Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi
Haya ninayoyasema wengi mtayaona kama utani, ila ni kweli yametokea!.
Kiukweli kabisa, Pesa ni Shetani!. Watu Utu Umewatoka Kabisa Umebakia Unyama!. Kutokana na Kupigika Uchumi wa Magufuli, Pesa Imekuwa Ngumu Sana Kiasi Kwamba, Baada ya Rais Magufuli Kutoa Milioni 1.5 kwa kila aliyefariki, Kuna Watu Wametamani Ndugu Zao Ambao Hawana Faida, Bora Wangekufa tuu Maji Ukerewe, Kwenye Ajali ya Kivuko ili Familia Angalau Zipate Hiyo Milioni 1.5 ya Ubani wa Rais Magufuli kwa kila aliyekufa, kwa hoja kuwa baadhi ya ndugu zao ni hasara tupu, hata kama wangeishi maisha yao yote, wasingeweza hata kuleta 100,000 nyumbani, hivyo kama mtu kafa familia inapata million 1.5, then afadhali hata wangekufa!.
Mimi nimemsikia kwa masikio yangu mwenyewe, mama mmoja, akisema, kwa jinsi mume wake alivyo mlevi wa gongo, anahangaika na vimala.. mbwa kwenye bar za mataputapu, hana kazi yoyote ya maana zaidi kusubiri vibarua vya kubeba zege, hawezi hata kununua sare ya mtoto anayesoma St. Kayumba, huyo mama akasema anatamani mumewe angekuwepo kwenye hicho kivuko, hiyo miloni 1.5 ingebadili maisha yao!.
Hivi kweli huu umasikini wa kipato ni kweli umetufikisha hapa sisi Watanzania, hadi kukosa utu hivi, kuthamini pesa kuliko uhai!. Kuthamini kitu kuliko utu?. Hivi kweli Watanzania tumefikia stage ya unyama wa kiasi hiki mtu kutamani binadamu afe ili upate pesa?!.
Ningeweza hadi kulitaja jina la huyu mwanamke, ila sio busara kuusema kila ukweli unaousikia, ukweli mwingine is best if kept silent.