Pesa ni Mfalme wa watu wote

Pesa ni Mfalme wa watu wote

Pro Biznesi

Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
9
Reaction score
10
Najua mada hii inaweza kuwa nyeti kwa baadhi ya watu, hivyo basi samahani sana kwa mtu atakayekereka. Katika vitu vinavyojulikana sana duniani, Pesa inashika nafasi ya kwanza, sababu hadi watoto wa chekechea wanajua umuhimu na matumizi ya pesa kuridhisha hamu zao kununua vitu vya kumung'unya na kutafuna.
Nikisema kuwa Pesa ni mfalme, najumlisha sehemu hizi tatu:

1: Maisha ya kila siku, ambayo kama huna pesa yatakuweka katika nafasi ya mwisho ya watu wenye thamani duniani. Unaweza hata wewe mwenyewe ukajiona huna thamani kabisa kama huna pesa mfukoni. Kila kitu tunachotumia kinagharimu pesa, maji, chakula, nguo na hata hewa ya kupumulia ina gharama nyingi ukiwa ICU. Pole kama hali ya maisha yako ni ngumu ila usichoke, endelea kupambana tu.

2: Mahusiano ya watu. Sijui kama watu unaojuana nao wanaleta faida ghani kwenye maisha yako, ila ukweli ni kwamba hata kuwasiliana na marafiki na ndugu uwapendao kuna gharama nyingi sana, na ukitaka kuwenda kuwatemembelea, siyo vizuri kwenda ukiwa mikono mitupu. Pesa inaweza kufanya ufurahie mahusiano yako na watu wengine lakini uhaba wake unaweza ukafanya hata simu za watu usipokee kabisa.

3: Mashindano na Vita. Upo msemo kwenye biblia kuhusu kupiga mahesabu kabla hujaamua kushindana na mtu aliyekuzidi uwezo vitani. Ukienda mahakamani na mfuko wako umetoboka itakuwa ni vigumu kupata hata wakili msamaria mwema akusaidie kesi yako, na mafanikio ya wetu wengi ni kama vile upo uwanja wa vita kupambana na vikwazo vingi ili uweze kupata vinono vya dunia hii. Hakikiksha unazo pesa za kutosha kama unalenga kufanikiwa katika makubwa vinginevyo anza kidogo kidogo tu. Wanasema, "mdogo mdogo ndiyo mwendo". Labda ni kweli ila kama huna pesa, mwendo wako unaweza ukawa mfupi sana na kukata tamaa.

Changia fikra zako. Je, unadhani inatawala maisha ya watu wengi? Vipi maisha yako, pesa ina nguvu gani kwenye maisha yako?
 

Attachments

  • money-ge6881aa2f_1280.jpg
    money-ge6881aa2f_1280.jpg
    190.1 KB · Views: 13
Pesa na matatizo
Matatizo na pesa

Pesa inakanuni zake

Pata pesa upate mapenzi au pata mapenzi upate pesa

Mapenzi bila pesa ni sawa na wazo la biashara bila mtaji

Unahitaji pesa kuliko pesa inavyokuhitaji
Pesa sabuni ya roho,
Pesa inaongea pesa inaapa,
 
Back
Top Bottom