Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Juma Mgunda ana msemo wake mzuri sana. Anakuambia 'Ball itembee'.
Na ukichunguza ni kweli bana, ball ama mpira, muda wote huwa unatembea.
Vivo hivyo, pesa kama ball tu, huwa ina kawaida ya kutembea. Ukiwa na pesa mfukoni lazima kutatokea sababu ya kuitumia hiyo pesa kwa sababu pesa siku zote ipo kwenye mzunguko.
Pesa sio kama leso eti utaiweka mfukoni mda wote bila kuigusa. Ndo mana unaona kuna thread nyingi hapa Jamii Forum wadau wanalalamika kwamba wamekula mshahara ndani ya siku moja.. Hii ni kwa sababu pesa ipo kwenye mzunguko.. Ukishaipata lazima zitapatikana sababu kede kede za kuitumia.
Wajuzi wa haya masuala wanakuambia ukitaka kuona thamani ya pesa inayokuja kwenye njia yako i.e. mshahara au pesa za madili... Usikae sana na mpira kama Sakho, yaani ukiupata tu mpira mpe chama haraka ili ampe phiri ili goli lipatikane...
Yaani unatakiwa uogope kukaa na pesa cash kuliko kufumaniwa na mke wa mtu.. Unasubiria ka milino ka mshahara.. kakiingia tu.. mda huo huo itume kama laki tano ukashika kiwanja kwa wazee wa viwanja, au kwa wazee wa financial markets itupie kwenye hisa au bond haraka sana..
Ni hayo tu nimewiwa kuwaeleza wakati wengi wetu tukikaribia pay days...
Ball itembeee.... Mgunda Fundi sana