Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Ameandika kwenye ukurasa wake wa X

Hatua ya KWANZA kuhusu GEKUL ndiyo hiyo hapo πŸ‘‡. Natarajia Mahakama ya Wilaya ya Babati itatimiza WAJIBU wake kwa wakati, ili Kuanzia Jumatatu tarehe 11 Disemba 2023 hatua nyingine za KISHERIA ziendelee.

Hatua hiyo nimeichukua chini ya kifungu cha 128(2) na (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (The Criminal Procedure Act).

Msishangae kuona GEKUL anashitakiwa KIJINAI bila KUIHUSISHA ofisi ya DPP. Someni kifungu cha 128(2) na (4) hapo.
===
Napenda KUISHUKURU πŸ™πŸ» Mahakama ya Wilaya ya Babati Kwa KUIPOKEA kwa Wakati,Malalamiko (Complaint) ya MTEJA wangu HASHIM ALLY dhidi ya PAULINE PHILIPO GEKUL.

Muda wowote kuanzia jumatatu tarehe 11 Disemba 2023, nitapeleka NYARAKA HALISI za KESI ili MAHAKAMA ianze KUSIKILIZA KESI.


Pia soma:

Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake
 
Sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai Ina kifungu Cha mtu binafsi kuendesha shitaka la jinai, ila lazima apate kibali Cha mahakama.

Ninavyoona, Madeleka anamuharibia kesi huyu dogo, Dola itafanya juu chini kumuhujumu dogo ili kumkomesha Madeleka.

Kama dogo ana akili aachane na hawa wanasiasa waliojivika uanasheria
 
I concur with you…
 
Hata wamsafishe vipi huyo pauline, mbele ya uso wa Mungu hakubaliki, mbele ya uso wa jamii hakubaliki labda kwa wakatili wenzake.

Madeleka apunguze kuweka kila kitu kwa social media. Kama amekusudia kuwa mwanasheria wa huyu kijana aweke siasa na visasi pembeni.
 
Waliojivika uana sheria au walisomea uanasheria?
 
Kazi ya Madeleka ni kutimiza wajibu wa Kiraia.

Gekul hakuna wa kumshitaki hata serikali haina uwezo huo.
Mark my words
 
Tena hatoishi kwa amani labda amani ya kujilazimisha
 
Subirini upelelezi ukamilike Jamhuri impeleke mahakamani
 
Ninavyoona, Madeleka anamuharibia kesi huyu dogo, Dola itafanya juu chini kumuhujumu dogo ili kumkomesha Madeleka.
Kwa kuwa dola ya kishenzi inafanya mambo ya kishenzi ya kupindisha haki kwasabb za kishenzi basi hata kesi ikifunguliwa na kuendeswa na malaika dola ya kishenzi itaharibu tu.
 
Remember our judicial system recognize also private prosecution in criminal cases however, DPP at any stage may intervene either to procecute or to withdraw with or without notice
 
chiembe wewe ni mwanasheria ama ni mwanasiasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Wafanyeje Kama serikali inamlinda Gekul. Serikali haitaki kufungua mashtaka wafanyeje Kama sio wao kwenda mahakamani kuomba kibali.
 

Hiyo sio charge ni complaint. Ni maombi ya kutaka mtuhumiwa afunguliwe mashtaka.

Inaonekana Public Prosecutor anataka kukwepesha kesi ndio maana madeleka anaomba kibali afungue kesi kwa niaba ya Jamhuri. Jamhuri ni jamii yote ya Tanzania sio serikali.
 
😳 we ni malaika wa Mungu, right?
 
Jamhuri gani?. Jamhuri ni party to the case sio mfungua mashtaka. Anaye fungua mashtaka ni Public Prosecutor. Yani kwenye kesi ya jinai mlalamikaji ni Prosecutor kwa niaba ya Jamhuri au jamii.
Huna akili hata 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…