Tulibumi Kasebele
New Member
- Sep 14, 2022
- 1
- 1
PESA INAYOTAFUTWA KWA JASHO NA WAZAZI INAVYOGEUKA KILIO
Imeandaliwa na Tulibumi Richard Kasebele
”Sitaki wanangu wateseke kama mimi nilivyoteseka” ni kawaida wazazi kusema maneno haya kama hamasa kwao kufanya kazi jambo ambalo ni la msingi katika maisha, Pongezi nyingi ziwafikie wazazi wanaofanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuwapatia watoto wao mahitaji , Mathalani kuamka mapema na kuwahi kazini, Kushinda muda mrefu kazini na kuchelewa kurudi ama kurudi usiku kabisa.
Pamoja na juhudi zote zinazofanywa na wazazi Je umewahi kujiuliza ni kwanini idadi ya watoto wanaonyanyaswa kingono yaani kubakwa na kulawitiwa inaongezeka siku hadi siku? Je ni kwanini idadi ya watoto wanaojihusisha na madawa ya kulevya inaongezeka siku hadi siku? Je ni kwanini idadi ya watoto wanao uliwa inaongezeka siku kwa siku? Je ni kwanini mimba za utotoni na biashara ya ngono kwa watoto inaongezeka siku hadi siku? Je ni kwaninini idadi ya watoto wanaokataa au kuacha shule inaongezeka siku baada siku? Je ni kwanini idadi ya watoto wanaohusika na wizi pamoja uporaji inaongezeka siku hadi siku? Ukweli ni kwamba watoto wamekosa malezi thabiti na ulinzi kutoka kwa wazazi. Je unapokua kazini huwa unatumia hata dakika tano walau kufikiri kwamba katika muda huu je? Mwanangu atakua wapi na akina nani? Atakua akifanya nini? Je huwa unatumia walau dakika tano kupiga simu nyumbani ujue wanao wanaendeleaje?, wameshindaje? Wamekula nini?
Katika muktadha huu je pesa inayotafutwa kwa jasho inafanikisha lile kusudio la wazazi kwa watoto wao ama inageuka kilio? Ni kweli pesa utaipata lakini je ataitumia nani kama mwanao atauliwa kwa vitendo vya kiunyanyasaji? Je utamlipia nani ada kama mwanao atakua mtumiaji wa madawa ya kulevya? Au shoga na kukataa shule? Kwa mujibu wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu kuanzia mwezi wa kwanza hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka 2021 watoto 11499 walifanyiwa matendo ya kikatili na jambo la kusikitisha zaidi watu wanohusika sana katika matendo haya ya kikatili ni watu wa karibu mfano binamu zao, baba zao wadogo, baba wa kambo, mama wa kambo, wafanyakazi wa ndani na ndugu wengine wa karibu. Jambo la kuogopesha zaidi ukatili huu unafanyika sana majumbani na mashuleni, Zile sehemu ambazo wazazi wanafikili ni sehemu salama ndio zimekuwa sehemu hatarishi sana kwa watoto wetu.
Kutokana na kuongezeka kwa matendo ya kiunyanyasaji kwa watoto Wazazi wanashauriwa kujenga upendo wa hali ya juu kwa watoto wao, Mzazi jenga ukaribu na urafiki kwa watoto wako imba nao , cheza nao, wapeleke sehemu mbali mbali kulingana na uwezo wako , wanunulie zawadi hata pipi (watoto wanaridhika haraka sana na wanachohitaji sana ni muda wako kuliko vitu unavyowapatia. )Hii itawasaidia wao kuwa karibu na wewe aghalabu itawafanya wawe wazi kwako na kukueleza changamoto yeyote ile wanayoipata. Pia mzazi tumia muda huo kuwadadisi kwa ujanja wa hali ya juu kujua kama kuna changamoto wanazokumbana nazo kama vile kufanyiwa vitendo vya kikatili (Angalizo wakati ukifanya udadisi watoto wasijue kama unawadadisi) kwani hii hupelekea watoto kua waoga na kuacha kukupatia taarifa unazozihitaji.
Wazazi wanashauriwa kuwajibika kwa hali na mali kuhakikisha wanatoa malezi na usalama kwa watoto wao,Jua wanao wanacheza na nani na wanacheza michezo ipi, wanashinda na nani, wanaangalia nini kwenye runinga?, wameshindaje?, wamekula nini? Uliza siku yao kwa ujumla imeendaje. Jambo la malezi na usalama kwa watoto wako lichukulie kama la “abiria chunga mzigo wako katika chombo cha usafili wa uma” kwani usipompa mwanao malezi na usalama ni vigumu kwa mtu mwingine kufanya kwa niaba yako hivyo hata kama una mfanyakazi wa ndani kumbuka hao sio watoto wake na wahenga walisema “uchungu wa mwana aujuaye mzazi wake” pata walau muda wa kuwaogesha ujue kama kuna mabadiliko yoyote katika miili yao.
Ewe mzazi mjengee mwanao ujasiri kwamba hakuna mtu yeyote yule anaeweza kumfanyia kitu kibaya kama vile kumpiga,kumuumiza kumuua nakadhalika kwa kosa la kumwambia mzazi wake ukatili aliofanyiwa mjengee Imani kwamba wewe upo kwa ajili ya kumlinda na kitu chochote kile kibaya na watu wabaya muhakikishie kwamba upo kuhakikisha kwamba hakuna kitu wala mtu atakae mdhulu
Wazazi wanashauriwa kuweka mipaka ya wapi watoto wao washinde, aina ya marafiki zao, kwani baadhi ya watoto wanajihusisha na tabia mbaya kama vile kuangalia picha za ngono, matumizi ya madawa ya kulevya hivyo ukishajua kundi la mwanao sio zuri fanya lolote uwezalo kumtenganisha mwanao na kundi hilo ovu kabla mwanao hajaharibikiwa kwani “usipoziba ufa utajenga ukuta”.Ni vizuri pia kuhakikisha usalama wa malazi ya watoto usiruhusu wanao kulala na wageni au wafanyakazi. Kwani wengi kwa kufanya hivyo wameambulia kilio baada ya watoto wao kunyanyaswa kingono na watu waliowaruhusu walale nao
Wazazi tunashauriwa kuwa makini na mtu, ndugu au mgeni ambaye mtoto anaonesha kumuogopa na kuwa na wasiwasi anapokua karibu nae jambo hili usilichukulie kawaida mara zote mtoto akiwa karibu na mtu anaemnyanyasa hukosa ujasiri, huogopa na kukaa katika hali ya wasiwasi sana. Pia mzazi unatakiwa kuwa makini na mtu anaempa zawadi mwanao mara kwa mara,fanya udadisi kila zawadi unayoikuta kwa mwanao au kama akikupa taarifa ya kupewa zawadi kwani baadhi ya zawadi zinatumika mithili ya mchele unaorushwa kwa lengo la kumkamata kuku mkanye mwanao asipokee zawadi hovyohovyo
Wazazi tunashauriwa kutowaruhusu wafanyakazi wa ndani kuwaadhibu watoto kwani baadhi yao hutumia mwanya huo kuwanyamazisha pale wanapowafanyia vitendo vya kiukatili kama mwanao amefanya kosa mzazi uletewe taarifa Punde upokeapo taarifa fanya uchunguzi kwanza na kupata ukweli kwani baadhi ya mashitaka huwasi ya kweli bali hutumika kama fimbo ya kuwanyamazisha watoto ili waendelee kunyanyasika
Wazazi wanashauriwa kuweka mazingira ya nyumbani vizuri ili yaweze kuwavutia watoto wapende kucheza maeneo ya nyumbani na itawasaidia kucheza na marafiki zao mazingira ya nyumbani hivyo kurahisisha swala zima la usalawa wao ,kwani “Fimbo ya mbali haiuwi nyoka”, lakini Kama kipato kinakuruhusu funga kamera nyumbani kwa ajili ya ulinzi huku ukifanya uchunguzi wa mara kwa mara mfano wahi kurudi nyumbani kabla ya muda uliozoeleka au jifanye haupo kumbe upo ndani ili tu ujue ni kitu gani hufanyika kwa watoto wako pale unapo kuwa haupo nyumbani.
Izingatiwe kwamba wazazi wanapokua wanatafuta pesa wahakikishe wanawapatia watoto malezi bora na usalama ili pesa wanazozitafuta zisije zikageuka kilio,kabla hujasema namuachia Mungu awalinde wanangu hakikisha umefanya jitihada zako zote kuwapatia malezi na usalama kisha yanayosalia Muachie Mungu

Attachments
Upvote
1