Waungwana nini sababu ya PETE ya ndoa kuvikwa kaika kidole maalum, kinachoitwa kidole cha pete? au hii ni katika hali ya kuiga ustaarabu wa wenzetu wa magharibi? Wachungaji Mapadre na Mashekh na wale ma MC hawaelezei maana halisi ya wanandoa kuvishana pete katika kidole hicho kwa nini mtu asiveshwe kwenye kidole Gumba???? Wana JF Pamoja na michango na michanganuo kuhusu mada hii lakini kama kuna daktari au mwana bailojia naomba anifahamishe .......... nimeambiwa kuwa ........ asili na chanzo kikuu cha PETE YA NDOA kuwa na kidole maalumu ni kwamba kidole kinachoveshwa mkono wa kushoto kina mshipa uluokwenda moja kwa moja katika moyo wa binadamu, hivyo kuvesha pete katika kidole hicho ni ishara ya upendo wa mke na mume katika mahusiano ya ndoa ambao unaunganishwa na moyo wa kila mmoja kupitia ishara ya PETE narudia wana baiolojia na madaktari wanaojua ukweli kusu hili wanisaidie!