Pete za Ndoa

Pete za Ndoa

Shemeji kutovaa pete ; akihofia kumpigwa shoti!

"Kama anampenda mkewe angeivaa na kuiua wakati wa kazi ""

swali langu lipo hapo, kuvaa pete kunahuckanaje na kupenda/upendo wa mtu alionao kwa mtu wake?
 
Kuna shemeji yangu ni fundi umeme yeye amemwambia dada yangu hataki kuvaa pete kwa sababu ya nature ya kazi yake kwamba akivaa pete anaongeza hatari ya kupigwa na shoti ya umeme.

Hahahaha hawa mafundi umeme kwa wake za watu kiboko lazima ni mmegaji hodari huyo shem wako.
 
Imekuwa kama kasumba siku hizi, wadada na wamama wengi walio katika ndoa huwa hawapendi kuvaa pete za ndoa zao. Hii hata kwa wakaka na wababa pete za ndoa zimekuwa kama ni sumu kwao pia. Ajabu wadada wasiokuwa na ndoa utawaona wametinga pete tena kwenye kile kidole cha kuvaliwa pete ya ndoa. Hivi pete zinaficha nini? Kuvaa ama kutokuvaa kunabadili heshima ya mtu?

Asilimia kubwa ya walio ndani ya ndoa wanacheat hata wanavaa pete au hawavai. Sasa umuhimu wake uko wapi? Mtu anatembea nje ya ndoa huku pete ya ndoa akiwa kaivaa au mwingine ni lazima aivue kabla ya kitendo. Hivi kuna tofauti kweli kati ya watu kama hawa? Baadhi ya ndoa za ugenini wana ndoa hawazipi uzito mkubwa pete hizo kwa kutukuwepo kabisa siku ya harusi yao.
 
Kuna jamaa angu ana Guest House anasema siku za week end watu wanasahau sana pete za ndoa mjengoni.
Watumiaji wa hii kitu jamani tunaomba ufafanuzi ukivua ndo tuseme unakuwa humsaliti mwenzio?
...Inawezekana wakiwa wanamegwa/kumega na pete kidoleni handasi zinapotea maana anahisi kama mwenye mali anamkodolea mimacho!
 
Yangu niliiamua kuivua baada ya Mr. kuvua yake kisa eti anashikashika maji sana. Ok, mbona basi wkend au siku mnapotoka wote asiivae,yeye niwakukumbushwa tuu kila siku.
 
"Kama anampenda mkewe angeivaa na kuiua wakati wa kazi ""

swali langu lipo hapo, kuvaa pete kunahuckanaje na kupenda/upendo wa mtu alionao kwa mtu wake?

Pete ni alama ya wanandoa; ni heshima ya upendo wako kwake! Kumpenda mtu ni pamoja na kumheshimu! Mie nashinda shambani natembea na pete ukifika wakati wa kazi ngumu za shamba naivua na nikimaliza kazi naivaa! Sijisikii huru nisipoivaa kwa muda mrefu nimejiwekea utamaduni huo kama ishara ya heshima yangu kwa mama watoto; Siwezi kuja na visingizio lukuki ilimradi nisivae pete! La hasha; Vivyo hivyo kwa bwana umeme; si muda wote anakuwa ananing'inia kwenye nyaya! lakini hata hivyo mwishowe ni jinsi mtu mwenyewe anavyolichukulia suala zima.
 
Pete katika ndoa kwa upande wa dini ni mapokeo tu ambayo watu walijitungia.Hakuna maandiko hasa agano jipya yanayodhibitisha umuhimu wa Pete kwenye makubaliano ya ndoa.Hivyo watu wavae au wasivae yote sawa tu ni mapambo.Uaminifu wa mtu ni tabia ya mtu kama anavaa pete ama havai.
 
Priest: "Do you take Mama_Enock as your lawful wife, to have and to hold, from this day forward, for better or for worse, for richer or for poorer, in sickness and in health, to love and cherish until death do you part?"

Baba_Enock: "I do"

Baba_Enock: "I take this ring as a sign of my love and faithfulness in the name of the father, the son and the holy spirit." "
 
Baba Enock Pete ni alama tu ya upendo na uaminifu. Kweli kabisa but nadhani kwa siku hizi sidhani kama pete za ndoa zinabeba maana halisi ya ndoa na ndio maana mtu haoni haya kutongoza au kukubali kutongozwa yukingali na pete ya ndoa. Za siku hizi ni mapambo tu!
 
Nyamayao!dada 6 yrs mbona ngoma bado mbichi?unakimbilia wapi kufikiria kuvua pete?Subiri upigwe kama 10 yrs halafu uje hapa na ujeuri huo.
Na bthw ukisema hujawahi kuivua una maana kuoga,kufua imo tu?Na mbona hukuusemea moyo wa mwenzio ?Angalau ungesema sisi 6 yrs hatujawahi kuzivua,au yeye kiishaisukumia mbali?vuta mwendo karibu unakaribia ile miaka ya utamu wa ndoa dada!:hug:
 
Mh nyie watu mnanikumbusha mbali mie wangu baada ya mwaka mmoja wa ndoa alinunua nyingine ya silver, kumwuliza akasema haipendezi siku akiwa anajisikia kuvaa bracelet yake ya silver achanganye na gold (pete) haiendi na wakati. Kuja kutahamaki ikawa inavaliwa tu ya silver iwe amefunga cuflinks za gold ama zambarau - bado aliivaa ya silver sidhani kama anakumbuka hata ilipo ile ya gold.

Mimi- Niliwahi kuivua siku moja nikatafuta famba la silver ili nami niende na wakati nikaona dhamira ikinisuta- (pamoja na kuwa mbali naye kwa muda sasa- sijawezaivua hii ya gold) Iwe kufua, kuoga, kupika unless namenya ndizi.
 
Yangu niliiamua kuivua baada ya Mr. kuvua yake kisa eti anashikashika maji sana. Ok, mbona basi wkend au siku mnapotoka wote asiivae,yeye niwakukumbushwa tuu kila siku.
Ikitoke hv ata ningekuwa mimi ningevua pole
 
Mwanajamii................
ndio utavaaje gold wakati unavaa kidani cha diamond na white gold? really ppl it doesnt make sense in terms of fashion 😀

but mwaka mmoja ulikuwa mrefu mno kufikia maamuzi hayo.......mie first day ya ndoa nilivua 😀

went to reception sijaivaa coz i was in white gold ........
 
Gaijin ningeyajuaje hayo wakati mie wa bush??

But seriously nini maana ya kubariki pete za ndoa basi kama kuna wakati itavuliwa na kureplace na nyingine? Nilishindwa kuelewa kwa mantiki hiyo
 
mwanajamii .....................kila mtu anavyochukulia kitendo cha kubariki pete

mie i think pete ya ndoa si muhimu mbele ya Mungu................i believe bibi na babu yangu waliishi miaka zaidi ya 50 ya ndoa bila ya kuvalishana pete. so haina umuhimu sana kwangu.

na hapo kuna tofauti kubwa ikiwa mmoja anaamini on pete mwengine haamini.
 
Baba Enock Pete ni alama tu ya upendo na uaminifu. Kweli kabisa but nadhani kwa siku hizi sidhani kama pete za ndoa zinabeba maana halisi ya ndoa na ndio maana mtu haoni haya kutongoza au kukubali kutongozwa yukingali na pete ya ndoa. Za siku hizi ni mapambo tu!

MwanajamiiOne,

hata sasa hivi bado maana "original" ya pete ya ndoa iko palepale. Wote wanao-abusive hizi pete bado dhamira zao zinawasuta na mara kwa mara utaona wanajisikia vibaya au kujishuku wanapokutana na watu wanaowafahamu wakiwa hawajavaa pete.
 
Kuna jamaa angu ana Guest House anasema siku za week end watu wanasahau sana pete za ndoa mjengoni.
Watumiaji wa hii kitu jamani tunaomba ufafanuzi ukivua ndo tuseme unakuwa humsaliti mwenzio?

"Pokea pete hii, iwe ukumbusho wa pendo langu na uaminifu wangu kwako.................. Nikupende, na kukutumikia kwa uaminifu hata kifo kitakapotutenganisha"
Mie mume wangu ana akili sana ndo maana nampenda! Yake iko juu ya dressing table mwaka sasa, anasema inampwaya (ajabu nguo zinam-bana). Afadhali anaacha nyumbani kuliko angesahau guesthouse( ni ya dhahabu aisee!!)
 
Ikitoke hv ata ningekuwa mimi ningevua pole

Licha ya hilo shostito, madai mengine kwa yeye ni msabato eti pete kwao ni mwiko...ok mbona ulizileta mbele kiapo na tukazivaaa. Na pia kwa nini siku hio hio asiseme tuzivue wote maana hazikubaliwi na wasabato. Ndoa yenyewe serikalini...usabato wapi na wapi. Uwizi mtupu! acha tuwege free na sisi tukatongozegwe mweeeeh!. Watu weeeeeeeeeeee :target: hakuna kulala...THIS IS THE 20TH CENTUARY...let the sleep dog sleep and the one awake let it bake, whuu, whuuu, whuuuuuuuuuu.
 
Mhhffffffffffffffff!!
 
Back
Top Bottom