Pep Guardiola kwenda Juventus FC?

Pep Guardiola kwenda Juventus FC?

Chambou255

Member
Joined
Feb 15, 2019
Posts
16
Reaction score
19
Katika taarifa za kushtusha inatipotiwa kwamba kocha wa Man City Pep Guardiola amekubaliana kwa mdomo kujiunga na Juventus.

Mwandishi wa habari Luigi Guelpa ameiambia radio ya CRC kwamba chanzo chake cha kuaminika ambacho kimempa taarifa hizo ndicho kilichomwambia kuhusu CR7 kwenda Juventus, mwandishi huyu ndiye wa kwanza kusema Cristiano anaenda Turin.

Luigi Guelpa ameendelea kwa kusema chanzo chake kimemuambia Mcatalan huyo amepewa ofa ya miaka minne Juventus.

Guardiola tangu atue Etihad 2016 akitokea Bayern Munich amebeba kombe la Carabao 2017 wakimfunga Arsenal 3-0, akabeba ndoo EPL msimu wa 17/18 na kombe la hisani 2018 na sasa wanaongoza ligi kwa pointi moja wakiwa na pointi 71 wakipumuliwa na Liverpool wenye pointi 70, wanatarajiwa kukipiga na Schalke 04 kwenye mechi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ndani ya Etihad wakiwa na ushindi wa 3-2 mkononi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Possible mission. Haka kajamaa kana tamaa sana ya mataji kila ligi usijeshangaa akaja fundisha timu za afrika maana ni kama anakusanya rekodi za makombe ligi zote chini ya FIFA

Nnachompendea huyu mwalimu huwa harembirembi mtu...nnamuona Ronaldo akipigwa bench 😂😂😂😂
 
Kama kweli Guardiola ni kocha anayejiamini, aende Cardiff akachukue kombe. Kwanini anapenda kwenda timu kubwa tu?
Katika taarifa za kushtusha inatipotiwa kwamba kocha wa Man City Pep Guardiola amekubaliana kwa mdomo kujiunga na Juventus.

Mwandishi wa habari Luigi Guelpa ameiambia radio ya CRC kwamba chanzo chake cha kuaminika ambacho kimempa taarifa hizo ndicho kilichomwambia kuhusu CR7 kwenda Juventus, mwandishi huyu ndiye wa kwanza kusema Cristiano anaenda Turin.

Luigi Guelpa ameendelea kwa kusema chanzo chake kimemuambia Mcatalan huyo amepewa ofa ya miaka minne Juventus.

Guardiola tangu atue Etihad 2016 akitokea Bayern Munich amebeba kombe la Carabao 2017 wakimfunga Arsenal 3-0, akabeba ndoo EPL msimu wa 17/18 na kombe la hisani 2018 na sasa wanaongoza ligi kwa pointi moja wakiwa na pointi 71 wakipumuliwa na Liverpool wenye pointi 70, wanatarajiwa kukipiga na Schalke 04 kwenye mechi ya pili ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ndani ya Etihad wakiwa na ushindi wa 3-2 mkononi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaenda Juve kuwapa Uefa au ligi? Maana huyu jamaa Rekodi ya kubeba uefa imeishia Barcelona tu sio Bayern wala City ataweza fanya hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chambou255

Screenshot_20190310-234641_Instagram.jpg
 
Guadiola na PSG ndio wameparamisha bei ya wachezaji Ulaya. Yaani hawa hawaoni hatari kununua mchezaji bei ya Airbus.
 
Kuacha umbea huwezi?
Huyo Guadiola unaemsema lini amenunua mchezaji wa bei kuliko alionunua morinho.
 
Stop nonsense and Google uone Guadiola ashatumia paundi milioni ngapi kununua wachezaji tangu atue Manchester city. Nikikukuta pesa unayoweza kununua Airbus kumi na Airport kabisa
 
Back
Top Bottom