But binafisi nimesema siku nyingi, naona hii ndio njia pekee, japo wengi tunatofautiana kila nikilizungumzia. Nchi hii tumeishi kinafiki kwa miaka mingi, japo tuna katiba bora zaidi ya zote Afrika lakini tumevurugwa kiakili na viongozi na kuishia kuchukiana hata bila sababu.
Igawanywe vipande tu ili tuagane kila upande uende unakotaka. Tumeishi mkao wa kufuata mkumbo na maagizo ya viongozi, leo hii hata hiyo mnaita People republic, ikitokea Kalonzo na Raila wagombane, mtaigawa vipande zaidi, pia ikitokea Uhuru na Ruto wawe na ugomvi, hicho kipande mtakachotuachia itabidi tukigawe zaidi. Yaani nchi tunaendesha kwa hisia za viongozi.
Kiongozi wa kule akigombana na wa huku mnagawa nchi, wa hapa akigombana na wa pale mnagawa nchi zaidi, huo ni mtindio wa ubongo. Kwamba kesho ya kesho Mudavadi akigombana na Wetangula hata Uluhyani itabidi wagawane, kabogo akigombana na Kiraitu tunagawa mkoa wa Kati.....upuzi mtupu.
Halafu unafiki ndio zetu, hamna upande wowote unaoweza kulekeza kidole kwa wa pili, mlengo wa NASA unaongozwa na viongozi wakabila watupu, vile vile Jubilee hawana utofauti wowote.
Naomba hiyo tarehe 26 ifike mapema kama pachimbike pachimbike tu, kama tutatengeneza tutengeneze, lakini ndio iwe mwisho wa haya malumbano, kila Mkenya awe tayari kulipia gharama, wa kufa afe, wa kuishi aishi lakini akiwa na amani akilini, aidha tuigawe nchi vipande au tuiboreshe lakini baada ya hiyo tarehe 26 lazima kieleweke. Sio kila wakati kiongozi akishindwa kwenye uchaguzi, kinachomjia akilini ni kuvuruga na kuharibu kila kitu, lazima tufike mwisho wa haya.