PENIELA
SEASON 4
EPISODE 6
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Damn ! you Joshua.Unajifanya wewe una akili sana basi nitakuonyesha namna ulivyo mjinga!!.akawaza Dr Kigomba akiwa garini akielekea kwa Dr Joshua .Akachukua simu na kumpigia Jacob Kateka.
“ Habari za asubuhi Dr Kigomba? Akauliza Jacob baada ya kupokea simu
“ Habari nzuri Jacob.Nimekupigia simu kukufahamisha kuhusu sarakasi za Yule mtu wetu,Nimetoka katika hoteli niliyokuwa nimewatafutia Hussein ana ujumbe wake,nimekuta wameamishwa hoteli alfajiri ya leo.Nimempigia simu Dr Joshua nikamuuliza kama analifahamu jambo hili akasema kwamba ni yeye aliyetoa amri ya kuwahamisha Hussein na ujumbe wake na amegoma kabisa kunieleza mahala alikowahamishia.Zote hizi ni harakati zake za kutaka kuniengua katika mpango wetu na kumiliki kila kitu mwenyewe.Nitakuja kuonana nawe jioni ya leo ili tupange mikakati mizito nini tufanye” akasema Dr Kigomba akaagana na Jacob Kateka kwa miadi ya kuonana jioni.
ENDELEA…………………………..
Miale ya jua la asubuhi ilipenya katika dirisha na kumfanya Mathew afumbue macho.
“Kumekucha!!.. Akasema na kujiinua sofani alikokuwa amelala kwani hakutaka kulala kitandani na Peniela .
“Usiku ulikuwa mfupi sana.Sikumbuki hata ni muda gani nilipitiwa na usingizi” akawaza na kuinuka akaenda kufunua pazia akachungulia nje.Eneo lile lilizungukwa na miti mingi.Kulikuwa na majengo kadhaa kulizunguka jengo lile walilokuwemo
“Siku imeanza vizuri lakini sijui itakwishaje. I don’t know whats going to happen today” akawaza Mathew akageuka na kumtazama Peniela ambaye bado alikuwa amelala kitandani .Alionekana kuzama katika usingizi mzito.
“ Nahitaji sana kujua nani aliyechoma nyumba yangu ,nataka kujua Anitha ,jaji Elibariki na Naomi wako wapi? Waliteketea ndani ya ule moto? Rosemary Mkozumi alikuwamo katika chumba cha chini je naye aliteketea? Natakiwa kupata majibu ya maswali haya haraka kabla ya jua kuchwea jioni ya leo kwani bila kufanya hivyo itakuwa ni fursa kwa Dr Joshua kutekeleza mpango wake wa kukiuza kirusi Aby kwani kwa mujibu wa mipango yao makabidhiano yatafanyika muda wowote kati ya leo au kesho.I must do something very quick to prevent this to happen.No…..”
Mathew akastushwa toka mawazoni na kengele ya mlangoni akaenda kuufungua mlango akakutana na sura yenye tabasamu ya Yule mwanamke aliyewaandalia chumba jana usiku.
“ Naweza kuingia ndani? Akauliza Yule mwanamke mrembo
“ Bila wasi wasi.Karibu ndani” Mathew akamkarbisha ndani .Mkononi alikuwa amebeba sanduku dogo.Peniela akakurupuka toka usingizini aliposikia kama kuna watu wanazungumza mle chumbani.
“ Mmeamkaje? Poleni na uchovu wa toka jana” akasema
“ Tumeamka salama kabisa” akajibuMathew
“ Vizuri .Baadae asubuhi hii mtakwenda kuonana na baba askofu lakini kabla ya hapo Mathew unatakiwa ukaangaliwe jeraha lako ,atakuja muuguzi kukuchukua .Baada ya hapo mtapata kifungua kinywa halafu tutaondoka kuelekea kwa baba askofu.Katika sanduku hili kuna mavazi mtakayovaa leo .Anzeni kujiandaa” akasema na kuondoka.Mathew akamfuata Peniela aliyekuwa amekaa kitandani
“ Umeamkaje Peniela?
“ Thanks God its another day.I had an awfull night .Had so many bad dreams”
“ Pole sana.Amka tuanze kujiandaa kama tulivyoelekezwa.” Akasema Mathew.Peniela akamshika Mathew mkono na kusema
“ Mathew naomba njoo hapa karibu yangu.I need your strong arms to hug me tight.I feel so weak and I need strength.Please hold me tight Mathew” akasema Peniela.Mathew akamtazama na kumsogelea
“ She’s so weak.Mambo yaliyotokea jana yamemkatisha tamaa kabisa,Inauma sana kumuona binti mzuri kama huyu anakumbana na misuko suko hii mikubwa.Namlaumu sana John kwa kumuingiza Peniela Team SC41.I must help and protect her” akawaza Mathew na kumkumbatia Peniela ambaye alikilaza kichwa chake katika kifua cha Mathew
“ I feel so safe around this man.Nimekutana na nimekutana na wanaume wengi but this one is different from all.Ana vitu vingi ambavyo wanaume wengi hawana.I need to know him better because I’ve started to love him.Yes ! kuna sauti kubwa nasikia ndani mwangu inaniambia this is my man” akawaza Peniela na kufumbua macho akamtazama Mathew
“ Mbona unanitazama hivyo Peniela? Mathew akauliza
‘ Do you trust me Mathew?
“ Yes I do”
“ How much do you trust me?
“ I don’t know how much but I do trust you with my life”
Peniela akatabasamu na kusema
“ Hajawahi kutokea mtu aliyeniamini kiasi hicho,nashukuru sana.Hata hivyo kuna kitu nataka uniweke wazi.Who are these people? Ni askofu gani tunayekwenda kuonana naye? Mambo haya yanayoendelea toka jana usiku yananichanganya sana.Please tell me the truth” akasema Peniela
“ Relax Penny.Relax Baby.You are so safe.Later you’ll know everything” akasema Mathew huku akimuachia Peniela baada ya kengele ya mlangoni kulia
“ Nadhani huyo atakuwa muuguzi.Ngoja nikatibu jeraha langu,wewe endelea kujiandaa” akasema Mathew na kwenda kuufungua mlango.Ni kweli aliyekuwa mlangoni ni muuguzi ambaye alimchukua Mathew kwenda kumtibu jeraha.
“ He called me baby!!..Mathew called me baby!!.” Akawaza Peniela huku uso wake ukiwa katika tabasamu kubwa baada ya Mathew kutoka mle chumbani
“ Sidhani kama alitamka maneno yale kwa bahati mbaya.Naona ni kama vile kuna kitu kinaanza kujengeka kati yeti.Mungu anisaidie Mathew atokee kunipenda” akawaza na kuinuka akaenda bafuni kuoga
Baada ya dakika kumi na tano Mathew akarejea chumbani na kumkuta Peniela tayari amekwisha jiandaa
“ Wow ! Umependeza sana.Aliyekuchagulia mavazi hayo kama vile alikupima kwanza” akasema Mathew.Peniela akatabasamu ,Mathew akaingia bafuni akaoga halafu naye akavaa mavazi aliyoletewa.Wote walipokuwa tayari mlango ukagongwa Mathew akaenda kuufungua alikuwa ni Yule mwanamama.
“ Watu hawa ni kama vile wanatuangalia kupitia vyombo maalum kwani baada tu ya kumaliza kujiandaa tayari wamefika.Who are these people? Akaendelea kujiuliza Peniela kuhusiana na watu wale.Yule mama akawaomba wamfuate wakaongozana hadi katika chumba cha chakula ambako kuliandaliwa mlo wa asubuhi.Ndani ya chumba kile cha chakula kulikuwamo na watu wawili waliovalia suti nyeusi na miwani myeusi.Walikuwa wamesimama wakiwatazama akina Mathew.Walipomaliza kupata kifungua kinywa Yule mama akaja tena
“ Sasa tunaweza kuondoka.Hakuna kitu chochte mlichokisahau? Hatutarudi tena hapa”
Mathew na Peniela wakatazamana kisha Mathew akasema
“ Hakuna tulichokisahau.Hatukuwa na kitu chochote.Yule mama akawaambia wamfuate.Nyuma yao wakafuata wale jamaa wawili .Walishuka kwa kutumia lifti halafu wakaufuata ujia uliokuwa na maua mazuri .Baada ya mwendo wa dakika kama tano wakatokea mbele ya helkopta ya rangi nyeupe.Mmoja wa wale walinzi akawahi na kuufungua mlango na yule mwanamama akawa wa kwanza kuingia ndani halafu Mathew na Peniela wakafuata.Mlinzi akafunga mlango na kusogea pembeni rubani akaiwasha helkopta na baada ya muda helkopta ikapaa na kuondoka ikikatiza juu ya jiji la Dare s salaam.
*******
Toka kulipopambazuka nyumbani kwa Dr Joshua kulikuwa na heka heka nyingi za maandalizi ya mazishi ya Flaviana.Asubuhi hii kijiusingizi kilimpitia jaji Elibariki kwani kwa usiku mzima hakuwa amepata usingizi kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo.Sauti ya mlango kugongwa ndiyo iliyomstua akakurupuka na kwenda kuufungua mlango akakutana na Dr Joshua na walinzi wake
“ Mheshimiwa karibu ndani” akasema jaji Elibariki na Dr Joshua akaingia ndani akawataka walinzi wake wamsubiri nje
“ Umeamkaje Elibariki? Akasema Dr Joshua huku akitazama huku na huo mle chumbani
“ Nimeamka vizuri kabisa mzee.” Akasema jaji Elibariki
“ Nilikuwa natazama kumbe hukuwekewa luninga humu ndani” akasema Dr Joshua.Jaji Elibariki akabaki anashangaa kwa nini alisema vile
“ Kulikuwa na taarifa ya muhimu katika taarifa ya habari ya leo asubuhi lakini kwa vile hukuitazama nitakufahamisha kwa ufupi” akasema Dr Joshua na kuegemea mezani
“ Jana tulipoachana usiku nilizungumza na kamanda wa polisi kanda ya Dar es salaam na dhumuni kuu likiwa ni kutafuta namna ya kukusafisha kutokana na tuhuma zilizokuwa zinakukabili za kusababisha kifo zilizokuwa zinakukabili.Tuliongea kwa kirefu sana na akaniahidi kutafuta namna ya kufanya.Leo asubuhi katika taarifa ya habari imetengazwa taarifa kwamba majambazi manne yameuawa katika majibizano ya risasi na Polisi katika msitu wa Makenge.Baada ya taarifa ile nikampigia simu akanifafanulia kwamba jana usiku baada ya kumpatia ile kazi ya kuhakikisha anakusafisha dhidi ya tuhuma za kusababisha kifo cha Flaviana,alikumbuka kuwapo kwa taarifa za majambazi waliokuwa wakiutumia msitu wa makenge kama maficho yao.Usiku huo huo kikatumwa kikosi cha askari na kwenda kuvamia maficho ya majambazi hao wakawaua watatu na wawili wakafanikiwa kutoroka.Baada ya tukio hilo aliongea na wanahabari na kuwataarifu kuwa wewe ndiye uliyewapa taarifa za uwepo wa majambazi hayo katika msitu wa makenge.Alisema kwamba majambazi hayo yalikuteka nyara na kukulazimisha umpigie simu Flaviana na mpange sehemu ya kukutana waliyokuelekeza na lengo lao kubwa likiwa ni kumteka Flaviana ili wajipatie fedha toka kwangu.Baada ya Flaviana kufika sehemu mliyopanga mkutane majambazi hayo yalitaka kumteka lakini wakakumbana na kikazo cha walinzi wa siri waliokuwa wanamfuatilia Flaviana na ikatokea tafrani ya kurushiana risasi.Baada ya jaribio lao kushindwa majambazi hayo yaliendelea kukushikilia katika maficho yao hadi ulipofanikiwa kutoroka jana.Kwa taarifa hiyo tayari umesafishwa na sasa si mhalifu tena bali unaonekana shujaa.”
“ Thank you Lord !! Jaji Elibariki akashukuru Mungu.
“Elibariki,kutokana na taarifa ile ,watakufuata watu kutaka kukuhoji namna ilivyokuwa,nafahamu maafisa usalama na waandishi wa habari watataka kukuhoji pia lakini unachotakiwa kufanya ni kujieleza kwa ufupi sana .Baadae leo utakutana na kamanda wa polisi Dar es salam na atakuelekeza namna ya kuongea pindi ukiulizwa maswali na mtu yeyote kuhusiana na kile alichokisema kamanda wa polisi kanda ya Dar es salaam. Kwa sasa don’t say anything to anybody hadi hapo utakapokuwa umeonana na kamanda .Tumeelewana jaji?
“ Ndiyo mzee nimekuelewa.Ahsante sana kwa jambo hili kubwa la kulisafisha tena jina langu”
“ Nilikuahidi nitafanya hivyo na nimetekeleza kwa hiyo usiogope tena.Kwa sasa ni wakati wa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuikabili siku ya leo.Itakuwa siku ndefu na ngumu sana kwako but be strong.” Akasema Dr Joshua na kuondoka.
“ Now I’m free !! akasema jaji Elibariki kwa furaha baada ya Dr Joshua kuondoka
“ taarifa hii aliyonipa Dr Joshua itatawala sana katika vyombo vya habari leo hii na itazidi kunifanya nifahamike zaidi” akawaza na kwenda kuketi kitandani
“ Hili la kwanza nimelimaliza najua yatakuwepo maswali ya hapa na pale kama alivyosema Dr Joshua lakini nitakabiliana nayo,kubwa lililobaki ni namna ya kukabiliana na siku ya leo.Siku ya leo ni moja ya siku ngumu mno katika maisha yangu.Mke wangu anakwenda kufukiwa kaburini na yote haya niliyesababisha ni mimi.Endapo nisingekuwa na kiherehere cha kutaka kuingilia mambo ya watu hadi leo hii Flaviana angekuwa bado hai.Najilaumu mno kwa ujinga nilioufanya.Hakuna chochote nilichokipata zaidi ya hasara Nimepoteza mke wangu na kibaya zaidi nimetengeneza mgogoro mkubwa na watu waliojitoa maisha yao kuhakikisha ninakuwa salama.Nimewatenda vibaya mno Mathew na wenzake.Zaidi sana nimemtenda vibaya Peniela mwanamke ambaye ninampenda mno,na nilikuwa radhi hata kuachana na mke wangu Flaviana kwa ajili yake.Yeye ni sababu ya mambo haya yote kutokea kwani kama nisingetaka kufahamu muuaji wa Edson mambo yasingefika hapa yalipofika.Ninajuta sana kumfahamu Peniela.Sijui amejificha wapi mida hii,nina hamu sana ya kutaka kufahamu mahala alipo na anaendeleaje “ akawaza jaji Elibariki na kumkumbuka Mathew mwili wote ukamsisimka.
“ Nimejiingiza katika mgogoro mkubwa na rafiki yangu Mathew.Endapo atagundua kwamba mimi ndiye niliyemsaliti na kumuachia huru Rosemary Mkozumi that man will haunt me till the day I die.Namfahamu vizuri Mathew na nimeshuhudia namna anavyofanya kazi.Ni mtu hatari sana.Nitafanya nini kujiepusha naye? Akawaza na huku akihisi woga mwingi sana.
“ Natakiwa kuhakikisha Mathew anapatikana haraka sana kabla ya harakati za mimi kumrithi Dr Joshua hazijaanza.Bila ya Mathew kupatikana hakuna chochote itakachofanikiwa.Jambo zuri ni kwamba tayari tunaye Anitha.Yule ndiye atakayetuongoza mahala aliko Mathew.Nitaongea na Dr Joshua na kwa kutumia uwezo wake Mathew atapatikana tu.Naandaliwa kushika nafasi nyeti mno katika taifa hili kwa hiyo sihitaji vikwazo vya aina yoyote hapo muda utakapowadia.Kikwazo kikuu kwa sasa ni Mathew.Huyu ndiye natakiwa kufanya kila ninalowezekana hadi nihakikishe anapatikana.Sintajali kama tumekuwa marafiki au la.Ninachojali mimi ni maisha yangu ya usoni na ili mambo yangu yafanikiwe natakiwa kusahau yote yaliyotokea na….” Elibariki akastuliwa na mtu aliyegonga mlango,akaenda kuufungua ,alikuwa ni Anna.
“ Ouh Anna,karibu ndani” akasema jaji Elibariki na Anna akaingia ndani
“ Karibu kiti Anna” akasema jaji Elibariki
“ Hapana nitasimama” akasema Anna huku akimtazama Elibariki kwa macho makali
“ Elibariki nimekuja hapa kwa jambo moja tu ,I want to know why you are here??
Jaji Elibariki akamtazama Anna kwa sekunde kadhaa akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Take a sit Anna”
“ No! I will stand.I want to know why you are here? Wewe ndiye uliyenihakikishia kwamba baba anahusika na vifo vya mama na Flaviana na hata wewe mwenyewe ulikuwa mafichoni ukimkwepa yeye iweje ghafla tu umejitokeza na mmekuwa marafiki as if nothing happened? Whats going on? Tell me the truth who killed my mother and my sister? Akasema Anna kwa ukali
“ Anna calm down.I’m here because I’m Innocent na hakuna anayeweza kunizuia kuhudhuria mazishi ya mke wangu” akasema jaji Elibariki kwa sauti ya juu kidogo.
“ Jeshi la polisi wanakusaka kila kona kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Flaviana.Kama unadai huna hatia ni kwa nini ulikimbia na kujificha? Na kama si wewe nani basi aliyesababisha kifo cha Flaviana?
Jaji Elibariki akabaki anamtazama Anna bila kujibu chochote
“ Answer me Elibariki!! Akasema Anna
“ Ina maana mpaka sasa hujapata taarifa za kilichotokea? Hujatazama taarifa ya habari leo asubuhi kufahamu kilichotokea? Akauliza jaji Elibariki
“ Sina muda wa kutazama taarifa habari” akasema Anna
“ Katika taarifa ya habari leo asubuhi kumeelezwa kila kitu kuhusiana na kilichotokea .Ningependa kukueleza kila kitu lakini hatuna muda wa kutosha nakuomba tutafute wasaa tukae na nitakueleza kila kitu.Please Anna” akasema jaji Elibariki.Anna akamtazama kwa muda halafu akasema
“ You and I will have a serious talk later!! Akasema Anna na kuufungua mlango akatoka.
“ Lazima kutakuwa na jambo linaloendelea hapa.Hainiingii akilini mtu ambaye jeshi la polisi linamsaka kwa tuhuma za kusababisha kifo halafu ghafla tu anaibuka na kuwa huru.Vipi kuhusu yale aliyonieleza kwamba baba anahusika katika vifo vya mama na dada? Alikuwa ananidanganya?...Nitaufahamu tu ukweli wote”Akawaza Anna baada ya kutoka chumbani kwa jaji Elibariki.
“ Katika watu ambao watanipa wakati mgumu ni huyu Anna.Tatizo kubwa ni kwamba hapo awali nilimueleza kwamba baba yake anahusika katika vifo vyote vilivyotokea katika familia yao yaani vifo vya mama na dada yake.Kwa sasa baada ya kuungana na baba yake natakiwa kuitengua kauli yangu na kufunika maovu yote ya Dr Joshua.Sina namna nyingine ya kufanya nimechagua mwenyewe kumfuata shetani hivyo lazima nifanane naye.Sikuwahi kufikiri hapo kabla kwamba itafika siku moja mimi kama jaji wa mahakama kuu ambaye jukumu langu ni kutafuta haki nitakuwa sehemu ya watu wanaodhulumu haki za watu lakini tayari imetokea kilichobaki ni mimi kufunga buti na kuendelea na safari hii mpya ya maisha niliyoyaanza.Flaviana is gone,everything is gone so I need new life and this is my new life.” Akawaza jaji Elibariki halafu akaingia bafuni kuoga na kujiandaa.
******
Mlango wa chumba alimofungiwa Anitha ukafunguliwa taa ikawashwa na watu wawili wanaume wenye miili iliyojengeka wakaingia mle chumbani
“ Ooh Mungu nisaidie hawa ni wale watesaji.Wanataka kunitesa tena ili niwaeleze mahala aliko Mathew.Mateso ya jana yalikuwa makali na yalinidhoofisha sana lakini hata wanitese vipi sintofungua mdomo wangu kuwaeleza chohote kuhusu Mathew. Niko tayari kufa lakini si kusema kile wanachonitaka niseme.These people are devils.Nimeshindwa kupata jibu ni shetani gani alimuingia jaji Elibariki na kumfanya atusaliti kwa watu hawa.Jitihada zote tulizozifanya za kukiokoa kirusi Aby zimegonga ukuta na yote hii ni kwa sababu ya jaji Elibariki..” akawaza Anitha na kushikwa kichwa na mmoja wa wale jamaa akamtazama kwa muda halafu akasema
“ Sifurahii kukutesa mwanamke mrembo kama wewe lakini nipo kazini na bosi wangu, ananitaka nikutese hadi umpe kile anachokihitaji.Tafadhali mrembo usiache mateso haya yaendelee,mweleze Madam Rose kile anachokihitaji toka kwako ili akuachie huru.Ukimya wako utazidi kumpandisha hasira na anaweza hata akakuua.Usitake mambo haya yafike huko “ akasema Yule jamaa kwa sauti ya upole
“ Hivi sasa tunakupeleka katika chumba cha mateso na yeye atakuja kushuhudia ukiteswa na atakutaka kwa mara nyingine umueleze kile anachokitaka.Usikubali kuteseka ,mweleze ukweli ili akuachie huru uende zako” akasema Yule jamaa na kumfungua Peniela akamnawisha uso halafu wakambeba hadi katika chumba cha kutesea
“ I’m so weak ad scared.Lakini vyovyote itakavyokuwa niko tayari kufa kuliko kumsaliti Mathew” akawaza Anitha wakati anafungwa katika kitanda maalum cha kutesea.Vifaa vikaanza kuandaliwa kwa ajili ya kumtesea,akaingiwa na woga mwingi
“ Help me God !! I’m so scared !!....akaomba Anitha kwa woga baada ya Yule mtesaji kugusanisha nyaya na chehe kutokea.Baada ya kuweka kila kitu sawa mmoja wao akamfahamisha Rosemary Mozumi kwamba kila kitu kiko tayari.Hakuchukua muda mrefu akafika mle chumbani
“ Good.Kama kila kitu kiko tayari anza kazi yako mara moja,hatuna muda wa kusubiri,leo lazima atasema tu” akasema Rosemary ambaye alikuwa anatembea kwa kuchechemea akisaidiwa na fimbo akamsogelea Anitha
“ Binti naomba usiendelee kunijaribu ,nakutaka kuona nikikasirika ninakuaje.Nieleze haraka aliko mwenzako Mathew.Ukinisaidia kumpata nakuahidi kukuachia huru kwani shida yangu mimi si wewe bali ni Mathew pekee”
“ Go to hell !! akasema Anitha na kumpandisha hasira Rosemary ambae akamgeukia Yule mtesaji
“ Show her how the hell looks like!! Akasema kwa ukali
Anitha aliteswa mno hadi akapoteza fahamu lakini hakuthubutu kutamka chochote kuhusu Mathew
“ Wake he up !! akasema Rose kwa ukali baada ya Anitha kupoteza fahamu
“ Madam this is enough !! Siwezi kuendelea kumtesa zaidi ya hapa kwani lazima atapoteza maisha.”
“ Fernando I worn you,don’t try me,Wake her up !!!
“ I cant madam.Hiki ni kiwango cha mwisho cha mateso na hajasema chochote ,mtu huyu hata ateswe vipi hataweza kusema chochote.Tafuta namna nyingne ya kumfanya aweze kusema lakini si kwa njia ya mateso.” Akasema Fernando .Rosemary Mkozumi akapandwa na hasira kazi akazitimua nywele zake halafu akamgeukia Fernando.
“ Take her back to her room.I’ll find someone else to do my job.For the first time you’ve disappointed me Fernando !! akasema Rose na kutoka mle chumbani
“Mathew na wenzake nI watu wa namna gani? Mateso aliyoteswa Yule msichana ni ya kiwango cha juu mno na hayavumiliki lakini hajathubutu kufungua mdomo wake kusema chochote.Fernando yuko sahihi kabisa njia ya mateso naona kama haisaidii kitu na hataweza kusema chochote.I must find another way to break her…Natakiwa kumpata Mathew haraka sana na kadiri ninavyochelewa ndivyo anavyozidi kujipanga na ndivyo inavyozidi kuwa ngumu kumpata.Hata hivyo sikati tamaa.Nitamshawishi Dr Jshua tuunganishe nguvu na kumsaka Mathew hadi tumpate” akawaza Rose
******
Helkopta waliyopanda akina Mathew ilikatisha katika anga la jiji la Dar es salaam na kuvuka bahari ya hindi kuelekea Kigamboni.Taratibu rubani akaanza kuishusha chini kuelekea katika jumba moja kubwa la kifahari mno.Helkopta ile ikatua katika sehemu maalum iliyojengwa kwa duara na kuandika herufi H ikiwa na maana ya helkopta
“ Tumefika” akasema Yule mwanamama waliyeongozana naye.Watu wanne waliovalia suti nyeusi wakaisogelea helkopta ile baada ya injini kuzimwa,mmoja wao akafungua mlango na wa kwanza kushuka alikuwa Yule mwanamama halafu wakafuata Mathew na peniela.Mathew akamshika mkono Peniela wakaongozana na Yule mwanamama na nyuma yao wakiwafuata wale walinzi watu wanne.
“ What a beautifull place.Ama kweli Tanzania hii kuna watu wanaishi kama wako peponi” akawaza Mathew.Mlango mkubwa ukafunguka mara tu walipokimbia halafu Yule mwanamama akawaongoza hadi katika chumba Fulani na wakatakiwa kusimama wakiwa wameinua mikono juu.Taa ya kijani ikawaka na kuwamulika kwa sekunde kadhaa halafu ikazima na kuwaka nyeupe kisha mlango ukajifungua wakatoka.
“ Mtumishi gani wa Mungu anakuwa na ulinzi mkali kiasi hiki? Askofu wa aina gani huyu mwenye utajiri mkubwa kiasi hiki? Akajiuliza Peniela wakati wakipanda ngazi kuelekea ghorofani.Hatimaye wakatokea katika sebule kubwa iliyokuwa na uzuri wa ajabu.Mathew na Peniela wakakaribishwa na kukirimiwa kila mmoja alichohitaji.Wakiwa pale sebuleni wakitazama muziki wa dini katika luninga kubwa akaingia dada mmoja akaongea na Yule mwana mama aliyeongozana na akina Mathew walionekana wanaelekezana jambo halafu Yule mama akawarejea akina Mathew.
“ Baba askofu ana kikao kifupi na wachungaji kwa hiyo tuendelee kumsubiri.Mara tu atakapomaliza kikao hicho itakuwa ni zamu yenu kuonana naye”
Yule mwanamama akawaambia akina Mathew .Waliendelea kusubiri huku wakitazama muziki wa dini.Hakukuwa na maongezi mle sebuleni kila mmoja alikuwa anafuatilia muziki kimya kimya.
“Natamani kufahamu anachopanga Mathew kuhusiana na kilichotokea.Toka tulipotua kwa hawa jamaa hatujaongea chochote juu ya kilichotokea na sijui ana mipango gani kwani kila tulichokipanga kimevurugika.Hata mimi mwenyewe najitahidi kuwaza namna ya kufanya nakosa jibu .Je hii ina maana kwamba juhudi zetu zote za kuzuia uuzwaji wa kirusi Aby zimeshindikana? Hapana siamini kama Mathew anaweza akakubali hilo litokee najua lazima kuna kitu anakifikiria.Ngoja niendelee kuwa mvumilivu nione kitakachotokea” akawaza Peniela
“ Sijui nini kinachoendelea kuhusiana na msiba wa John Mwaulaya.Natamani sana kama ningeshiriki mazishi yake lakini haiwezekani tena.Team SC41 wananitafuta kila kona.Kuna mtu mmoja tu ndani ya Team SC41 ambaye anaweza kunipa taarifa za kila kinachoendelea kule ambaye ni Josh .Nitatafuta namna ya kuwasiliana naye “ akawaza Peniela
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……