Penye nia ya kisiasa pana njia ya kisiasa

Penye nia ya kisiasa pana njia ya kisiasa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
51,453
Reaction score
41,274
Mwanasiasa mzuri na mahiri hutumia na kubadilisha changamoto anazokumbana nazo katika majukwaa ya kisiasa na kua fursa ya kujiimarisha na kujizatiti zaidi kufikia ndoto, lengo, matarajio na azma yake ya kisiasa..

Mathalani, kushindwa uchaguzi ni fursa muhimu sana ya kujitahimini, kujisahihisha, kujirekebisha, kujifunza na kuongeza uelewa na ufahamu zaidi, wa mbinu, mazingira na mikakati mbadala itakayokuwezesha kujiamini zaidi na kujipanga vizuri zaidi kimkakati na kuwa na uhakika mkubwa zaidi wa kushinda uchaguzi unaofuata, au hata kua the most vibrant, respected, trusted, Powerful, Vocal or feared oppositions.

Kulalamikia, kususa au kugomea masuala ya kdemokrasia hususani chaguzi, kumewachelewesha sana na kuwapotezea uelekeo na malengo wanasiasa wengi hasa vijana walioshindwa kubuni namna bora ya kubadili changamoto kua fursa ya kujiimarisha zaidi kisiasa, na badala yake, wamejikita na kujipotezea wakati na muda mwingi mathalani kwenye kesi za fujo mahakamani, uchochezi na ukaidi wa Sheria bila shuruti na maandamano ambayo mara nyingi, kwa mfano Tanzania yamekua hayana maana wala faida yoyote kwa wanasiasa.

Vijana viongozi wanasiasa, ndani ya vyama vya siasa humu nchini mnalo jukumu muhimu sana la kufanya uamuzi mgumu wa kuchagua jukwaa ambalo walau lina uhakika wa kuamua au kufikia ndoto na matarajio yeko katika siasa.

Hamjachelewa bado, ni muhimu sana kuchangamana, kuambatana na kuandamana sambamba na walio fanikiwa katika siasa na mambo mengine kwasabb ni rahisi zaidi nanyi kufanikiwa. kung'ang'ana na walioshindwa ni kujichelewesha.

penye nia, dhamira na malengo ya dhati ya kisiasa, pana mikakati na njia za kisiasa kutimiza ndoto na matarajio ya kisiasa, usichoke, usivunjike moyo na usikate tamaa 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom