PostGE2025 Peramiho: Mtoto wa Jenista atemwa, CCM yamteua DC Komba kugombea

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan imemteua Mkuu wa Wilaya (DC) wa Kalambo, Dkt. Lazaro Komba kuwa mgombea ubunge wa Peramiho, Mkoa wa Ruvuma.
618666839_1306297454857783_342177531591008073_n.jpg

Uteuzi huo umefanyika Jumapili, Januari 25, 2026 katika kikao kilichofanyika visiwani Zanzibar.

Uchaguzi mdogo wa ubunge wa Peramiho utafanyika Alhamisi ya Februari 26, 2026 ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Jenista Mhagama ambaye alifariki dunia Desemba 11,2025, katika Hospitali ya Benjamin Mkaра kwa ugonjwa wa moyo.

Katika kura za maoni ndani ya CCM zilizofanyika Januari 22, 2025, Dkt. Komba alishika nafasi ya tano kati ya watia nia 27 kwa kupata kura 213 kati ya 9,167 zilizopigwa huku Victor Mhagama, mtoto wa Jenista akiongoza kwa kupata kura 3,040.

Wengine na kura zao kwenye mabano ni Getrude Haule (2,913), Dkt. Joseph Mhagama (943), Frank Matola (215), Dkt. Lazaro Kiomba (213), Dkt. Damas Mapunda (200) na Isabellah Mwampamba (131).

Soma Pia: Mtoto wa Jenista Mhagama ajitosa kumrithi mama yake jimbo la Peramiho

Wengine ni Joseph Masikitiko (126), Erasmo Mwingira (124), Allen Mhagama (114), Schoral Ngonyani (84), Lazaro Ndenji(68), Davis Ngonyani(62), Thea Ntara (57), Emil Ngaponda (51), Serafina Mkuwa (48), Clemence Mwinuka (35), Emelian Mbawala (24), Benjamin Kamtawa (23), Prosper Luambano (22), Dominic Mahundi(19), Fredrick Millinga (17), Sixmund Rungu (9), Rose Shawa (7), Rosemary Ngonyani(6), Enoc Moyo (6).

Chanzo: Mwananchi Digital
 
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan imemteua Mkuu wa Wilaya (DC) wa Kalambo, Dkt. Lazaro Komba kuwa mgombea ubunge wa Peramiho, Mkoa wa Ruvuma.
Uteuzi huo umefanyika leo Jumapili, Januari 25, 2026 katika kikao kilichofanyika visiwani Zanzibar.

Uchaguzi mdogo wa ubunge wa Peramiho utafanyika Alhamisi ya Februari 26, 2026 ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Jenista Mhagama ambaye alifariki dunia Desemba 11,2025, katika Hospitali ya Benjamin Mkaра kwa ugonjwa wa moyo.

Katika kura za maoni ndani ya CCM zilizofanyika Januari 22, 2025, Dk Komba alishika nafasi ya tano kati ya watia nia 27 kwa kupata kura 213 kati ya 9,167 zilizopigwa huku Victor Mhagama, mtoto wa Jenista akiongoza kwa kupata kura 3,040.

Wengine na kura zao kwenye mabano ni Getrude Haule (2,913), Dk Joseph Mhagama (943), Frank Matola (215), Dk Lazaro Kiomba (213), Dk Damas Mapunda (200) na Isabellah Mwampamba (131).

Soma Pia: Mtoto wa Jenista Mhagama ajitosa kumrithi mama yake jimbo la Peramiho

Wengine ni Joseph Masikitiko (126), Erasmo Mwingira (124), Allen Mhagama (114), Schoral Ngonyani (84), Lazaro Ndenji(68), Davis Ngonyani(62), Thea Ntara (57), Emil Ngaponda (51), Serafina Mkuwa (48), Clemence Mwinuka (35), Emelian Mbawala (24), Benjamin Kamtawa (23), Prosper Luambano (22), Dominic Mahundi(19), Fredrick Millinga (17), Sixmund Rungu (9), Rose Shawa (7), Rosemary Ngonyani(6), Enoc Moyo (6).

Chanzo: Mwananchi Digita
Hivi kura za maoni za CCM zina tija gani? Inaonekana mazafakas wa Kamati Kuu pekee yao wanatosha—wanajua nani hasa ndio chaguo la wananchi.
 
Sa itakuaje na mafao ya mama kamalizia kwenye kampeni 😂
Ndiyo hapo sasa. CCM ni wahuni sana. Hiki kikundi ni hatari kuliko watu wanavyofikiri.

Wamemuingiza chaka, "tumia tu pesa ya mama, ndani ya miezi 6 itarudi yote". Mtu kaenda kupukutisha akiba yote.

Ila watamkumbuka, si muda mrefu utasikia ni DC mahali fulani.
 
Katika kura za maoni ndani ya CCM zilizofanyika Januari 22, 2025, Dk Komba alishika nafasi ya tano kati ya watia nia 27 kwa kupata kura 213 kati ya 9,167 zilizopigwa huku Victor Mhagama, mtoto wa Jenista akiongoza kwa kupata kura 3,040.
Hizo kura za maoni jimboni hazina maana tena kwa wenye chama chao.
 
Ndiyo hapo sasa. CCM ni wahuni sana. Hiki kikundi ni hatari kuliko watu wanavyofikiri.

Wamemuingiza chaka, "tumia tu pesa ya mama, ndani ya miezi 6 itarudi yote". Mtu kaenda kupukutisha akiba yote.

Ila watamkumbuka, si muda mrefu utasikia ni DC mahali fulani.
Yaani huyu hata akijakaza mbel za watu alifika chumbani lazima analia 😂😂😂 kakosa mama na pesa katapeliwa
 
Back
Top Bottom