Pesa ya Breki ndio sababu abiria kuuziwa chakula ghali sana njiani

Pesa ya Breki ndio sababu abiria kuuziwa chakula ghali sana njiani

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Wale wanao milki migahawa njiani huwalipa Madreva pesa ya Breki, maana yake Dereva akiingiza Basi pale hata nusu ya abilia wasipo kula yeye pesa yake iko pale pale na kumbuka kuna abiria wagumu ana shuka anaenda washroom akitoka hapo anarudi kwenye basi hanunui kitu na pia kuna abiria wana safari na vyakula vyao na pia wapo wao wananunua soda tu na biskuti.

Sasa inaonekana pesa ya Break inakatwa kwenye chakula ndio maana unaweza uziwa chai ya rangi sh 10000/ ukauziwa wali magaragwe sh 4000/ na wali nyama finyango 3 sh 7000/.

Ushauri ni kwamba LATRA walazimishe mabasi yakiingia stend kubwa yasimame pale nusu saa abiria wakale jirani na stendi hapo, make Dereva anacho fanya ni kuuza abiria kwa wenye migahawa na kuna competition kubwa sana.

Ushauri mwingine ni abiria wabebe Lunch Box zao, kwa chakula cha safarini haina haja kubebana na Wali, bali vyakula vikavu, kama nyama na pia mikate na matunda inatosha kabisa.

Kubeba chakula chako mwenyewe ni njia nzuri sana kwa sababu hasa ya quality, na hata hio migahawa pamoja na kuuza chakula ghari bado quality ni changamoto kubwa sana kwao.

Nakumbuka kuna wakati nilipanda basi kutokea Moshi kwenda Dar tumefika Korogwe abiria waligoma kushuka Liverpol pale enzi zile na Dereva saaa kwa kuwakomoa alipiga gia hadi Dar.
 
images (1).jpeg
 
Hiyo migahawa inayouza chakula bei kubwa...dawa yao ni ukisafiri beba chakula chako wabaki wanaambulia mia2 za kukojoa tu
 
Pale Mombo kuna hotel flan magari huwa yanaingia mkono wa kushoto kuelekea Korogwe. Huwa wanauza nyama zimeoza.
 
Bora mara 100 barabara ya Arusha to Dar vyakyla na hotel ni bora kuliko safari za Dar to Mbeya, Dodoma to Mwanza, Dodoma to Arusha na Arusha to mwanza.

Hotel za njia hizo ni mashaka matupu
 
Mimi wakina G wamesafiri nmepika viazi, ndizi nkanunua kuku weka kwenye kontena hamna kupoteza hela kizembe
Wakakaa na tablet zao kwenye gari safii hamna kelele
 
Bora mara 100 barabara ya Arusha to Dar vyakyla na hotel ni bora kuliko safari za Dar to Mbeya, Dodoma to Mwanza, Dodoma to Arusha na Arusha to mwanza.
Hotel za njia hizo ni mashaka matupu
Hotel za Dar - Mbeya ni uchafu.
 
Bora mara 100 barabara ya Arusha to Dar vyakyla na hotel ni bora kuliko safari za Dar to Mbeya, Dodoma to Mwanza, Dodoma to Arusha na Arusha to mwanza.
Hotel za njia hizo ni mashaka matupu
Arusha to Dar hakuna kitu pia...bora Dar to mwanza allys huwa wanaingia hotel za kueleweka japo ni bei.
Shinyanga restaurant yao inauza vitu vizuri, hotel ya Singida pia wanayoingia ipo magoli, dodoma pia pako poa.
Swala ni bei tu ila kwakweli nilifurahia kusafiri na ally's star.
 
Tena mikoa kama morogoro pale hakuna uhaba hata wa vitu unashangaa wal maharag 5000.
Singida kama unaend mwanz
Maj ya sh 500 wao wanauza 1000.
Njia ya kaskazin ndio balaa.chai rang 1000 andaz 1000 kitunbua 1000 yan haina kupinga.
Nafikri sheria iweke angalau kusimama bas vituo vikubwa vya mikoa dk 10 kama wanavyofanya kwenye mahotel
 
Back
Top Bottom