dah mbona Pep pale Bayern jana hakua na Messi na alitisha mno?
achiliambali kushnda vikombe tele huko Ujerumani?
Nadhani hujaelewa, ama hujaelewa vya kutosha. Ngoja nkujaze maarifa kidogo kuhusu mrembo pep guardiola, anayependa copy and paste vya wanaume wenzake.
Pep kabeba makombe mengi Barca sababu alikuwa na Messi, na kumbuka kipindi kile hii style ya Barca tiki taka ilikuwa ikisumbua sana timu pinzani.
Mashabiki wa Barca tulimuona Pep ni mwehu pale timu inaposa plan b baada ya kubanwa. Timu pinzani zikipata chance ya kuongoza ushindi basi wanazuia mwanzo mwisho. Barca hii ya sasa umewahi kuona inawekewa makontena?
Pep alikuwa na Henry, tukampaga Ibra ijapokuwa eto'o hakustahili kuondoka. Alikuwa na Villa pia, hawa wote wanaweza wakafunga hata nje ya Box endapo mkawekewa kontena, hawa wote pia counter attack walikuwa wanaziweza, Pep alijali hilo? Matokeo yake akaanza kuwapa namba akina Tello, Cuenca n.k hata leo hii Pep angekuwa Barca usingemuona Neymar akiacheza mwanzo mwisho, angetokea bench kumpokea Pedro. Usingemuona Suarez pale.
Kuhusu kubeba makombe Bayern hata wewe unaweza, Bayern = PSG. Ligi haina ushindani, utashindwa kubeba makombe? Jiulize kwanini haendi kufundisha timu ambazo zinahitaji kusukwa upya? Kuna Man U, Chelsea n.k zote hizi alizitolea nje.
Bayern kabeba makombe sababu nyingine ni kwamba timu kaikuta na ilikuwa inabeba makombe hivyo hivyo. We ngoja uone atakavyohenya huko EPL.