Pesa X: Kampuni ya ukopeshaji mitandaoni inayolimbikizia watu madeni ya kubumba

Pesa X: Kampuni ya ukopeshaji mitandaoni inayolimbikizia watu madeni ya kubumba

Pesa x wamekuwa wanabambikia watu madeni hovyo hovyo huku wakitishia kuwatangaza waliotishiwa mitandaoni waziri wa fedha aziangalie hizi kampuni ni sumu kwenye uchumi wa nchi
Dawa ya deni ni kulipa! Kila siku mnaambiwa muwe mnasoma masharti na vigezo ya hayo makampuni….! Hao wamesajiliwa ! Kwa hiyo kama unaona wanakunyonya usikope wewe kopa bank
 
Hawa wanakosha 10,000 wanakudai 20,000 ndani ya siku 6 , mi nashangaa BOT wako wapi ??
Kwani ni usishangae hao ambao Bado wanakopa huko?

Ila kwa ufupi, kama hujali kutukanwa nao, unaweza usilipe, na hawawezi kwenda popote. Hawako kisheria Wala kikanuni. Wacha wakutukane mwisho watachoka tu. Kama huna impact kwenye jamii usiogope.
 
Usilipe mkuu hawana cha kukufanya, me nafanya kazi kwenye kampuni yao inaitwa Singularity ni ya wachina tupo hapa Makumbusho, hizo meseji za vitisho tunazituma sisi wafanyakazi ili kuwatisha tu na kutetea kibarua chetu ila hawawezi kukufanya chochote usipolipa.
 
Dawa ya deni ni kulipa! Kila siku mnaambiwa muwe mnasoma masharti na vigezo ya hayo makampuni….! Hao wamesajiliwa ! Kwa hiyo kama unaona wanakunyonya usikope wewe kopa bank

Upo sahihi, lakini BOT inayo mamlaka ya kusimamia na kuweka viwango vye unafuu kwa mkopaji
 
Back
Top Bottom