SEASON 3
SEHEMU YA 38
MTUNZI : PATRICK.CK
Ni saa sita za usiku sasa bado jaji Elibariki chukuswa yuko sebuleni akiendelea kupitia kitabu chake cha sheria .Katika meza ndogo kulikuwa na vitabu vingine zaidi ya saba vya sheria.Aliendelea kufungua ukurasa baada ya ukurasa.Alionekana kuwa na mawazo mengi mno.Wakati akiendelea kupitia kurasa za kitabu kile mke wake akaingia pale sebuleni akiwa na kikombe cha kahawa, akakiweka mezani halafu akainama na kumbusu mumewe.
“ You need to take a rest now.Tommorow is your big day” akasema Flaviana mwanamke mwenye uzuri wa kipekee.Elibariki akakifunika kitabu chake na kumtazama mkewe ,akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo na kusema
“ Natamani sana nipumzike lakini sina hakika kama nitapata usingizi.”
Mke wake akamuangalia kwa makini halafu akasema
“ Kuna jambo nataka nikuulize mume wangu”
“ Uliza usihofu ”
“ Najua kesi hii ni moja kati ya kesi kubwa na ngumu kwako.Hukumu unayotarajia kuitoa kesho inasubiriwa kwa hamu kubwa sana na umma wa watanzania.Wewe ni jaji na nina imani maamuzi yako utakayoyachukua ni sahihi kabisa,lakini swali langu ni je Yule msichana ana hatia?
Swali lile lilionekana gumu sana kwa jaji Elibariki.Akainama akafikiri kidogo halafu akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo na kumtazama mkewe.
Hakukuwa na nafasi tena ya kukaa ndani ya chumba cha mahakama kutokana na watu kujaa.Ni siku ya hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili mmiliki wa maduka makubwa ya mavazi ya Penny Fashion,Peniela Salimote.Kesi hii iliyovuta hisia za watu wengi na kuwafanya wafurike ili kuja kusikia hukumu ilikuwa inaonyeshwa moja kwa moja katika runinga.ILikuwa ni kesi ya kwanza kubwa kurushwa moja kwa moja katika runinga.Katika kila kona ya nchi watu walikuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya kesi hii ambayo hukumu yake ilikuwa inasubiriwa na watu wengi.
Ndani ya chumba cha mahakama ilikuwepo familia ya rais ikiongozwa na mke wa rais,Dr Flora Johakim ambaye alikuwa ameambatana na binti zake wawili Flaviana na Anna.Familia ya Edson Kobe kijana anayedaiwa kuuliwa na Peniela nayo ilikuwepo mahakamani hapo ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka.Familia ya Edson na ile ya rais zilikuwa ni familia rafiki kwa muda mrefu sana.Kwa upande wa Penny hakukuwa na ndugu yake yeyote aliyefika mahakamani pale zaidi ya rafiki zake wachache.
Tayari mtuhumiwa amekwisha ingizwa mahakamani na aliyekuwa akisubiriwa ni jaji anayeisikiliza kesi ile aweze kuingia na kuisoma hukumu.Wakati wakimsubiri Jaji aingie,Jason Patrick mwanasheria anayemtetea Penny alikuwa akibadilishana mawili matatu na mteja wake .
“ Jason,kabla hukumu haijaanza ninaomba nikwambie kitu.” Akanyamaza kidogo na kuendelea.
“ Nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.Umenisimamia katika kesi hii kwa kila namna ulivyoweza.Najua chochote kinaweza kikatokea siku ya leo hivyo nakuomba endapo ikitokea nikakutwa na hatia na kufungwa kifungo cha maisha au kifo uhakikishe yale yote niliyokuandikia katika karatasi unayatimiza.Wewe ni zaidi ya rafiki.Wewe ni ndugu yangu pekee ninayekutambua.Ninakukabidhi kila kilicho changu endapo mambo yataenda kinyume na matarajio yetu." Akasema Penny huku machozi yakimtoka
“ Penny naomba usikate tamaa hata kidogo.Nimepambana vya kutosha kuhakikisha kwamba tunashinda kesi hii lakini kama mambo yataenda tofauti na matarajio yetu hautakuwa ni mwisho.Nitapambana hadi nihakikishe haki imepatikana.” Akasema Jason na mara jaji akaingia.
NIMEONA NIWAFARIJI KIDOGO😀😀😀😎😎😎😎😎😉