Aaah, ni swali gumu sana kulijibu, ila tatizo la Kenya lilitokana na mzee Jommo Kenyatta kushindwa kuwa na maono au lengo la kujenga taifa la Kenya, alidhani wananchi watakuwa kitu kimoja automatically bila kufanya juhudi za makusudi za kuwaleta pamoja, matokeo yake ndio haya tunayoyaona sasa. Jambo la kushangaza wananchi wengi wa Kenya wanaishi maisha ya nadharia sana kwa kujifanya hali hii ya mgawanyiko haipo ni maneno tu ya watu wasioipenda Kenya, wanajidanganya kufuata demokrasia sawa na nchi zisizo na matatizo ya ukabila, walipaswa kuchagua mfumo wa demokrasia ambao ungetilia maanani ukabila wao na kuingiza katika katiba yao ili kuongoza nchi, kwa mfano huku Tanzania tulipoungana na Zanzibar, tulitengeneza katiba ambayo ilitilia maanani utofauti huo wa Tanganyika na Zanzibar, tukafanya kwamba urais uwe ni wakupokezana kati ya Bara na Zanzibar, hatukujidanganya kama wanavyojidanganya wakenya kwa kusema, mtu yeyote agombee tu bila kujali tofauti zilizopo ndani ya nchi, eti kw kigezo cha demokrasia ndiyo inataka hivyo, huko ni kujidanganya, kwa sababu makundi yanaidadi tofauti ya watu, kuna baadhi ya jamii hazitokaa ziongoze milele, kama watu hawajali tofauti zao kama huku Tanzania, hilo sio tatizo, lakini kwa nchi iliyogawanyika kama Kenya, ni lazima kuwa mfumo wa makusudi wa kuhakikisha kila kabila lina uhakika kuna siku watatawala nchi, hata kama ni baada ya miaka mia mbili ijayo, watakuwa wanajiona nao ni raia sawa na kabila lingine lolote nchini, ila kwa sasa, mtaita ana uhakika hata baada ya miaka elfu moja hawezi kuwa rais wa Kenya, njia pekee ni kujitenga ambako huko kunaweza kuwahakikishia nafasi ya kupata kuwa rais.
Kwa kifupi Kenya ni lazima ichague kati ya haya mawili
1)Iweke sheria ya kupokezana nafasi ya urais na makamo rais kufuata makabila, hii itaifanya Kenya iendelee kuwa nchi moja
2)Nchi igawanywe kama inavyopendekezwa na baadhi ya wakenya