Pesa bhana, kama Mwanamke Mzuri vile (Pisi Kali) usipompa attention anakukimbia

Pesa bhana, kama Mwanamke Mzuri vile (Pisi Kali) usipompa attention anakukimbia

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
767
Reaction score
1,657
Kwanza kabisa napenda kuwasalimu Jf family. Ni tumaini langu u buheri wa afya. Kama sivyo nakuombea upate afya njema ili uendelee na kazi zako zakusaka noti.

Leo nataka nikuonyeshe jambo kuhusu pesa na pengine itakusaidia kubadili fikra zako vile unavyoiwazia pesa.

Kwa wanaosoma nyuzi nazoandika hapa JF wanafahamu nimekuwa naweka msisitizo sana kwamba pesa inafuata Value. Kwamba ukiwa unatoa value zaidi katika kazi zako kupitia ujuzi ulio nao basi pesa lazima itakuwa upande wako.

Sasa leo nataka nilizungumzie hili kwa namna nyingine nikiwa na tumaini watu wengi zaidi wataelewa na hivyo kutumia ufahamu huu mpya kuanza Kutengeneza pesa.

Kabla sijaanza kukuonyesha kwa namna gani pesa ni kama mwanamke mzuri aliyepo hapo mtaani kwako, nataka kwanza niseme wazi pesa ni rahisi sana kuzipata kama utaelewa mambo nayoenda kukuonyesha katika uzi huu.

Are you ready?

Ok tuanze...

1 • Ukitaka kumpata mwanamke mzuri inabidi uweke ego pembeni. Inabidi umfuate umwambie ya moyoni. Sawa sawa kabisa na pesa inavyopatikana.

Wakuu tuseme wazi hapa, mbinu ipi ni bora kumpata mwanamke mzuri? Kukaa kimya na kujifanya humtaki au kumuweka wazi vile unavyompenda na kuonyesha kwa vitendo unamjali?

Kwangu mimi njia sahihi ni hiyo ya pili. Na hiyo ni sawa sawa na kupata pesa.

Unajua usipokuwa tayari kuifuata pesa ilipo na kweli kutia bidii ili uipate basi mtu wangu wewe utakuwa poor maisha yako yote. Lazima ufahamu my brother michongo ya pesa inatengenezwa, haijileti yenyewe.

Kuna baadhi ya watu ni zumbukuku kweli kweli.

Wao siku zote wanawazia kupata pesa lakini hakuna chochote wanachofanya kuzipata pesa wanazohitaji.

Ni kama vile wanadhani siku moja wataamka asubuhi pesa zitakuwa zimejaa chumbani mwao. Hii ni sawa kabisa unamtaka mdada mzuri, humwambii kitu unabaki kujidanganya atakupenda mwenyewe kwahiyo atakuja hapo ghetto kwako. Stupid.

Mwanamke mzuri anahitaji kumpigia hesabu kali ili umuweke kwenye himaya yako. Inabidi uhangaike, umpatie attention, ukifanya hivyo utashangaa anabaki kwako all day everyday.

Pesa na yenyewe hivyo hivyo. Inabidi uweke mipango vile utakavyoipata. Inabidi uipatie attention ya kutosha. Tena si siku moja wala mwezi mmoja au mwaka mmoja. Ni siku zote. Ukionyesha haupo interested na yenyewe wala haijali unashangaa michongo inakauka.

Hapo vipi? Unakubaliana na mimi?

Tuendelee...

2 • Ukimtaka mwanamke mzuri, inabidi umpatie zawadi au pesa hapa mwanzo ili ukamate attention yake. Sawa kabisa na kupata pesa. Inabidi uanze na kutumia muda wako au pesa hapa mwanzo kufanya investment kwaajili ya faida ya baadaye.

Wakuu, sasa hivi kupata pisi kali inabidi utumie resource hapa mwanzo. Au nadanganya?

Kwamba unatumia pesa + vizawadi kumvuta kwako na mwisho ananasa.

Tofauti na mbinu hii inakuwa ni kazi ya kichaa. Utabaki kuwaita wanawake wazuri mashemeji tu.

Hiyo ni sawa kabisa na kupata pesa.

Hapa mwanzo inabidi ukubali kufanya aina fulani ya investment ambayo itakuchomoa pesa mfukoni lakini ukiwa unafahamu baada ya muda pesa yako itarudi.

Sasa kuna watu wao wanataka pesa lakini kamwe hayupo tayari kutumia hata kumi kufanya investment. Hatumii hata kumi kujifunza skills mpya zitakazomwezesha Kutengeneza pesa zaidi baadaye. Kama wewe upo kwenye group hili utashangaa mvi zinakuja hujafanya lolote.

3 • Ukitaka kumiliki pisi kali inabidi ujiandae kwa changamtoto zaidi.

Wakuu, wanawake wazuri wanachangamoto sana. Hiyo ni sawa na kuwa na pesa nyingi kwasababu changamoto au niseme responsibilities zakuhakikisha kila siku pesa au miradi inaenda vizuri ni kubwa kuliko unavyodhani.

Unajua ukiwa na pisi kali inamaana upo kwenye mapambano na manyang’au wengine wanaotamani na wao waonje kidogo asali. Sasa hii hali ikizidi ni shida. Pisi yako ikitoka na marafiki zake unapata wasiwasi je atakuwa salama kweli huko anapoenda?

Sawa sawa na kuwa na pesa nyingi. Lazima utakuwa na mawazo si tu jinsi utakavyozidi kuziongeza lakini pia jinsi utakavyolinda Business au michongo yako. Kwasababu kwa vyovyote vile lazima kutakuwa na washindani wako wanaotamani wachukue nafasi yako. Sasa ukizubaa tu, unajikuta umepoteza.

Binafsi nimeshakuwa na pisi kali mara kadhaa. Tena pisi kazi na level za kitaifa na kimataifa.

Nilichojifunza wengi wao wanasumbuliwa na wanaume wengi kwahiyo ukizubaa tu au kutompatia attention basi muda si muda utashangaa ameshakukimbia.

4 • Mwanamke mzuri atazidi kuwa mzuri ukimjali na kumuhudumia zaidi. Sawa sawa na pesa zitazidi kuongezeka iwapo tu utatia bidii na kujali mishe zako zinazokupatia pesa.

Kuna baadhi ya wanaume wakishampata mwanamke mzuri wanadhani hiyo pekee inatosha kwahiyo hawatii tena bidii kuwahudumia ili wanawake zao wazidi kupendeza. Wanasahau sababu ya kwanza iliyowavuta kwa hawa wanawake ni uzuri walionao. Na kama unavyofahamu ukiona kitu kizuri fahamu kuna gharama kubwa kukitunza kibaki katika ubora wake.

Sasa wanaume hawa wanajisahau na kwasababu pisi kali zinafahamu uzuri wao ni moja ya investiment yao basi taratibu na yeye ataanza kuwa interested na wanaume wengine waliotayari kuprovide ili amentain uzuri wake.

Pesa nayo ni ipo hivyo. Kama ulifanikiwa labda kuanzisha business na gafla ukaacha kutoa huduma nzuri kwa wateja basi utaona pesa nazo zinaondoka kwasababu wateja hawaoni ukiwajali watasema kwanini wabaki kwako wakati kuna sehemu nyingine wanapohudumiwa vizuri? Kufahamu hili ni simple sana lakini watu wengi wanashindwa, hatahivyo.

Kwakumalizia niseme tu inanishangaza watu wengi wanambinu zakumiliki pisi kali lakini wanashindwa kutumia mbinu na ujasiri huu kuuhamishia kwenye entrepreneurship na kutengeneza pesa. Kwasababu kama nilivyoonyesha kwenye hizi point 4 kuna uhusiano kati ya pesa na mwanamke mzuri. Sasa kama unambinu zakuwapata wanawake wazuri unashindwaje kupata pesa? Seriously inabidi unitafute.

Ok ngoja niishie hapa.

Cheers 🥂
 
Uko vizuri sanaa...

Mimi ni mfanyakazi mwenye ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa.

Mapambano yangu yanasonga, naamini ipo siku nitaacha hii Kazi na kujikita total kwenye biashara hiii.

Nashukuru Mungu, biashara inasonga na ajira inasonga ila ipo siku nitaacha kazii na kuwa "full time enterprenuer"

Let's Save then INVEST.

Asante kwa SoMo zuri.

#YNWA
 
Back
Top Bottom