Mpaka sasa bado sijaona saana umuhimu wa ndege vita kwa upande wa ukraine. Hadi kufikia sasa Russia ameshindwa kuteka hata 40% ya Ukraine, na sehemu alizoshikilia bado mapambano yanaendelea na kwingine Ukraine ameanzisha mashambulizi.
Kitu kikubwa anachotaka Ukraine ni kupewa Air Defence Systems bora pamoja na MRLS za masafa marefu. Russia ameacha kutumia ndege, vifaru mara kwa mara na magari vita, ila anatumia makombora ya masafa marefu. Na hii ni baada ya kuona ndege zake hazifui dafu pale Ukraine.
Ukraine atahitaji Air Defence ili kuzima mashambulizi ya Russia, huku na yeye apewe silaha za kushambulia ili kuweza kukomboa kile alichopoteza, hayo masuala ya ndege nafikiri ni kwa baadae sana kama US alivyoona, tusisahau pia Kurusha ndege ni cost kubwa, sasa kwa hali ya Ukraine ya sasa anapata wapi pesa ya kurusha hizo ndege? Pengine ndio maana US ameona muda bado wa Ukraine kupewa ndege vita hizo.