A: Ni kweli mikopo halali na inayozingatia sheria na utu ni mzuri tu na inawatoa watu. Mikopo hii ni kama huu, kwamba, Mimi
The Palm Beach namkopesha ndugu
Muhsin Snr TSh. 100 imtatulie shida au afanye mtaji wa biashara.
Kwa kuwa anakaa nayo kwa mwezi mzima (kwa mfano), basi nitkubaliana naye kuwa ukifika wakati wa kurejesha, anirudishie na faida ndogo (let say ya TSh. 20) kwa hiyo badala ya 100 basi alete 120.
Kwa scenario hiyo👆👆mkopo wa namna hiyo hauna ubaya wowote na kwa mkopo wa aina hii, basi kanuni ya "
dawa ya deni kulipa" ina apply.
B: Lakini kuibia watu kwa jina la "
mikopo" na kwa kuwa watu hawa wana shida au matatizo ukijua hawana cha kufanya hata wakiweka masharti na riba mbaya na kubwa namna gani, basi hiyo inakuwa SI HALALI NA HAIKUBALIKI.!!
Just think, hivi inawezekana vipi (kwa mfano) umpe mtu pesa TSh. 10,000 halafu ndani ya wiki moja akurudishie 20,000 kwa interest ya 100% na akishindwa kurejesha kwa wakati unaanza kumdhalilisha kwa kila namna ya madhalilisho? Ni haki kweli hata kama "
dawa ya deni ni kulipa?". Hii kwa mtazamo wowote ule, sio haki na mtazungushana sana na pengine kuumizana na mwisho pesa ipotee!!
Na mnaodai kuwa "
dawa ya deni ni kulipa" lakini mkumbuke kuwa deni la namna hii siyo deni tu bali ni "mkopo - deni"
Kwa hiyo hawa watu wawili wakishitakiana, mahakamani, kitachoangaliwa sio tu "
dawa ya deni ni kulipa" bali cha kwanza ni
terms & conditions za deni hilo.
Mlipeana mkopo wa kindugu/kirafiki? Mlikopeshana kibiashara? Kama ni mkopo biashara, masharti yake yana - comply na masharti au kanuni za mikopo kwa mujibu wa sheria kama zilivyowekwa na mamlaka zenye jukumu la kusimamia sekta ya fedha nchini?
C: Ndugu
Mbaga Jr yeye kawa harsh kidogo bila kufikiri kwa hekima na busara kabla ya kuandika. Anauliza, "
wakati mtu anakopa anakuwa amekatwa kichwa?".
Hopefully, jibu lake ni
NDIYO watu wanaoiendea mikopo hii for sure kabisa wengine huwa wanakuwa wamekatwa vichwa/shingo zao na shida za dunia hii. Ndio maana watu hujiingiza kwenye mambo haramu au njia zisizo salama kwao ili wapate fedha na kutatua changamoto zinazowakabili kwa wakati huo bila kujua kuwa wanatatua shida hiyo na kutengeneza nyingine tena!
Kama wewe ndugu
Mbaga Jr na wenzio mliong'ang'ana na kauli tu ya "
dawa ya deni ni kulipa" hamjawahi kujikuta mko kwenye engo mbaya na hatari ya uhitaji wa fedha na kuwa tayari kupewa pesa kwa sharti lolote na yeyote ili mradi tu utoke kwenye shida hiyo kwa wakati huo, basi mshukuru Mungu sana kwa sababu amekupa neema hiyo!
In case hamjui, muulizeni Rais Samia Suluhu Hassan na Ng'wigulu Nchemba (waziri wa fedha wa sasa) wawaambie imekuaje wamejiingiza kwenye mikopo ya ajabu ya kuiuza nchi kabisa. Wauza bandari zetu, mapori zaidi hekta milioni 9.9 za hifadhi ya misitu yetu, madini, gesi, uwanja wa KIA nk
ANYWAY. WALIOKOPA NA KUJIKUTA WAMEINGIA KWENYE SHIDA HII HATA KUTUKANWA NA KUDHALILISHWA NA WAKOPESHAJI HAWA WAFANYEJE?
Definitely, walichukua pesa ya watu. Kukaa na kitu au fedha ya mtu mengine bila ridhaa yake kuwa ameachia, sio sawa.
Na ili kuyamaliza wanapaswa kuwarudishia wenyewe kwa kufuata utaratibu na ushauri ufuayayo;
1. Wakae chini (mkopaji na mkopeshaji) wazungumze. Wewe uliyekopa mwambie aliyekukopesha kuwa, nilikuwa na shida. "
Kichwa changu kilikuwa kimekatwa na shida/changamoto yangu na sikuwa namna". Kwa kuwa nilikuwa so desperate na kiasi cha kutoona na kujali masharti yenu magumu na ya hovyo kiasi kwamba yanavunja sheria za mikopo ya fedha. Nakurudishia pesa yako halisi (principal amount) uliyonipa na kiasi hiki (unachomudu, kwa utaratibu na muda mtakaokukubaliana).
Kama mkopeshaji huyo akikataa kupokea pesa yake, mwambie, basi huna la kufanya zaidi. Akitaka, atafute mtu wa tatu (hasa mahakama) awasikilize na kuwaamua!!
2. Kuna watu wanashauri kuwa WALIOKOPA pesa hizi na sasa wamebananishwa kulipa hivyo hivyo kwa riba zilizokwisha jilimbikiza, eti wakatae tu kulipa. Kuna mwingine anasema na kushauri kuwa, watu wakope makampuni mengi au yote Ili watumie fedha hizo waanzishe biashara na kisha kwa sababu ya masharti yao mabaya hawa WAKOPESHAJI, wagome kuwalipa kwa sababu watakuwa hawana la kuwafanya.
Huu ni ushauri mbaya, hatari na mtu akiufuata, tendo hilo litamvuruga na kumuumiza maisha yake yote.
Mungu hakubaliani na hili hata kidogo. Hata hiyo biashara atakayoianzisha mtu wa namna hii haitafika popote maana ameianzisha kwa hila na kwa pesa za dhuluma.
Huwezi kufanya dhuluma kwa sababu wewe umedhulumiwa. Tunaambiwa
tuushinde ubaya kwa wema. Mtu hawezi kushinda ubaya kwa ubaya!
Kwa hiyo, ushauri wangu kwa hili, kila mtu anapokuwa kwenye changamoto au shida ya uhitaji wa fedha, basi hatua ya kwanza ni kujaribu kuwa mtulivu na mvumilivu ili kuiruhusu akili kuja na suluhu isiyozalisha shida nyingine.
Biblia mahali fulani inasema, "
kila jaribu (changamoto/shida inapomjia mtu, basi Mungu huandaa na mlango (njia sahihi na isiyo na maumivu) ya kutokea au kutatulia shida hiyo".
Ukihamaki ukiwa
so desperate pamoja na woga na hofu iliyoletwa na shida hiyo kiasi cha kukosa utulivu wa akili, basi tambua kabisa kuwa hutaweza kuuona mlango huo wa kukuokoa na shida yako ambao Mungu anakuwa alishakuandalia kitambo!
Na badala yake you will easily fall into devil's trap kwa kuuona mlango wa mauti wa shetani ambao naye huwa ameutegesha kwa ajili yako.
Upi? Ndio hii
mikopo ya kausha damu.
Na watu wasidanganyike hata kidogo, mikopo hiyo ni mpango mzima wa Ibilisi ili kuwaumiza na kuwaua watu.
Na wengi wamedhalilika na wengine kufa kwa presha za usumbufu na kudhalilishwa. Mungu Yehova hawezi kukausha damu watu wake. Mungu yeye anaponya na kuokoa!
3. MWISHO: Kwa utafiti tuliofanya.
Mosi ni kweli kabisa mikopo hii "kausha damu" ipo na inakiuka masharti na kanuni za ukopeshaji fedha.
Pili, watu wana shida kwelikweli na wakimpata mtu wa kutoa fedha za namna hii, huchukua bila kujali athari zake.
Lakini ni kweli pia kuwa wengi huchukua pesa hizi si kwa sababu wana shida maalumu sana inayohitaji kutatuliwa haraka. Bali wengi huchukua kwa ajili ya matumizi ya kawaida sana ikiwemo kumywea pombe, vocha za Simu nk.
Ushauri kwenye hilo👆👆:
Fikiria mara mbili kabla ya kuchukua fedha hizi. Tujifunze kuweka akiba kwa kidogo tunachopata katika shughuli zetu za kutuingizia kipato ili kitufae wakati wa shida.
Asanteni