Pep Guardiola, Nakutaka Radhi. Nisamehe!

mwanakaya

Member
Joined
Mar 17, 2012
Posts
56
Reaction score
183
Wakati anaanza kufundisha Timu ya Barcelona kutoka kwa mtangulizi wake Frank Rijkaard mwaka 2008, wengi nikiwemo mimi hawakuamini kama Josep Pep Guardiola anaweza kufanya makubwa hasa kutokana mafanikio na aliyokuwa ameyapata mtangulizi wake pamoja na umri wake mdogo wa miaka 37. Pep alichukua timu akiwa hana uzoefu mkubwa akitokea kufundisha Barcelona B.

Baada ya muda mfupi Pep alitengeneza Falsafa yake ya pasi fupi fupi maarufu kama Tiktak kupitia wa vijana aliotoka nao La Masia Iniesta, Xavi na Messi. Pamoja na mafanikio hayo wengi tuliendelea kutoa sababu mbalimbali za kumkosoa ikiwemo kubebwa na ubora wa wachezaji, urahisi wa ligi n.k.

Pep aliendelea kuridhihirisha ubora wake kwa kuendelea kuwanyanyasa washindani wao Real Madrid anavyotaka kila walipokutana. Lakini zaidi alifanya jambo geni zaidi baada ya kuinyanyasa vibaya timu ya Sir Alex Ferguson kocha mwenye mbinu kali na mkongwe kwenye fainali za UEFA mwaka 2009 na 2011.

Baada ya kuchukua kila taji Hispania alienda Ujerumani ambako alifanikiwa kutawala ligi ya Ujerumani japo hakuweza kuchukua kombe la Ulaya. Wapinzani wake waliendelea kumbeza kwamba Bundesliga ni ligi ya timu moja kwa hiyo hana jipya.

Sasa ni msimu wa tatu Pep yuko kwenye ligi inayofuatiliwa zaidi ya Nchini England. Hapa sasa ndiko utetezi wa wengi nikiwemo mimi unapofika mwisho. Ndani ya muda mfupi Pep ameweza kufanya kila analotaka kwenye ligi hiyo. Amebadili aina ya mchezo wa Man City na kuwa mpira wa pasi nyingi za kuvutia.

Kwa sasa nadiriki kusema Pep ni kocha bora zaidi wa kizazi cha sasa ndani ya miaka 10 baada ya kizazi cha Ferguson, Capello, Ancheloti kuondoka.

Naomba radhi Pep kwa kejeli juu yako. Nisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jurden klopp kiboko yake..ila ni kocho bora duniani kwa sasa hilo halina ubishi..sio mhuni yule aliyepale Old Traford kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
kiboko yake kivipi? Rekodi zitakumbukwa kwa mataji waliyoshinda kama klopp lengolake ni kumfunga tu ila sio kuchukua vikombe basi akiondoka tu liver na rekodi yake imesahauliwa.
 
Gardiola akikutana na klop,,, mwendo unachange
IMG-20180405-WA0007.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati anaanza kufundisha Timu ya Barcelona kutoka kwa mtangulizi wake Frank Rijkaard mwaka 2008, wengi nikiwemo mimi hawakuamini kama Josep Pep Guardiola anaweza kufanya makubwa hasa kutokana mafanikio na aliyokuwa ameyapata mtangulizi wake pamoja na umri wake mdogo wa miaka 37. Pep alichukua timu akiwa hana uzoefu mkubwa akitokea kufundisha Barcelona B.

Baada ya muda mfupi Pep alitengeneza Falsafa yake ya pasi fupi fupi maarufu kama Tiktak kupitia wa vijana aliotoka nao La Masia Iniesta, Xavi na Messi. Pamoja na mafanikio hayo wengi tuliendelea kutoa sababu mbalimbali za kumkosoa ikiwemo kubebwa na ubora wa wachezaji, urahisi wa ligi n.k.

Pep aliendelea kuridhihirisha ubora wake kwa kuendelea kuwanyanyasa washindani wao Real Madrid anavyotaka kila walipokutana. Lakini zaidi alifanya jambo geni zaidi baada ya kuinyanyasa vibaya timu ya Sir Alex Ferguson kocha mwenye mbinu kali na mkongwe kwenye fainali za UEFA mwaka 2009 na 2011.

Baada ya kuchukua kila taji Hispania alienda Ujerumani ambako alifanikiwa kutawala ligi ya Ujerumani japo hakuweza kuchukua kombe la Ulaya. Wapinzani wake waliendelea kumbeza kwamba Bundesliga ni ligi ya timu moja kwa hiyo hana jipya.

Sasa ni msimu wa tatu Pep yuko kwenye ligi inayofuatiliwa zaidi ya Nchini England. Hapa sasa ndiko utetezi wa wengi nikiwemo mimi unapofika mwisho. Ndani ya muda mfupi Pep ameweza kufanya kila analotaka kwenye ligi hiyo. Amebadili aina ya mchezo wa Man City na kuwa mpira wa pasi nyingi za kuvutia.

Kwa sasa nadiriki kusema Pep ni kocha bora zaidi wa kizazi cha sasa ndani ya miaka 10 baada ya kizazi cha Ferguson, Capello, Ancheloti kuondoka.

Naomba radhi Pep kwa kejeli juu yako. Nisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama yeye fundi akafundishe WH tuone.
 
Huenda kweli ni kocha bora ila pesa nayo inasaidia! Siku nikimuona yupo Levante afu akachukua ubingwa nitamsifu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Pesa inasaidia hilo halina ubishi lakini pia Pep anajua namna ya kutumia hizo pesa kwa kununua wachezaji sahihi. Pep amewafanya wachezaji waliokuwa wanaonekana wa kawaida akina Sterling, Sane, KDB, n.k kuwa hatari zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pep anakwambia alienda kuisoma invincible ya arsene wenger ya 2004 ,akachukua zile mbinu ,akachanganya na mpira wa Johan cryuf ,Akapata hii tik tak unayoiona Leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hamna kitu mule..angeeda man u..akakimbilia kwa wenye hela zao..misimu mitatu kishatumi £600m
 
Back
Top Bottom