Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Mmmh police gan mwenye Masters? PhD? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aaah wee hapanaa.
Si sahihi kutaja majina ya watu hapa ila phd's police wapo. Masters ndio kabisa zipo za kutosha. Makamishna wengi ni master holders.
 
Mmmh police gan mwenye Masters? PhD? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aaah wee hapanaa.
Wapo ma kamishner wa magereza wana phd, kwa polis masters ipo ila ni very rare thing to find. I know sababu wachache sana niliwah soma nao. Phd kwa polis ndio sijawahi sikia
 
Ni kweli, kinatakiwa kiundwe chombo kingine Maalumu Cha kipolisi ili kuweza kulisimamia na/au kulichunguza Jeshi la Polisi pale linapotuhumiwa .Kwenye nchi karibia zote zenye tawala za Kidemokrasia kuna Taasisi za namna hii. Zipo Taasisi Maalunu kabisa za Kipolisi ambazo zinajitegemea (Independent Police Organizations), kazi yake ni kushughulikia malalamiko dhidi ya Polisi au Jeshi la Polisi sambamba na kufanya Upelelezi dhidi ya Polisi. Tàasisi hizo huwa zinakuwa na Mamlaka yote ya Kipolisi, lakini Upolisi wao huwa wanaufanya dhidi ya Mapolisi au Jeshi la Polisi la kawaida. Taasisi za Kipolisi za namna hii huwa zinakuwa na Utawala wake binafsi unaojitegemea, hawana mwingiliano wowote wa kimajukumu au kiutendaji na Jeshi la Polisi la kawaida. Kwa mfano, Nchi ya Afrika ya Kusini wana Taasisi ya namna hii, inaitwa IPID ( The Independent Police Investigative Department, IPID). IPID ni Jeshi la Polisi la Kujitegemea ambalo kazi yake Kuu ni kufanya kazi za Kipolisi dhidi ya Jeshi la Polisi la kawaida, yaani kufanya Upelelezi na Kumshitaki Mahakamani Askari Polisi yoyote yule anayetuhumiwa au kulalamikiwa bila kujali cheo chake, hata kama ni Polisi huyo anayetuhumiwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi la kawaida.
Mbona nao yanayolalamikiwa huku hata kwao ni yale yale,Rushwa,uonevu,ukoloni mambo leo.
 
Naisi weledi ni shida,Kuna mmoja nikisoma nae muda wa kuandaa proposal ulipofika hakumuona supervisor(Dr) mwisho wa siku akaibuka na research report,simply mwaka huo hakugraduate.Naisi terms zibadilishwe za kuajili walau kuendana na mabadiliko ya kidunia.
 
Madhara ya chama kimoja hasa hiki changu Cha CCM kukaa madarakani muda mrefu,Hadi jeshi la police linashindwa kuwatumikia wananchi linatumikia chama na watawala yaani kuwapendeza watawala!!

Mimi naamini chama Chama upinzani ni sehem ya taifa coz wanachama waliopo huko wanalipa Kodi SAWA na chama Tawala!!

Tunaendelea kupoteza utaifa wetu siku Hadi siku!!
 
Polisi Tanzania ni aibu kubwa kabisa. Ina maana jeshi lote limejaa wajinga tu? Hakuna angalau watu wenye ku reason kwa kutumia logic? Je hakuna wenye ufahamu wa utawala wa kisheria?

Kuna mambo jeshi la polisi wanafanya yanakufanya ujiulize maswali mengi ya kukera.
Ila ndio wanaokulinda ukiwa unajijambia na mkeo.vile vile siamini km polisi wanakuzidi we kwa ujinga. Hilo likibatala limelewa sifa ht yeye anaweza kula mvua za kutosha. Kesi zake nyingi anashindaga kwa kutoa rushwa kwa majaji siyo akili wala kujua sheria
 
Madhara ya chama kimoja hasa hiki changu Cha CCM kukaa madarakani muda mrefu,Hadi jeshi la police linashindwa kuwatumikia wananchi linatumikia chama na watawala yaani kuwapendeza watawala!!

Mimi naamini chama Chama upinzani ni sehem ya taifa coz wanachama waliopo huko wanalipa Kodi SAWA na chama Tawala!!

Tunaendelea kupoteza utaifa wetu siku Hadi siku!!
Sasa nyie nyumbu mtalalamika mpk lini, uongozi hupatikana kwa kura siyo kulalamika humu
 
Polisi ni failure wa kidato cha nne halafu aende mahakamani kubishana kwa hoja na wakili msomi wa pale Law school 😅😅😅Hawana weledi wa kuisimamia Sheria maana hawaijui
 
these shemless and shenanigans political activist must be responsible to co-oparate with our very able police unit and for sure must be prosecuted arconding to the law of the land in regards of their confirmed offences 🐒

hii stori mingi na porojo za hawa maadvocate wa kutafuta kiki na kujulikana ni useless kabisa, na haviwezi kuzuia polisi kufanya kazi yake na mahakama kutekeleza wajibu wake ipasavyo 🐒

upotoshaji hauna faida wala maana yoyote. By the way tuache hatua stahiki za kisheria viendelee 🐒
 
Nakumbuka mwaka 1996 pale Tunduma , ujambazi ulikua unafanywa na polis. Mitaa ilikua inafungwa saa nne usiku. Waliletwa polis Toka makao makuu kuja kukomesha matukio ya uhalifu, polis kadhaa walidakwa.
 
Sasa nyie nyumbu mtalalamika mpk lini, uongozi hupatikana kwa kura siyo kulalamika humu
Nani nyumbu!!?

Halafu tangu lini idadi ya kura kuwa nyingi zikahalalisha ushindi wa mtu hasa katika nchi zetu za Dunia ya tatu!!?hata huko america idadi ya kura hazihalalishi ushindi wa urais!!

Hujui kura zinahalalisha yule aliechaguliwa tayari na wenye mamlaka ya nchi!?na sio idadi.na uwingi wa kura za mgombea!!?

Ingekua idadi ya kura inahalalisha ushindi was urais bas maalim seif,Lowasa,Tundu Lisu,Mrema wangeshaapishwa kuwa Marais was nchi hii!!hata secretary clinton angeshinda!!
 
Ni kweli, kinatakiwa kiundwe chombo kingine Maalumu Cha kipolisi ili kuweza kulisimamia na/au kulichunguza Jeshi la Polisi pale linapotuhumiwa .Kwenye nchi karibia zote zenye tawala za Kidemokrasia kuna Taasisi za namna hii. Zipo Taasisi Maalunu kabisa za Kipolisi ambazo zinajitegemea (Independent Police Organizations), kazi yake ni kushughulikia malalamiko dhidi ya Polisi au Jeshi la Polisi sambamba na kufanya Upelelezi dhidi ya Polisi. Tàasisi hizo huwa zinakuwa na Mamlaka yote ya Kipolisi, lakini Upolisi wao huwa wanaufanya dhidi ya Mapolisi au Jeshi la Polisi la kawaida. Taasisi za Kipolisi za namna hii huwa zinakuwa na Utawala wake binafsi unaojitegemea, hawana mwingiliano wowote wa kimajukumu au kiutendaji na Jeshi la Polisi la kawaida. Kwa mfano, Nchi ya Afrika ya Kusini wana Taasisi ya namna hii, inaitwa IPID ( The Independent Police Investigative Department, IPID). IPID ni Jeshi la Polisi la Kujitegemea ambalo kazi yake Kuu ni kufanya kazi za Kipolisi dhidi ya Jeshi la Polisi la kawaida, yaani kufanya Upelelezi na Kumshitaki Mahakamani Askari Polisi yoyote yule anayetuhumiwa au kulalamikiwa bila kujali cheo chake, hata kama ni Polisi huyo anayetuhumiwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi la kawaida.
Kenya wanacho
 
Mmmh police gan mwenye Masters? PhD? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aaah wee hapanaa.
Wapo wengi sana personally nawafahamu zaidi ya 20 wana masters na phd kuna mmoja phd alikuwa ocd wa mbweni, kuna dr mangu nilisoma nae ifm , kuna mmoja anauza sana magari kinondoni etc wengi sana
 
Kipigo cha Mbwa Koko Afande Moroto baada ya kustaafu Polisi kwa sasa ni Security Manager Kampuni ya Tembo Nickel Ngara,ni Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na Uchimbaji wa Madini ya Nickel Ngara,kwa kifupi analipwa Mshahara mkubwa kuliko aliokuwa analipwa Polisi
Yes very true
 
NCHI HII KUBWA: Bora Taharuki kuliko Mauaji.

ANAANDIKA BABA ASKOFU BENSON BAGONZA

Sifa moja muhimu ya kiongozi ni kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa jamii.

Nyumba inapoungua moto, ni bora kuokoa hata godoro moja kuliko kuua panya wanaokimbia moto unaounguza nyumba.

Mitandao ya kijamii usiku wa leo (25/4/2024) imejaa habari za Mwanaharakati wa haki za kijamii Malisa GJ na Mwanasiasa/Mwanaharakati Jacob Boniface kukamatwa na polisi kwa KUSABABISHA TAHARUKI wakati wanaripoti “mauaji” ya mtu mmoja aitwaye Mushi.

Kama ningelikuwa jeshi la polisi ningetafakari haya kabla ya kufanya maamuzi:

1. Nchi hii ni kubwa sana. Jeshi la polisi ni dogo kuliko uhalifu. Wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu ningewafanya marafiki kuliko maadui.

2. Ni kweli Mushi amekufa. Ningeshughulika na wauaji kuliko kushughulika na waliosababisha taharuki.

3. Ningejiuliza; taharuki imesababishwa na ripoti ya kifo au kifo chenyewe? Kifo kisicholeta taharuki si kifo kamili.

4. Malisa GJ ameisharipoti matukio mengi ya kihalifu ambayo jeshi la polisi ama halikujua au lingepata taabu sana kujua. Kwa hili la kifo cha Robert Mushi, Jeshi la polisi lingemzawadia nishani ya utumishi wa kujipendekeza kwa polisi kuliko kumkamata na kumpekua.

5. Badala ya kumpekua Malisa GJ na Boniface Jacob, ningewatumia na mitandao yao kutafuta na kujua gari linalodaiwa kumgonga marehemu Moshi.

6. Kwa kuwa nchi ni kubwa sana; ningetumia muda kuchunguza ndani na nje ya jeshi la polisi kuhusu uwezekano wa polisi vishoka wanaodaiwa kumkamata marehemu Robert Mushi kabla ya kifo chake!

7. Ningeazimia kuwalinda wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu kuliko wanaodaiwa kukosea katika kutoa taarifa za uhalifu ili kwa njia hiyo niongeze wigo wa watoa taarifa za uhalifu.

Lakini kwa kuwa mimi si Jeshi la polisi bali ni mtu ninayejifanya Askofu wakati hata uaskofu umenishinda, nabakia kutamani kuwa polisi huku nikijua kuna polisi wanatamani kuwa Askofu.

Natamani Jeshi la polisi liwaachie huru Malisa GJ na Boniface Jacob ili linufaike na harakati zao katika kukomesha uhalifu wa kidola na kiraia.
Huyu kaandika vizuri sana
 
Mkuu naunga hoja Kibatala na ya kwako. Pamoja na hayo nami napendekeza yafuatayo:

1. Muundo wa polisi ubadilishwe uwe ni wa kuhudumia wananchi. Badala ya kuwa police force ya mkoloni iwe police service ya kisasa.

2. Jeshi la polisi la sasa ligawanywe katika sehemu mbili zinazo jitegemea. Pawepo na huduma ya polisi na huduma ya upelelezi inayojitegemea kimuundo, kiuongozi, kimamlaka na kiutendaji

3. Polisi waboreshwe maslahi yao, angalau yakuweza kukimu/kumudu maisha ya sasa badala ya kutuma upolisi wao na bundiki kuendesha maisha yao. Huu ndio mzizi wa rushwa ndani ya polisi.

4. Askari polisi wote na vitengo vyao waishi kambini. Kambi zao ziboreshwe za kufaa kuishi binadamu. Ila askari upelelezi ndio waishi mtaani /changanyikeni/uraiani maana shughuli zao zinataka hivyo.

5. Katika mafunzo yao, mbali na mazoezi pawepo na somo la lazima la uelewa wa sheria, katiba, muongozo wa polisi na haki za raia kwa kila askari.

6. Kwa upande wa askari upelelezi pawepo na ukomo wa muda wa upelelezi, muda usizidi miezi 3, vinginevyo mahakamani ndio iongeze muda iwapo pana ulazima na usizidi miezi 3.

7. Katika zoezi lolote la ukamataji wa raia, raia yeyote wa jirani aruhusiwe kuchukua video ya tukio zima, video hiyo itumike kama sehemu ya ushahidi mahakamani ya mwenendo wa askari katika ukamataji na kusimamia haki ya raia.

9. Polisi wapewe vitendea kazi muhimu kama magari, pikipiki, fenicha, stationery na kadhalika kwa wakati ili kutimiza majukumu yao kwa ueledi bila ubabaishaji kama ilivyo sasa.

10. Ofisi, choo na mahabusi za polisi ziwe na hadhi nzuri kwa design, rangi na space. Hii itawamotivate askari kutenda haki. Majengo mengi ya polisi ukifika tu, unajua haki huipati! Nyingi ni mahabusu za kikoloni. Pia pawepo na vituo vya polisi kila ilipo ofisi ya serikali ya mtaa ili kurahisisha huduma.

11. Polisi iwatumikie raia wote kwa usawa. Jeshi la polisi lifuate sheria. Lisiwe jeshi la chama tawala lilojaa upendeleo. Ambalo kila askari ni mwanachama chama wa chama hiko na kusimamia ilani na sera za chama hicho. Lisiegemee upande wowote wa siasa.

Pawepo na clear separation.

12. Pawepo na muangalizi huru na maalum wa polisi ambaye kwa maoni yangu aweze kupokea malalamiko ya raia dhidi ya polisi, kuchunguza na kukarapia na kusimamisha askari yeyote kazi. Hii italeta nidhamu kwa askari dhidi ya raia.

13. Mwisho pawepo na utaratibu wa kila baada ya miaka 10, kupitia na kuoverhaul jeshi la polisi ili liweze kuendana na muda na mazingira ya dunia ya wakati huo.

Nawasilisha!
Naunga mkono hapo kwenye no 7, afu ilivyotoka 7 badala ije 8 we umeandika no 9
 
Back
Top Bottom