Peniela (Story ya kijasusi)

wadau mm mpenzi wa mpira .nimshabiki wa liverpool inacheza someni hizo 2 .game ikiisha nabwaga mzigo mwingine
Lege naona levepool mkiwa kwenye kiwango bora kabisa mpaka sasa mshampiga mtu viwili na chelsea wanautafta kwa tochi ni iman yangu kua ukija utashusha seson 3 yote kutoka na furaha ya ushindi mtakaoupata
 
PENIELA SEASON 3

EPISODE 1



ILIPOISHIA SEASON 2


“ John this is the last chance ..are you Peniela’s father? Akauliza Mathew kwa ukali.John akajibu kwa kumfanyia ishara kwamba haelewi chochote.Mathew akakasirika na kuchomoa bastora yake.Peniela akaogopa sana
“ Mathew what are yo doing? Akauliza lakini Mathew hakumjali
“ Mathew unataka kufanya nini? Akauliza Peniela kwa wasi wasi

“ I’ll count to three and if you cant answer me I’m going to kill you John ! akasema kwa ukali Mathew

“ Mathew No ! Don’t do that !! akasema Peniela huku akilia
“ Jason hold her” Mathew akamuamuru Jason amshike Peniela ili asimsogelee.
“ Three…..!!!akaanza kuhesabu Mathew huku amemuelekezea John bastora

“ Two ….!!!!

“ Mathew noo!!!!..dont do that !!..akapiga kelele peniela.
“ On………..” Kabla Mathew hajamaliza kutamka John Mwaulaya akasema
“ Ok ok..I’ll tell you..put your gun down” akasema John mwaulaya aliyekuwa akitetemeka

“ ok tell her the truth! akasema kwa ukali Mathew huku akimtazma John kwa macho ya hasira
John akamfanyia ishara peniela asogee karibu na kuanza kumsimulia kilichotokea kuhusiana na wazazi wake.Alisimulia mkasa mzima uliotokea na kupelekea kuwaua wazazi wote wa peniela.Peniela alibubujkwa na machozi mengi.John akamgeukia Mathew

“ Hiyo ndiyo historia ya Peniela.Nilishindwa kabisa namna ya kumueleza nikiogopa kumuumiza na ndiyo maana nilitaka afahamu kuhusu yeye baada ya mimi kufariki dunia.Nilijua lazima atanichukia sana akifahamu kwamba mimi ndiye niliyewaua wazazi wake.Nilimuwekea kila kitu kuhusiana na historia yake katika makasha matatu ikiwamo na picha za wazazi wake.” Akasema John.Peniela alimuangalia kwa hasira huu machozi yakimtoka.

“Leo nilikuja kwa ajili ya Peniela.Safari ijayo nitakuja rasmi kwa ajili yangu.Jiandae “ akasema Mathew na kutoka Peniela akamfuata
“ Mathew thank you so much.Umenisaidia nimefahamu jambo kubwa sana.Sikuwa nikifahamu chochote kuhusiana na wazazi wangu.John amenificha siri hii kwa miaka mingi.I hate that bastard so much.”akasema Peniela
“ Elibariki aliniomba nikusaidie kuufahamu ukweli kuhusiana na asili yako na ninashukuru ukweli umedhihiri.Naomba ukweli huu usivuruge mipango yetu.”
“hakuna kitakachovurugika Mathew.I’m a very strong woman.Kila kitu kitakwenda kama tulivyokipanga.hata hivyo nina swali nataka kukuuliza.”

“ Uliza Peniela”

“ Ulipomuelekezea John bastora na kuanza kuhesabu,ulidhamiria kumpiga risasi kama asingesema chochote ?
Mathew akatabamu kidogo na kusema

“ No ! I just wanted him to talk”
“ ahsante Mathew.Ahsante sana.Tutaonana jioni .Mwambie Elibariki nashukuru sana kwa kunijali.Bila yeye kuwa na mawazo haya nisingeufahamu ukweli kuhusu wazazi wangu“ akasema peniela na kurejea tena ndani akakuta hali ya John mwaulaya imebadilika ghafla.Ikawalazimu wawaite haraka wale madaktari wawili waliokuja toka marekani kwa lengo la kuja kuangalia afya yake.



ENDELEA SEASON 3
EPISODE 1 ……………………..


Saa saba na dakika ishirini za mchana,gari zipatazo saba ziliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Anna mtoto wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akashuka toka mojawapo ya magari yale na kuongozana na maafisa wa usalama pamoja na ndugu wengine alioambatana nao hadi katika sehemu ya kupumzikia.Katika siku hii ya leo binti huyu mrembo aliyafunika macho yake yaliyokuwa mekundu kwa miwani myeusi . Ni wazi ilionyesha alikuwa Amelia sana.
Dakika kumi baadae kikasikika king’ora cha gari la wagonjwa likiwasili pale uwanjani.Gari hili lilimbeba Flaviana akitokea katika hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda afrika ya kusini kwa matibabu zaidi.Bila kupoteza muda madaktari na wauguzi wakasaidiana kumshusha Flaviana toka ndani ya gari lile la wagonjwa akiwa bado hana fahamu na kuingizwa moja kwa moja katika ndege iliyokwisha andaliwa maalum kwa ajili ya kumsafirisha kuelekea afrika ya kusini.Taratibu zilipokamilika Anna akaagana na ndugu zake na watu wengine alioambatana nao na kuanza kupiga hatua kuelekea ndegeni.Kabla hajakanyaga ngazi za ndege ,mmoja wa walinzi akamkimbilia na kumpa simu

“ Mzee anataka kuongea nawe” akasema Yule mlinzi.Anna akachukua simu na kuiweka sikioni.
“ Hallow dady “ akasema Anna.Dr Joshua akasikika simuni akivuta pumzi ndefu kisha akasema
“ Hallow Anna.Tayari kila kitu kimekamilika?
“ Ndiyo baba.Kila kitu kimekamilika na kwa sasa tunaingia ndegeni tayari kwa safari”
“ Sawa Anna.Ningependa sana kuongozana nanyi kuelekea huko afrika ya kusini lakini kikao kile cha wakuu wa nchi za afrika ya mashariki ni cha muhimu sana kuna mambo ya msingi sana ambayo yananilazimu niwepo .Hata hivyo jioni baada ya kumaliza kikao nitakuja kuungana nanyi huko afrika ya kusini” akasema Dr Joshua
“ Usijali baba ninaelewa majukumu uliyonayo .Tuzidi kumuombea Flaviana aweze kupona” akasema Anna.
“ Ni kweli Anna inatubidi tusimame pamoja kama familia na nina hakika Mungu atamponya Flaviana.Mungu awatangulie katika safari yenu na mfike salama” akasema Dr Joshua na kuagana na Anna kisha akakata simu. Anna akarejesha simu kwa Yule afisa wa usalama akapanda ndegeni na mlango ukafungwa.Haikuchukua muda mrefu ndege ikapaa na kuelekea afrika ya kusini.Michirizi ya machozi ikaonekana machoni kwa Anna.
“ Ee Mungu msaidie dada yangu Flaviana aweze kupona.Bado ninamuhitaji sana katika maisha yangu.” Anna akaomba kimya kimya huku akijifuta machozi.Shangazi yake aliyekuwa pembeni yake akamuonea huruma sana na kumshika bega

“ Anna usilie,utazidi kuumiza kichwa.Flaviana atapona tu” shangazi yake akamfariji

“ Shangazi ninaumia sana kwa mambo yanayotokea katika familia yetu.Kwanza alifariki mama,Elibariki mume wa Flaviana akanusurika katika shambulio na hata muda haujapita Flaviana naye anapatwa na janga hili kwa kweli mambo yanayoumiza sana.Mambo mazito yametokea katika kipindi kifupi sana” akasema Anna.Shangazi yake akamtazama akamuonea huruma sana na kusema

“ Anna unatakiwa uwe jasiri sana kwani kwa sasa sote tunapita katika kipindi kigumu sana.Ni wakati wa kumuomba Mungu awape nguvu ya kuhimili misuko suko hii mizito.Nina hakika kabisa vyombo vya usalama viko macho na vitamsaka na kuhakikisha vinampata huyu aliyemfanyia Flaviana ukatili huu mkubwa.Sikuwahi kufikiria hata siku moja kama jaji Elibariki angeweza kufanya jambo kama hili la kikatili kwa mke wake wa ndoa.Sijui ni shetani gani aliyemuingia na kumshawishi akafanya ukatili huu mkubwa uliopitiliza.Ninakuhakikishia Anna kwamba hataweza kujificha kamwe na na atapatikana tu ili aweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria” akasema shangazi yake anna
“ Kwa kweli inashangaza sana kwa kitendo alichokifanya Elibariki.Ni wazi alikuwa na lengo la kuua kabisa” akasema Anna halafu ghafla akakumbuka kitu
“ Kuna kitu bado kinanipa mashaka sana kuhusiana na tukio hili la kushambuliwa Flaviana.Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inasema kwamba Elibariki alipanga shambulio lile kutokana na wivu wa mapenzi akitaka kulipiza kisasi kwa Flaviana baada ya kugundua kwamba Flaviana alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje ya ndoa.Ninapata mashaka kidogo kukubaliana na kauli hii kwa sababu ninamfahamu vyema Flaviana hakuwa na tabia hii na hata siku moja hakuwahi kunieleza kama ana mahusiano ya siri nje ya ndoa yake.Ninafahamu ndoa yao ilitawaliwa na migogoro mingi lakini hata siku moja Flaviana hakuwani kunieleza chochote kuhusiana na kuwa na mpenzi nje ya ndoa na wala kuwa na hisia za kuwa na mahusiano mbadala.Kama ingekuwa ni kweli tayari angekwisha nieleza kwani mimi ndiye niliyekuwa msiri wake mkubwa na hata siku moja hajawahi kunificha jambo lolote hata liwe kubwa kiasi gani.Hii inanipa ugumu sana kukubaliana na kauli hii eti ya kwamba shambulio lile lilikuwa ni kwa ajili ya kulipiza kisasi.Kingine kinachonipa mashaka nisikubaliane moja kwa moja na kauli hii ya jeshi la polisi ni utayari wa Elibariki kutenda jambo kama hili la kutaka kumtoa uhai mke wake.Mimi na Elibariki hatukuwa katika maelewano mazuri kwa muda mrefu na baada ya kufanya maamuzi ya kesi ile iliyomkabili Peniela tulizidi kuwa maadui zaidi lakini pamoja na yote yaliyotokea kati yetu ninamfahamu vizuri Elibariki hana roho mbaya kiasi hicho hadi kufikia hatua ya kutaka kuua.Ni mmoja kati ya wanaume wavumilivu sana .Ninamfahamu dada yangu ni mkorofi na ana matatizo yake lakini Elibariki amevumilia mambo mengi sana toka kwa Flaviana kwa sababu alimpenda sana.Nakumbuka wakati wa msiba wa mama ni Elibariki aliyehatarisha uhai wake kwa kufanya uchunguzi kuhusiana na kile kilichomuua mama na alifanya hivi kwa ombi la Flaviana.Amenusurika katika shambulio ambalo polisi wanadai kwamba lilifanywa na mtu ambaye anasadikiwa kuwa katika mahusiano na Flaviana kwa lengo la kutaka kumuua Elibariki na baada ya hapo Elibariki akapotelea mafichoni.Akiwa huko aliwasiliana na Flaviana usiku ule na kumtaka afanye juu chini ili aipate taarifa ile ya madaktari bingwa waliofanya uchunguzi kuhusiana na kilichosababisha kifo cha mama.Kuhusiana na taarifa ile ninapata shaka kidogo namna baba alivyoweza kumpatia taarifa ile kwa haraka na wepesi wakati hapo kabla hakuwa tayari kabisa taarifa ile iguswe na mtu mwingine yeyote zaidi yake.Kuna picha ambayo nimeanza kuipata hapa nikiunganisha matukio haya yote nikianzia na kifo cha mama na hadi shambulio la Flaviana.” Akawaza Anna
“ Ukiunganisha mtiririko wa matukio utagundua kwamba kuna jambo linaloendelea.Kwa picha ninayoipata nashawishika kuamini kwamba si Elibariki aliyefanya kitendo kile cha kumshambulia Flaviana.Alichokuwa akihitaji Elibariki usiku ule ni taarifa ile ya madaktari na hakuwa na lengo la kumdhuru Flaviana.Kama si yeye aliyefanya shambulio lile nani basi alitaka kumuua Flaviana na kwa nini? Akajiuliza Anna

“ Kuna kitu nimekumbuka.Siku ile usiku Flaviana alikuja chumbani kwangu na kutumia simu yangu kuwasiliana na Elibariki.Bado zile namba alizotumia zipo katika simu yangu.Nadhani ni yeye ndiye ana majibu yote ya kilichotokea usiku ule.Kwa kuwa nimeondoka na simu yangu nikifika afrika ya kusini nitafanya mawasiliano na Elibariki kwa kutumia namba ile ya simu .Ni yeye pekee kwa sasa ambaye anaufahamu ukweli wa kilichotokea usiku ule” Anna alizama katika mawazo mengi sana.
“ Nakumbuka usiku ule tulijadiliana na Flaviana kuhusiana na mambo yanayotokea ndani ya familia yetu tukianzia na kifo cha mama.Tuligundua kwamba baba hakuonyesha kabisa kuweka uzito katika kufuatilia chanzo cha kifo cha mama Tabia aliyoionyesha baba toka wakati wa msiba wa mama inatia shaka sana.Nilimsikia kwa masikio yangu Dr Kigomba akitoa amri ya kuwakamata madaktari waliokuwa wakitaka kufanya uchunguzi wa kilichomuua mama lakini baba alidiriki kusimama na kumtetea Dr Kigomba kwa nguvu zote.Hata mimi ninaanza kupata picha Fulani ambayo si nzuri kuhusiana na baba na matukio yaliyotokea.Kuna ulazima wa kulifanyia uchunguzi jambo hili na kwa hili Elibariki anaweza kuwa na msaada mkubwa sana kwangu” akaendelea kuwaza Anna halafu akajiegemeza kitini na kijiusingizi kikampitia



********

Madaktari wawili waliongozana na Nickson Strawberry kutoka Marekani walirejea haraka sana nyumbani kwa John Mwaulaya baada ya kutaarifiwa kwamba hali ya John Mwaulaya ilibadilika ghafla.Wote walishangaza sana na mabadiliko yale ya ghafla ya hali ya John.Si muda mrefu sana walipoongea naye na alionekana kutokuwa katika hali mbaya sana kama aliyokuwa nayo sasa.Bila kupoteza wakati wakatoa mashine zao na kuwaomba Peniela na John watoke mle chumbani isipokuwa Martin ambaye ana taaluma ya udaktari na ambaye amekuwa akimuhudumia John kwa muda mrefu.

“ I’m so scared Josh.I don’t know if he’s going to make it…” akasema Peniela kwa wasi wasi mkubwa wakiwa nje ya mlango wa chumba cha John Mwaulaya .John akamtazama na kumshika bega
“ Usiogope Peniela.John atapona.He’s a strong man and he’s going to survive” Josh akampa Peniela maneno ya faraja.Peniela akafuta machozi na kusema
“ Pamoja na mambo mengi mabaya aliyoyafanya John Mwaulaya kwangu na kwa wengine lakini yeye ni sababu ya mimi kuwepo hapa nilipo.Alipewa amri aniue lakini hakufanya hivyo na badala yake aliniacha hai na akahakikisha ninalelewa vyema.Japokuwa nimeishi bila ya wazazi wangu lakini nimeishi maisha mazuri na kupatiwa kila kitu na hii yote ni kwa sababu ya John .Ingawa ni mtu mwenye roho ngumu na ya kikatili lakini ana sehemu ndogo ya huruma na upendo ndani ya moyo wake na ndiyo maana hakudiriki kuniua.Nikipima kati ya mazuri na mabaya aliyonifanyia ninakuta mazuri ni mengi kuliko mabaya kwa hiyo nina deni kwake” akasema Peniela
“ Uko sahihi Penny.John ni mtu katili lakini ana huruma sana.Yeye ndiye aliyeniokota toka katika maisha yangu mabaya niliyokuwa nayo na akanifikisha hapa.Nimekuwa mlinzi wake kwa muda mrefu na nimejifunza mambo mengi toka kwake .John ameniamini sana kuliko mtu mwingine yeyote na kwa mambo mengi aliyonifanyia hata mimi ninadiriki kukiri kwamba nina deni kuwa kwake” akasema Josh

“ Mungu amsaidie John apone” akasema Peniela akiwa ameifumbata mikono kifuani.Josh akakaa kimya halafu akasema

“ Peniela do you trust these guys? Are they real doctors?

“ Kwa nini unauliza hivyo Josh ? akauliza Peniela

“ Nina mashaka kidogo na hawa watu wanaotoka Marekani wakidai kutaka kumtibu John.Awali John hakuonyesha kukubaliana nao na ndiyo maana alinituma nimuue Dr Burke.Aliniambia kwamba Dr Burke hakuwa na lengo la kuja kumtibu bali kumuua” akasema Josh na Peniela akamtazama Josh kwa wasi wasi na kuuliza

“ John alikueleza ni kwa nini Dr Burke alitaka kumuua? Kwa nini Team Sc41 wanataka kumuua?
“ Peniela mimi nimekuwa mtu wa karibu na John Mwaulaya kwa muda mrefu lakini nakuhakikishia John ni mtu msiri sana.Maisha yake yamezungukwa na siri nyingi kwa hiyo sifahamu mpaka leo sababu ya Dr Burke kutaka kuja kumuua” akasema Josh.Peniela akainama kidogo akafikiri na kusema
“ Josh hisia zako zinaweza kuwa za kweli.Hatupaswi kuwaamini hawa watu hata kidogo.Nina hakika lazima ipo sababu iliyopelekea Dr Burke kutaka kumuua John.Nilikwisha wasiliana na daktari mmoja ambaye ni rafiki yake mkubwa na John na anajiandaa kuja kumfanyia John upasuaji.Maandalizi yamekwisha kamilika na wanaosubiriwa ni madaktari hao tu wafike na kuifanya operesheni hiyo.Kinachonishangaza ni kwamba nimewaeleza akina Edwin kuhusiana na suala hili na wamelipinga vikali.Hawataki kabisa mtu yeyote ambaye hawamjui ashughulike na ugonjwa wa John.Wanadai kwamba hakuna haja ya kuwaleta madaktari kwa kuwa wao wanatosha na wamekuja kwa ajili ya kazi hii moja ya kumtibu John,hata hivyo sina kabisa imani na watu hawa na ndiyo maana nimefikiria ku…..” Peniela akataka kusema kitu lakini akastuka
“ Ouh my gosh ! nimejisahau na kutaka kutamka mpango wangu wa kuimaliza team SC41 mbele ya josh.Huu ni mpango wa siri ambao hatakiwi kuufahamu mtu mwingine yeyote toka ndani ya team sc41” akawaza Peniela
“ Umesema unafikiria kufanya nini Peniela? Akauliza Josh

“ Nafikiria namna ya kumsaidia John.We cant just sit here and give these guys chance to kill him.We have to get in there and see what they are doing” akasema Peniela huku akianza kupiga hatua kuuelekea mlango wa chumba cha John lakini Josh akawahi kumshika mkono.

“ Hapana Peniela hatuwezi kuingia humo ndani kwa sasa.Tuwaache kwanza wafanye kazi zao ila tusiache kuwafuatilia kwa karibu kuona kama kweli wana lengo la dhati la kumtibu John” akasema Josh
“ Ndani ya chumba cha John Mwaulaya madaktari wale wawili toka marekani wakisaidiana na Dr Martini ambaye amekuwa akimuuguza John mwaulaya kwa muda mrefu waliendelea na jitihada za kuhakikisha hali ya John inarejea kuwa ya kawaida.Wakati kazi hiyo ikiendelea mmoja wa madaktari wale ambaye alikuwa karibu sana na Martini akamuuliza
“ Dr Martin hebu nieleze nini hasa kilichotokea na kusababisha hali ya John kubadilika ghafla na kuwa mbaya kiasi hiki? Kuna dawa yoyote au sindano uliyomchoma iliyopelekea hali yake kubadilika ? akauliza Dr Edwin Hurdosn.Swali lile likambabaisha kidogo Martin kulijibu.

“ Martin nini kilitokea na kusababisha hali ya John iwe hivi? Akauliza tena Dr Edwin
“ Hakuna dawa niliyompa ambayo imebadilisha hali yake kuwa hivi.Dawa alizotumia ni zile ambazo amekuwa akizitumia kila siku .Hali yake ilibadilika ghafla tu” akasema Martin

“ Martin tumekuja sisi toka Marekani kwa ajili ya kazi moja tu ya kushughulikia ugonjwa wa John na kulifahamu tatizo lake.Hili si suala dogo kama unavyofikiria kwani John ni mtu mwenye nafasi ya juu sana ndani ya Team Sc 41 kwa hiyo ugonjwa wake unapewa uzito mkubwa.Mimi na mwenzangu ni mabingwa katika mishipa ya fahamu na tuna hakika tutaokoa maisha ya John lakini tunahitaji sana taarifa kamili za kuhusiana na ugonjwa wake.Najua tutayaongea hayo baadae kidogo lakini kwa sasa tunatakiwa kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kurejesha hali yake iwe kawaida ndipo tuanze kuchukua vipimo na kugundua tatizo lake kwa maana hiyo tunahitaji kufahamu ukweli kama kuna dawa yoyote ulimpa au kuna sindano ulimchoma kabla ya kuendelea na matibabu mengine”
Martin akabaki kimya akitafakari

“ Martin !!!!..Edwin akamstua

“ Toka asubuhi hali ya John ilikuwa nzuri na alitumia dawa zile zile ambazo amekuwa akizitumia siku zote .Kilichotokea ni kwamba baada ya nyie kuondoka kuna watu Fulani waliingia ghafla kuja kuonana na John” akasema Martin
“ Watu ?!!..Andrew akashangaa
“ Watu gani hao? Walifuata nini? Akauliza
“ Watu hao mimi siwafahamu ila wanafahamiana na Peniela”
“ Hauwafahamu? Hujawahi kuwaona watu hao hapo kabla? Unakumbuka waliongea nini na John? Dr Edwin akauliza maswali mfululizo.Wakati huo mwenzake aitwaye Alexander Piscat aliyekuwa akishughulika kuweka sawa baadhi ya mashine alikwisha maliza kuunganisha mashine ile na kuwasogelea akina Edwin.
“ Edwin kila kitu tayari sasa tunaweza kuendelea na kazi yetu” akasema Dr Alex
“ Kabla hatujaendelea ,nilitaka kufahamu kilichotokea na kusababisha hali ya John kubadilika ghafla.Kuna jambo Martin amenieleza limenistua kidogo.Anasema kuna watu walifika nyumbani kwa John ambao hawafahamu na hajawahi kuwaona pale na walizungumza na John na baada ya hapo ndipo hali yake ilipobadilika ghafla” akasema Dr Edwin

“ Martin ni akina nani hao waliokuja nyumbani kwa John? Akauliza Dr Alex

“ Siwafahamu watu hao ni mara yangu ya kwanza kuwaona lakini wanafahamiana na Peniela” akasema Dr Martin halafu akasita kidogo na kuendelea
“ Martin tafadhali naomba utueleze kila kilichotokea.Watu hao walihitaji nini na waliongea kitu gani na John? Akasema Alex

“ Nilikuwa humu chumbani nikiwa na Peniela na mara mlango ukafunguliwa akaingia Josh akiwa ameongozana na watu wawili ambao siwajui ila Peniela alionekana kuwafahamu watu hao kwani aliwaita hata kwa majina yao Mathew na Josh.Kwa jinsi nilivyoona watu wale walikuwa wakifahamiana na John kwa sababu baada tu ya kuwaona John alistuka sana.Yule jamaa aitwaye Mathew alimtazama John kwa ukali na ninakumbuka maneno Fulani aliyasema.Alisema kwamba japokuwa ni miaka mingi imepita lakini ana uhakika John atakuwa akimkumbuka vyema.Aliendelea kusema kwamba kwa siku ya leo hakuja kwa ajili yake bali kwa ajili ya Peniela.”
“ alikuja kwa ajili ya Peniela? Dr Alex akauliza

“ Ndiyo .Alitaka John aeleze ukweli kuhusiana na historia ya Peniela.Alimtaka John aeleze wazi wazi mahala waliko wazazi wa Peniela.”
“ John alijibu nini? Akauliza Edwin
“ John alikataa kutofahamu chochote kuhusiana na walipo wazazi wa Peniela ndipo Mathew alipochomoa bastora na kumlenga John.Alitishia kumpiga risasi na akaanza kuhesabu .Kabla hajafika tatu John akakubali kueleza ukweli.Alieleza kila kitu kuhusiana na wazazi wa Peniela kwamba ni yeye aliyewaua kisha akamchukua Peniela na kumlea”
Dr Edwin na Alex wakabaki wanatazamana

“ Siku zote huwa ninamuita John ni shetani mweusi.Ni mtu wa kuogopwa sana” akasema Edwin kwa sauti ndogo

“ Nini kilifuata baada ya hapo ? Dr Alex akauliza

“ Baada ya John kueleza ukweli kuhusiana na Peniela ,Mathew akamwambia John kwamba anaondoka lakini atarejea tena mara ya pili na atakaporejea itakuwa ni maalum kwa ajili yake.John alionekana wazi kuogopa sana na mara tu Mathew na Jason walipoondoka ndipo hali yake ilipobadilika” akasema Martin na kuwaacha Alex na Edwin wakitazamana

“ Huyu Mathew ni nani? .Anaonekana kumfahamu sana John na kwa hiyo kuna uwezekano atakuwa akifahamu kuhusiana na Team Sc41.Huyu anaweza akawa ni mtu hatari sana kwetu” akasema Edwin

“ Ahsante Dr Martin kwa maelezo hayo.Tutayafanyia kazi lakini kwa sasa tunatakiwa kuyaokoa kwanza maisha ya John.Tutaongea mambo mengine baadae” akasema Alex na kumshika mkono Edwin akamvuta kuelekea katika kitanda cha John Mwaulaya wakaendelea na zoezi la kujaribu kurejesha mapigo ya moyo ya John katika hali ya kawaida



***********


“ Mathew kwa kweli sikutegemea kabisa kusikia yale niliyoyasikia toka kwa John kuhusu Peniela.Huu ni ukatili mkubwa sana amemfanyia .Ninaapa lazima nimsaidie Peniela kwa kila namna niwezavyo ili aweze kuipata haki yake.John Mwaulaya ni mtu katili sana na ambaye hastahili kabisa kuwa huru katika jamii iliyostaarabika.Ninaapa nitapambana hadi nihakikishe haki imetendeka na John amefikishwa mbele ya sheria. Bado sijasahau namna walivyoniteka na kunifanyia ukatili mkubwa ndani ya jumba lile. Maskini Peniela ameteseka sana.Nitapambana kwa ajili ya kumsaidia kuipata haki yake !! akasema Jason kwa masikitiko makubwa wakiwa garini baada ya kutoka nyumbani kwa John Mwaulaya.
“ Hakuna haja ya kufanya hivyo !!!..akasema Mathew
“ What ?!!...Jason akashangaa
“ John mwaulaya amewaua wazazi wa Peniela kwa mkono wake .Unajua ni maumivu kiasi gani aliyo nayo sasa Peniela baada ya kuufahamu ukweli kuhusiana na wazazi wake? Japokuwa hataki kuonyesha lakini ni wazi ameumia.Kama mimi imeniuma hivi vipi kuhusu muhusika mwenyewe? John is a monster na anatakiwa akafie gerezani.Nakuhakikishia Mathew siwezi kukaa kimya katika jambo hili,lazima nihakikishe John anatupwa gerezani kwa kitendo hiki alichokifanya.Sintojali ugonjwa wake ninachojali mimi ni haki itendeke.Hakuna anayeweza kunizuia katika hili.I swear no bo body is going to stop me on this” akasema Jason.

“ Achana kabisa na suala hili Jason.Hutakiwi kufanya chochote kuhusiana na suala hili” akasema Mathew kwa sauti ya juu kidogo.Jason akamtazama Mathew kwa macho makali na kusema
“ Are you out of your mind Mathew? Are you real want to let this go ? No ! Peniela is my friend,I love her and her pain is my pain as well so I swear I wont let this go.I must do something !!.Mimi ni mwanasheria na siku zote lengo langu ni kuhakikisha kwamba haki inapatikana .I must fight for her “ akasema Jason
“ No Jason !!.You cant do anything..” akasema Mathew kwa ukali
“ You cant do anything about this.You cant take down team Sc41.You cant fight John.He’s on bed right now but he’s still a very dangerous man and above all you don’t know anything about him.If you love Peniela and you want to help her,stay out of this !!!!... akasema Mathew .Jason akamtazama kwa hasira kisha akasema
“ Mathew mimi na Elibariki ndio tuliokupa kazi hii kwa hiyo kama sisi ndio tunaokulipa huwezi ukatupangia nini cha kufanya.Kuniambia kwamba siwezi kufanya lolote kuhusiana na suala hili ni sawa na kuniambia I’m not a real man.Hufahamu chochote bado kuhusiana na mimi na nini ninaweza nikafanya.Hufahamu chochote kuhusu mimi na Peniela na nimefanya mambo mangapi hadi sasa Peniela yuko huru.Kwa maana hiyo nina..!!..” Kabla hajamaliza alichotaka kukisema Mathew akamkatisha
“ Stop it Jason !! akasema Mathew kwa ukali

“ Naomba nikuweke wazi kwamba ni kweli mlinikabidhi kazi hii lakini nilikubali kuifanya kwa sababu ya ukaribu wangu na Elibariki na wala sikuwa nikikufahamu wewe.Japokuwa ilikuwa ni kazi yenu lakini kwa sasa hii ni kazi yangu na ninaifanya kwa namna ninavyotaka mimi kwa hiyo naomba ukae pembeni na uniache niifanye kazi yangu na usijihusishe na suala lolote linalohusiana na Peniela.Huna sababu yoyote ya kuhatarisha maisha yako kwa sababu ya Peniela.She loves Elibariki and no matter what you try to do, she’ll never change her mind and love you.Kwa hiyo Jason usitake kujiumiza bure kwa jambo hili.This is my job,this is my mission let me finish it !!..” akasema Mathew.Jason akamuangalia usoni kwa hasira na kusema
“ Stop the car !!!..akasema Jason kwa ukali

“ Unataka kushuka? Akauliza Mathew

“ Mathew simamisha gari nishuke !!!..akasema Jason .Mathew hakujibu kitu akaendesha gari hadi katika kituo cha daladala kilichokuwa karibu akasimamisha gari na Jason akashuka kwa hasira na kuubamiza mlango na kutamka neno ambalo Mathew hakulisikia vizuri.Mathew hakumjali akaingiza gari barabarani na kuendelea na safari yake

“ stupid !!..akasema Mathew

“ Katika maisha yangu yote ndani ya kazi hii nimekutana na watu wengi makatili lakini si kama John Mwaulaya.Mtu huyu aliiteketeza familia yangu bila huruma na ametoa roho za watu wengi.Hata hivyo siku zake zinahesabika .Nitarudi tena kwake kwa mara nyingine na hii itakuwa ni zamu yangu.Picha za moto ule mkubwa ulioiteketeza familia yangu bado haijafutika kichwani kwangu.Nitamuua John taratibu sana na kwa mateso makali ” akawaza Mathew huku akiuma meno kwa hasira


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
PENIELA SEASON 3


EPISODE 2


MTUNZI : PATRICK.CK


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Stop the car !!!..akasema Jason kwa ukali
“ Unataka kushuka? Akauliza Mathew

“ Mathew simamisha gari nishuke !!!..akasema Jason .Mathew hakujibu kitu akaendesha gari hadi katika kituo cha daladala kilichokuwa karibu akasimamisha gari na Jason akashuka kwa hasira na kuubamiza mlango na kutamka neno ambalo Mathew hakulisikia vizuri.Mathew hakumjali akaingiza gari barabarani na kuendelea na safari yake
“ stupid !!..akasema Mathew
“ Katika maisha yangu yote ndani ya kazi hii nimekutana na watu wengi makatili lakini si kama John Mwaulaya.Mtu huyu aliiteketeza familia yangu bila huruma na ametoa roho za watu wengi.Hata hivyo siku zake zinahesabika .Nitarudi tena kwake kwa mara nyingine na hii itakuwa ni zamu yangu.Picha za moto ule mkubwa ulioiteketeza familia yangu bado haijafutika kichwani kwangu.Nitamuua John taratibu sana na kwa mateso makali ” akawaza Mathew huku akiuma meno kwa hasira


ENDELEA……………………..



Hatimaye baada ya jitihada kubwa Dr Edwin na Dr Alex wakisaidiana na Dr Martini walifanikiwa kuirejesha hali ya John Mwaulaya katika hali yake ya kawaida.Mapigo ya moyo yalirejea katika hali ya kawaida japokuwa bado John bado hakuwa na fahamu.
“ Ouh ahsante Mungu ! akasema Dr Edwin baada ya mashine inayoonyesha mwenendo wa mapigo ya moyo kuanza kuonyesha kwamba sasa yalianza kwenda kawaida.Kwa takribani dakika mbili wote walibaki kimya wakimtazama John.Dr alex akamuita Edwin pembeni wakaongea kwa zaidi ya dakika kumi huku wakielekezana jambo fulani halafu wakamfuata Martin
“ Martin tunahitaji kuonana na Peniela” akasema Dr Alex.Martin akatoka na baada ya dakika tatu akarejea akiwa ameongozana na Peniela na Josh

“ Dr Alex vipi hali ya John? Akauliza Peniela kwa wasi wasi.Dr Alex akamshika mkono na kumketisha sofani

“ Peniela hali ya John mwaulaya siwezi kusema ni nzuri kwa sasa japokuwa mapigo ya moyo yamerejea katika hali yake ya kawaida.Inaonekana alipatwa na mstuko mkubwa na ndiyo maana hali yake ilibadilika ghafla.Tumejitahidi kwa kila tulivyoweza na tumefanikiwa kuyarejesha mapigo ya moyo katika hali yake ya kawaida.Pamoja na hayo ninaomba niwe muwazi kwako kwamba tatizo la John linaonekana ni kubwa tofauti na tulivyokuwa tunafikiria.” Akasema Dr Alex na kuzidi kumuogopesha peniela
“ Dr Alex mmegundua nini kinamsumbua John? Akauliza Peniela
“ Ni mapema sana kutamka chochote kwa sasa hadi hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika.Kwa sasa kuna kitu tunahitaji “

“ Kitu gani Alex? Sema chochote “

“ Kutokana na hali ya John ilivyo kwa sasa anatakiwa afanyiwe uchunguzi mkubwa sana katika mfumo wake wote wa fahamu.Kwa vifaa tulivyo navyo hapa zoezi hilo haliwezi kufanikiwa kwa hiyo tunahitaji kupata hospitali yenye vifaa ambavyo tunaweza tukafanya uchunguzi wa kina na kubaini kile kinachomsumbua John hospitali yenye usalama mkubwa kwani matibabu ya John yanatakiwa yawe ni siri kubwa” akasema Dr Alex

“ Hospitali itapatikana bila wasi wasi .Naomba dakika mbili nifanye mawasiliano ” akasema Peniela na kutoka mle chumbani akachukua simu yake na kumpigia daktari mkuu wa hospitali ile kubwa yenye aliyosaidiwa na Dr Joshua na kumtaarifu kwamba angempeleka John muda si mrefu kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya.Baada ya kuwasiliana akarejea tena chumbani
“ Gari la wagonjwa litafika hapa muda si mrefu kwa hiyo tuanze kumuandaa mgonjwa.Tunampeleka katika hospitali kubwa ambayo huwatibu viongozi wakuu wa serikali na hata rais mwenyewe hutibiwa hapo.Kuna vifaa vyote mnavyovihitaji na hata usalama wake ni mkubwa sana” akasema Peniela

“ Josh gari la wagonjwa litafika hapa muda si mrefu nenda kawasubiri nje uwapokee.Dr Alex,Edwin na Martini tuanze kumuandaa mgonjwa” akaamuru Peniela
Gari la wagonjwa lilifika kwa haraka na John Mwaulaya akachukuliwa na kuwahishwa hospitali.Ndani ya gari hilo walipanda Dr Alex ,Dr Edwin na Martin.Peniela na Josh wao walifuata nyuma kwa gari la Peniela.Mara tu alipofikishwa hospitali John akapokelewa na bila kupoteza muda madaktari wa hospitali ile wakisaidiana na akina Dr Edwin wakaanza taratibu za kumfanyia uchunguzi wa kina .Madaktari katika hospitali ile walijitahidi kwa kila wawezavyo kutoa huduma za kiwango cha juu kwa John wakijua ni ndugu wa rais.
Kwa kuwa hakufahamu uchunguzi ule ungechukua muda gani , Peniela akaamua aondoke akaendelee na majukumu mengine kwani alikuwa na miadi na Anitha .Walipanga waonane ili aweze kumkabidhi vifaa maalum ambavyo vitawasaidia katika kumfuatilia Dr Kigomba.

“ Josh utaendelea kukaa hapa na kufuatilia kila kinachoendelea.mimi ninatoka kidogo nina miadi ya muhimu na mtu.Utanifahamisha kila kinachoendelea hapa” akasema Peniela na kuondoka zake



********

Mathew aliwasili nyumbani kwake akashuka garini na kumkuta jaji Elibariki peke yake sebuleni wakasalimiana

“ Anitha yuko wapi? Akauliza Mathew

“ Aliondoka hapa muda si mrefu na kusema kwamba anakwenda kuonana na Peniela kwa ajili ya kumpatia vifaa vile vya kusaidia kumfuatilia Dr Kigomba.”

“ Ok good.Kuna habari yoyote mpya? Akauliza Mathew

“ Hakuna habari yoyote mpya Mathew.Mimi niko humu ndani na sijui ni kitu gani kinachoendelea huko nje kwa hiyo nategemea sana kupata habari na taarifa toka kwako.Kwema huko utokako? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akachukua glasi ya maji akanywa halafu akaketi sofani akavuta pumzi ndefu na kusema

“ Ulikuwa sahihi jaji Elibariki,kuna mambo mengi ambayo Peniela hakuwa akiyafahamu kuhusiana na wazazi wake.John lied to her.Lakini nashukuru leo tumeufahamu ukweli wote.Peniela amefahamu kila kitu kuhusiana na historia ya maisha yake na kuhusu wazazi wake.” Akasema Mathew na kumsimulia jaji Elibariki kila kitu kilichotokea.Hii ilikuwa ni habari iliyomstua sana jaji Elibariki
“ Masikini Peniela.Sipati picha maumivu aliyonayo sasa baada ya kuufahamu ukweli kuhusiana na wazazi wake.Hata mimi nimeumizwa sana na jambo hili. Peniela needs someone to comfort her right now.Huyu John mwaulaya ni shetani mkubwa.Amemuumiza sana mwanamke ninayempenda kwa moyo wangu wote.Hana hata chembe ya ubinadamu huyu mtu na laiti kama ningekuwa karibu yake ningeweza kumfanya jambo lolote baya” akasema jaji Elibariki kwa hasira
“ Ni kweli inauma sana jaji Elibariki.John Mwaulaya ni mtu katili na ameumiza watu wengi sana .Picha ya moto ule mkubwa ukiiteketeza nyumba yangu ambayo ndani yake ilikuwamo familia yangu bado haijafutika kichwani kwangu” akasema Mathew halafu akainuka na kwenda ukutani kulikokuwa na picha kubwa iliyowaonyesha watu wawili mwanamke na mwanaume wakiwa katika tabasamu kubwa.Picha hii ikamkumbusha mbali sana Mathew ,hizi zilikuwa ni siku za furaha alipokuwa na mke wake aliyempenda sana

“ Get ready John.Your days are numbered.Kipimo kile kile ulichokitumia kuiteketeza familia yangu ndicho hicho nitakachokitumia kuhakikisha kwamba unakufa kwa mateso makali sana” akasema Mathew kwa sauti ndogo
“ Kwa hiyo nini kinaendelea hivi sasa Mathew? Huyu John tunamfanya nini? akauliza jaji Elibariki

“ Just relax judge.I’ll handle this ,don’t worry” akajibu Mathew halafu akaelekea katika ofisi yake
“ Sasa ni wakati wa kuufahamu ukweli wa kile kilichomo katika zile nyaraka zilizopoteza uhai wa Edson na wenzake nyaraka ambazo zina thamani ya mabilioni ya fedha.” Akawaza Mathew huku akiiwasha kompyuta yake na kuitafuta barua pepe kutoka kwa Yash.Barua pepe hiyo iliandikwa hivi


“ Mathew,nimechelewa kidogo kurudisha majibu ya kile ulichoniomba nikusaidie kukifanyia uchunguzi.Hii ni kutokana na jambo lenyewe kuwa kubwa tofauti na nilivyokuwa nikilifikiria.Ilinilazimu kuwashirikisha jopo la mabingwa wa sayansi ili kwa pamoja waweze kutambua kilichoandikwa katika zile karatasi.Baada ya uchunguzi wa kina imebainika kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni ya kutengeneza kirusi hatari sana ambacho kinaweza kufanya maangamizi makubwa endapo kitatumika kama silaha.Hiki kitu kimetustua sana sote.Wamenihoji sana wakitaka kujua mahala nilikozipata karatasi zile hatari na ni mwanasayansi gani aliyeandika kanuni zile lakini sikuwaeleza chochote kwa kuhofia kuingilia uchunguzi wako lakini Mathew ukae ukijua kwamba yeyote uliyemkuta na karatasi hizi ni mtu hatari sana na lengo lake si zuri hata kidogo.Yeyote uliyemkuta na karatasi hizi anatakiwa ashikiliwe kwa nguvu zote ili aweze kutoa maelezo ya kina kuhusiana na karatasi zile.Nimekuwekea pia viambatanisho kadhaa ili uweze kupata picha halisi ya nini kinaweza kutokea endapo kirusi hicho kikiweza kutengenezwa kwa kutumia kanuni hizo.Mathew jambo hili ni hatari sana kwa usalama wa nchi yako na dunia kwa ujumla kwani sifahamu mtu aliyekuwa na karatasi hizi alikuwa na malengo gani ila ninachokuomba jitahidi kufanya kila kinachowezekana kuzuia kirusi hiki kisitengezwe na kama tayari kimetengenezwa fanya kila uwezavyo kuhakikisha kwamba kinapatikana mahala kilipo kabla ya kuleta maangamizi makubwa.Binafsi niko tayari kukupa msaada wa namna yoyote ile utakaouhitaji muda wowote .Najua kwa sasa uko katika uchunguzi wako na mimi sihitaji kuingilia jambo unalolichunguza ila narudia tena kukuomba kwamba jambo hili ni hatari kwa nchi yako na dunia kwa ujumla kwa hiyo jitahidi kwa kila utakavyoweza kuhakikisha kwamba wale wote wenye lengo ovu hawafanikiwi lengo lao.Ninategemea kupewa tena taarifa nyingine kutoka kwa wanasayansi ambao bado wanaendelea kufanyia uchunguzi kanuni zile kwa kina zaidi na mara tu nikiipokea taarifa hiyo nitakutaarifu mara moja.”


Hivyo ndivyo ilivyosomeka barua pepe ile kutoka kwa Yash kijana anayefanya kazi katika shirika la kijasusi la Israel Mossad .Mathew akairudia tena kwa mara ya pili kuisoma barua pepe ile pamoja na viambatanisho vyake vyote kwa lengo la kuwa na uelewa mpana sana kuhusiana na kile alichokisema Yash .Alipomaliza kusoma akavua shati na kubakiwa na fulana ya ndani,alihisi joto kali

“ Anything wrong Mathew?
Sauti ya jaji Elibariki ikamstua Mathew.Kwa muda wa dakika kadhaa Elibariki alikuwa amesimama mlangoni akimtazama Mathew bila ya yeye kuwa na habari.

“ Ouh ! Elibariki.Karibu” akasema Mathew

“ Nimesimama mlangoni kwa dakika zaidi ya kumi .Akili yako yote umeihamisha katika hicho unachokisoma katika kompyuta yako. Is Eeverything ok Mathew? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akamfanyia ishara avute kiti aketi,akamtazama kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Eli,kila uchao jambo hili linazidi kuwa kubwa na kuchukua sura mpya.” Akasema Mathew
“ Kazi ya kwanza uliyoniomba nikufanyie ilikuwa ni kuchunguza kuhusiana na kifo cha Edson .Tumekwisha fahamu ni kwa nini Edson aliuawa lakini yameibuka mambo mengine makubwa.Katika uchunguzi huo tumefanikiwa kugundua mambo kadhaa makubwa kiasi cha kutulazimu tuendelee kuyachimba hadi mzizi wake.Tumefanikiwa kuzipata karatasi ambazo zilisababisha kifo cha Edson na wenzake na kama utakumbuka karatasi zile ziliandikwa lugha ya kisayansi kiasi kwamba sote tulishindwa kuelewa nini kilichokuwa kimeandikwa.Ilinilazimu kuomba msaada toka kwa washirika wangu .Ninaye rafiki yangu mmoja anaitwa Yash yeye anafanya kazi katika shirika la ujasusi la Isrel Mossad na ni mtaalamu sana wa masuala ya silaha za kibaolojia.Pamoja na utaalamu wake katika sayansi lakini alishindwa kutambua kilichoandikwa ikamlazimu kuwashirikisha wanasayansi wakubwa.Kwa kushirikiana na jopo la wanasayansi wakubwa wamezifanyia utafiti karatasi zile na kugundua kilichoandikwa na leo hii Yash amenitumia majibu ndiyo maana nilikuwa nimeelekeza akili yangu yote huko nikiisoma taarifa yake.” Akasema Mathew
“ Wow ! That’s good news.Amegundua nini? Akauliza jaji Elibariki.Mathew akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Katika uchunguzi wao wamegundua kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni za kutengeneza kirusi hatari ambacho kinaweza kusababisha maangamizi makubwa endapo kitatumika kama silaha iwapo kitatua katika mikono isiyo salama.Kwa mujibu wa Yash,kirusi hicho ni hatari mno iwapo tayari kimetengenezwa au kikitengenezwa.” Akasema Mathew
“ Ouh Mungu wangu !!!...” jaji Elibariki akastuka sana.Kikapita kimya kifupi .

“ Kwa taarifa hii ya Yash,tayari tumeanza kupata picha ni kwanini karatasi hizi zilitaka kuuzwa kwa thamani kubwa sana.Kumbuka mtu ambaye anatajwa kutaka kununua karatasi hizi alitaka kuzinunua kwa mabilioni ya fedha.Ilitia shaka kidogo kwa mtu kutaka kununua karatasi kwa fedha nyingi kiasi kile kumbe alifahamu kilichoandikwa katika karatasi hizo.” Akasema Mathew

“ mambo yanazidi kuwa makubwa.Sikutegemea kabisa kama suala hili lingekuwa kubwa kiasi hiki.Ni nani aliyetaka kununua karatasi hizo kwa fedha nyingi kiasi hicho na alitaka kuzipeleka wapi? Do you know him? Akauliza jaji Elibariki

“ Tayari tunamfahamu mtu aliyetaka kuzinunua karatasi hizo.Anaita Habib Soud ni tajiri toka nchini Saudi Arabia.Bado hatujui ni kwa nini alizihitaji karatasi zile na kwa sasa inabidi tumfanyie uchunguzi mkubwa sana huyu mtu ili tufahamu nini hasa lilikuwa lengo lake la kutaka karatasi zile .Yawezekana akawa na mafungamano na makundi ya kigaidi na yawezekana akawa alihitaji karatasi zile kwa ajili ya kutengeneza kirusi ambacho wangekitumia katika mashambulio ya kigaidi.Tutafahamu haya yote baada ya kufanya uchunguzi wa kina.Pamoja na hayo bado kuna maswali ya kujiuliza mfano Ni nani aliyeandika kanuni zile? Ni wazi hazikujiandika zenyewe lazima kuna mtu ambaye aliziandika,kama ni hivyo ni nani basi aliyeandika? Tutanatakiwa tulitafutie majibu swali hili.Pili karatasi zile zilifikaje katika ikulu yetu na kuhifadhiwa pale? Tatu ,kama nyaraka zile zilihifadhiwa ikulu basi ni lazima kuna mtu au watu waliokuwa wakifahamu mahala zilipo na katika hao wachache lazima kuna mmoja wao aliyevujisha siri na kupelekea kuibiwa. Kwa unyeti wake karatasi hizi lazima zilikuwa zikihifadhiwa sehemu ya siri sana ambako si rahisi kwa mtu kama Edson kufahamu kwa hiyo ninapata picha kwamba Edson lazima alielekezwa mahala zilipo na akaziiba.Kama ni hivyo mtu huyo ni nani? Tunatakiwa kumfahamu pia.Kingine kikubwa ambacho tunatakiwa tukifahamu ni je kirusi hicho tayari kimekwisha tengenezwa au bado? Kama tayari kimekwisha tengenezwa kiko wapi? Kama bado lazima tufute kabisa mipango yote ya kukitengeneza kwa kuwatia nguvuni wale wote wanaohusika katika suala hili.Lazima tulichimbe jambo hili hadi mzizi wake na hakuna hata mmoja ambaye anahusika na suala hilo atabaki salama.” Akasema Mathew

“ Mathew nimekosa neno la kusema lakini ni wazi nimestushwa mno na taarifa hii” akasema jaji Elibariki

“ Hii ni taarifa ambayo hata mimi imenistua mno .Wakati ninaisoma taarifa hii mwili ulikuwa unanitetemeka.Sikuamini kama jambo hili linaweza kuwa kubwa kiasi hiki.Hapa nilipo ninahis joto kali sana na ndiyo maana unaniona nimevua hadi shati.Si kwamba nimeogopa ila nimestuka tu kwani ni mara ya kwanza kwa kitu kama hiki kupatikana hapa nchini kwetu.Pamoja na ukubwa wa jambo lenyewe lakini lazima tutalichimba hadi mzizi wake na kuhakikisha tunazizuia njama zote ovu .Tutafahamu karatasi hizi zimetoka wapi, nani kaandika na zilifikaje ikulu na nini lilikuwa lengo la Yule aliyetaka kuzinunua.” Akasema Mathew halafu akasita kidogo na kusema

“ Kuna wazo limenijia.Suala hili haliwezi kuwa na mahusiano na lile suala tunaloendelea kulichunguza kuhusiana na package ambayo Dr Joshua anataka kuiuza? Mpaka sasa hakuna yeyote ambaye anafahamu chochote kuhusiana na kilichomo ndani ya package hiyo .Dr Joshua yuko tayari kufanya chochote kile kuhakikisha kwamba mpango wake unafanikiwa na hii inaonyesha uthamani mkubwa wa package hiyo. Lakini hata hivyo ni mapema sana kusema chochote.Kila kitu kitajulikana baada ya uchunguzi.” Akasema Mathew na kuinama chini akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akasema

“ Katika nyakati hizi ninamkumbuka sana Noah.Alikuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa sana kwangu na katika wakati huu angenisaidia sana.” Akasema Mathew
“ Mathew tafadhali usinikumbushe kuhusu Noah.Picha ya usiku ule bado haijafutika haijafutika kichwani kwangu.Kama si yeye tayari ningekwisha kuwa marehemu sasa lakini Noah aliyatoa maisha yake kwa ajili yangu.Nina deni kubwa sana kwake na namna pekee ya kuweza kulipa deni hilo ni kuwapata wale wote waliosababisha kifo chake.I don’t know how I’m going to do this but I promise you we’re in this together.” Akasema jaji Elibariki kwa hisia kali sana.
“ Samahani Elibariki kwa kukukumbusha kuhusu Noah.He was a good guy.Binafsi nimefanya naye kazi kwa muda mrefu and that’s why it’ll take a long time to forget him. Hata hivyo hakijaharibika kitu na tutaifanya kazi hii mpaka mwisho.Niko mimi ,Anitha pamoja na wewe.Tunaweza kuifanya kazi hii.Anitha ni mtu ambaye atatusaidia sana katika suala hili.Ni mtaalamu mkubwa sana wa teknolojia na ni mwepesi sana katika kufikiri na kuchambua mambo.Binafsi ninapokuwa naye katika kazi Fulani basi huwa sifikirii kushindwa hata kidogo katika jambo lolote na hata katika hili nina hakika tutafanikiwa tu” akasema Mathew halafu akachukua simu na kumpigia Anitha

“ Hallow Mathew ,uko wapi? Akauliza Anitha baada ya kupokea simu
“ Tayari nimerejea nyumbani.Wewe uko wapi? Akauliza Mathew

“ Niko njiani ninarejea nyumbani.Nimetoka kuonana na Peniela na tayari nimemkabidhi vile vifaa na jioni ya leo atakapokutana na Dr Kigomba tutaanza kupata kila taarifa toka kwa Dr Kigomba.” Akasema Anitha

“ Good job Anitha.Ninakusubiri hapa nyumbani.Kuna suala zito linalotukabili”

“ Kuna jambo jipya ? akauliza Anitha kwa wasi wasi kidogo
“ Si jipya sana lakini ni mwendelezo wa kile ambacho tumekuwa tunaendelea nacho” akasema Mathew
“ Sawa Mathew .Niko njiani ninakuja sasa hivi” akajibu Anitha na kukata simu


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…