Penye nia pana njia: Ni wiki ya 5 sasa sijatia soda mdomoni, kumbe inawezakana kabisa

Inawezekana ila ni ngumu mie ilikuwa ninakunywa wastani wa soda 6 kwa siku,
Asubuhi kabisa moja , baada ya chai asu supu moja , katikati ya mchana na asubuhi moja. Chakula cha mchana lazima kiambatane na coke baridi , Jioni moja na wakati wa chakula cha usiku lazima ipatikane coke baridi pia

Ilitokea siku moja , nikawa nakunywa soda ila sipati ladha yoyote nikaamua kuacha
miaka 2 sasa ila cha ajabu ile hamu ya coke baridi hasaa baada ya supu ya asubuhi imerudi tena at rime nakunywa moja moja japo siruhusu initawale tena.
 
Hii kitu ni addictive kuliko tunavyodhani, we fikiria kila siku watu wanaambiwa madhara ya kutisha ya soda lakini nado wanakunywa, sio kwamba wanapenda kufa , hapana, ila soda ukiacha kunywa ina Arosto kali sana kama Cocaine, ni balaa.
nikweli soda in arosto,Mimi pia nipo addicted na COCA-COLA hile yenye nembo nyekundu,

Hila nipo kwenye mkakati wakutaka kuacha kunywa soda
 
Yaani mtu anaanzaje kupenda soda hadi anakua Addicted??? Ni sawa uniambie eti una hamu ya bia. Bia inakupaje hamu jamani
Omba tu yasikukute , addiction ni balaa, sio rahisi kama unavyodhan ku control uraibu
 
Wakati mwingine ni maamuzi tu ya mtu binafsi , binadamu timamu lazima afanye valuation kadiri umri unavyosogea , kuna mambo unatakiwa uyaache na kuna mambo unatakiwa uanze kufanya , sio kweli kila mabadiliko anayofanya mtu yatokane na kupata tatizo,
 
Hii kitu ni addictive kuliko tunavyodhani, we fikiria kila siku watu wanaambiwa madhara ya kutisha ya soda lakini nado wanakunywa, sio kwamba wanapenda kufa , hapana, ila soda ukiacha kunywa ina Arosto kali sana kama Cocaine, ni balaa.
Punyeto na soda,kipi kina arosto zaidi ?
 
Soda mimi hazinitesi kabisa hata kama nakunywa huwa simalizi soda yote nitakunywa nusu chupa tena kwa kuweka na ice km ipo karibu.
 
Nilifikiri unaongelea bia, kumbe unaongelea vinywaji vya watoto.
 
Ndo nilikua hapa nakula wali maharage na ka sod ka mirinda nyeusi kabaridiiiii. Nikasema niingie JF huku nakula taratibu nakutana na hii post. Nikasema wacha ninyweee nileeee maisha hayana fumyula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…