Chambou255
Member
- Feb 15, 2019
- 16
- 19
Katika taarifa za kushtusha inatipotiwa kwamba kocha wa Man City Pep Guardiola amekubaliana kwa mdomo kujiunga na Juventus.
Mwandishi wa habari Luigi Guelpa ameiambia radio ya CRC kwamba chanzo chake cha kuaminika ambacho kimempa taarifa hizo ndicho kilichomwambia kuhusu CR7 kwenda Juventus, mwandishi huyu ndiye wa kwanza kusema Cristiano anaenda Turin.
Luigi Guelpa ameendelea kwa kusema chanzo chake kimemuambia Mcatalan huyo amepewa ofa ya miaka minne Juventus.
Guardiola tangu atue Etihad 2016 akitokea Bayern Munich amebeba kombe la Carabao 2017 wakimfunga Arsenal 3-0, akabeba ndoo EPL msimu wa 17/18 na kombe la hisani 2018 na sasa wanaongoza ligi kwa pointi moja wakiwa na pointi 71 wakipumuliwa na Liverpool wenye pointi 70, wanatarajiwa kukipiga na Schalke 04 kwenye mechi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ndani ya Etihad wakiwa na ushindi wa 3-2 mkononi.
Sent using Jamii Forums mobile app