwili vyenye nyaya akavichomeka katika lile sanduku halafu akaliunganisha katika umeme kisha akavigusanisha vyuma vile vikatoa cheche.Rosemary Mkozumi akatumbua macho “ Unataka kufanya nini? Akauliza.Mathew hakumjibu kitu akarekebisha kiasi cha umeme anaouhitaji na kisha akasogea kitandani na kugusisha vyuma vile vyenye umeme katika pingu aliyofungiwa Rosemary mguuni.. "Aaaaaggggghhhhh!!!!!!!!!!!!!!!...”Rosemary akapiga kelele kubwa..Mathew akatulia kidogo halafu akarudia tena zoezi lile..Rose akaendelea kupiga kelele kubwa
“ Give me the names!!...akasema kwa ukali Mathew.Halafu akatulia
“ Give me the names!! nani u nashirikiana nao? Akauliza .
“ There is..there..iiii..there are no names..” akasema Rosemary huku akitetemeka mwili.mathew akagusisha tena vyuma vile katika pingu na kuendelea kumtesa Rosemary..
“ Stop that.!!.please stoooop !!!!!..” akalia Rose.Mathew akasimama
“ Ni akina nani ulishiriana nao katika mpango ule? Akauliza Mathew. “No one..sijashirikiana na mtu yeyote na wala siufahamu huo mpango unaousema..” akasema Rose huku akitweta.
“ This is not working…!!! Akasema Mathew kwa sauti ndogo.Akavua shati na kubakiwa na fulana ya ndani akamshika Rosemary kwa nguvu akamfunga mikono yake kwa pingu.
“ Nilikuonya toka mwanzo kwamba usiombe ukutane na mimi lakini ukapuuza.Utanieleza kila kitu leo ”akasema Mathew halafu akachukua kisu na kukata kijisehemu kidogo katika kidole cha mguu wa kulia wa Rose halafu akachukua bomba la sindano akavuta dawa fulani nyeupe toka katika kichupa kidogo na kudondoshea matone kadhaa mahala palipokuwa panatoa damu.Rose akagalagala pale kitandani huku akipiga kelele kubwa kwa maumivu aliyoyasiki..Mathew akachukua gundi na kumfunga mdomo ili asiweze kutoa ukelele halafu akadondoshea tena matone kadhaa mahala alipopakata..Rosemary akaendelea kugugumia kwa maumivu makubwa.Mathew akamfungua ile gundi aliyomfunga nayo mdomo akamuuliza
“ Uko tayari kuniambia ninachokihitaji?Akiwa ndani ya maumivu makali sana akasema
“ You go to hell you devil !! Mathew akamfunga tena mdomo na kumkata kidogo shingonihalafu akadondoshea matone kadhaa mahala alipokata..Rose akaruka ruka kana kwamba anakata roho.Mathew akamuangalia halafu akamfungua ile gundi mdomoni. “ Utanijibu nilichokuuliza? Akauliza Mathew lakini Rose hakumjibu kitu akabaki analia kwa maumivu makali.
“ C’mon Rose ..nijibu haraka nilichokuuliza !!!! akasema Mathew kwa ukali Rose akaendelea kulia kwa maumivu makali sana aliyoyasikia.
“ Dah ! sijawahi kukutana na mwanamke mwenye roho ngumu kama huyu mama.Lakini leo hii atanieleza kila kitu ninachotaka.”akawaza Mathew.Akaelekea mezani kwake na kuchukua kifaa kidogo cha kukatia akakiwasha na kukijaribu
“R ose umetaka mwenyewe tufike hapa tulipofika na nilikuonya toka mapema kwamba usiombe ukutane na mimi.I’ m a monster na ninachokwenda kukufanyia kitabaki katika kumbu kmbu za uzao wako daima.Nitakukata kidole kimoja kimoja nikianzia na vidole vya miguu na halafu nitakuja mikononi na halafu nitanyunyiza dawa hii inayouma na utajihisi kamaumetupwa katika shimo la moto kwani mwili wote utawaka moto kwa maumivu utakayoyasikia..Utasikia maumivu makali mno ambayo hujawahi kuyasikia toka umezaliwa.Ukitaka nisifanye hivyo nijibu haraka kile nilichokuuliza” akasema Mathew lakini Rosemary hakujibu kitu bado aliendelea kulia kwa maumivu makali.Mathew akachukua kile kifaa akakiwasha na kisha akakishika kidole cha mwisho cha mguu wa kulia wa Rosemary na kukikata. Rosemary akapiga ukulele mkubwa sana
“ C’mon Rose,usinilazimishe nikakufanyia hivi.Niambie kile ninachokitaka” akasema Mathew kwa ukali.Bado Rose aliendelea kugalagala huku akilia kwa maumivu makali mno.
“ Bado anaendelea kuwa na kiburi ..leo lazima nimbadilishe sura yake..Atanieleza tu .” akawaza Mathew na kukishika tena kidole kinachofuata akakata.Rose akapiga ukele mkubwa hadi sauti ikaanza kumkwama..
“ Please stop !!.stop hurting me !!!!!!!!!!..akasema Rosemary..
“ Are you ready to tell me what I want? akauliza Mathew
“ I will tell you..i will tell you everything ..stop hurting me…” akasema Rose huku bado akiendelea kulia kwa maumivu makali.Mathew akachukua bandeji na kufunga mguu ule wenye majeraha halafu akamchoma sindano ya kupunguza maumivu.
“ Now tell me everything” akasema Mathew
“ I will tell you everything you want..please don’t hurt me
ROSE ATAMUALEZA NINI MATHEW? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………
OkPENIELA SEASON 3
SEHEMU YA 26
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Elibariki amenifanyia kitendo cha aibu sana na ameniumiza mno.Nilimpenda sana lakini kwa kitendo alichokifanya sitaki tena kuendelea naye.Nimeanza kuvutiwa na Mathew.Ni kijana mzuri anajitambua na kujiheshimu tofauti na Elibariki ambaye anaonekana kuwa na tamaa.Mathew anaonekana ni mtu mwenye msimamo kwani toka mke wake alipofariki hajawahi kujiingiza tena katika mapenzi na mwanamke mwingine .Sina hakika kama ananipenda lakini nina hakika na kitu kimoja kwamba ana hisa Fulani juu yangu.Nina uhakika huo kutokana na namna alivyokuwa ananiangalia .Hii ni sehemu nzuri kwa kuanzia .” akawaza Peniela.
Aliandaa chakula chepesi haraka haraka kisha akarejea chumbani .Bado Mathew alikuwa amekaa katika jaccuzi akioga.Kichwa chake kilijaa mawazomengi sana.Mara mlango wa bafu ukafunguliwa akaingia peniela akiwa amejifunga taulo.Mathew macho yakamtoka pima.Peniela akamtazama akatabasamu na kusema
“ Mbona umestuka Mathew? Umestuka kuniona hivi? Akauliza Peniela huku akitoa kichekokidogo
“ Usiogope Mathew kwani hakuna kitu ambacho hujakiona.”akasema Peniela na kuliangusha taulo akabaki mtupu.
ENDELEA……………………………
“ Ouh my God !!..Huyu Peniela anataka kufanya nini ? Mbona ananiingiza katika jaribu kubwa ? Akawaza Mathew huku mwili ukimsisimka kwa kuushuhudia wazi wazi mwili ule mwororo wa Peniela uliokuwa uking’aa kama malaika.
Huku akitabasamu,Peniela akaingia ndani ya jaccuzi ,Mathew akabaki anamtazama.Ghafla Picha ya moto mkubwa ukiiteketeza nyumba yake ambayo ndani yake walikuwemo mke wake na wanae wawili ikamjia tena kichwani , akainuka na kutoka ndani ya jaccuzi akaelekea chumbani na kuvaa nguo zake.Peniela akashangaa sana naye akatoka ndani ya jaccuzi akamfuata Mathew chumbani.Alikuwa mtupu.Mathew akachukua taulo na kumvalisha
“ Mathew what’s wrong? Unaogopa nini? Akauliza Peniela huku akionyesha kushangaa
“ C’mon Mathew.Usiogope tafadhali “ akasema Peniela.
“ I cant do that Peniela .Tafadhali nenda kaoge kisha tuondoke “ akasema Mathew
“ Mathew usiwe muoga namna hiyo.No body is watching us.Its just me and you.Tafadhali Mathew naomba unisaidie kuniondolea machungu ya kuumizwa na Elibariki.I need you just for few minutes”
“ Peniela naomba unielewe kwamba siwezi kufanya kitu hicho unachotaka tufanye” Mathew akaendelea kusisitiza.Peniela akamfuata na kusimama karibu yake akamtazama kwa macho yake malegevu na kusema
“ Mathew its been years since your wife passed away so you need this.Najua unahitaji sana kufanya mapenzi na mimi na ndiyo maana hata sasa nyeti zako zimefura.Tafadhali usiendele kujitesa Mathew.Let us do it”
“ Peniela nimekwisha kwambia kwamba siwezi kufanya hicho kitu.Ni kweli mke wangu amefariki muda mrefu sasa na toka alipofariki sijajihusisha tena katika mahusiano na sitaki kufanya hivyo.”
“ Kwa nini Mathew unajitesa hivyo? Akauliza Peniela
“ Because I still love her !! akajibu Mathew
“ Hahahaha Mathew ,your wife is gone and she will never come back so you have to move on.Mathew naomba nikuweke wazi kwamba ninakutamani sana na mwili wangu uko tayari kwa ajili ya kukufurahisha .Please Mathew…” akasema Peniela.Mathew akaitazama saa yake na kusema
“ Peniela muda unakwenda sana.Kesho ni siku ndefu na tuna kazi nyingi kwa hiyo jiandae tuondoke.Utanikuta ninakusubiri sebuleni” akasema Mathew na kuanza kupiga hatua kuondoka mle chumbani.Peniela akamuita
“ Mathew !!..
Mathew akageuka na kumtazama
“ Mathew are you sure that you don’t want to make love with me? Akauliza Peniela.Mathew akamtazama na kusema
“ Yes ! I’m sure”
Peniela akamsogelea na kusema
“ Ninajifahamu mimi ni mzuri na uzuri wangu ni kama ua lenye harufu nzuri ambalo huwavutia nyuki kutua na kuling’ang’ania .Sifahamu ni kitu gani ninacho ambacho huwafanya wanaume wachanganyikiwe na mimi na hiyo imenifanya niamini kwamba hakuna mwanaume ambaye nitamtaka katika hii dunia ataniambia hapana na haijawahi kunitokea kwa mwanaume kuniambia hapana lakini kwa usiku wa leo kwa mara ya kwanza nimekutana na mwanaume ambaye amenitazama nikiwa mtupu akanitazama machoni na kuniambia Hapana.Si kunitamkia tu neno hilo bali ameokota taulo na kunivisha ili asiendelee kunitazama nikiwa mtupu.Wanaume wengine wote hufurahi na kuchanganyikiwa wakiniona nikiwa mtupu lakini kwako imekuwa tofauti.Mathew thank you so much.Kitendo cha kunikatalia kufanya mapenzi usiku huu kimeonyesha ni namna gani unavyonithamini.Uliokota taulo na kunivisha kunionyesha kwamba mwili wangu una thamani kubwa na hautakiwi kuachwa utupu bila sababu.Mathew wewe ni wa kipekee kabisa na kitendo hiki cha leo kimenifanya nizidi kutamani kukufahamu zaidi kwani nahisi bado sijakufahamu vizuri wewe ni mtu wa aina gani.You are different from all men I know ” akasema Peniela.Mathew akamtazama na kusema
“ Tukiwa nyumbani uliniuliza swali ni mwanamke wa aina gani ninayemuona ndani yako na nikakujibu kwamba ninapokuona ninamuona mwanamke jasiri,mwenye ndoto na ambaye yuko tayari kwenda hadi ncha ya mwisho wa dunia ili azitimize ndoto zake,mwanamke asiye kata tamaa ,mwanamke mwenye nguvu kubwa ndani yake licha ya mwili wake kuwa mdogo, mwanamke mwenye sauti laini lakini inayoweza kupenya hadi ndani ya mioyo ya watu wenye nguvu na wakavifunga vinywa vyao kumsikia.Mwanamke wa aina hii ni mwanamke ambaye binafsi ninamuheshimu sana zaidi ya ninavyoweza kueleza na sistahili hata kuugusa mwili wake.Peniela hata mimi ni binadamu na nina matamanio kama wengine na ninakiri kwamba hili ni jaribu langu kubwa sana kuwahi kunitokea lakini siwezi kuuchezea mwili wako kwa sababu ninakuheshimu sana ,na ninaomba nikuweke wazi kwamba moyo wangu unaniuma sana pale ambapo mwili wako hutumika kufanikisha baadhi ya mambo kama ilivyotokea leo kwa Deus.Ili kupata taarifa tulizohitaji ulilazimika kuutoa sadaka mwili wako na ndipo akakueleza kile tunachokitaka.Mwili wako umegeuzwa bidhaa and no body cares..jambo hili linaniumiza sana na ndiyo maana ninasema kwamba muda sio mrefu jambo hili litafikia mwisho na utaishi maisha yako kwa uhuru na amani na wala hutalazimika tena kuutumia mwili wako huu wa thamani kubwa kwa ajili ya kupata taarifa mbali mbali kama ufanyavyo sasa kwani katika wakati huo hakutakuwa tena na team SC 41. “ akasema Mathew . Peniela akashindwa kujizuia akamfuata na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakimtoka.
“ Mathew ulikuwa wapi? Wewe nI mwanaume ambaye nilikuwa ninakuhitaji sana katika maisha yangu.Ee Mungu Ahsante sana kwa kuniletea kijana huyu ambaye ndiye haswa niliyekuwa ninamtafuta katika maisha yangu.Ananijali na kunithamini huyu ndiye atakayenifaa . Huyu ndiye mwanaume wa maisah yangu. “ akawaza Peniela
“ Thank you Mathew.Thank you so much.Sina neno la kusema kwa hayo maneno mazito uliyoyatamka” akasema Peniela huku machozi yakimdondoka.Mathew akamfuta machozi na kusema
“ Peniela muda unakwenda kwa kasi kwa hiyo jiandae ili tuweze kuondoka” akasema Mathew na kuitoa mikono ya Peniela iliyokuwa imeng’ang’ania halafu akafungua mlango wa chumbani na kutoka akaelekea sebuleni
“ Ee Mungu ahsante kwa kunipa nguvu ya kulishinda jaribu hili kubwa.Haikuwa rahisi ,Ilihitaji nguvu ya ziada kuweza kulishinda .Hata Peniela mwenyewe ameshangaa sana na kushindwa kuamini kwamba nimekataa kufanya naye mapenzi licha ya ushawishi wote alioufanya.kwa maelezo yake mwenyewe ni kwamba hajawahi kukutana na mtu ambaye ameuona mwili wake na akakataa kufanya naye mapenzi.” Akawaza Mathew wakati akielekea sebuleni
“ Team SC41 wamemfanya Peniela aondoe kabisa thamani ya utu wake na ndyo maana yuko tayari kuutoa mwili wake kwa mwanaume yeyote Yule ili mradi kuna kitu anakkitaka kwake.Peniela ni mwanamke mzuri na anayestahili heshima kubwa na hapaswi kuuchezea mwili wake kama afanyavyo sasa.Nitahakikisha anakuwa na maisha yake ya kawaida ambayo hayatamlazimu kuutumia mwili wake kama chambo” akawaza Mathew.Akaketi sofani na kujimiminia mvinyo kidogo katika glasi akanywa
Baada ya dakika kumi Peniela akatokea .Alikuwa amependeza sana.
“ Dah ! mwanamke huyu ana uzuri wa ajabu sana. Kila ninapomuona mwili wote unanisisimka.Nina wasiwasi kwamba nisipokuwa makini yawezekana na mimi nikajikuta nimeanguka na kuzama katika penzi zito na malaika huyu..” akawaza Mathew
“ Mathew samahani sana kwa jambo lililotokea chumbani.” Akasema Peniela
“ Usijali Peniela.Ni jambo la kawaida.”
“ Mathew kuna jambo ninataka kuliomba toka kwako.”
“ Jambo gani?
“ Ninaomba baada ya mambo haya kumalizika ,mimi na wewe tupate nafasi ya kwenda mahala na kupumzika hata kama ni nje ya nchi .I want to spend much time with you.I want to know you better” akasema Peniela,.Mathew akatabasamu na kusema
“ Tutaangalia kama itawezekana .”
“ Thank you Mathew “ akasema Peniala na kuchuua simu ambayo huitumia kuwasiliana na Dr Joshua akabonyeza namba Fulani na kuiweka sikioni.
“ namba yako ya utambulisho tafadhali ” ikasema sauti ya upande wa pili iliyopokea simu.
“ pkp46 “ akasema Peniela
“ Ok subiri kidogo” akasema yule mwanadada aliyepokea simu.Baada ya kama dakika moja hivi sauti nzito ya kiume ikasikika katika simu
“ Hallow Peniela” ilikuwa ni sauti ya Dr Joshua
“ Dr Joshua “ akasema Peniela
“ Hallo my queen..Unaendeleaje? Nimestuka kidogo ulipoamua kutumia njia hii ya dharura.” Akasema Dr Jshua
“ Dr Joshua najua si matumizi sahihi ya simu hii ya dharura lakini sikuwa na namna nyingine ya kuweza kuwasiliana nawe .Lengo langu ni kutaka kukujulia hali na kukupa pole sana kwa kifo cha Flaviana.Nimesikitishwa mno na kifo hiki.Pole sana my love” akasema Peniela
“ Peniela ahsante sana.Madaktari walijitahidi kwa kila namna walivyoweza lakini ikashindikana haikuwezekana kupona.”
“ Pole sana Dr Joshua.”
“ Ahsante sana Peniela”
“ kwa hiyo lini mwili wa Flaviana utarejeshwa nchini kwa mazishi? Akauliza Peniela
“ Kesho saa tano asubuhi mwili wa Flaviana utarejeshwa nyumbani kwa ajili ya maandalizi mazishi.”
“ Ahsante kwa taarifa Dr Joshua.Tutashirikiana pamoja katika kuupokea mwili na hadi tutakapohitimisha safari ya mwisho ya Flaviana.”
“ Ahsante sana Peniela"
“ Pamoja na hayo Dr Joshua nina ombi moja kwako”
“ Peniela nimekwisha kupa ruhusa ya kuomba chochote kile unachokitaka bila hata ya kuniuliza kwanza”
“ Ahsante Dr Joshua.Nnajua kesho utakuwa na shughuli nyingi lakini ninataka utafute nafasi tuonane hata kwa dakika ishirini tu.Nina maongezi nawe na ninataka nitumie dakika hizo chache kukufariji mpenzi wangu.Nataka tukutane katika ile nyumba yetu kule ufukweni” akasema Peniela
“ Uliponiambia kuna kitu unataka kuniomba nilidhani kuna jambo kubwa na zito kumbe ni hilo tu,basi usijali Peniela kesho mara tu baada ya kutua na kuelekea nyumbani nitatafuta muda na tutaonana.Saa saba za mchana tutaonana.Hata mimi nina hamu sana ya kukuona malaika wangu.Ninahitaji sana faraja yako na vile vile kuna jambo ninataka tuongee mimi na wewe linalohusu maisha yetu” akasema Dr Joshua
“ Ahsante sana kwa kunikubalia ombi langu mpenzi wangu.Basi naomba nikutakie usiku mwema na safari njema hiyo kesho.Tutaonana hiyo kesho.I love you so much” akasema Peniela na kukata simu kisha akaitupa pembeni na kumtazama Mathew
“ Samahani Mathew kwa kusikia maongezi yangu na huyu mzee lakini hivi ndivyo huongea naye.Anachotaka kukisikia Dr Joshua toka kwangu ni kwamba ninampenda sana nami siku zote huwa ninajaribu kumuhakikishia kwamba ninampenda lakini laiti angeweza kuusoma moyo wangu na namna ninavyomchukia angeniogopa kama kifo.Ninamchukia sana Yule mzee lakini sina namna nyingine ya kuweza kumuepuka lazima nikubali kumpenda ili mipango yetu ifanikiwe.” Akasema Peniela
“ Usijali Peniela.Mambo haya yatakwisha muda si mrefu.” Akasema Mathew.
“ Huyu mwanamke ana kitu gani anachokitumia kuwachanganya wanaume akili kiasi hiki? KIla mwanaume anayetembea naye anachanganyikiwa kabisa kama alivyomchaganya rais wa nchi.Peniela ni mwanamke mwenye uwezo wa kipekee na ni hatari zaidi ya watu wanavyomchukulia.Kama ameweza kupenya hadi kujenga mahusiano na rais wa nchi basi anaweza kuingia sehemu yoyote ile na akafanya chochote .Kuna nyakati hata mimi mwenyewe ninamuogopa kutokana na uwezo alionao wa kushawishi mtu yeyote Yule.Wasiwasi wangu ni kwamba hata mimi najihisi kwamba muda si mrefu ninaweza nikajikuta nimeshindwa kuendelea na msimamo wangu na kujikuta nikizama mapenzini na kimwana huyu kwani kadiri ninavyozidi kukaa naye karibu ndivyo ninavyojikuta nikizidi kuvutiwa naye na kutamani kuwa naye karibu zaidi na zaidi…………..” akawaza Mathew kisha akasema.
“ Peniela jambo kubwa lililotuleta hapa kwako ni kuzungumza na Dr Joshua na tayari umekwisha ongea naye.Nadhani sasa tunaweza kuondoka.” Akasema Mathew
“ Mathew are you sure you don’t want to spend time here at my house? Usihofu hapa ni sehemu salama sana “ akasema Peniela
“ Hapana Peniela tunatakiwa turejee nyumbani kwangu .Ninaamini sana usalama ulioko pale kuliko sehemu nyingine yoyote ile.” akasema Mathew.Peniela akaenda kufunga chumba chake halafu wakaingia garini na kuondoka
“ Peniela kuna mambo uliniambia unataka tuyajadili,mbona hukunikumbusha tena ili tujadili? Akauliza Mathew wakiwa garini
“ Ah ! usijali Mathew tutajadili siku nyngine tena kama tukifanikiwa kupata nafasi nzuri kama tuliyoipata leo.” Akasema Peniela na Mathew akatabsamu
“ Tutapata nafasi Peniela usijali.Bado tuna muda mwingi wa kuweza kukaa na kujadili mambo mengi tu “ akasema Mathew na mara simu ya Mathew ikaita.Alikuwa ni Anitha
“ Hallow anitha.Bado hujalala mpaka mida hii? Akaulzia Mathew
“ Nitalala vipi bil akuhakikisha umerejea salama? Akasema Anitha
“ Ahsante sana Anitha kwa kunijali.Kuna jambo jipya?
“ Mathew unakumbuka kuna wanati Peniela alitumia simu ya hapa ndani kumipigia mtu wake na kumfahamisha kwamba hatarejea leo?
“ Ndiyo ninakumbuka ,alimpigia Josh” akasema Mathew
“ Basi kijana Yule yuko katika laini ya simu anataka kuongea na Peniela” akasema Anitha.Mathew akampa simu Peniela
“ Josh wants to talk to you” akasema Mathew
“ Hallow” akasema Peniela.
“ Peniela ngoja nikuunganishe na Josh anataka kuongea nawe” akasema Anitha na kumuunganisha josh na Peniela
“ hallow Peniela” akasema Josh
“ Josh,is everything ok? Akauliza Peniela
“ Peniela you are being followed “ akasema Josh
“ Followed by whom? Peniela akashangaa
“ Ulionekana kupitia kamera zilizofungwa nyumbani kwako ukiingia kwako usiku huu ukiwa umeongozana na Mathew na hivyo wakatuma watu kuja kukuchunguza ulikuwa wapi na unafanya nini.Wako nyuma yako wanakufuatilia.Kuwa makini sana” akasema Josh
“ Ouh my gosh !! akasema Peniela
“ Peniela kuna nini?
“ Team SC41 wanatufuatilia” akasema Peniela.Nikweli kupitia kioo cha pembeni Mathew akagundua kwamba kuna gari lilikuwa linawafuatilia .
“ Hata mimi nilihisi kuna gari linatufuatilia toka tulipoondoka nyumbani kwako.Get ready.We must do something…” akasema Mathew na kuongeza mwendo wa gari.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO
AsantePENIELA
SEASON 4
EPISODE 12
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ I love him .Ananijali sana.Ninyi vijana hamuwezi kunimudu gharama zangu.Hata wewe nitakupa tu penzi kwa sababu bila hivyo usingekubali kunisaidia.Anyway tuachane na hayo,muda unakwenda haraka .Nenda kafanye kazi niliyokutuma halafu nitakupa maelekezo sehemu ya kukutana.Nataka umlete Anna mwenyewe sitaki aongozane na mtu mwingine yeyote” akasema Peniela huku akiinuka na kuagana na Kareem akaelekea katika gari lake.Mathew naye akarejea katika gari lao wakaondoka kurejea nyumbani
“ Mathew endapo Kareem atafanikiwa kumpata Anna,nimuelekeze amlete wapi? Akauliza Peniela wakiwa njiani kurejea nyumbani
“ Sehemu pekee yenye usalama kwa sasa ni katika makazi yetu.Utamuelekeza amlete Anna pale.”
“ Are you sure ? akauliza Anitha
“ Usihofu Anitha ,hakutakuwa na tatizo” akajibu Mathew na safari ikaendelea kimya kimya
ENDELEA………………..
Profesa Savatory Ulomi mjomba wa Flaviana ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati iliyoshughulikia mazishi ya Flaviana alitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia ya rais baada ya shughuli ya mazishi kumalizika na waombolezaji walianza kuondoka taratibu kwani tayari jua lilianza kuchwea.
“ lazima nionane na Elibariki.I need to know what’s real going on” akawaza Anna huku macho yake akiwa ameyaelekeza kwa jaji Elibariki aliyekuwa amezungukwa na watu wakimpa pole.Wakati Anna akisubiri watu waliokuwa wakimpa pole jaji Elibariki wapungue ili apatae nafasi ya kuonana naye ,akatokea mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam ambaye aliwataka radhi watu wale waliokuwa na jaji Elibariki na kuondoka naye
“ Amechukuliwa tena,nitamtafuta hata baadae.Leo lazima nifahamu ni kitu gani hasa kinachoendelea kwa sababu mambo yaliyotokea ndani ya kipindi kifupi yamenipa wasi wasi mwingi lazima nijue kin….” Anna akastuka baada ya kuguswa bega ,akageuka na kukutana na Kareem mlinzi wa baba yake
“Kareem “ akasema Anna
“ Anna naweza kuongea nawe kidogo? Akasema Kareem wakasogea pembeni
“ Unasemaje Kareem,?
“ Anna nimeelekezwa na rais nikupeleke sehemu Fulani kuna mtu unatakiwa kuonana naye”
“ Anataka tukaonane na nani? Mbona hajanitaarifu ? Akasema Anna huku akionyesha mshangao kidogo kwa safari ile ambayo baba yake hakuwa amemtaarifu
“ Sifahamu unakwenda kuonana na nani lakini inaonekana ni mtu muhimu sana” akasema Kareem.Anna japokuwa alibaki anajiuliza maswali juu ya nani anayekwenda kuonana naye lakini hakuwa na wasi wasi hata kidogo na Kareem kwani ni mtu ambaye anaaminiwa sana na baba yake.Bila kupoteza muda wakaongozana hadi katika gari la Kareem wakaondoka.Kareem akamtumia Peniela ujumbe katika simu akimtaka amuelekeza mahala ambako Anna atakutana na huyo mtu anayehitaji kuonana naye.Mara tu baada ya kuyaacha makazi ya Dr Joshua ukaingia ujumbe katika simu ya kareem uliotoka kwa Peniela aliyempa maelekezo ya mahala pa kumpeleka Anna
Hakukuwa na maongezi mengi garini,muda mwingi Anna alikuwa amejiinamia akiwaza
“ I’m all alone now.All my loved ones are gone.Edson,mama na sasa ni Flaviana.Kitu gani hasa kinachoendelea katika familia yetu? Why always us? Akajiuliza na kufuta machozi.
“ Hakuna kifo kimeniuma kama cha Flaviana.Amekwenda na uzuri wake.Halafu cha kushangaza mtu ambaye jeshi la polisi lilitangaza kumsaka kwa kusababisha kifo cha Flaviana yupo huru kana kwamba hakuhusika katika tukio lile.Ni filamu gani inayochezwa hapa? Akaendelea kuwaza Anna
“ Nikiwa afrika ya kusini niliwasiliana na Elibariki na akanihakikishia kwamba baba ndiye muhusika mkuu wa vifo vya mama na Flaviana lakini cha kushangaza ameibuka toka alikokuwa amejificha na amekuja akiwa ameongozana na baba .Hapana siwezi kuruhusu akili yangu ikubaliane na sinema hii inayoendelea Halafu kingine kinachonishangaza ni hizi taarifa nilizozisikia eti Elibariki alikuwa ametekwa na alifanikiwa kutoroka.Mimi niliongea naye kwa simu akaniambia kwamba yuko mafichoni kuna watu wanaomtafuta wamuue sasa hizi hadithi za kwamba alikuwa ametekwa na kufichwa msituni zinatoka wapi? Yeye na wote anaoshirikiana nao watawadanganya watu wengine lakini si mimi. “ akaendelea kuwaza Anna huku safari ikiendelea.
Kareem alifuata maelekezo yale aliyopewa na Peniela na kujikuta akitazamana na geti jeusi
“ Ni hapa” akawaza Kareen halafu akamgeukia Ann a ambaye bado alikuwa amejiinamia
“ Anatia huruma sana huyu binti.Imemtokea misiba mfululizo ya watu wake wa karibu.Ni nani huyo mtu anayehitaji kuonana naye? Anataka nini kwa Anna? Sehemu hii ni salama? Akajiuliza Kareem
“ Lakini sina wasi wasi na Peniela,endapo kugekuwa na hatari yoyote asingeweza kuniomba nimlete Anna .”
Mara uso wa Kareem ukachanua tabasamu baada ya kumkumbuka Peniela
“ Muda mrefu sana nimekuwa nikimtamani Peniela na leo siamini kama nitaipata nafasi ya kujivinjari naye .Japokuwa ninajiweka katika matatizo makubwa endapo Dr Joshua atagundua lakini siwezi kuiacha nafasi hii adimu “ akawaza Kareem na kumshika Anna bega
“ Anna we’re here” akasema Kareem na kushukja garini akaenda getini akabonyeza kengele
Mathew na akina Anitha Wakiwa katika ofisi yao walisikia kengele ya getini na wote wakaenda katika chumba kidogo ilimo luninga iliyounganishwa na kamera za ulinzi
“ Kareem” akasema Peniela
“ Anitha utaenda kufungua geti mimi sitaki kuonana na Anna.Akiniona tu hatakubali kuingia humu ndani.Wakishainga ndani utamuacha Anna sebuleni na Mathew halafu utamleta Kareem chumbani kwangu.Wakati mimi na y eye tukiwa chumbani ninyi mtaongea na Anna na mkisha maliza utagonga mlango na Kareem atatoka” akasema Peniela.Mathew akamtazma na kutaka kusema kitu lakini kabla hajasema chochote Anitha akasema
“ That’s a good plan.Ngoja nikawafungulie geti” Anitha akatoka akaenda kufungua geti akakutana na Kareem wakasalimiana
“ Kareem karibu sana"Akasema Anitha huku uso wake ukiwa na tabasamu kama vile anafahamiana sana na Kareem
“ Ahsante sana! akajibu Kareem
Anitha akawaongoza akina Kareem hadi sebuleni ambako walimkuta Mathew ambaye naye aliwakaribisha kwa furaha.Anna alikuwa anashangaa hakuwafahamu watu wale aliowakuta katika ile nyumba.
“ hawa ni akina nani? Akajiuliza.Anitha akawakirimu wageni wao vinywaji halafu akasema
“ Kareem na Anna karibuni sana.Mimi naitwa Anitha na Yule mwenzangu pale anaitwa Mathew ambaye ndiye anayehitaji kuongea machache na Anna.Kareem naomba tuwaachie nafasi Mathew na anna ya kuzungumza.” Akasema Anitha.Kareem naye alipatwa na mshangao kidogo lakini hakutaka kuonyesha mbele ya Anna
“ Kareem what’s this? What’s going on here? Akauliza Anna kwa mshangao
“ Relax Anna usiwe na wasi wasi.You are safe here.I’ll be just next door.”
“ No kareem you stay here !! akasema Anna.Kareem akamsogelea na kumnong’oneza kitu sikioni halafu yeye na Anitha wakaondoka pale sebuleni wakamuacha Anna na Mathew
“ Usiogope Anna.Uko salama na hakuna chochote kibaya kitakachokutokea” akasema Mathew.Anna akamtazama Mathew kwa macho makali na kusema
“ Who are you? How do you know me? Why do you want to see me? Akauliza Anna.Mathew akamfanyia ishara aketi kitini na baada ya sekude kadhaa akasema
“ Naitwa Mathew,ni mpelelezi wa kujitegemea.Nimewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa lakini kwa sasa ninajishughulisha na kazi binafsi” akasema Mathew .
“ Mimi na wewe hatujawahi kukutana na wala kufahamiana na ndiyo maana nimeamua kumtumia Kareem kutukutanisha.” Akasema Mathew.Anna akapatwa na mshangao
“ So he lied to me? Aliniambia kwamba baba alimtuma anilete huku kuna mtu ambaye natakiwa kuonana naye.Kareem must pay for this..How could he sell me like this? Akasema Anna kwa hasira huku akiinuka
“ I’m going..mwambie huyo mwenzako uliyemtumia kunidanganya kwamba nimeondoka and he is going to answer to my father.!! Akasema Anna kwa hamaki. Huku akianza kupiga hatua.Mathew akasimama
“ Anna you are not leaving!! Akasema Mathew kwa ukali na kumfanya Anna ageuke ,akajikuta anatazama na bastora,pochi aliyoishika ikamponyoka na kuanguka kwa woga
“ Oh my gosh !! Kareem set me up..This is a trap “ akawaza Anna huku akihisi miguu ikimuisha nguvu.
“Are..a..are..you..goi…going to shoot me?? Akajikaza na kuuliza
“ If I have to ,Yes !!!!..akasema Mathew kwa ukali
“ Sikiliza Anna,sijakuita hapa ili kukutisha au kukufanyia kitu chochote kibaya bali uko hapa mida hii kwa sababu moja kubwa nayo ni kuhitaji msaada wako”
“ msaada wangu?? Akauliza Anna
“ Ndiyo nahitaji msaada wako”
“ Umenielekezea bastora na wakati huo huo unahitaji msaad wangu ?? Siwezi katu kukusaidia.I’m leaving and if you want to shoot me go ahead,shoot me !! akasema Anna kwa ukali na kuinuka akaanza kuelekea mlangoni
“ Anna please help me find who killed your mother and your sister” akasema Mathew.
“ What?? Akauliza Anna na kugeuka
“ What you’ve just said?
“ Help me find who killed your mother and your sister Flaviana
"
Kwa dakika mbili Anna akasimama akimkodolea macho Mathew
“ Naomba uketi Anna.Kuna mambo mengi ya kuongea mimi na wewe” akasema Mathew na bila ubishi Anna akaketi sofani.
“ Anna najua nimekugusa sana kwa hili nililolitamka na ninapenda kwanza kutumia nafasi hii kukupa pole sana kwa misiba mizito uliyoipata.Pole sana Anna” akasema Mathew kwa sauti ya upole.
“ Do you know who killed my mother and my sister? Akauliza Anna huku akilengwa na machozi
“ Yes I know” akajibu Mathew
“ tell me please” akasema Anna na kuchukua kitambaa akajifuta machozi
“ Ni hadithi ndefu kidogo ila nitakueleza kila kitu kilichotokea na nini kinachoendelea hivi sasa” akasema Mathew
“ Kabla sijasema chochote nataka nikuombe samahani sana kama nitakuwa nimekukumbusha machungu ya vifo vya wapendwa wako”
“ Go ahead,tell me everything” akasema Anna
“ Nitaanzia mbali kidogo kwa aliyewahi kuwa mchumba wako Edson.Kabla ya kifo chake,Edson alikuwa katika mahusiano na msichana mmoja anaitwa Peniela ambaye ndiye aliyekuwa mtuhumiwa mkuu wa kifo cha Edson.Baada ya kesi kusikilizwa, mahakama ilijiridhisha kwamba Peniela hakuwa na hatia na ikamuachia huru.Jaji aliyeisikiliza kesi ile alikuwa ni jaji Elibariki ambaye ni mume wa dada yako.Wakati wa kusikilizwa kwa kesi ile ,jaji Elibariki aligundua kwamba kuna nguvu kubwa ilikuwa inatumia katika kuhakikisha Peniela aliyekuwa anatuhumiwa kumuua Edson,anakutwa na hatia na hatimaye kufungwa,jambo ambalo lilimfanya jaji Elibariki ajiulize kulikoni? .Baada ya kesi kumalizika ilimlazimu jaji Elibariki atake kufahamu ukweli wa jambo lile na kumpata muuaji halisi wa Edson kwani alimini Peniela hakumuua Edson” Mathew akatulia kidogo halafu akaendelea
“ kwa kuwa jaji Elibariki ni mbobezi katika mambo ya sheria ilimlazimu kutafuta mtu ambaye amebobea katika mambo ya uchunguzi na kwa kua mimi na yeye tunafahamiana akanifuata na kuniomba nimsaidie kufanya uchunguzi huo ili kubaini ni nani hasa aliyemuua Edson? Nilikubali kumfanyia kazi hiyo na katika kuifanya kazi hiyo niliungana pia na wenzangu wawili ambao hufanya nao kazi pamoja.Wenzagu hao ni Noah ambaye kwa sasa ni marehemu na Anitha huyu aliyewakaribisheni hapa.Vile vile nilimshirikisha pia Jason wakili aliyekuwa anamtetea Peniela” Mathew akanyamaza na kumtazama Anna aliyekuwa makini akimsikiliza
“ Uchunguzi wetu ulitupelekea kugundua mambo kadhaa ,kwanza tuligundua kwamba Peniela hakumuua Edson kama ilivyodaiwa bali Edson aliuawa kwa amri ya rais..”
“ My father ??..that cant be …” akasema Anna
“ Ndiyo Anna.Baba yako ndiye aliyetoa amri Edson auawe.”
“ Mathew I cant believe you…Baba hawezi kabisa kumuua mpenzi wangu,that’s not true !!! akasema Anna
“ Sababu kubwa iliyosabisha Edson auawe ni baada ya kuazisha mahusiano na Peniela ,kwani Peniela alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Dr Joshua”
“ What ??!! Anna akastuka sana
“ Usishangae Anna huo ndio ukweli.Peniela na baba yako wana mahusiano ya siri ya kimapenzi.Alipogundua kwamba Peniela na Edson wana mahusiano Dr Joshua alichukia mno na akatoa amri Edson auawe’
“ Siamini kama hicho unachonieleza ni kitu cha kweli” akasema Anna huku akitokwa na machozi ,Mathew akaendelea
“ Kitu kingine tulichokibaini ni kwamba Edson alikuwa na mtandao wake ambao walimtumia kuiba nyaraka Fulani ikulu.Nyaraka hizo zilikuwa na kanuni ya kutengeneza kirusi hatari kinachoweza kusababisha maangamizi makubwa.”
Anna akashika kichwa kwa mshangao.Muda ulizidi kwenda na Mathew akaendelea
“ Wakati tukiendelea na uchunguzi ,tukagundua uwepo wa kikundi fulani cha watu wachache kijulikanacho kama Team SC41.Kikundi hiki kipo hapa nchini na kinaendesha shughuli zake kwa siri kubwa na kazi zake ni kulinda maslahi ya Marekani hapa nchini.Tuligundua kwamba Peniela naye n mmoja wa Team SC41 na mahusiano yake na Dr Joshua yalikuwa ni kwa sababu maalum.Team Sc41 kuna kitu fulani wanakitafuta toka kwa Dr Joshua ambayo ni package Fulani ambayo imehifadhiwa mahala pa siri ndani ya ikulu na ndani ya package hiyo kuna kirusi hatari kinachoitwa Aby.Hiki ni kirusi hatari kwa dunia kwani hakina kinga wala tiba hadi sasa na kinaweza kuleta maangamizi makubwa duniani endapo kitaachiwa kisambae hewani.Dr Joshua kwa kushirikiana na washirika wake wa karibu akiwemo Dr Kigomba wanataka kukiuza kirusi hicho kwa pesa nyingi mno.Katika mpango huo Dr Joshua anashirikiana na washirika wake wa karibu ambao ni Dr Kigomba na Captain Amos ambaye kwa sasa ni marehemu”
“ Dr Amos is dead?? Anna akazidi kushangaa
“ yes he’s dead” akajibu Mathew
“ Oh my God ! what’s going on? Akajiuliza Anna
“ Captain Amos” Mathew akaendelea
“ Alikuwa katika kundi moja na Peniela la Team SC41na wote wawili kwa pamoja walikuwa na lengo la kukipata kirusi hicho” Mathew akatulia kidogo halafu akaendelea
“ Marehemu Dr Flora alifahamu kuhusu mpango huu wa Dr Joshua kukiuza kirusi Aby na akajitahidi sana kutaka kuzuia jambo hili lisifanyike kwani aliyafahamu madhara yake lakini akashindwa .Hatua ya mwisho aliyotaka kuichukua ni kwa kuwaelezeni ukweli wewe na Flaviana lakini hakuweza kufanya hivyo kwani alifariki ghafla kabla hajawaelezeni chochote.Kifo chake kilitokana na kuchomwa sindano ya sumu na aliyefanya hivyo kwa amri ya rais ni Captain Amos.”
Haikuwa rahisi kwa Anna kukubali moja kwa moja kama baba yake angeweza kufanya kitendo kama kile
“ No ! No ! No !...baba yangu katu hawezi kufanya kitendo kama hicho.Tafadhali naomba usizidi kunichanganya kichwa changu!! Please tell the truth who killed my mother?? Akauliza Anna huku akilia.
“ Baada ya kifo cha Dr Flora,kuliwekwa zuio la kutaka kufanya uchunguzi wa kubaini sababu za kifo chake bali ikatolewa sababu nyepesi tu kwamba ni shinikizo la damu.Flaviana hakuridhika na kilicho kuwa kinaendelea akamuomba mumewe jaji Elibariki amsaidie kupata ukweli kuhusu kifo cha mama yake.Jaji Elibariki alinifuata na kuniambia nimsaidie kuupata ukweli huo.Haikuwa kazi nyepesi lakini mwishowe tulifanikiwa kujua kilicho muua Dr Flora .Jaji Elibariki aliwasilisha kwenu ripoti ya uchunguzi tulioufanya lakini Dr Joshua kwa kufahamu kwamba ilikuwa inasema ukweli aliipinga vikali.Kutokana na ripoti ile tayari Dr Joshua akaingiwa na wasi wasi na ili siri ya Dr flora isivuje iliamriwa kwamba jaji Elibariki auawe kwani tayari alikwisha kuonekana ni mtu hatari kwao.Lilipangwa shambulio la kushtukiza na katika shambulio hilo jaji Elibariki akanusurika kufa baada ya kuokolewa na mmoja wa washirika wangu aliyekuwa naye garini .Noah alipoteza maisha wakati akimuokoa Elibariki asiuawe kwa risasi.Shambulio hilo lililopofanyika alitokea mwanamke mmoja ambaye hadi leo hatujamfahamu ambaye alimchukua Elibariki na kumpeleka kwa Peniela”
“ Peniela again? Akauliza Anna kwa mshangao
“ Anna I’m sorry to tell you this but Peniela na Elibariki walikuwa na mahusiano ya siri”
“ This woman is a devil!!...Mpenzi wangu ,baba yangu,shemeji yangu wote ni wapenzi wake,what kind of a woman is she?? Everywhere Peniela ,Penelal!!! Akasema Ana kwa ukali.Mathew hakumjali akaendelea
“ Kama nilivyokueleza awali kwamba Peniela ni mwanamke anayetumiwa kufanya kazi maalum na Team SC41.Ukimuona yuko na mwanaume Fulani basi fahamu kwamba si kwa ajili ya mapenzi bali kuna kitu anakitafuta.Jaji Elibariki baada ya kunusurika kuuawa yeye mwenyewe alichagua kujificha kwa Peniela na baadae akanipigia simu nikaenda kumchukua na kumuhifadhai nyumbani kwangu . Kuna mambo mengi ambayo tumeyagundua lakini kutokana na muda sintoweza kukueleza yote ila kuna jambo moja nataka ulifahamu.Tuligundua kwamba kuna mtu mmoja tajiri aishiye nchini Saudia Arabia ambaye ndiye mnunuzi wa kirusi hicho na ambaye alitakiwa kuingia nchini jana kuja kukichukua kirusi hicho.Bado sijafahamu huyu Hussein ni nani na ana malengo gani na kirusi hicho ila ninachokifahamu ni kwamba Marekani kwa kutumia Team SC41 wanakutaka kirusi hicho ili kuleta maafa makubwa hapa nchini kwa lengo la kuchota rasilimali za nchi.Kama hili litafanikiwa maelfu ya watu wataangamia kwani kirusi Aby kunasambaa kwa njia ya hewa na ndani ya muda mfupi maelfu ya watu wataangamia”
“ Oh my God…!! Akasema Anna kwa woga
“ Jaji Elibariki akiwa mafichoni ,msako mkali uliendeshwa na jeshi la polisi wakimtafuta kwa kusababisha kifo cha Flav……”
“ Hebu ngoja kwanza Mathew” Ana akamkatisha Mathew
“ Bado hujanieleza ni nani aliyemuua Flaviana ?
“ Oh sorry nilijisahau ,mambo ya kukueleza ni mengi.Kuhusu kifo cha Flaviana ni kwamba baada ya Dr Joshua kuikataa taarifa aliyoileta jaji Elibariki kuhusiana na kilichosababisha kifo cha Dr Flora, walitengeneza ripoti ambayo walidai kwamba ni ya madaktari bingwa toka katika hospitali kuu ya taifa .Jaji Elibariki alitaka kuipata taarifa hiyo ili tufanye uchunguzi kubaini ukweli kwa hiyo akampigia simu na kumuelekeza sehemu ya kukutana ili aweze kumpatia zile karatasi .Flaviana hakujua kama kulikuwa na watu waliotumwa kumfuatilia ambao dhumuni lao ni kumpata Elibariki.Baada ya kufika sehemu tulikopanga wakutane likatokea shambulio la ghafla na katika shambulio hilo Flaviana akajeruhiwa kwa risasi na hivyo ndivyo sababu ya kifo chake.Hata hivyo tulipata taarifa hiyo na tukaifanyia kazi tukabaini haikuwa na ukweli wowote kwani madaktari wale wote walioorodheshwa katika taarifa hivyo kwamba walishiriki kufanya uchunguzi kubaini kifo cha Dr Flora hakuna hata mmoja anayefanya kazi katika hospitali kuu ya taifa wala hawapo katika orodha ya madaktari nchini”
“ Jesu Christ !!!..akasema Anna.Mathew akaendelea
“ Dr Joshua alipata fununu kwamba jaji Elibariki na Peniela wana mahusiano na kwamba amejificha nyumbani kwa Peniela.Ili kupata uhakika kuhusu hilo akamtuma Dr Kigomba amchunguze lakini naye akajikuta akianguka katika mahusiano na Peniela.
“ Again???.Peniela again???.Jamani huyu mwanamke ana tatizo gani? Mbona wanaume wote mji huu ni wake? Anna akazidi kushangaa
“ Kama nilivyokueleza Anna ni kwamba Peniela akiwa katika mahusiano na mtu huwa ni kwa ajli ya jambo Fulani lakini kwa Dr Kigomba hakuwa akifanya kazi ya Team SC41 bali alikuwa anashirikiana na sisi “
“ My God !!!even you?? .. akasema Anna kwa mshangao
“ Naomba nikuweke wazi Anna kwamba kwa sasa tunafanya kazi pamoja na Peniela “
“ No ! that’s not true !!! Tell me its not true ..” akasema Anna
“ Its true Anna ila ni hadithi ndefu kidogo nitakueleza siku nyingine ila kwa sasa naomba uelewe hivyo kwamba tunafanya kazi bega kwa bega na Peniela” akasema Mathew na kwa sekunde kadhaa wakabaki wanatazamana
“ Juzi usiku nilimsindikiza Peniela nyumbani kwake na wakati tukirejea akataarifiwa na mmoja wa vijana toka Team SC41 kuwa achukue tahadhari kuna watu wanamfuatilia.Usiku huo yakatokea mapambano kati yetu na watu waliotumwa kumfuatilia Peniela.Tulizidiwa nguvu lakini tulifanikiwa kuwatoroka na tulipofika kurejea nyumbani kwa Peniela tulikuta nyumba yake inateketea kwa moto.Wakati sisi tukipambana na Team SC41 ,nyumbani kwangu pia kulitokea tukio baya.Jaji Elibariki alimpiga Anitha na kitu kizito kichwani akapoteza fahamu ,akamfungua Rosemary Mkozumi wakaiteketeza nyumba kwa moto wakamchukua mateka Anitha na kuondoka naye.Anitha alipelekwa kwa Rosemary Mkozumi ambako aliteswa sana ili aeleze mahala nilipo lakini kwa jitihada zake binafsi alifanikiwa kutoroka na kuungana nami tena.Jaji Elibariki amerudisha nyuma juhudi zetu zote za kukipata kirusi Aby.Mpaka sasa hatufahamu ni kwa nini alifanya vile .Hata hivyo baada ya haya yote kutokea tumejipanga upya na tunaendelea na operesheni yetu ya kuhakikisha tunakipata kirusi Aby na kuzuia maangamizi makubwa yanayoweza kutokea nchini kwetu au sehemu nyingine yoyote ambako kirusi hiki kingeweza kuachiwa hewani.Kwa hiyo Anna nimekuita hapa nikueleze ukweli wa kila kinachoendelea ili tusaidiane mosi kukipata kirusi Aby na kuiepusha nchi yetu na dunia dhidi ya janga kubwa linaloweza kutokea iwapo kirusi Aby kitaachiwa kisambae hewani.Pili kuhakikisha kwamba wale wote waliohusika katika vifo vya mama na dada yako wanafikishwa katika vyombo vya sheria bila kujali ni akina nani.Katika kufanikisha haya tunahitaji mno msaada wako” akasema Mathew.Anna akainama na baada ya kama dakika mbili akafuta machozi na kusema
“ First I want to tell you that I believe you” Anna akafuta machozi tena na kuendelea
“ Bnafsi nilikwisha hisi kuna jambo linaloendea na hata usiku ule Flaviana aliposhambuliwa nilikuwa naye ila aliniacha sehemu nikimsubiri na kabla hatujaachana ,tuliongea kuhusu jambo hilo na baada ya kuchambua masuala kadhaa tukapata picha kwamba kuna kitu kinachoendelea.Nikiwa afrika ya kusini nilimpigia simu jaji Elibariki na nikamtaka anieleze ukweli kama baba anahusika katika matukio yale ya vifo vya mama na dada na akanihakikishia kwamba ni kweli baba ndiye muhusika mkuu wa matukio yale yote.Tulipanga na kuongea zaidi pindi nitakaporejea toka afrika ya kusini lakini nilistuka jana usiku nilipomuona Elibariki akiwasili msibani akiwa ameongozana na baba.Sikuweza kupata nafasi ya kumuhoji yeye wala baba.Leo asubuhi nimetolewa taarifa katika vyombo vya habari kwamba kuna majambazi wameuawa usiku wa kuamkia leo katika msitu wa Makenge.Kwa mujibu wa taarifa hizo ni kwamba majambazi hao ndio waliokuwa wamemteka jaji Elibariki na ndio waliohusika katika kusababisha kifo cha Flaviana.Baada ya mazishi ya Flaviana nilitaka nimtafute nimuhoji lakini alikuwa amesongwa sana na watu wakimpa pole na baadae alifika mkuu wa polisi kanda ya Dar es salaam akaondoka naye.Sikuweza kumfuatilia tena kwani Kareem alifika na kunichukua akanileta huku.Mathew maelezo uliyonipa yamenifumbua macho na sasa nimeelewa kilichotokea na kinachoendelea .Nashukuru kwa kunieleza ukweli halisi bila kujali kama ukweli huo utaniumiza ama vipi.Ni kweli nimeumia mno kwa mambo uliyonieleza na hasa kwamba baba yangu ndiye muhusika mkuu wa matukio ya vifo vya mama na Flaviana.Kwa namna moyo wangu unavyosononeka kwa vifo vya watu niliowapenda na kwa sababu hiyo nitaungana nanyi katika kuhakikisha wale wote waliosababisha vifo hivyo awe ni baba au nani lazima wanafikishwa mbele ya sheria.Tafadhali naomba nieleze Mathew unahitaji nini ili tuweze kuwafikisha hawa watu mahakamani? Unahitaji nikusaidie jambo gani? Niko tayari kufanya jambo lolote hata kama ni la hatari kiasi gani ili mradi nihakikishe watuhumiwa wote wanafikishwa mbele ya sheria tukianza na baba yangu.” Akasema Anna huku akifuta machozi.Mathew akamtazama kwa makini usoni
“ She’s deeply hurt and she’s ready to do anything.Huyu atakuwa msaada mkubwa kwetu” akawaza Mathew.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………
Ni tamu vile vileNzuri
Ipo bomba namimi nianze kuifuatilia ?Hii story imenifanya nilale saa nane usiku na Leo Niko kama teja daahh!
Mnooo!Ipo bomba namimi nianze kuifuatilia ?