Pep aache visa bana. CR 7 yuko sahihi. Kacheza Man U kachukua UEFA Champ, kaenda Real Madrid kachukua tena mara tatu mfululizo. Sasa kaamua kwenda nchi nyingine timu kubwa nyingine ambayo inakilakitu ila tu haijachukua hili kombe na ina uchu wa kulichukua, sasa CR7 kujiunga na timu hii sio changamoto mpya?! Maana timu haijamsajili kuwasaidia kuchukua kombe la ligi au lingine lolote ni UEFA, hii ni changamoto kubwa sana kwa CR7. Yeye kwenda ujerumani alikua anafata hela na sio changamoto kwa kazi yake ni sawa, tuna uhuru wa kila mtu kua na mtazamo kwenye kazi yake.