Kuna series moja inaitwa REVOLUTION ningekushauri ukaiangalie!. Labda kama hujui tu maisha ya binadamu wengi yanategemea teknolojia sasa hivi mfano mdogo tu ni hii IoT (internet of thing) ambayo kila kifaa kinajaribu ungwa na internet mpaka umeme unanunua kwa simu yako tu!, sasa Bomu la Nuclear likipigwa inamaana litaenda disrupt any electrical devices, fikiria leo hii kwa masaa 24 tu huduma zote muhimu zisimame itakuwaje!?.
Serikali yeyote inapofeli iwe kiuchumi, kisiasa, kijamii basi ndio mwisho wa Taifa hilo mfano mdogo chukulia Syria, Yemen na Iraq. Sasa hiyo hali ikuze dunia nzima!.
MAD waasisi ni hao lakini sio kwamba wao pekee wataifanya hiyo sera, India na Pakistan ni Paka na Panya wao pia wanaweza ifanya, Iran na Israel nao pia wanaweza ifanya.
Nilipokupa mfano wa Kenya nilijaribu kukuonyesha ni jinsi gani tutaweza athirika kupitia MAD sababu leo hii US akiweka kambi Kenya usitegemee atatumia silaha za kawaida ni ataleta mpaka Nuclear bombs pale, sasa unategemea Russia atapiga mabomu yake yote USA wakati amejua hata akiilevel America bado Second strikeitatokea Kenya, si itambidi ailevel na Kenya!.
Sera ya MAD ni "kuwa na uwezo wa kurudisha shambulizi sawa sawa pale utakaposhambuliwa" haitatokea eti wakubaliane sasa 'tumalizane!'.
Tambua zamani mabomu yalikuwa yanatengenezwa MAKUBWA kupiga SEHEMU KUBWA lakini siku hizi yanazalishwa MADOGO kupiga SEHEMU KUBWA ndio maana kama lile Minuteman lina version tofauti, linazidi kuwa dogo lakini likiwa na effects kubwa zaidi. Sasa hapo ya nini kuwa na mabomu mengi ikiwa machache yataweza ifanya kazi ile ile. INF treaty imevunjwa what else kama sio testing zaidi!.
Maisha ya binadamu kwa wenzetu yameangaliwa sana ndio maana wanaendelea tengeneza Nuclear Bunkers ambazo kipindi cha vita sio lazima Taifa zima likajifiche ili mradi wachache wakiweza survive!. Ukisoma kitabu kinaitwa "Death by China" utaelewa ni kwa jinsi gani hata mchina anawekeza kwenye ujenzi wa mahandaki milimani!.
Mabaki ya Nuclear Fallout yatabebwa na Upepo+Mvua mpaka maeneo mengine kabisa!.
Movies pamoja na Series ni nzuri sana pia nazipenda ila katika baadhi ya mambo ni vyema kujikita zaidi katika tafiti za kutosha ili kujikusanyia facts ama taarifa za kisomi zaidi.
Maana kuna filamu nyingi sana ulimwenguni kuhusiana na masuala haya lakini zina fictions nyingi sana na mapungufu mengi ya kiutafiti ambazo haziwezi kutumika kama kielelezo katika kuyaelezea masuala mbalimbali ya kidunia na mwenendo wa maisha ya kibinadamu.
Shukrani kwa hiyo recommendation.
Tukiachana na hilo;
Je, unafahamu kuwa uwepo wa mifumo au makazi ya kujikinga ama kwa lugha nyingine, Massive Scale Shelters kunauondoa kabisa msingi mkuu wa Mutual Assured Destruction?
Je, unafahamu kuwa uwepo wa Missile Defense Systems na kuongezeka kwa uwekezaji wake kwa kiasi kikubwa pia kunaifanya Mutual Assured Destruction kutoweza kuwa implemented?
Kuna masuala ya Counter value na Counter force katika vita ya kinyuklia, ambapo kwa namna moja ama nyingine ni kipingamizi kwa Mutual Assured Destruction kufanikiwa.
Mutual Assured Destruction haiishii katika kushambuliana sawasawa, bali ili Mutual Assured Destruction iwe implemented na msingi wake mkuu ni lazima mwishoni kuwe na "Total Destruction on Both Sides". Tofauti na hapo, MAD haipo.
Msingi wa hoja upo katika Full Scale Nuclear War kati ya Marekani na Urusi ambapo ndipo nadharia hii ya Mutual Assured Destruction ilipoasisiwa.
Unapozungumzia suala la mgogoro wa Pakistan na India ni scenario tofauti kabisa maana hata Military Doctrines zao ni tofauti ukilinganisha na upande wa Marekani na Urusi. Mfano, programs za kinyuklia za Pakistan zinahusisha kitu kinachoitwa N-Deterrence ambayo ni Minimun Nuclear Deterrence kitu ambacho ni kinyume kabisa na MAD, same applies kwa upande wa India.
Tukija kwa Israel na Iran, pia hapo hakuna uwezekano wa Mutual Assured Destruction kabisa kwa sasa. Isitoshe hakuna taarifa zozote kuhusiana na silaha za nyuklia za Iran na kwa kifupi tu ni kuwa hapo kuna utofauti mkubwa tena kupita kiasi wa nguvu za kinyuklia ambapo ni kinyume kabisa na nadharia ya Mutual Assured Destruction.
Umezungumzia kuhusu Nuclear Bunkers au pia Fallout Shelters.
Ndiyo maana nikasema, na pia utakubaliana na mimi kuwa kuna factors nyingi za kulidhoofisha shambulizi la kinyuklia na moja wapo ni hiyo uliyoitaja kitu ambacho ni kinyume kabisa na Mutual Assured Destruction Doctrine.