mwanakaya
Member
- Mar 17, 2012
- 56
- 183
Wakati anaanza kufundisha Timu ya Barcelona kutoka kwa mtangulizi wake Frank Rijkaard mwaka 2008, wengi nikiwemo mimi hawakuamini kama Josep Pep Guardiola anaweza kufanya makubwa hasa kutokana mafanikio na aliyokuwa ameyapata mtangulizi wake pamoja na umri wake mdogo wa miaka 37. Pep alichukua timu akiwa hana uzoefu mkubwa akitokea kufundisha Barcelona B.
Baada ya muda mfupi Pep alitengeneza Falsafa yake ya pasi fupi fupi maarufu kama Tiktak kupitia wa vijana aliotoka nao La Masia Iniesta, Xavi na Messi. Pamoja na mafanikio hayo wengi tuliendelea kutoa sababu mbalimbali za kumkosoa ikiwemo kubebwa na ubora wa wachezaji, urahisi wa ligi n.k.
Pep aliendelea kuridhihirisha ubora wake kwa kuendelea kuwanyanyasa washindani wao Real Madrid anavyotaka kila walipokutana. Lakini zaidi alifanya jambo geni zaidi baada ya kuinyanyasa vibaya timu ya Sir Alex Ferguson kocha mwenye mbinu kali na mkongwe kwenye fainali za UEFA mwaka 2009 na 2011.
Baada ya kuchukua kila taji Hispania alienda Ujerumani ambako alifanikiwa kutawala ligi ya Ujerumani japo hakuweza kuchukua kombe la Ulaya. Wapinzani wake waliendelea kumbeza kwamba Bundesliga ni ligi ya timu moja kwa hiyo hana jipya.
Sasa ni msimu wa tatu Pep yuko kwenye ligi inayofuatiliwa zaidi ya Nchini England. Hapa sasa ndiko utetezi wa wengi nikiwemo mimi unapofika mwisho. Ndani ya muda mfupi Pep ameweza kufanya kila analotaka kwenye ligi hiyo. Amebadili aina ya mchezo wa Man City na kuwa mpira wa pasi nyingi za kuvutia.
Kwa sasa nadiriki kusema Pep ni kocha bora zaidi wa kizazi cha sasa ndani ya miaka 10 baada ya kizazi cha Ferguson, Capello, Ancheloti kuondoka.
Naomba radhi Pep kwa kejeli juu yako. Nisamehe
Sent using Jamii Forums mobile app