Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

Kwa hisani ya LEGE ambaye kwa hivi sasa ypo busy nchini Botswana

PENIELA
SEHEMU YA 21
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Dr Flora hakutikisa hata ukope.Haraka haraka Winifrida akakimbilia katika simu akampigia Captain Amos daktari wa familia ya rais ambaye alifika mara moja na vipimo akampima na kuamuru liitwe gari la wagonjwa haraka.Gari la wagonjwa likafika Dr Flora akapakiwa na kukimbizwa katika hospitali ya jeshi.Pale akapimwa na kukutwa tayari amekwisha fariki.Baada ya kuthibitishwa kwamba amefariki dunia Captain Amos akampigia simu Dr Joshua
“ Hallow Captain” akasema Dr Joshua
“ Mr President its done.She’s dead”
“ Thank you Captain Amos.Niko njiani narejea Dar es salaam” akasema Dr Joshua na kukata simu.Captain Amos alibaki amesimama ameegemea mti.Alikuwa na mawazo mengi sana.
“ I’ve killed the first lady…Please forgive me lord” akawaza Captain Amos

ENDELEA…………………………

Ndege aliyopanda Peniela akitokea jijini Arusha ilitua katika uwanja wa ndege wa kiataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam .Pale uwanjani kulikuwa na gari mbili zimeandaliwa kwa ajili yake .Moja ikiwa ni kwa ajili ya yeye kupanda na nyingine ilikuwa na walinzi wanne wa kumlinda.Baada ya kuingia katika gari akaomba apelekwe moja kwa moja katika nyumba ambayo Dr Joshua alimtaka ahamie mara tu atakaporejea Dar es salaam.
“ Nimerejea Dar es salama kama malkia.Naya penda maisha haya lakini ni kwa muda mfupi tu.” Akawaza penny akiwa garini.Uso wake haukukaukiwa na tabasamu .
Waliwasili katika jumba ambalo Dr Joshua alikuwa amempatia.Lilikuwa ni jumba kubwa zuri la kifahari la ghorofa tatu lililokuwa kandoni mwa bahari ya Hindi.Toka lilipojengwa halikuwahi kukaliwa na mtu yeyote.Alifunguliwa mlango na kuingia ndani,ambako kulikuwa na uzuri wa kipekee.Kulikuwa na samani za kupendeza za hali ya juu za gharama kubwa bila kusahau nakshi mbali mbali za kuvutia mno.Alishindwa kuizuia furaha yake pale alipoingia katika chumba cha kulala.
“ Wow ! This is amazing” akasema kwa furaha.Kilikuwa n i chumba kikubwa na kizuri mno chenye kila kitu cha thamani ambacho angehitaji kiwepo chumbani.Alienda katika dirisha kubwa na kuishuhudia madhari ya kupendeza ya bahari ya Hindi
“ This place is like paradise” akasema
“ Nimeipenda sana hii nyumba ni nzuri mno.Ina kila kitu ninachokihitaji” akasema Penny huku ajkishuka na kwenda kuangalia muonekano wa n je.Nje ya jumba lile la kifahari kulikuwa na viwanja vya michezo mbali mbalikama kikapu ,tenisi na wavu.Kulikuwa pia bwawa la kuogelea na bustani nzuri yenye maua na miti ya kupendeza.Lilikuwa ni jumba la kifahari mno.
“ Nimelipenda mno jumba hili na ninatamani kama ningeishi hapa lakini sintoweza.Nlimkubalia Dr Joshua kule Arusha lakini ni vigumu sana kwa mimi kukaa hapa.Sina mpango wa kuwa na mahusiano ya muda mrefu na yeye.Baada tu ya kazi yangu kumalizika mimi na yeye hatutakuwa na mahusiano tena.Uhusiano wetu utakuwa umefikia mwisho.” Akawaza Penny akiwa njiani kueleka nyumbani kwake
“ Natamani nifahamu jaji Elibariki na Jason wamefikia wapi kuhusiana na mpango wao wa kufanya uchunguzi juu ya kifo cha Edson.Sitaki waendelee na mpango wao ule kwa sababu ni hatari kubwa kwao.Sitaki wapate madhara yoyote yale kwani ni watu wangu wa karibu na wana umuhimu mkubwa katika maisha yangu. Kwa maana hiyo basi itanilazimu kutafuta namna nitakayoweza kuwafanya wasiendelee na mpango wao ule.Lazima niuvuruge ili kuwasaidia “ akawaza
Aliwasili nyumbani kwake akafunguliwa geti na kuingia ndani .Akaagana na wale walinzi wakaondoka.
“ Home sweet home”akasema kwa furaha alipoingia tena katika sebule yake
“Ninaipenda mno nyumba yangu na katu siko tayari kwenda kuishi sehemu nyingine”akawaza huku akipiga hatua kuelekea chumbani kwake.
Mara tu alipoingia chumbani kwake alipatwa na mstuko wa ghafla.Aligundua vitu havikuwa sawa.
“ Someone was here.Kuna mtu aliingia humu ndani ” akasema kwa hasira na woga
“ Vitu vyangu haviko sawa kama nilivyoviacha.Kuna mtu alikuja kupekua nyumba yangu.Atakuwa nani huyu ? Kitu gani walikuwa wanatafuta? Akawaza Penny akiwa amekasirika kupita kiasi na mara akakumbuka kitu,akaiwasha kompyuta yake na kupitia anuani yake ya barua pepe akaziona picha za mtu aliyefungua kasiki lililokuwa ukutani.Kasiki lle lilikuwa na kamera ya siri ambayo huchkua picha ya kila anayelifungua na kuirusha moja kwa moja katika anuani ya parua pepe ya Peniela.
“ Bastard !! akasema Penny kwa hasira baada ya kuiona picha ya jamaa mmoja aliyevaa glovu nyeusi mikononi akiwa ameshika heleni zake alizokuwa amezihifadhi katika kasiki
“ It’s them !!..”akasema na kuvuta pumzi ndefu
“ Kitu gani awlikuwa wakikitafuta humu ndani?.Watu hawa sasa wameanza kunichosha.Nilipatwa na matatizo na kunusurika kuingia gerezani lakini hawakunisaidia lolote.They are monsters.” Akawaza na kukaa kitandani
“Najilaumu sana kuingia katika kazi hii.Kwa sasa siwezi tena kujiengua.They have me in their hands.They control me” akainama na kudondosha chozi
“ kama ingekuwa ni kwa ridhaa yangu basi nisingekubali kujiunga nao .Nimekasirishwa mno na kitendo chao cha kuingia ndani mwangu na kupekua bila ruhusa yangu.Huu ni ukosefu wa adabu na ustaarabu.Ninafanya kazi zao vizuri lakini bado hawataki kuniacha walau niwe na maisha ya kawaida.Nilitegemea baada ya kumaliza mwaka mzima nikiwa gerezani nikiendelea na kesi yangu wasingesumbuka nami tena lakini walipofahamu nimeshinda kesi mara moja wakaendelea kuniandama na kunitaka niendelee na kazi yao .I’m tired with this life.I’m tired with them.Baada ya kazi hii kumalizika sitaki tena kufanya kazi yoyote tena.Chochote kitakachotokea na kitokee tu lakini nimechoka sasa.I need to live a normal life.I need my freedom back.” Akawaza Penny na mara akastuliwa na mlio wa simu ya mezani.Katika meza ya simu kulikuwa na simu tatu na iliyokuwa ikiita ilikuwa ni simu ya rangi nyeusi.
“ Its them ! akasema kwa hasira nakuichukua simu ile akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ hallow “ akasema kwa sauti ya juu yenye kuonyesha wazi alikuwa amekasirika
‘ hallow Peniela” Ikasema sauti ya upande wa pili.Penny akastuka kidogo kwani haikuwa ile sauti aliyoizoea
“ Welcome back Peniela” akasema tena Yule jamaa upande wa pili
“ Who are you ? and where is he? Akauliza Penny
“ Relax penny.From now on you’ll be talking to me.My Code is 00P688.Muda wowote ukiwa na shida yoyote kubwa na unahitaji ufumbuzi au msaada wa haraka nitafute kwa kutumia code hiyo na utasaidiwa haraka sana.By the way where were you? Akauliza Yule jamaa ambaye alikuwa akiongea kwa taratibu sana
“ Kwa nini nyumba yangu imepekuliwa ? Don’t you trust me? Akauliza Penny kwa ukali
“ I’m sorry penny ,lakini ulipotea ghafla na hatukujua uko wapi kwa hiyo ni jukumu letu kuhakikisha kwamba uko salama na ndiyo maana tukaingia ili kufahamu kama umepatwa na tatizo lolote.Ni jukumu letu kuhakiki usalama wako Penny”
“ Naomba iwe ni mwanzo na mwisho kuingia ndani mwangu wakati sipo na wala sitaki kufuatiliwa na mtu yeyote Yule.Ninafanya kazi zangu vizuri kama mnavyotaka kwa hiyo naomba msivue mipaka.” Akasema Penny kwa ukali
“ Ok nimekuelewa Penny lakini siku nyingine kama una safari au unahitaji faragha, nitaarifu nifahamu li tujue kwamba uko salama.Vipi kuhusu mahusiano yako na mheshimwa rais yakoje toka umemaliza kesi?Mmeonana tayari? Akauliza Yule jamaa ambaye hakutaka kujitambulisha jina
“ Mahusiano ni mazuri,tunaendelea vizuri.Tayari nimekwisha mrudisha katika mstari na sasa ninaweza kuendelea kuimalizia kazi yangu.”
“ Ok vizuri penny.Jitahidi kwenda kwa kasi kidogo kwa sababu muda uliopangwa kwa operesheni hii unakaribia kumalizika na tusipofanya haraka kilakitu kitavurugika.” Akasema Yule jamaa
“ Hii si kazi rahisi kama mnavyodhani na haiwezi kwenda kwa haraka kama mnavyotaka.Inahitaji kutumia akili sana ili kuikamilisha kwa hiyo naombeni msiniharakishe.Niacheni niifanye kazi hii kadiri ninavyoona inawezekana.Pale ikulu si kama uwanja wa disko.Ile ni sehemu ngumu mno kuingilika kwa hiyo kuweni na subira” akasema penny
“ Nakuelewa penny lakini operesheni hii imechukua muda mrefu sana tofauti na tulivyokuwa tumeipanga.Na hii ilisababishwa na wewe kusahau kazi yako na kujiingiza katika masuala ya kimahusiano hadi kupelekea ukakutwa na yale matatizo.Jitahidi operesheni hii i malizike haraka kwani bado kuna kazi nyingi zinakusubiri” akasema Yule jamaa na kumstua Penny
“bado kuna kazi nyingine? I’m sorry guyz,nikisha kamilisha kazi hii nahitaji mapumziko.I need a break .I need back my normal life” akasema penny
“ Hahahaa..!! Penny we don’t have normal life and we don’t have time to rest.We workd day and night to make sure the nation is safe and people live their normal life.That means we’ve sacrificed our life for the people of this nation.Without us they cant sleep,so forget about break !.Nahitaji kuuona mpango kazi wako kabla ya saa mbili usiku leo ili nione kama unaenda katika njia sahihi.” Akasema Yule jamaa
“ Ok nitakutumia mpango kazi lakini ni baada ya siku mbili.Kuna mambo ambayo lazima niyaweke sawa kwanza.” Akasema penny
“ hakuna siku mbili Peny.Nahitaji leo kablaya saa mbili usiku uwe umenitumia.! Akasema kwa sauti ya juu Yule jamaa
“ tafadhali naomba usiniamrishe namna hiyo.You don’t know what I’m going through right now.You all depend on me to complete this mission so you’ll have to listen to me.Nimesema nitakutumia baada ya siku mbili and that’s final” akasema Penny
“ Ok Peny ,One more thing ,usiache kuvaa heleni yako hata siku moja.Ile ndiyo njia peke e ya mawasiliano kati yetu na wewe.” Akasema Yule jamaa na kukata simu.Penny alikuwa akitweta kwa hasira.Yule jamaa alikuwa amemchefua sana.
“ Who is this guy? Yule wa zamani amekwenda wapi? Akajiuliza.
“ Sifahamu nimepata wapi ujasiri wa kubishana na mtu huyu.These people controls me all over.when will I be free? When I will live a normal life? ..akawaza Penny
Akiwa amejilaza kitandani mwingi wa mawazo simu anayoitumia kuwasiliana na rais ikaita
“ Huyu mzee atapata uchizi mwaka huu.Kila wakati anataka kuongea na mimi” akawaza Penny halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea
“” Hallow Dr Joshua”akasema
“ Hallo Penny.Umeshafika?
“ Ndiyo nimekwisha fika Dr Joshua na kwa sasa niko kitandani nimepumzika”
“ Ok pole na safari.Ulikwenda kuiona nyumba?
“ Ndiyo,nilikwenda kuiona.Ni nyumba nzuri mno.”
“Umeionaje inakufaa? kama haikufai niambie nikupatie nyingine.Ninazo nyumba nyingi tu hapa jijini”
‘ Dr Joshua nyumba ile ni nzuri mno na ni nyumba ya ndoto zangu.Ina kila kitu ninachokihitaji na kukipena katika nyumba”
“ nafurahi kusikia hivyo Penny.Nifahamishe una hamia lini?”
“ Dr Joshua I’m sorry.Sintoweza kuhamia katika ile nyumba”
“ kwa nini penny? Mbona tulikwisha kubaliana uhamie pale ili iwe rahisi kwa mimi kufika muda wowote ninaoutaka?
“ Nimebadili mawazo Dr Joshua.Baada ya kuiona nyumba ile nimegundua kwamba siwezi kuishi pale.Its too big for me. I need normal and simple house” akasema Penny
“ Penny my angel wewe ni mwanamke ninayekupenda kuliko ninavyoweza kukueleza.Nina mipango mikubwa sana juu yako.Nataja uishi maisha kama ya malikia.I am the president of United republic of Tanzania and I can give you anything you want.Nataka upate kila starehe ya dunia hii.Tafadhali naomba ukubali kuuishi katika ile nyumba Penny” akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua nadhani unafahamu toka tumefahamiana sijawahi kukutamkia neno hapana.Nimekuwa mtu wa kusema ndiyo kwa kila jambo unaloniambia lakini leo naomba niseme hapana.Sintoweza kuishi katika ile nyumba.Nitaendelea kuishi hapa katika nyumba yangu hii ndogo”
“ Ok Penny kama unapenda kuendelea kuishi hapo niruhusu basi niifanyie ukarabati mkubwa ili iwe na mandhari ya mke wa rais.Please don’t say No Peniela”
Peniela akatabasamu na kusema
“ Siwezi sema ndiyo kwa haraka Dr Joshua .Let me think about it” akasema penny
“ Ok Ahsante Penny.Halafu kuna jambo nataka nikutaarifu”
“ jambo gani Dr Joshua?
“ My wife is dead”
Kimya cha sekunde kadhaa kikapita,Penny akauliza
“ When did this happen?
“ Amefariki mchana huu.Hivi sasa niko katika maanadalizi ya kurejea Dar es salaam.”
“ So sorry for your loss Dr Joshua.”
“ Thank you so much the next first lady.Nitakupigia simu baadae .I have to go ,ndege iko tayari”akasema Dr Joshua na kukata simu.
“ Dr Flora is dead ?! This is weird! Amekufa kwa ugonjwa gani? Nilimuona siku ya hukumu ya kesi yangu alikuwa mzima wa afya akiwa ameongozana na wanae,iweje afariki ghafla namna hii? Akajiuliza penny
“ Lakini mbona Dr Joshua haonyesi kuguswa na kifo cha mkewe? Anaongea nami kama vile hakuna kilichotokea na hapo hapo anafanya utani kwa kuniita the next first lady.Si mara moja amekuwa akinitamkia kauli hii ya kwamba mimi ni mke wa rais mtarajiwa.Alijua kwamba mkewe atafariki muda si mrefu ? .Ninapatwa na mashaka kuhusianana kifo hiki cha Dr Flora”akawaza Penny halafu akachukua simu na kumpigia simu Jason akamfahamisha kwamba tayari amekwisha rejea.

*******************
Jaji Elibariki alikuwa akijiandaa kutoka ofisini kwake ili akakutane na akina Mathew waliokuwa wamemtaka aonanenao kuhusiana na ile fedha wanayoihitaji, mara simu ikaita.Akaitazama na kukuta ni mkewe Flaviana ndiye alipiga
“ Flaviana leo kaamua kunipigia simu !..Kashangaa
“ Yawezekana hasira zake zimekwisha ? Akajiuliza
“ kwa dharau alizonionyeshea sina hamu naye tena.”akawaza jaji Elibariki huku akivaa koti lake na kuiacha simu ikiita na kukatika bila kuipokea..Ikaanza kuita tena na kumlazimu aipokee
“hallow” akasema
“ hallow” ikasikika sauti ya Flaviana lakini ilionyesha kana kwamba analia
“ Flaviana why are you calling? akauliza jaji Elibariki huku sura yake ikiwa imekunja ndita kuonyesha kwamba hakupendezwa na simu ile ya mkewe.Flaviana hakujibu kitu akaendelea kulia
“ Flaviana kinachokuliza kitu gani? Kama huwezi kunieleza kilichokufanya ukanipigia simu I’m going to hang up now.I have so many things to do” akasema Jaji Elibariki
“ My mother is dead” akasema Flaviana
“ What ?!!!..jaji Elibariki akastuka
“ My mother…Is dead”akasema tena Flaviana
Jaji Elibariki akapatwa na mstuko mkubwa. Kwa sekunde kadhaa akabaki kimya halafu akauliza
“ Amefariki saa ngapi?
“ Mchana huu”
“ Uko wapi sasa hivi? Akauliza Jaji Elibariki
“ kwa sasa niko hapa katika hospitali kuu ya jeshi” akasema Flaviana
“ Ok ninakuja hapo sasa hivi” akasema jaji Elibariki huku akifuta kijasho kilichoanza kumchuruzika.Taarifa ile ya kifo cha Dr Flora ilimstua sana.
“ Nini kimemuua Dr Flora ghafla namna hii? Nafahamu alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu lakini hali yake haikuwa mbaya na jana usiku nilimsikia akizungumza na mwanae.” Jaji Elibariki alikuwa amekaa mezani akiwaza .Akachukua simu na kumpigia simu Jason akampa habari zile na kumtaka aende akaonane na akina Mathew ili alijadili suala lile la pesa wanazozihitaji,yeye akapanda gari na kuelekea hospitali kuu ya jeshi .
Aliwasili katika hospitali kuu ya jeshi na kukuta magari mengi yameegeshwa.Ulinzi ulikuwa mkali sana na watu haakuruhusiwa kuingia ndani bila sababu maalum.Alijitambulisha getini kama jaji wa Mahakama kuu na mume wa Flaviana mtoto wa Rais,akaruhusiwa kupita.Aliegesha gari na akashuka na kuangaza huku na huku akijaribu kumtafuta mkewe mara akamuona Genevive binamu yao akina Flaviana.Wakasalimiana na kumuuliza mahala aliko Flaviana.
“ Sina hakika kama unaweza kuonana naye muda huu.Amepumzishwa katika chumba alikuwa amepoteza fahamu baada ya kuonyeshwa mwili wa mama yake”
“ Nipeleke mahaal alipo.I need to see her” akasema Jaji Elibariki.Genevive akamuongoza hadi katika chumba ambacho Flaviana alikuwa amepumzishwa.Nje ya mlangow a chumba kile alikuwepo muuguzi aliyekuwa akizuia mtu yeyote asiingie mle chumbani kama si daktari.Jaji Elibariki akajitambulisha kama mume wa Flaviana na kuruhusiwa kupita.Flaviana alikuwa amelala kitandani na alipomuona mumewe akaangua kilio.Jaji Elibariki akamfuata pale kitandani akamkumbatia na kumfariji
“ Pole sana Flaviana.” Akasema.
“ Eli,mama yangu amekwenda.” Akasema Flaviana huku akilia
“ Tafadhali usilie Flaviana.Its gonna be ok.I’m right here” akasema jaji Elibariki huku akimfuta mke wake machozi .
“ Nini kimesababisha kifo cha mama? Akauliza jaji Elibariki
“ Mpaka sasa hivi hatufahamu chochote kuhusiana na nini kimemuua.Madkatari bado hawajasema chochote lakini daktari wa familia Captain Amos anasema ni shinikizo la damu.Eli,inaniuma sana kumpoteza mama yangu.Jana usiku nimeongea naye akanipigia simu na kuniambia kwamba leo anahitaji kuonana nasi mimi na Anna kuna jambo la maana mno anataka kutueleza lakini kabla ya kuonana naye amefariki dunia ghafla.Inauma sana Eli.Ninaumia mno”
“ Pole sana Flaviana” akasema Jaji Elibariki na kuendelea kumbembeleza mkewe.
“ Jambo gani alilotaka kuwaambia?
“ Sifahamu Eli,sijui alitaka kutuambia nini lakini alisisitiza mno.Inaonekana alikuwa na jambo kubwa la kutueleza.” Akasema Flaviana na kuendelea kulia
“ Kifo cha ghafla cha Dr Flora hata mimi kinanipa mashaka mno.Alitaka kuwaeleza nini wanae? Kwa nini afariki ghafla kabla hajakutana na wanae? Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusiana na kifo hiki” akawaza Jaji Elibariki
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
TUNAWATAKIA NYOTE WEEKEND NJEMA…
 
PENIELA
SEHEMU YA 22
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Nini kimesababisha kifo cha mama? Akauliza jaji Elibariki
“ Mpaka sasa hivi hatufahamu chochote kuhusiana na nini kimemuua.Madkatari bado hawajasema chochote lakini daktari wa familia Captain Amos anasema ni shinikizo la damu.Eli,inaniuma sana kumpoteza mama yangu.Jana usiku nimeongea naye akanipigia simu na kuniambia kwamba leo anahitaji kuonana nasi mimi na Anna kuna jambo la maana mno anataka kutueleza lakini kabla ya kuonana naye amefariki dunia ghafla.Inauma sana Eli.Ninaumia mno”
“ Pole sana Flaviana” akasema Jaji Elibariki na kuendelea kumbembeleza mkewe.
“ Jambo gani alilotaka kuwaambia?
“ Sifahamu Eli,sijui alitaka kutuambia nini lakini alisisitiza mno.Inaonekana alikuwa na jambo kubwa la kutueleza.” Akasema Flaviana na kuendelea kulia
“ Kifo cha ghafla cha Dr Flora hata mimi kinanipa mashaka mno.Alitaka kuwaeleza nini wanae? Kwa nini afariki ghafla kabla hajakutana na wanae? Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza kuhusiana na kifo hiki” akawaza Jaji Elibariki
ENDELEA…………………………………
Mathew na Anitha walirejea nyumbani na kukutana na Noah aliyekuwa amewasili kitambo akiwasubiri.
“ Welcome home Noah” akasema Mathew
“ Nimekwisha karibia kaka.Poleni na kazi”
“ Ahsante sana “ wakajibu Mathew na Anitha
“ Mtanisamehe kwa kuchelewa.Kuna kazi ambayo nimelazimika kuiacha ili kuja kuungana nanyi katika kazi hii.Mmefikia wapi mpaka hivi sasa? Mmekwishaianza kazi? Akauliza Noah
“ Usihofu Noah wala haujachelewa sana.Mpaka sasa hatujapiga hatua kubwa sana lakini kidogo kuna mwanga Fulani ingawa kadiri tunavyozidi kulichimba suala hili tunagundua kwamba suala hili haliko kama tulivyolitazamia.Suala hili ni zaidi ya mauaji ya Edson.Tunatakiwa tuzidi kulichimba zaidi lakini naomba niwaweke wazi ndugu zangu kwamba kadiri tunavyolichimba suala hili ndivyo tutakavyozidi kukutana na mambo mazito na ya hatari.Please guyz, no matter how danger we’ll be facing,don’t ever give up.Lets fight till the end.Sitaki kuwaficha ndugu zangu kazi hii ni ya hatari kuliko zote tulizowahi kuzifanya kwa hiyo naomba kabla hatujaenda mbali sana kila mmoja atafakari na afanye maamuzi .” Akasema Mathew
Dakika moja ikapita ya ukimya,kila mmoja alikuwa akitafakari.Anitha ndiye aliyekuwa wa kwanza kuuvunja ukimya
“ Mathew,wewe umekuwa ni mshirika wangu,tumekuwa kama mapacha,nimefanya nawe kazi nyingi na za hatari lakini mara zote tunapokuwa pamoja hakuna kazi imewahi kutushinda.Nikiwa pamoja nawe,sina wasi wasi hata kidogo na jambo lolote lile.Uliponieleza kwamba kuna kazi ambayo tunatakiwa tuifanye sikujiuliza mara mbili,niliachana na kazi ambayo nilikuwa nimeitwa nikaifanye nchini Brazili ,kazi yenye pesa nyingi sana ,nikaja kuungana nawe.Kwa moyo mmoja natamka kwamba niko tayari kwa lolote.I’m in”
“ Ahsante sana Anitha.Vipi kuhusu wewe Noah? Akauliza Mathew
“ Me also.I’m in” akasema Noah
“ Ok good.We’re team now.Naomba nisiwaogopeshe lakini tambueni tu kwamba tunakwenda kukutana na mambo mazito na tunatakiwa tusimame imara tusitetereke.This is war and we as soldiers we have to fight”
“ Mathew kama tulivyokueleza ni kwamba tuko tayari kwa mapambano.Siku zote hatuogopi kitu .Nielezeni mmefikia wapi mpaka sasa hivi? Akasema Noah
“ Tumeanza kwanza kumchunguza Edson alikuwa ni mtu wa namna gani.Tumegundua kwamba Edson alikuwa na mahusiano na dada mmoja aliyeitwa Brigita ambaye walikuwa wakiwasiliana kwa siri.Tumeipata laini ya simu ambayo Edson alikuwa akiitumia kuwasiliana na Brigita . Tumegundua kwamba Brigita alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na mzee mmoja aliyeitwa mzee Matiku.Mzee huyu ndiye mmiliki wa hoteli aliyokuwa akifanyia kazi Brigita na ndiye aliyemuwezesha kwa kila kitu.Alimjengea nyumba,akamnunulia gari na kila kitu.Kwa mujibu wa Subira ambaye alikuwa rafiki wa karibu sana na Brigita alisema kwamba Brigita alikuwa na mpango wa kumtoroka mzee huyo kwani hakuwa na mapenzi naye bali alimpendea pesa zake.Brigita alimweleza Subira kwamba alikuwa akitegemea kupata pesa nyingi kutoka katika biashara aliyoifanya na Edson ambayo hakuwahi kumueleza ni biashara gani ,pesa ambayo ingemuwezesha hata kwenda kuishi nje ya nchi.Hapa ninahisi walikuwa na mategemeo ya kupata pesa nyingi sana kutoka katika hiyo biashara.Subira alitueleza kwamba kuna siku Brigita alikuwa na wasi wasi sana na akamwambia kwamba kuna kitu amekichukua kwa mzee Matiku na ana wasi wasi endapo akigundua anaweza akamletea shida.Hakumueleza Subira ni kitu gani hicho na baada ya siku kadhaa akafariki dunia katika ajali ya moto.Inasemekana kwamba mtungi wa gesi ulilipuka na kusababisha nyumba ya Brigita kuteketea na kuwateketeza watu wote waliokuwamo ndani yake.Hii ilitokea wiki mbili tu baada ya Edson kuuawa.Wiki kadhaa baada ya Brigita kufariki dunia mzee Matiku naye alijiua kwa kujipiga risasi ya kichwa.Hadithi ya Edson,Brigita na Matiku ikaishia hapo kwa sababu hatufahamu ni biashara gani ambayo Edson na Brigita walikuwa wanaifanya na ambayo kupitia kwayo walitegemea kupata pesa nyingi . Hatuelewi pia ni kitu gani ambacho Brigita alikichukua kwa mzee Matiku .Picha tunayoipata hapa ni kwamba kuna kitu kilichokuwa kikiendelea baina ya watu hawa watatu.Watu hawa walikuwa na mahusiano na wote wamekufa tena vifo vya utata na ambavyo havikupishana katika kutokea sana.Alianza Edson akauawa kwa risasi,akaja Brigita akafa kwa moto,na mwisho akamalizia mzee Matiku ambaye alijipiga risasi. Lazima hapa kuna sababu iliyopelekea vifo vya hawa watu watatu.Tunatakiwa tuchunguze sababu hiyo ni ipi.” Akasema Mathew akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Huo ulikuwa ni upande mmoja tulioanza kuuchunguza.Upande mwingine ni msichana ambaye aliangushiwa tuhuma za mauaji ya Edson aitwaye Peniela .Huyu alikuwa na mahusiano ya wazi ya kimapenzi na Edson .Pamoja na kila aina ya ushahidi kutolewa mahakamani ukimuhusisha Penny na kumuua mpenzi wake ,bado jaji wa mahakama kuu aliyekuwa akiisikilza kesi ile Jaji Elibariki hakuridhika kwamba Penny alitenda kosa na akaamua kumuachia huru.Baada ya kumuachia huru ndipo alipoamua kufanya uchunguzi wa suala hili ili kuufahamu ukweli.Aliungana na Jason wakili aliyekuwa akimtetea Penny mahakamani na kwa pamoja wakaamua kunipa kazi hiyo mimi kwa kuwa wao hawana taaluma yoyote ya kufanya uchunguzi.Bado sijakutana na Peniela na kuongea naye kwa sababu toka nimeanza kazi hii hajaonekana na hajulikani yuko wapi lakini atakapoonekana ni lazima tutamuhoji na kufahamu vitu kadhaa .Nilipata wazo la kutaka kumchunguza Penny hivyo nikaenda nyumbani kwake nikatega butterfly camera na jioni niliporudi nikaona kitu cha kushangaza kidogo.Watu wawili waliingia ndani mwa Penny na kutega camera katika mlango wa kuingilia sebuleni.Sifahamu ni kwa madhumuni gani walitega kamera ile lakini kwa picha ya haraka haraka ilionyesha wazi kwamba walikuwa wakitaka kufuatilia nyendo za Penny.Iwapo wangekuwa ni watu wenye nia njema basi wasingeingia wakati mwenyewe hayupo. Hiyo ilikuwa ni jana.Leo asubuhi tulipomaliza kuongea na Subira watu wengine wawili walinaswa na kamera yetu wakiingia nyumbani kwa Penny.Hatufahamu walikuwa wakihitaji nini ndani mwa Penny lakini baada ya kutoka tuliwafuatilia wale jamaa wakatufikisha Miseko hospitali.Tuliwafuatilia kila sehemu waliyokwenda na kila walichokuwa wakikifanya na tukagundua kwamba walikwenda kumuona mtu aliyelazwa katika chumba PV 2 – 78 .Anitha aliingia katika mfumo wa kompyuta wa hospitali ile na kugundua kwamba aliyekuwa amelazwa katika chumba kile ni John Mwaulaya Albert.” Mathew akanyamaza akafikiri kidogo na kuendelea
“ Baadae tulimfuatilia pia daktari ambaye alikuwa na wale jamaa ndani ya chumba cha John Mwaulaya ,daktari huyu anaitwa Michael Rodriguerz .Tumegundua kwamba ana mtoto wake mmoja anaitwa Michael Jr anasoma katika shule ya kimataifa ya Tanganyika na kila siku huwa anaongozana na mfanyakazi wake aitwaye Lydie masawe kwenda na kurudi shuleni.Tayari tumekwisha ongea na Lydie na amekubali kufanya kazi yetu kwa malipo ya Tsh million saba.Kesho tutamteka mtoto wa Dr Michael na yeye ndiye atakayetupa taarifa zote kuhusiana na mgonjwa Yule aliyelazwa ndani ya kile chumba.Ninataka tupate uhakika kama kweli mgonjwa huyo ni John Mwaulaya ninayemfahamu.Kama ni mwenyewe,we’ll be dealing with something big…” kengele ya mlangoni ikalia.Akasitisha alichotaka kukisema akainuka na kwenda kuufungua akakutana na mlinzi ambaye alimweleza kwamba kuna mtu getini anaitwa .Mathew akamfuata Jason getini na kumkaribisha ndani
“ Hallow Jason,Karibu sana” Mathew akamkaribisha Jason ndani
“ Ahsante sana Mathew” akajibu Jason kisha wakaelekea ndani
“ Jason kutana na Anitha na Noah wale watu niliowataarifu kwamba nitashirikiana nao katika operesheni hii.” Mathew akafanya utambulisho mfupi.Jason akasalimiana na akina Anitha halafu akaketi
“ Nilimtegemea Jaji Elibariki jioni hii” akasema Mathew
“ Ndiyo.Ni Jaji Elibariki aliyetakiwa kufika hapa jioni hii lakini amepatwa na matatizo kidogo na hivyo kunilazimu mimi kusitisha shughuli zangu na kuja badala yake”
“Amepatwa na matatizo gani? akauliza Mathew
“ Mama mkwe wake amefariki dunia.Mke wa rais Dr Flora amefariki dunia leo alasiri”
“ Mke wa rais amefariki?!..Mathew akashangaa
“ Ndiyo amefariki”
“ Nini kimesababisha kifo chake?
“ Hakuna taarifa rasmi mpaka sasa hivi kwani madaktari wanaendelea na uchunguzi wao kubaini kilichomuua lakini kwa mujibu wa daktari wa familia ya rais anadai kilichomuua ni shinikizo la damu”
“ Dah ! mpe pole sana Jaji Elibariki” akasema Mathew halafu kikapita kimya kifupi
“ Mathew Jaji Elibariki alinielekeza kwamba kuna mzigo unatakiwa”
“ Ndiyo Jason.Tumekwisha ianza rasmi kazi na kuna taarifa Fulani ya muhimu ambayo tunaihitaji.Mtu ambaye atatusaidia ili tuipate taarifa hiyo anahitaji kiasi hicho cha pesa nilichomtaarifu Jaji Elibariki” akasema Mathew.
“ Mmefikia wapi mpaka hivi sasa? Kuna mwangaza wowote? Akauliza Jason
“ Kwa sasa ni mapema mno kusema chochote lakini kazi inakwenda vizuri na baada ya siku kadhaa tutakuwa na cha kusema kuhusiana na uchunguzi wetu lakini kwa sasa hatuwezi sema chochote.Tuachieni kwanza tuendelee kuchunguza.Timu hii unayoiona hapa huwa hishindwi na kitu chochote.Tutalichimba suala hili hadi mzizi wake na mtakipata kile mnachokihitaji” akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.Basi kama ni hivyo mimi sintakuwa mkaaji sana,nimewapitishia mzigo mliokuwa mkiuhitaji.” Akasema Jason na kufungua begi lake akatoa pesa na kumpatia Mathew
“ Milioni nane hizo.” Akasema
“ Ahsante sana Jason.” Akasema Mathew.Jason ambaye alionekana kuwa na haraka akainuka ishara ya kutaka kuondoka
“ By the way,umepata taarifa zozote za Peniela? Akauliza Mathew
“ Ndiyo.Penny amenipigia simu alasiri ya leo,tayari amekwisha rejea.”
“ Alikwambia alikwenda wapi?
“ Hapana hajanieleza chochote bado”
“ Ok Good.Anafahamu chochote kuhusiana na uchunguzi unaoendelea?
“ Tulimdokeza awali kwamba tunataka kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha Edson lakini kuhusu kuwakabidhi ninyi jukumu hilo bado hana taarifa zozote”
“ That’s great.Msimueleze chochote kwa sasa.Hatakiwi kufahamu chochote kuhusiana na uchunguzi unaoendelea hivi sasa.Tumuache kwanza apumzike ametoka katika matatizo makubwa” Akasema Mathew na kuagana na Jason
“ Kwa nini Jason alichagua kuwa mwanasheria? Akauliza Anitha baada ya Mathew kurudi akitoka kumsindikiza Jason
“ Kwani kuna ubaya gani akiwa mwanasheria? Akauliza Noah
“ He’s too handsome to be a lawyer” akasema Anitha
“ Kijana mzuri kama Yule alitakiwa awe rubani au meneja kama wa benki au kazi yoyote nyingine kubwa kubwa .” akasema Anitha
“ Hiyo ndiyo kazi ambayo yeye anaipenda na kwa taarifa yako Jason ni wakili mahiri sana hapa nchini ambaye hajawahi kushindwa na kesi.Alipenda kuwa wakili na anaifanya kazi yake kwa moyo mmoja” akasema Mathew
“ Pamoja na hayo bado sikubaliani na yeye kufanya kazi hii ya uwakili.Haimfai hata kidogo.Hapendezi kuwa wakili”
“ Kwani mawakili wakoje hadi Jason asipendeze akiwa wakili?
“ They have ugly faces because they are always angry” akasema Anitha na wote mle ndani wakaangua kicheko kikubwa.
“ Ok guyz lets get back to business.Kuna jambo ambalo toka mchana nimekuwa nikimuuliza Mathew na akaniahidi kunieleza tutakapo pata wasaa.Nataka kufahamu John Mwaulaya Albert ni nani? Akauliza Anitha.Mathew hakujibu akaenda katika friji akachukua vipande vya barafu akaweka katika glasi halafu akamimina mvinyo ndani yake akanywa.

********************

“ Mhh ! Anitha amenisisimua sana na macho yake.Ni mwanamke mzuri mno.Amenifanya nishindwe kukaa kwa muda mrefu pale ndani kwa jinsi alivyokuwa akinitazama.Macho yake mazuri ya kimalaika yanasisimua akikutazama” akawaza Jason akiwa ndani ya gari baada ya kuondoka nyumbani kwa Mathew
“ Kwa nini Anitha ameamua kuacha kazi zote na kuamua kuifanya kazi hii ya hatari ? Binti mzuri kama Yule hakupaswa kujihusisha kwa namna yoyote ile na kazi kama hizi za hatari.Gosh she’s so pretty.Lakini hawezi kuwa mzuri kumshinda Peniela” Akawaza Jason
“ Kwa sasa ngoja nielekee kwa Peniela.Sijamuona kwa siku kadhaa lazima nikaonane naye jioni hii.Lazima nimuulize alikwenda wapi? Na kwa nini hakuniaga? Dah ! Peniela ameniingia sana akilini.Haipiti saa bila ya kumuwaza.Ninampenda Peniela na kwa hilo siwezi kulificha.Kwa muda wa mwaka mzima nimekuwa na Peniela nikihangaika naye katika kesi na ninaamini nimemfahamu vyema.Nimejiridhisha kwamba ni mwanamke mwenye kunifaa kabisa katika maisha yangu.Ni mwanamke mzuri mwenye kila sifa.Ni mzuri kwa nje na ndani pia nadhani hii ndiyo sababu iliyomfanya hata Edson kuamua kumuacha binti wa rais na kumfuata Penny.Sitakiwi kuendelea kupoteza muda kumueleza ukweli wa moyo wangu kwani chelewa chelewa utakuta mwana si wako.Natakiwa nianze kuchukua hatua kuanzia sasa.Peniela anatakiwa afahamu kwamba ninampenda na niko tayari kufunga naye ndoa na kumsahaulisha mateso na maumivu yote aliyoyapata” akawaza Jason.
Saa mbili kasori dakika kumi na nne za usiku akawasili nyumbani kwa Penny.Akabonyeza kengele ya getini ikaita bila majibu.Takribani dakika tano aliendelea kubaki nje akibonyeza kengele bila geti kufunguliwa.Akachukua simu yake na kumpigia Penny akamfahamisha kwamba yuko pale nje.Hazikupita dakika mbili geti likafunguliwa
“ I’m so sorry Jason.Sikujua kama ni wewe ndiye uliyekuwa ukigonga.Sikuwa nikimtegemea mgeni yeyote Yule jioni hii” akasema Penny
“ Usijali Penny.Mimi ndiye mwenye makosa kwa kutokutaarifu kwamba nitakuja .Utanisamehe sana kwa kuingilia ratiba zako lakini nisingeweza kulala usiku wa leo bila kuja kukuona na kuhakikisha umerejea salama” akasema Jason
“ Usijali Jason.Hapa ni nyumbani kwako huna haja ya kunitaarifu kwamba unakuja.Muda wowote unakaribishwa” akasema Penny na kumfanya Jason atabasamu.Mezani kulikuwa na chupa kubwa ya whysky.Penny akauliza
“ Unatumia kinywaji gani Jason?
“ Wine” akasema Jason
“ Ouh Jason,tonight why cant you change? Try some whisky.I feel like I want something strong tonight.Join me” akasema Penny.Jason akatabasamu na kusema
“ Ok Penny lets have fun “ akasema Jason.Penny akammiminia whysky katika glasi wakaanza kunywa
“ Jason kwanza kabisa naomba samahani sana kwa kutokutaarifu kwamba sintakuwepo kwa siku kadhaa.” Akasema Penny
“ Usijali kuhusu hilo Penny.Nilifika hapa kwako na kukutana n makufuli.Nilipatwa na wasi wasi sana kuhusiana na usalama wako kwani hata simu yako haikuwa ikipatikana.Siku hizi zote nilikuwa nikiishi kwa wasi wasi mkubwa .Thanks God you are back” akasema Jason
“ Vipi wewe unaendeleaje ? akauliza Penny
“ Ninaendelea vizuri Penny.Just mised you”
“ I missed you too Jason.Naomba nikwambie ukweli Jason huko nilikokuwa hazikupita dakika mbili bila kukuwaza” akasema Penny.Jason akatabasamu
“ Kwani ulikwenda wapi Penny? Umerejea umebadilika sana.Umekuwa mrembo mno tofauti na Penny Yule niliyemzoea.Kama si sauti yako ningeweza hata kukupotea” akasema Jason na kumfanya Penny acheke kicheko kikubwa
“ Nilikwenda kufuatilia masuala yangu ya biashara.And you ? ,leo umetoka wapi kwa sababu umependeza mno tofauti na nilivyokuzoea ukiwa katika suti kila siku.Dont tell me you had a date” akasema Penny ambaye usiku huu alikuwa amechangamka sana
“ No ! I had to meet a friend.It wasn’t a date” akasema Jason.Penny akanywa funda moja na kuuliza
“ Jason kuna kitu nimekuwa nikitaka kukuuliza kila siku lakini sikuweza kutokana na kutingwa na kesi lakini kwa sasa kwa vile mambo yamekwisha naomba nikuulize”
“ Uliza Penny”
“ Where is your wife? Sijawahi kukusikia hata siku moja ukizungumizia masuala ya familia”
Jason akatabasamu na kusema
“ Sina mke wala familia”
“ What ?!..Huna mke? ..
“ Ndiyo sina mke.Mbona umeshangaa sana Penny?”
“ Nimeshangaa sana kwa sababu kwa kijana mzuri kama wewe tena msomi uliyebobea katka sheria huna mke.What are you waiting for Jason? Akauliza Penny.Jason akanywa funda moja la whysky akatabasamu na kusema
“ Ni kweli Peniela sina mke mpaka sasa lakini sababu kubwa iliyonifanya niwe hivi mpaka leo ni kutokana na kutingwa mno na kazi na hata kujisahau kwamba na mimi ninahitaji kuwa na maisha kama wengine.Kingine kikubwa ni kwamba bado sikuwa nimefanikiwa kumpata mwanamke Yule ambaye ataufanya moyo wangu usimame,ambaye atanifaa kuwa mke” akasema Jason .Penny akanywa funda la mvinyo na kusema
“ I’m curious.Why a handsome guy like you, you are still single up to now? Be honest with me Jason.Are you a gay? Akauliza Penny.Jason akastushwa sana kwa swali lile akashindwa kujibu akabaki amemtazama Penny .Walitazamana kwa sekunde kadhaa halafu Penny akanywa funda la whysky na kusema
“ Mbona hunijibu Jason? Is it true? Akauliza Penny.Bado Jason hakumjibu kitu.Penny akainuka toka katika sofa alilokuwa amekaa akamfuata Jason na kukaa karibu naye.
“ Jason tell me the truth.” Penny akamnong’oneza Jason sikioni.Mapigo ya moyo ya Jason yakaanza kwenda kasi baada ya Penny kumpumulia sikioni.Penny akamtazama usoni na kuwaza
“ There is only one way to find the truth”
Taratibu Penny akaupeleka mkono wake hadi katika maeneo nyeti ya Jason na ghafla akahisi kushika kitu kigumu
“ Gosh ! its serious” akasema huku akicheka.Jason hakuwa akicheka.mapigo ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio.Penny akaendelea kuchezea maeneo nyeti ya Jason yaliyokuwa yamefura.
“ Sorry Jason nilikufikiria vibaya.Umezidi kuwa mzuri” akasema Penny kwa sauti ya kunong’ona
“ what are you doing Penny ? What do you want? Akauliza Jason
“ Please Jason,make my night beautiful” akasema Peniela.Kwa kasi ya ajabu Jason akamvuta Peniela na kuanza kumwagia mabusu mazita mazito huku akimtoa nguo
“ Jason I need you..I need you Ja…!!..” akasema Penny
“ I’ve been waiting for so long for this chance.Leo utaongea lugha kumi na mbili” akasema Jason huku akivua nguo yake ya ndani
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………………
 
SEHEMU YA 23
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Gosh ! its serious” akasema huku akicheka.Jason hakuwa akicheka.mapigo ya moyo yalikuwa yakimuenda mbio.Penny akaendelea kuchezea maeneo nyeti ya Jason yaliyokuwa yamefura.
“ Sorry Jason nilikufikiria vibaya.Umezidi kuwa mzuri” akasema Penny kwa sauti ya kunong’ona
“ what are you doing Penny ? What do you want? Akauliza Jason
“ Please Jason,make my night beautiful” akasema Peniela.Kwa kasi ya ajabu Jason akamvuta Peniela na kuanza kumwagia mabusu mazita mazito huku akimtoa nguo
“ Jason I need you..I need you Ja…!!..” akasema Penny
“ I’ve been waiting for so long for this chance.Leo utaongea lugha kumi na mbili” akasema Jason huku akivua nguo yake ya ndani

ENDELEA……………………………

Jason you are a real man” akasema Peniela huku akitweta baada ya kumaliza mzunguko mmoja.Jason alikuwa amejilaza sofani akitiririkwa na jasho.Shughuli aliyoifanya haikuwa ndogo.Penny akajiinua toka katika zuria alikojikuta amelala,akajimiminia whysky katika glasi na kunywa
“ Uuupphhhhh…!!!” akavuta pumzi ndefu halafu akamtazama Jason
“ You are so wonderful Jason.I swear in heaven and earth,sijwahi kukutana na mwanaume anayeyajua mapenzi kama wewe.You are amazing” akasema Penny
“ Come here Peniela” akasema Jason .Penny akamfuata pale sofani.Jason hakusema chochote akamvuta na kumkumbatia kwa nguvu huku akimporomoshea mabusu mazito mazito .Penny akajikuta hajiwezi tena na alihitaji huduma kwa mara nyingine tena.Jason alikifahamu alichokihitaji Penny naye bila kumkawiza akaanza kumpatia huduma,wakaingia katika mzunguko wa pili.Sebule ikajazwa na vilio vya mahaba toka kwa Penny kuashiria raha aliyokuwa akiipata .Jason alimchezesha gwaride la uhakika na hadi wanamaliza mzunguko wa pili Penny alikuwa hoi amechoka
“ Dah ! Jason kweli kidume.Sikutegemea kama ana uwezo mkubwa kiasi hiki.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimepata mtu ambaye amenikuna kisawa sawa.Sikuwahi mpata mtu ambaye alinikimbiza mchaka mchaka kama huyu.Huyu ndiye mwanaume ambaye nimekuwa nikimuota kila siku nimpate katika maisha yangu,mwanaume ambaye anafahamu mwanamke anahitaji nini na akamtimizia.Wanaume kama hawa ni wachache sana siku hizi.What can I do to own him? “ akawazaPenny akiwa kifuani kwa Jason
“ Sikuwahi kufikiria hata mara moja kwamba itatokea siku moja nitamvulia nguo Jason kwa namna tulivyokuwa tukiheshimiana na kuchukuliana kama kaka na dada.Amenisimamia kesi yangu na nikashinda na katika siku zote hizo takribani mwaka mzima hata siku moja hakujawahi kujitokeza hisia zozote za kimapenzi kati yetu.Kuna kitu ninajiuliza,je kama tulikuwa tunachukuliana kama kaka na dada kitendo hiki tulichokifanya leo kimetokea kwa bahati mbaya au nilidhamiria kukifanya? Akajiuliza Penny huku akihisi raha ya aina yake pale Jason alipokuwa akiupitisha mkono wake katika sehemu ya uti wa mgongo
“ Haikuwa ni bahati mbaya.I wanted this to happen.Nilihitaji kufanya hivi kwa sababu maalum.Pamoja na hayo kuna kitu nimekigundua kilichokuwa kimejificha ndani mwangu.Ni wazi ninampenda Jason.I deeply love him na kwa hilo siwezi kubishana na nafsi yangu.Jason ndiye mwanaume ambaye ninamuhitaji katika maisha yangu .Kwa bahati mbaya sana haiwezekani kuwa naye katika maisha yangu.Ouh gosh what kind of life is this? Siwezi kuipata furaha niitakayo katika maisha yangu.Kwa nini ninaishi maisha kama haya? Nimekuwa na mahusiano na wanaume kadhaa mpaka sasa lakini Jason ni wa tofauti kabisa na hao wote na ninaamini ni mwanaume ambaye atanifaa sana lakini kwa mfumo wa maisha ninaoishi haitawezekana kuwa naye.Nasikitika sana kumkosa kijana kama huyu” Akawaza Penny
“ Penny unawaza nini? Akauliza Jason
“ Ninawaza mambo mengi sana,kikubwa ni kuhusu wewe.Mambo uliyonifanyia leo yamenifanya niwaze vitu vingi sana.” Akasema Penny.Jason akatabasamu na kusema
“ Usiku wa leo utakuwa ni maalum kwa ajili yako.Nataka niung’arishe usiku huu.I’ll take you to the sky and back.Nataka kuikata kiu yako ya mwaka mzima.I know you needed this and I’m here to give you all that you want” akasema Jason na kumuangushia Peniela busu zito
“ Its true Jason .It’s true I needed this.I needed a strong man tonight.After what you’ve done to me,I don’t think that I’ll let you go.I need you to stay with me Jason,not just for tonight but forever.I need you in my life” akasema Penny na kuufanya uso wa Jason upambwe na tabasamu pana sana.
“ Siamini kama mambo yanakwenda kama nilivyokuwa nataka.Huu ndio wakati niliokuwa nautafuta sana kwa siku nyingi .Ni wakati sasa wa kuweka kila kitu wazi.Siwezi kuipoteza nafasi hii nikaja kujilaumu baadae wakati kumbe hata yeye mwenyewe alikuwa akinitamani ” akawaza Jason na kuendelea kumporomoshea Penny mabusu mfululizo
“ Peniela hufahamu ni jinsi gani nimekuwa nikiota kuipata nafasi kama hii ya mimi na wewe kuwa kama hivi watupu.Leo hii ile ndoto yangu ya muda mrefu imetimia.I’m right here with you in my arms.” Akasema Jason.Penny akainua kichwa na kumtazama Jason
“ Were you dreaming for this to happen? Akauliza
“ Ndiyo Penny.To be honest I’ve been dreaming for this to happen for so long ” akasema Jason.
“ mhh…!..” Penny akaguna
“ Penny you’ve been in my dreams since the day we met.Wewe ndiye Yule mwanamke wa ndoto zangu ambaye maisha yangu yatakamilika endapo nitakuwa nawe.Penny nafahamu hukuwa umelitegemea hili lakini naomba nikueleze ukweli kwamba ninakupenda sana.Nimekuwa nikiomba kila siku itokee siku kama ya leo ambayo nitauweka wazi ukweli wa moyo wangu.Penny wewe ni mwanamke wa pekee kabisa katika dunia hii ambaye utayafanya maisha yangu yawe na furaha na maana.Nakuhakikishia kwamba niko tayari kuutunza moyo wako zaidi ya mboni yangu ya jicho endapo utaufungua na kuniruhusu niingie ndani yake.” Akasema Jason.Peniela aliyekuwa amelalia kifua cha Jason akainuka na kumuangalia kana kwamba ni mara ya kwanza wanaonana.Alitaka kusema kitu lakini akajikuta sauti ikikwama
“ Shhhh..!!!..” Jason akamzuia kwa kumuwekea kidole mdomoni
“ Don’t say anything yet .Take your time and think about it first. This is your life, this my life, this is our life so think carefully” akasema Jason
“ Jason…..uuhhmm..” akaita Penny
“ Sema Penny”
“ Nimekosa neno la kusema.Come here.Wewe ni kijana usiyeisha utamu.I feel like I need it again and again..” akasema Penny huku akimvuta Jason na kumporomoshea mabusu

***********************

Noah na Anitha walikuwa kimya kabisa wakisubiri kusikia atakachowaeleza Mathew aliyekuwa ameegemea kabati akiwaza huku mkononi akiwa na glasi ya mvinyo.Alionekana kuzama katika mawazo mengi.
“ Whats wrong with him? Who is John Mwaulaya? Akauliza Noah
“ Sifahamu mtu huyu John Mwaulaya ni nani lakini ninachofahamu Mathew alistuka sana alipoliskia jina hili .Ngoja akitulia atatueleza namna anavyomfahamu huyu mtu” akasema Anitha
Baada ya dakika zaidi ya tatu za kuzama katika mawazo mengi,Mathew akaketi kitini
“ Sorry guyz najitahidi kulazimika kutokuwaza lakini siwezi kuyaepuka mawazo kila ninapolisikia jina John Mwaulaya. “ akasema Mathew.
“ Who is this guy ? akauliza Noah.Mathew akainama akafikri kidogo na kusema
“ Ninyi ni washirika wangu nitawaeleza kila kitu ninachokifahamu kuhusiana na John mwaulaya” akasema Mathew halafu akainama tena chini akawaza kwa sekunde na kusema
“ Sijawahi kuonana naye ana kwa ana.John Mwaulaya ni mtu ambaye ninamfahamu kwa jina na vitendo na siifahamu sura yake ikoje.” Akanyamaza kidogo akameza mate na kusema
“ Mwaka 2006 nikiwa nafanya kazi katika idara ya ujasusi ya taifa tulipata taarifa za kuingia nchini mwanamke mmoja aitwaye Faizat AbdulOmar Fayed ambaye inasemakana alikuwa mmoja kati ya wafadhili wakubwa wa mtandao wa Alqaeda.Mwanamama huyu tajiri sana aliyeingia nchini akitokea nchini Oman,anamiliki visima vya mafutta nchini Saudi Arabia,Syria na Iraq,utajiri aliourithi baada ya mume wake Omar na wanae wawili kuuawa na vikosi vya marekani vilivyokuwa vikimfuatilia kwa muda mrefu.Omar alikuwa mmoja kati ya watu waliokuwa wakitafutwa kwa muda mrefu na serikali ya marekani kwa kuufadhili mtandao wa Alqaeda.Baada ya kifo cha mumewe na wanae wawili,Faizat aliapa kuendeleza mapambano na aliendelea kuufadhili mtandao wa Alqaeda kwa pesa na kufanikisha mashambulio mengi yaliyopoteza uhai wa watu wengi.” Akanyamaza akawatazama akina Anitha halafu akaendelea.
“ Baada ya kuzipata taarifa zile tulianza mikakati ya kumtia nguvuni kwani tulikuwa na taarifa zake zote.Tulifahamu mahala alipo na tukaweka mikakati ya kuweza kumpata.Tulizisoma nyendo zake na kufahamu kwamba Faizat alikuwa na tabia ya kujibadilisha muonekano na hivyo kukwepa vizingiti mbali mbali alivyowekewa vya kumkamata .” akakaa kimya kidogo halafu akaendelea
“ Ilikuwa ni siku ya alhamisi tuliyopanga kumvamia na kumkamata Faizat mahala alikokuwa amejificha,mimi ndiye niliyeongoza timu ya watu kumi na saba wenye ujuzi wa hali ya juu wa kukabiliana na magaidi toka katika idara ya ujasusi ya taifa.Tulikuwa tumejihami kwa silaha na kila aina .Saa saba za usiku tuliivamia nyuma alimokuwamo Faizat lakini tukamkosa.Nyumba ilikuwa tupu kabisa.Wakati tukijiuliza nini kimetokea wakati taarifa tulizokuwa nazo kiintelijensia zilionyesha wazi kwamba Faizat alikuwa katika nyumba ile,ghafla tukavamiwa na watu wasiojulikana na kuanza kutushambulia kwa silaha kali sana. Hatukuwa tumetegemea shambulio kama lile lililotokea kwa kitendo cha kufumba na kufumbua kwa hiyo tulijikuta tukipoteza kikosi kizima na ni mimi peke yangu niliyefanikiwa kutoka salama.Mpaka leo ninaamini nilifanikiwa kutoka katika shambulio lile kwa maongozi ya Mungu tu. Kila mara picha ya shambulio lile ikinijia mwili wote husisimka.Siwafichi ndugu zangu ni miaka kadhaa imepita sasa lakini mpaka leo hii nikikumbuka kilichotokea usiku ule huwa ninaogopa sana.Ni picha ambayo ni ngumu hata kuielezea” Akanyamaza kidogo na kuinama halafu akasema
“ Nilipofanikiwa kutoka salama eneo lile nilikimbia moja kwa moja hadi nyumbani kwangu lakini nikakutana na kitu cha ajabu ambacho mpaka leo hii picha yake haiwezi kunitoka kichwani.Nyumba yangu ilikuwa ikiteketea kwa moto.Familia yangu yote ilikuwa imeteketea katika moto ule mkubwa” Mathew akashindwa kuvumilia akainama na kuangusha chozi
MATHEW AMEANZA KUWAELEZEA WENZAKE KILICHOMTOKEA USIKU ULE,JE JOHN MWAULAYA NI NANI? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII KATIKA SEHEMU IJAYO….
 
PENIELA
SEASON 1
SEHEMU YA 24
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Hatukuwa tumetegemea shambulio kama lile lililotokea kwa kitendo cha kufumba na kufumbua kwa hiyo tulijikuta tukipoteza kikosi kizima na ni mimi peke yangu niliyefanikiwa kutoka salama.Mpaka leo ninaamini nilifanikiwa kutoka katika shambulio lile kwa maongozi ya Mungu tu. Kila mara picha ya shambulio lile ikinijia mwili wote husisimka.Siwafichi ndugu zangu ni miaka kadhaa imepita sasa lakini mpaka leo hii nikikumbuka kilichotokea usiku ule huwa ninaogopa sana.Ni picha ambayo ni ngumu hata kuielezea” Akanyamaza kidogo na kuinama halafu akasema
“ Nilipofanikiwa kutoka salama eneo lile nilikimbia moja kwa moja hadi nyumbani kwangu lakini nikakutana na kitu cha ajabu ambacho mpaka leo hii picha yake haiwezi kunitoka kichwani.Nyumba yangu ilikuwa ikiteketea kwa moto.Familia yangu yote ilikuwa imeteketea katika moto ule mkubwa” Mathew akashindwa kuvumilia akainama na kuangusha chozi

ENDELEA……………………………………..

Nilichanganyikiwa baada ya kuona nyumba yangu ikiteketea kwa moto.Nilitamani hata kujitupa ndani ya moto ule ili nami niteketee pia pamoja na familia yangu.Mara walitokea watu wawili ambao sielewi walitokea wapi ambao nilidhani walikuwa ni miongoni mwa majirani zangu,wakaniingiza katika gari na kuniwekea bastora kichwani wakinitaka nisifurukute bali nifuate kila watakachonielekeza.Kwa wakati huo nilikuwa kama mtu niliyechanganyikiwa na sikuwa nikiogopa chochote,nilianza kupambana nao na walipoona nimewashinda wakaamua kunitupa nje na kukimbia huku nikiwa nimejeruhiwa kwa risasi begani.” Mathew akavua shati na kuwaonyesha akina Anitha kovu mahala alikopigwa risasi
“ Nilikimbia na kujificha chini ya daraja,nikampigia simu mkurugenzi na kumfahamisha kilichotokea.Dr Wilbert Augustino mkurugenzi wa idara ya ujasusi aliyekuwapo wakati ule alifika mara moja mahala nilipokuwa nimejificha na kunichukua akanipeleka katika nyumba fulani kubwa.Akawapigia simu rafiki zake wawili madaktari wakafika na kunitoa risasi ile niliyopigwa begani.Nilijaribu sana kumuuliza mkurugenzi kama anafahamu chochote kuhusiana na shambulio lile lakini alinieleza kwamba hafahamu chochote.Aliniambia niendelee kukaa katika nyumba ile wakati wakiendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio lile la kustusha.” Mathew akainama na kuzama katika mawazo .Alikuwa amekumbuka mbali sana.
“ Kwa takribani siku kumi na nne “ akaendelea Mathew
“ Niliendelea kukaa ndani ya ile nyumba kubwa na nzuri ambayo haikuwa ikikaliwa na mtu mwingine yeyote zaidi yangu.Daktari alifika kila siku na kunitibu jereha.Mkurugenzi pia hakukosa hata siku moja kufika na kuniletea mahitaji mbali mbali ikiwemo chakula.Bado mkurugenzi aliendelea kunisihi nisijaribu kutoka nje kwani hali ya huko haikuwa bado nzuri kwa upande wangu.Alinieleza kwamba nilikuwa natafutwa sana lakini hakunieleza ni akina nani waliokuwa wakinitafuta.Hiki kilikuwa ni kipindi kigumu mno katika maisha yangu.Nililia mno kila siku nikiiililia familia yangu niliyoipenda kupita kitu chochote.Ilifika mahala sikutamani hata kuendelea kuishi kwani sikuona faida ya kuishi bila ya familia yangu iliyoteketezwa kikatili.” Mathew akainama kwa uchungu akikumbuka familia yake halafu akaendelea.
“ Siku moja mkurugenzi alikuja na kunikabidhi nyaraka za kusafiria na kunitaka niondoke nchini haraka sana kwa ajili ya usalama wangu kwani tayari nimekwisha julikana mahala ninakojificha.Niliondoka usiku huo kama mkimbizi nikielekea nchini japan.Tayari mkurugenzi alikuwa amekwisha suka mipango yote na nikafanikiwa kuingia nchini Japan kwa jina la Adrian Kusema nikiwa kama mtafiti wa kilimo ninayekwenda kufanya utafiti wa zao la mpunga.Mwenyeji wangu alikuwa ni mtu mmoja niliyemfahamu kwa jina moja tu la Yamazuka ambaye tayari alikwisha wasiliana na mkurugenzi wangu .Nilipelekwa katika kijiji kimoja cha wakulima wa mpunga ambako nilianza kujifunza kuhusu kilimo cha mpunga.Niliishi katika kijiji kile kwa muda wa miaka mitatu.Nilijifunza maisha ya ukulima.Watu wale walikuwa wakalimu sana.Walinifundisha mambo mengi .Yalikuwa ni maisha mazuri na niliyapenda.Nilijitahidi sana kuyazoea maisha yangu mapya na kuyasahau maisha yangu ya nyuma lakini pamoja na jitihada zote za kutaka kuyasahau maisha ya nyuma,bado picha ya usiku ule iliendelea kunitesa kila uchao.Kila nikifumba macho nilikuwa nikiwaona wenzangu namna walivyokuwa wakiuawa na mbaya zaidi ni ule moto mkubwa niliouona ukiiteketeza familia yangu.Nilishindwa kuiondoa kumbu kumbu ile kichwani kwangu hivyo kunilazimu kuondoka nchini japan nikaelekea Marekani ambako nilikutana na rafiki yangu mmoja aitwaye Jerry Washington ambaye anafanya kazi katika shrikika la ujasusi la marekani C.I.A.Huyu ndiye aliyenisaidia kufahamu kila kitu kuhusiana na kilichotokea siku ile usiku na hata mauaji ya familia yangu.” Mathew akainuka na kuchukua mvinyo akanywa kidogo na kuendelea
”Nchi ya Marekani kwa sasa ndiyo inayoongoza kwa uwekezaji mkubwa sana hapa Tanzania na katika eneo lote la afrika mashariki .Wamewekeza mabilioni ya dola katika sekta ya mafuta na gesi.Kwa sasa wanajenga kituo kikubwa kabisa cha mazoezi ya kijeshi cha wanamaji katika bahari kuu eneo la maji ya Tanzania.Hiki ni kituo kikubwa kabisa kuwahi kujengwa barani afrika.Kutokana na uwekezaji huu mkubwa ,serikali ya Marekani imelazimika kutafuta namna ambayo itayalinda maslahi yake katika eneo hili la ukanda wa afrika mashariki na ndipo walipounda kikosi kiitwacho Team SC41.Kikosi hiki kipo nchini Tanzania na kinaendeshwa kwa usiri mkubwa mno kiasi kwamba si rahisi kufahamu kama kuna kikosi kama hiki hapa nchini.Hata serikali ya Tanzania haifahamu chochote kuhusiana na uwepo wa kikosi hiki ndani ya ardhi yake.Team SC41 ni kikosi kidogo lakini hatari sana na kilichosheheni watu wenye uwezo mkubwa waliopata mafunzo ya hali ya juu nchini Marekani.Kikosi hiki kina uwezo wa kupata taarifa za kila kinachoendelea kila siku serikalini na lengo likiwa kuhakikisha maslahi ya marekani yanalindwa kwani uwekezaji huu mkubwa katika mafuta na gesi unauinua sana uchumi wa Marekani” Akanyamaza kidogo halau akaendelea
“ Makachero wa marekani walikuwa wakimfuatilia Faizat kwa siri toka alipotoka nchini Oman na kuzisoma nyendo zake.Hawakuwa na haraka ya kumkamata japokuwa uwezo huo walikuwa nao.Sisi hatukulifahamu hilo na ndiyo maana baada tu ya kupata taarifa za kuwepo kwa Faizat hapa nchini tulianza mara moja mikakati ya kumkamata bila kuishirikisha serikali ya marekani.Taarifa za mpango wetu ziliwafikia team SC41 hivyo wakawa wamejiandaa kutukabili ili tusiweze kufanikisha mpango wetu wa kumkamata Faizat.Hatukujua kilichokuwa kikiendelea hivyo wakatushambulia na lengo lao likiwa ni kuua kikosi chote kilichokwenda kumkamata Faizat. Hawakutaka siri ivuje kuhusiana kuonekana kwa Faizat hapa nchini.Ni mimi peke yangu niliyefanikiwa kutoka hai katika shambulio lile kwa hiyo ilikuwa lazima wanipate .Waliiteketeza nyumba na familia yangu wakiamini kwamba kwa kufanya vile watakuwa wamenichanganya kwa hiyo itakuwa rahisi kwao kunipata.Namshukuru sana mkurugenzi wangu Dr Wilbert Augustino ambaye alinisaidia nikatoroka nchini vinginevyo nisingekuwa hai mpaka muda huu.Kwa bahati mbaya Dr Wilbert naye alifariki dunia katika ajali tata.Hii yote ikiwa ni kazi ya Team SC41 .Mungu amrehemu sana Yule mzee” akasema Mathew na kunywa mvinyo kidogo halafu akaendelea.
“ Nikiwa nchini Marekani ,nilianza kufanya uchunguzi wa kina ili kujaribu kukifahamu kikindi hiki cha Team SC41 lakini juhudi zangu hazikufanikiwa kwa sababu kikundi hiki kinaendeshwa kwa usiri mkubwa mno na ni watu wachache hata ndani ya Pentagon wanaofahamu uwepo wa kikundi hiki hapa nchini kwa hiyo ni vigumu sana kuzipata taarifa zake.Kingine kikubwa nilichofanikiwa kukifahamu ni kwamba hapa nchini kikundi hicho kinaongozwa na mtu aitwaye John Mwaulaya Albert.Baada ya kukosa taarifa zake za kina niliamua kuachana nao na kujitahidi kuyasahau maisha yangu ya awali na ndipo nilipoanza kufanya kazi za kujtegemea.Kwa hiyo ndugu zangu naomba mtambue kwamba Team SC41 ni kikundi chenye nguvu lakini hatari sana.Ni watu wenye mafunzo na uwezo wa hali ya juu mno.” Akasema Mathew.Anitha na Noah walikuwa kimya kabisa wakisikiliza.
“ Kuna mawasli ambayo tunatakiwa tujiulize.Kwanza ni je Peniela ana mahusiano gani na kikundi hiki? Watu wale walioingia ndani mwa Penny walitoka na kuelekea moja kwa moja hospitali alikolazwa John Mwaulaya.Je wana mahusiano naye au wanamuwinda? Lakini je wanamuwinda kwa kitu gani hasa? Kama Peniela ana mahusiano yoyote na Team SC41 basi she is a very very dangerous woman.Na kama kweli ni Team SC41 basi nina hakika kabisa kwamba hata Edson aliuawa na watu hawa na kama ni hivyo basi lazima kuna sababu kubwa na ya msingi iliyopelekea kufanyika kwa mauaji hayo kwani team SC41 huwa inashughulika na masuala mazito yenye maslahi na nchi ya Marekani tu.Tuna kazi kubwa ya kufanya mbele yetu.I can say this is a victory or death.We have to get prepared for a big war” akasema Mathew.Anitha na Noah walikuwa kimya kana kwamba wamemwagiwa maji.Anitha akamtazama Mathew na kuvuta pumzi ndefu akasema
“ I’m scared.Real scared but I have to fight”
“ Me too.Hii ni mara yangu ya kwanza kuisikia Team SC41 “ akasema Noah.
“ Ndugu zangu naomba nisiwafiche hata mimi ninaogopa sana nikiwafikiria Team SC41.Tukio la siku ile usiku halitaweza katu kufutika kichwani kwangu.These people have got no souls.They are monsters.Lakini pamoja na hofu hiyo tuliyonayo sote lazima tupambane nao.Najua ni jambo la hatari kubwa sana kwani unapogusa Team SC41 unagusa taifa lenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi duniani kwa hiyo hawako tayari siri zao zijulikane na kuvuruga uhusiano mzuri ilionao na nchi za afrika mashariki na ndiyo maana nikawaambia kwamba this is a victory or death..” Akasema Mathew.Noah akafuta jasho usoni na kusema
“ Mathew sisi tuko tayari kuingia katika mapambano na Team SC41 ,lakini kuna swali ninajiuliza .Je tunatafuta nini kwa Team SC41.Is this about revenge ?
“ Hata mimi nakubaliana na mawazo yako Noah.Lazima tunapoingia katika mapambano na hawa jamaa tufahamu tunapambana kwa ajili ya kitu gani.” akasema Anitha
Mathew akacheka kidogo na kusema
“ Mapambano haya si kwa ajili ya kulipiza . Msingi mkuu tunaoenda nao ni mauaji ya Edson.Tunatafuta nani alimuua na kwanini.Kadiri uchunguzi wetu unavyoendelea mambo mengi yanazidi kujitokeza likiwamo na hili la Team SC41 na mengine mengi ambayo yatajitokeza mbeleni,lakini naomba tusipoteze msingi mkuu wa kazi yetu yaani kuchunguza kifo cha Edson.Ndani ya mauaji ya edson kutaibuka mambo mengi mazito ndani yake.Kwa hiyo tutachunguza endapo kuna mahusiano yoyote kati ya Peniela na Team SC41,tutachunguza endapo Team SC41 walihusika katika mauaji ya Edson na kama walihusika basi tufahamu ni kwa nini.Endapo tutagundua kwamba Team SC41 walihusika katika mauaji ya Edson basi mapambano yetu na wao yataanzia hapo.” Akasema Mathew
“ Nimekuelewa Mathew lakini nina wazo moja, kwa nini basi tusianze kwanza kumchunguza Peniela na kufahamu uhusiano wake na Team SC41? Hii inaweza ikaturahishia kazi sana” Noah akauliza
“ Not yet Noah.Suala hili ni kubwa na tutalichimba hadi mzizi wake kwa hiyo suala la kumchunguza Peniela lina wakati wake.Kwa sasa tuelekeze nguvu katika suala la kesho.Tuna kazi ngumu sana kesho” akasema Mathew na majadiliano yakaendelea kuhusiana na kazi kubwa waliyokuwa nayo kesho.

*********************

Ni asubuhi nyingine tena,nchi ikiwa inaendelea na maombolezo kufuatiwa msiba mzto wa Dr Flora Johakim mke wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Bado hakukuwa na taarifa rasmi zilizotolewa kuhusiana na nini kilichosababisha kifo chake cha ghafla.Salamu za rambi rambi zilimiminika toka kila pembe ya dunia,watu mbali mbali wakimpa pole Dr Joshua rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Jaji Elibariki akiwa miongoni mwa watu waliokuwa katika pilika pilika nyingi siku hii akastushwa na mlio wa simu .Akaitoa na kutazama mpigaji,alikuwa ni Peniela
“ Peniela !!...” akastuka kidogo.Hakuwa ametegemea kama angepigiwa simu na Penny
“Hallo Penny” akasema Jaji Elibariki baada ya kupokea simu ile
“ Jaji Pole sana kwa matatizo yaliyokupata.Nimestushwa sana na msiba wa mama mkwe wako” akasema Penny
“ Ahsante sana Penny.Ni mapenzi ya Mungu,yeye ndiye mwenye kutoa na kutwaa.Vipi unaendeleaje?
“ Ninaendelea vizuri Jaji Elibariki.” Akasema Penny
“ Nimekutafuta kwa siku kadhaa hukuwa ukipatikana kabisa.Nilipatwa na wasi wasi mkubwa kwamba pengine umepatwa na matatizo”
“ Naomba unisamehe sana Jaji Elibariki,nilipatwa na safari ya ghafla ikanilazimu kuondoka bila hata kuaga.”
“ Ok nashukuru kama umerudi salama.Siku nyingine usifanye hivyo.Unatupa wasi wasi sana sisi ambao tunajali usalama wako”
“ Ndiyo Jaji Elibariki.Siku nyingine sintofanya hivyo” akasema Penny halafu kikapita kimya kifupi
“ Jaji Elibariki samahani kwa kukusumbua mida hii lakini nimekupigia simu nina tatizo kidogo na ninahitaji msaada wako”
“ Una tatizo gani Penny?
“ Sintoweza kukueleza katika simu.Unaweza kupata muda sasa hivi tukaonana nikueleze?
“ Uko wapi mida hii? Akauliza Jaji Elibariki
“ kwa sasa niko nyumbani kwangu” akajibu Penny
Jaji Elibariki akafikiri kidogo na kusema
“ Ok ninapafahamu nyumbani kwako nitafika muda si mrefu.” Akasema Jaji Elibariki na kukata simu
“ Penny ana matatizo gani? akajiuliza jaji Elibariki akiwa bado amesimama katika maua
“ Yawezekana akawa na tatizo kubwa ngoja nikamuone” akawaza na bila kuaga mtu yeyote akaingia katika gari lake na kuondoka
“ Nina hakika lazima atakuwa na tatizo kubwa sana ambalo si rahisi kuelezeka simuni.Lazima nikamsikie ana tatizo gani kwani tayari nimekwisha jitolea kwa hali na mali kumsaidia ,kumlinda na kila anayetaka kumdhuru.Peniela tayari amekwisha niingia katika mishipa ya damu .Toka nilipokutana naye kwa chakula cha usiku,kichwa changu hakitulii,kila mara namfikiria yeye “ akawaza .
Penny alikuwa amejilaza kitandani wakati akiongea na jaji Elibariki
“ Mwili wote unaniuma kwa gwaride alilonichezesha Jason jana usiku.Dah ! Jason kweli ni kidume wa shoka.Mziki wake si mdogo.Anajua kuicheza ngoma na hachoki ana mapafu kama ya farasi.” Akawaza Penny halafu akainuka na kwenda kuchukua glasi ya maji ya matunda
“ Kwa kweli jana Jason amenikuna kiswa sawa na kunifikisha ninapopataka.Ni bahati mbaya sana kwamba siwezi kuwa na kijana huyu katika maisha yangu ingawa ninatamani sana kama angekuwa ni mume wangu nikaishi naye mpaka kifo kitutengenishe.Lakini haiwezekani kwa sababu tayari nimekwisha yaharibu maisha yangu na hayawezi kuwa sawa tena.Sintoweza kupata furaha kamwe..” akawaza Penny na kwenda sebuleni akajilaza sofani
Kengele ya getini ndiyo iliyomstua Penny toka katika kijiusingizi kilichoanza kumpitia.Akainuka na kwenda getini.Alikuwa ni Jaji Elibariki
“ Hallo jaji Elibariki.Karibu sana” akasema Penny na kumkaribisha ndani Elibariki kwa furaha
“ Karibu ndani Jaji Elibariki” Penny akamkaribisha sebuleni
“ Penny just call me Elibariki or Eli.Hayo mambo ya Jaji tuyaache mahakamani.” Akasema Jaji Elibariki na kumfanya Penny atabasamu
“ Ok Eli” akasema Penny huku akicheka kidogo
“ Eli unatumia kinywaji gani? akauliza Penny
“ Naomba mvinyo kidogo kama upo.” Akasema Jaji Elibariki.Penny akamtazama na kutabasamu akaenda na kuchukua chupa ya mvinyo akamminia Elibariki katika glasi
“ Pole sana Jaji Elibariki kwa matatizo yaliyowapata.Dr Flora alifariki kwa ugonjwa gani?
“ Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi iliyotolewa lakini kwa muda mrefu sasa Dr Flora alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na ninaamini hicho ndicho kilichomuua”
“ Pole sana Eli”
“ Nimekwisha poa Penny.Vipi wewe unaendeleaje ?
“ Ninaendelea vizuri sana Eli.Vipi wewe unaendeleaje?
“ Ninaendelea vizuri pia.Wasi wasi wangu ulikuwa ni juu ya usalama wako”
“ Nashukuru sana Eli kwa kunijali.” Akasema Penny na kimya kifupi kikapita
“ Nimestuka sana uliponiambia kwamba una tatizo nikaona nikimbie mara moja nije nikuone.Una tatizo gani Penny? Akauliza Jaji Elibariki
“ Eli nina tatizo ambalo nataka nikueleze lakini kwanza unaonekana umechoka sana.Unaonekana hukupata usingizi wa kutosha usiku.Hii ni hatari kwako Jaji Elibariki kuendesha gari katika hali hii.You need some rest” akasema penny
“ Ni kweli nimechoka Penny.Mambo yalikuwa mengi sana msibani.”
“ Ok Jaji Elibariki,naomba kwanza kabla ya kurejea msibani upate wakati wa kupumzika walau kidogo hapa kwangu .”
“Penny nikitoka hapa nitaelekea moja kwa moja nyumbani kupumzika.”
“ Hapana Elibariki.Huwezi kuendesha gari ukiwa katika hali hii ya uchovu. Utapumzika hapa na utakapoamka utakuwa tayari kuendelea na majukumu mengine.Naomba usiogope Jaji Elibariki.Hapa ni sehemu salama” akasema Penny.Jaji Elibariki hakujibu kitu akatabasamu
“ Kabla ya kupumzika,twende nikupeleke ukaoge kwanza ili uondoe uchovu.Ninayafahamu mambo ya msiba yanavyokuwa,hutapata hata wasaa wa kujimwagia maji”
“ Kweli kabisa Penny.Mambo ya msibani ni mengi mno” akasema jaji Elibariki.Penny akainuka na kumuongoza hadi chumbani kwake akamfungulia bafu ili Jaji Elibariki aweze kujimwagia maji.
“ Dah ! Kweli Penny anajua kuchunguza watu.Ni kweli nimechoka sana na ninahitaji mapumziko.Toka jana sijapata wasaa wa kupumzika.” Akawaza Jaji Elibariki huku akivua nguo akijiandaa kujimwagia maji
“ Penny anataka kunieleza nini? Ana tatizo gani? akajiuliza
“ Sikuwahi hata mara moja kuingia katika nyumba ya Penny.Ni kubwa na nzuri.Dah ! Penny ni mzuri jamani.Ukimuangalia tu hadi unapatwa na msisimko “ akawaza Jaji Elibariki na mara mlango wa bafuni ukafunguliwa.Jaji Elibariki alipatwa na mstuko wa mwaka.Hakuamini kile alichokuwa akikiona.Macho yalimtoka pima.
“ P…pe..Pee..” akataka kusema lakini maneno hayakutoka
Mlangoni alikuwa amesimama Peniela akiwa na tabasamu usoni huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………………………
 
SEASON 1
SEHEMU YA 25
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Dah ! Kweli Penny anajua kuchunguza watu.Ni kweli nimechoka sana na ninahitaji mapumziko.Toka jana sijapata wasaa wa kupumzika.” Akawaza Jaji Elibariki huku akivua nguo akijiandaa kujimwagia maji
“ Penny anataka kunieleza nini? Ana tatizo gani? akajiuliza
“ Sikuwahi hata mara moja kuingia katika nyumba ya Penny.Ni kubwa na nzuri.Dah ! Penny ni mzuri jamani.Ukimuangalia tu hadi unapatwa na msisimko “ akawaza Jaji Elibariki na mara mlango wa bafuni ukafunguliwa.Jaji Elibariki alipatwa na mstuko wa mwaka.Hakuamini kile alichokuwa akikiona.Macho yalimtoka pima.
“ P…pe..Pee..” akataka kusema lakini maneno hayakutoka
Mlangoni alikuwa amesimama Peniela akiwa na tabasamu usoni huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa

ENDELEA……………………….

Jaji Elibariki alipangusa maji usoni ili aweze kuangalia vizuri kitu alichokuwa akikiona mbele yake.Haikuwa ni ndoto,msichana aliyesimama mbele yake alikuwa ni Peniela akiwa mtupu huku akitabasamu
“ Ouh my..!!...” Jaji Elibariki akashangaa.
“ Penny..what..what are you doing here ?!! akauliza kwa sauti yenye kukwama kwama
“ Relax Eli.” Akasema Peniela kisha akafunga mlango wa bafu na kuanza kupiga hatua akimsogelea Jaji Elibariki ambaye bado aliendelea kumtumbulia macho asiamini alichokiona.Penny akamsogelea karibu
“ Aren’t you happy to have a bath with me Eli? Akaliza Penny kwa sauti laini.Jaji Elibariki alishindwa aseme nini .Mapigo ya moyo wake tayari yalikwisha anza kwenda mbio .Umbo zuri la Peniela lilimchanganya mno.
“ What do you want Penny? Akauliza Jaji Elibariki
“ What do you want from me Eli? Penny naye akauliza
“ I want you out of here” akasema Jaji Elibariki.Penny akatabasamu na kusema
“ No Eli.You don’t want me to go away.You want me so badly just like I want you.” Akasema Peniela na kumsogelea Jaji Elibariki ,akamkumbatia na kuzigusisha chuchu zake za moto katika kifua cha Elibariki na ghafla maeneo nyeti yakakasirika na kusimama.Elibariki akaanza kutweta ,mwili wote ukamsisimka .
“ Siamini kama jambo hili linatokea kweli.Nilikuwa nikitafuta sana fursa kama hii ya kujivinjari na mtoto mzuri kama huyu lakini leo imekuja yenyewe.Peniela amekuwa katika kichwa changu na kunifanya nimfikirie kila saa.Hii ni ndoto au ni kweli? Akajiuliza Jaji Elibariki.Taratibu akiinua mikono yake na kuanza kuipitisha katika mgongo wa Penny
“ Hapana si ndoto.Hii ni kweli.Niko na Peniela.Huyu mtoto ni kama mchawi amejuaje kwamba nimekuwa nikimuota usiku namchana? Amejuaje kwamba nilikuwa nikiitafuta kwa udi na uvumba fursa kama hii? Akaendelea kuwaza jaji Elibariki akiwa amefumba macho huku akisikia raha ya aina yake wakati mikono ya Penny ikichezea ikulu iliyokuwa imekasirika na kusimama kwa hasira.
“ Ouh Penny…ouh..aah...” akalalama Jaji Elibariki.Penny hakumjali akaendeleza utundu wake kwa kutumia mikono halafu taratibu akapiga magoti na kuanza manjonjo kwa kutumia mdomo wake.Jaji Elibariki nusura apige ukulele kwa raha aliyoisikia akajikaza na kubaki akilalama.
“ I’m yours Eli.I want you now so badly.Please hold me tight in your hands ” akasema penny kwa sauti lain iliyokuwa ikitokea puani.Jaji Elibariki alikuwa katika hali mbaya na hakuweza tena kuvumilia.Wakaingia mchezoni.Ulikuwa ni mpambano mkali baina ya Jaji Elibariki na Peniela.Ni Elibariki ambaye alionyesha kuutawala mchezo.Alibadili kila aina ya mfumo wa uchezaji ili mradi kujihakikishia ushindi mnono mwisho wa mchezo.Hadi wanamaliza raundi ya kwanza wote walikuwa wakitweta kama wakimbiaji wa mbio ndefu.
“ Thank you Eli.Thank you so much” akasema Peniela huku akitabasamu .Jaji Elibariki hakusema kitu alikuwa ameinama akitweta.Alionekana kuwa na mawazo mengi.
“ Unawaza nini eli? Akauliza penny
“ Ni mara yangu ya kwanza kuisaliti ndoa yangu” akasema Elibariki
“ C’mon Eli..Huna sababu ya kusikitika .You wanted this ,right? Akauliza penny.Elibariki hakujibu kitu akabaki akimuangalia
“ Yes you wanted this so badly.Toka siku ya kwanza nilipokutana nawe kwa chakula cha usiku nilibaini kwamba ulikuwa ukinihitaji sana. Sina sababu yoyote ya kunizuia kukupatia kile unachokihitaji kwa sababu wewe ni mtu muhimu sana katika maisha yangu na zaidi ya yote hata mimi nilikuwa nakuhitajipia. Hii ni ahsante yangu kwako Elibariki kwani bila ya wewe hivi sasa ningekuwa gerezani.kwa hiyo usijisikie vibaya.Hujafanya kosa lolote.” Akasema penny huku akimchezea Jaji Elibariki kifuani.
“ Penny..” Elibariki akataka kusema neno lakini Penny akamzuia.
“ Don’t say anything Eli.” Akasema Penny
“ Spend this day with me Eli.I need you so badly today”
Elibariki akambusu na kusema
“ Penny you are wonderfull woman.Unajua kuyasoma mawazo ya mtu.Ni kweli nilikuwa nakuhitaji sana lakini nilishindwa namna ya kuweza kukupata. Penny mimi nina mke wa ndoa na ninampenda lakini sielewi ni kitu gani kimenitokea kwani baada ya kuanza kusikiliza kesi yako nilijikuta nikianza kuvutiwa nawe na kila nilipokuona ndivyo moyo wangu ulivyozidi kuvutwa kwako kama sumaku.Mimi ni mtu mwenye msimamo sana hususani katika kuilinda ndoa yangu lakini kwako nimeshindwa kuwa na msimamo na kwa mara ya kwanza nimejikuta nikiisaliti ndoa yangu.Penny nakupenda sana na ndiyo maana nikafanya kila linalowezekana kukuachia huru na bado ninaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha mazuri na yenye furaha na amani.For you I’m ready for anything”akasema Jaji Elibariki.Penny akatabasamu akambusu Elibariki na kusema
“ Eli ulichokuwa ukiwaza na ndicho mimi nilichokuwa nikikiwaza.Nilipokuona tu mara ya kwanza nilianza kuvutiwa sana nawe.I need someone like you.Wewe ni mtu mwelewa ,unayejua kupenda na unayejali.Sintajali kama una mke lakini hata mimi nakupenda sana Eli.Niko tayari kukupatia kila kitu zaidi ya anavyokupatia mkeo .Nitakupa kila aina ya raha ya dunia hii na sintahitaji kitu chochote toka kwako zaidi ya penzi lako tu.” Akasema Peniela .Elibariki akatabasamu na kusema
“ Usijali Penny.Kuanzia sasa hutanikosa muda wowote ukinihitaji.Antime you need me just call my name and I’ll be there.Kwako ninahisi furaha ya ajabu niliyoikosa kwa miaka mingi.Nikiwa nawe najiona kama niko peponi.Unajua kunichanganya sana.” Akasema Jaji Eibariki.Peniela akafurahi na kuendelea kumwagia mabusu mfululizo.Baada ya dakika kadhaa wakaingia tena katika mzunguko wa pili.Hadi wanamaliza peniela alikuwa hoi na hakutaka tena waendelee kwani simu ya elibariki ilikuwa ikipigwa sana bila kupokelewa.
“ Elibariki nashukuru sana kwa raha ulizonipa..Sijawahi kupewa raha ya namna hii na mtu yeyote Yule .Natamani kama tungeendelea lakini kwa sasa unahitajika msibani ndiyo maana hawaishi kukupigia simu.Tafadhali kama ukipata muda jioni ya leo unaweza ukatoroka na kuja kuniliwaza kidogo? I feel so lonely .I need someone by my side.Nitafarijika sana kama nikipata wasaa wa kuwa nawe jioni ya leo” akasema Penny huku Jaji Elibariki akitabsamu kila alipoendelea kuushuhudia uzuri wa kipekee wa Peniela akiwa mtu.
“ usijali penny.Nitakuja jioni ya leo.Hata mimi nahitaji faraja hususani katika kipindi hiki cha matatizo .Licha ya msiba wa mama mkwe lakini hata mimi nina matatizo yangu binafsi na ninahitaji faraja.Wewe ndiye utakayekuwa mfariji wangu Peniela kwa hiyo usihofu jioniya leo nitakuja na ikiwezekana usiku wote nitakuwa nawe.” Akasema jaji Elibariki na kumfurahisha sana Penny .Baada ya mapumziko Elibariki akaagana na Penny akaondoka kuelekea nyumbani kwake kubadili nguo kabla ya kuelekea msibani.
“ Good.Mpango wangu unakwenda vizuri kama ninavyotaka.Tayari wote nimewatia mikononi.Dah ! wanaume kukamatika ni kitu kidogo .Ni majasiri kwa nje lakini kwa ndani wana udhaifu mkubwa sana.Ninachokisubiri sasa ni boom ” Akawaza Penny baada ya jaji Elibariki kuondoka.
“ Inaniuma sana kwa ninachotaka kukifanya lakini sina budi kukifanya.Hii ni kwa faida yao wenyewe.Hakuna namna ninayoweza kuwashawishi wakaachana na mpango wao wa kuchunguza kifo cha Edson .Kuendelea kuchunguza mauaji yale ni hatari sana kwa usalama wao na mimi sitaki wadhurikike hata kidogo “ akawaza Penny
“ Ngoja nijilaze nipumzike.mwili wote hauna nguvu hata kidogo.Nimekimbizwa mchaka mchaka na Jason usikukucha na sasa hivi nimekutana na gwaride lingine la Elibariki.” Akainama akazama katika mawazo
“ lakini nitaendelea na maisha haya ya kuutumiamwili wangu kwa ajili ya kila ninachokihitaji hadi lini? Mwili wangu umekuwa ndiyo suluhisho la kila kitu.I’m tired with this kind of life.Nahitaji kuishi maisha ya kawaida kama wenzangu wanavyoishi” akawaza Penny na kujitupa kitandani

*****************

Ni saa nne za asubuhi,Mathew na wenzake tayari wamekwisha jiandaa kwa kazi kubwa waliyonayo katika siku hii.
“ Kila kitu kiko sawa? Akauliza Mathew
“ Kila kitu kiko sawa sawa.” Akajibu Noah
“ Anitha mitambo yako yote iko sawa sawa? Mathew akamuuliza Anitha
“ Ndiyo,kila kitu kiko sawasawa.”
“ Ok guyz.Kila kitu ni kama tulivyokipanga.Kama hakuna tatizo its time now” akasema Mathew halafu akaingia katika gari akaondoka.Noah na Anitha nao wakaingia katika gari lingine nao wakaondoka.Mathew alielekea moja kwa moja Mseko hospitali anakofanyia kazi Dr Michael.Noah na Anitha wakaelekea Tanganyika Internation school anakosoma Michael Jr mtoto wa Dr Michael.
“ Anitha kuna jambo ambalo nataka nikuweke wazi wewe kama rafiki yangu wa siku nyingi ila naomba usimwambie Mathew” akasema Noah wakiwa garini
“ jambo gani Noah? Akauliza Anitha aliyekuwa makini katika usukani
“ Nimefikiria sana kuhusu hatari iliyoko mbele yetu.Kuna kitu nimekigundua.Mathew is using us”
“ using us ?!Anitha akashangaa
“ yes ! he’s using us”
“ Hebu nieleweshe Noah.Mathew anatutumia kivipi?
“ Anatutumia kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa Team SC41”
“ You are wrong Noah.”
“ Kweli nakwambia Anitha.Mathew anatutumia kulipiza kisasi.Sikufichi ningejua kama kazi ninayokuja kuifanya ni hii katu nisingekuja.Hii ni kazi ya hatari kubwa sana.”akasema Noah.Anitha akapunguza mwendo wa gari na kulisimamisha pembeni mwa barabara,akashuka na kwenda kuufungua mlango upande aliokaa Mathew
“ get out of the car “ akasema kwa ukali
“ Kwani vipi Anitha?
“ Ninasema shuka !! akafoka
“Kwani vipi Anitha?Kumetokea nini?
“ Kwa taarifa yako sisi hatukutegemei wewe katika kazi hii.Hata usipokuwepo wewe bado nitaendelea kumsaidia Mathew kuifanya kazi hii na tutafanikiwa tu.Kwa hiyo una sekunde thelathini za kufanya maamuzi.Unaendelea na sisi au unaachana nasi” akasema anitha kwa ukali
“ I’m sorry Anitha.Nilikuwa nakupima tu.Ingia garini twende tunachelewa” akasema Noah huku akicheka.Antha akamtazama kwa makini halafu akaubamiza mlango kwa hasira akarejea garini na kuwasha gari wakaendelea na safari
“ Nimeanza kuwa na wasi wasi mkubwa na huyu Noah.Sina hakika kama atavumilia kuwa nasi muda wote.Mtu huyu anaweza kuwa hatari sana kwa usalama wetu.Kuanzia sasa nitaanza kumchunguza kila anachokifanya” akawaza Anitha
“ Anitha usinielewe vibaya ndugu yangu,sikuwa nikimaanisha chochote kwa maneno yale niliyokwambia.Unajua siku nyingi sijakutania kwa hiyo nilitaka kukuchemsha kidogo.Mathew ni mtu wangu wa karibu sana na niko tayari kufa kwa ajili yake.Amenitoa mbali hadi kunifkisha hapa.It was just a joke” akasema Noah huku akicheka.Anitha hakujibu kitu akaendelea kuendesha gari kimya kimya
Waliwasili Tanganyika international school,wakasimamisha gari katika maegesho ya magari.Ilipata saa tano na dakika kumi na tatu
“ Tumejitahidi sana kwenda na wakati” akasema Anitha akachukua simu yake na kumpigia Lydie akamfahamisha kwamba tayari wamekwisha wasili pale shuleni.Baada ya dakika kama kumi hivi ,Lydie akatoka akiwa amemshika mkono mtoto mdogo .Moja kwa moja akanyoosha katika gari la akina Anitha wakaingia ndani kisha wakaondoka.
Walifika katika kituo cha mafuta cha Alnoor,Anitha akamuomba Lydie ashuke wakaelekea katika vyoo .
“Lydie,mzigo wako huu hapa.Milioni saba kamili”akasema Anitha akitoa mabunda ya noti katika mkoba wake na kumkabidhi Lydie.
“Ahsante sana Anitha”akasema Lydie huku akizipakia noti zile katika mkoba wake.
“ Ok nitakuacha hapa utachukua taksi mpaka nyumbani kwako utachukua begi lako na utaelekea ubungo.Natumai mpaka mida hii bado kuna magari ya kuelekea Arusha.Panda basi na uondoke Dar es salaam leo hii.Nenda kaanze maisha mapya.Nakutakia maisha mema” akasema Anitha
“ Ahsante Anitha”akajibu Lydie.Anitha akarejea garini na kumuachia Noah usukani yeye akakaa nyuma ya gari na Michae Jr.
“ tayari tumempata mtoto” Anitha akamtaarifu Mathew.
“ Good job Anitha.Ok sasa twende hatua ya pili.Umekwisha kamilisha kila kitu?
Akauliza Mathew
“Kila kitu tayari Mathew.Utatumia jina lile lile la Dr Emanuel kaboba.Tayari nimekwisha ingiza kila kitu .Ninaingia katika mtandao wa hospitali na muda si mrefu nitakuwa nikikuona na kukupa maelekezo.hata sisi tuko njiani tunaelekea huko” akasema Anitha
“ Where is my aunt Lydie ? akauliza Michael Jr
“ Your aunt has got an emergency .We’re taking you to your father” akajibu Anitha
Wakati akiongea na Anitha Mathew alikuwa mbali kidogo na hospitali.Alipohakikishiwa kwamba kila kitu kiko tayari,akawasha gari na kuelekea hospitali,akipita katika geti wanalopitia madaktari.Aliegesha gari katika maegesho na kwa haraka sana akaangaza macho na kuliona gari la Dr Michael.
“ Good..Dr Michael bado yupo”akasema kimoyo moyo na kupeleka kidole chake sikioni akakigusa kile kifaa cha mawasiliano kilichomo sikioni
“ Anitha nimekwishafika,sasa naingia ndani ya jengo la ofisi.Tayari mmekwisha fika? Akauliza Mathew
“ Tunakaribia kufika Mathew lakini tayari nimekwishaingia katika mtandao wa hospitali na tayari ninaziona kamera.Ok you can go in now” akasema Anitha
Taratibu Mathew akaanza kupiga hatua kuelekea katika jengo lenye ofisi za madaktari.Alipoukaribia mlango ukafunguka akajikuta ametokeza katika kijichumba Fulani ambacho kulikuwa na mashine mfano wa zile mashine za kutolea fedha.
“ Anitha niko katika ile mashine yenye kusoma alama za vidole” akasema Mathew.
“ Ok ingiza namba zile nilizokupa halafu weka mkono wako wa kulia na baada ya sekunde kumi itasoma na mlango utafunguka.” Akasema Anitha
Mathew akaisogelea mshine ile akabonyeza namba alizokuwa amepewa na Anitha halafu akaweka kiganja cha mkono mahala palipochorwa alama ya vidole.Baada ya sekunde kumi kama alivyokuwa ameambiwa na Anitha ikawaka taa ya kijani na maandishi yakatokea
“ Thank you Dr Emanuel Kaboba.Now you can go in” Mara mlango ukafunguka.Mathew akatabasamu na kuingia ndani.
“ Tayari niko ndani” akasema Mathew
“ Ok Mathew.Ofisi ya Dr Michael iko ghrofa ya pili chumba namna 35. “ akasema Anitha.Mathew hakutaka kupanda lifti akapanda kwa miguu hadi ghorofa ya pili na moja kwa moja akaelekea chumba namna 35 alichoelekezwa kwamba ndicho chumba cha Dr Michael.Alikuwa akikutana na madaktari wakati akipanda lakini hakuna aliyemtilia wasi wasi kwani huwezi kuingia ndani ya jengo lile bila kuwepo katika mfumo wa kompyuta wa pale hospitalini.
Moja kwa moja Mathew akaelekea chumba namba 35 akagonga mlango na sauti toka ndani ikamruhusu aingie
“ Dr Michael” akasema Mathew huku akitabasamu.Dr Michael akainua kichwa na kumtazama Mathew.Akastuka kidogo kwani hakuwahi kumuona.
“ Dr….” Akasema Dr Michael huku akimshangaa Mathew
“ Dr Emanuel Kaboba” akasema Mathew hukuakimpa mkono Dr Michael
“ Ouh Dr Emanuel ,are you new here? Akauliza Dr Michael
“ Yes I’m new here” akajibu Mathew halafu akatoa kitu Fulani kama simu akakiweka mezani na kubonyeza kitufe chekundu chenye maandishi Scan.Baada ya sekunde kama ishirini hivi kikatoa ukelele
“ Mathew tayari tumekwisha scan chumba chote .Hakuna kitu chochote kilichofungwa cha kumfuatilia Dr Michael.Unaweza kuendelea” Anitha akamtaarifu Mathew ambaye alikichukua kifaa kile na kukirudisha mfukoni.
“ What can I help you Dr Emanuel? Akauliza Dr Michael huku akiendelea kumshangaa Mathew.Mathew akainuka na kuchomoa bastora mfukoni
“ Dr Michael mimi si daktari ila nimekuja hapa kwa sababu nina shida kubwa na wewe” akasema Mathew na Dr Michael aliyekuwa amepatwa na mstuko mkubwa akataka kusimama
“ Kaa chini Dr Michael.Kuanzia sasa utafuata kile nitakachokuelekeza.!
“ Unataka nini toka kwangu? Wewe ni nani? Akauliza Dr Michael kwa wasi wasi
“ Anitha,niko na Dr Michael hapa .Niunganishe na mwanae” Mathew akamwambia Anitha
“ Ok Mathew,angalia simu yako”
Mathew akachukua simu yake na mara picha ya Michael Jr akiwa ndani ya gari ikatokea,akampatia Dr Michael ile simu.Alistuka sana alipoiona sura ya mwanae.Mwili ukamtetemeka.
“ Huyu ni mtoto wangu Michael” akasema
“ Ndiyo ni mtoto wako lakini kwa sasa tunaye sisi “
“ Mnaye ninyi? Kivipi mko naye ninyi wakati yuko shule? Ninyi ni akina nani? Akaulzia Dr Michael kwa wasi wasi mwingi
“ Dr Michael mwanao tumemtoa shuleni,yuko nasi .Hatuna lengo baya na mwanao kama utatupa ushirikiano tunaoutaka” akasema Mathew
“ Mbona sikuelewi.Mwanangu yuko wapi? Akasema Dr Michael kwa hamaki na kutaka kuinuka
“ Shhhh..kaa hapo hapo ulipo na tafadhali usipaaze sauti.Ukitaka mwanao aendelee kuwa hai tafadhali fuata kile ninachokuelekeza kufanya” akasema Mathew kwa ukali
“ Ok Ok..niambie unataka nini? Tafadhali naomba msimuumize mwanangu wala kumfanya kitu chochote kibaya.Niko tayari kufanya unachokitaka” akasema Dr Michael kwa wasi wasi
“ Nataka unipeleke chumba PV2 – 78” akasema Mathew.Dr Michael macho yakamtoka pima.Alistuka mno.Midomo ikabaki ikimcheza.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………………
 
Back
Top Bottom