Peter Msechu acha comedy kwenye afya yako, utakufa premature utuachie mkeo, watoto wako watateseka

Langa alikufaje embu tuambie
 
Ukibatika kufika uzee na ukawa mnene namna hiyo na ni mwanaume hakyanani utapata tabu sana.
Kuna jamaa yangu husema kitambi ni uchafu, yani hilo tumbo umejaza nnya tupu.

Unene haufurahishi, unene unachosha, unakua mzito mzito kila wakati hata kunyanyw mguu, kukwepa hatari fulani ya gafla ni kazi maana limwili linakusaliti.
Unene unatesa basi tu, wengi wao umeshawaletea uvivu wa kuuondoa.

Pumzi pia inakua haba, kupiga mshipi muda mrefu sio rahisi, na tumbo kubwa kwa mwanaume hufanya kikojoleo kiingie ndani zaidi.
 
Unene uluopitiliza kwa mwanaume ni hasara nyingi kuliko faida,yaani hii kufia kifuani kwa mwanamke au kufia usingizinini jambo la kawaida kabisa
 
Unene uluopitiliza kwa mwanaume ni hasara nyingi kuliko faida,yaani hii kufia kifuani kwa mwanamke au kufia usingizinini jambo la kawaida kabisa
Sure mkuu, unene sio mzuri kabisa na unatesa mno.

Ukikaa na mtu mnene karibu utaona jinsi anapata tabu kupumua.
 
Okay.
Is the JF platform the right place to give advice to someone regarding their body maintenance.
How personal issues, you make it public?
Hii ni jamii forums, elewa neno jamii.
Jamii ni pamoja na wewe, bahati mbaya/nzuri kwa Msechu ni kua yeye ni mtu maarufu, kuongelewa kwa umbo, sauti, maisha, ndoa nk ni takwa la mashabiki zake wamjuao.

Na bila shaka yeye karuhusu hilo ndio maana haoni shida kuliongelea mitandaoni, maisha yake na familia yake kaiweka public.

Sasa wewe ni nani yake hadi utake kukataza asishauriwe?? Ushauri wa hapa utawatoa tongotongo vibonge wengine, kama alivyo kioo cha jamii badi jamii inajifunza kupitia yeye.

Hata wewe ukiwa maarufu utajadiliwa tu, ndio maana mods hawajaufuta uzi, unafaa kwa jamii.
 
Hivi yule mtt wa Ambani ilishindikana nn jamani alioa juzi juzi. Ina maana pesa ilishindwa? ....unene wa hivi no.
Kaka nilijiuliza Sana mm pia nakamwili Ka Baba levo tayari najichukia na sababu kubwa Nina Mambo ya kiuchumi sijayapangilia .ila ifikapo mwezi WA 6 naingia gym kabisa staki ujinga
 
Kupunguza unene ni shughuli ndefu hususan kwenye baadhi ya miili, mazoezi tu hayatoshi, kwa mfano mimi hapa hutumia mazoezi na mfungo wa kila siku, yaani chakula cha mwisho huwa nakula saa tisa hadi kesho yake nafungua saa tatu asubuhi.
Hiyo ni masaa 18 bila kula, na masaa 6 ya kula, eating window.
Licha ya yote hiyo, kupungua kwenyewe hunijia taratibu sana, mwezi unaweza ukaisha sijapunguza kitu au hata kuna mwezi ninaongeza unene badala ya kupunguza.
Ni safari ndefu yenye misukosuko ila ukipania utapunguza.
Hatua ya mwanzo ni kukubali kwamba aina yako ya mwili sio kawaida kama binadamu wengine, mmeng'enyo wako wa chakula una mapungufu, hivyo unajikubali kuwa na huo ulemavu na kuishi nawo.
 
Pole na hongera kulijua hilo
 
Unakubaliana na GENTAMYCINE kwamba wewe ni kilaza kisa ni bonge?
 
Jamii = "Society" according to (English Translation)

Ukisoma vizuri maana ya neno "Jamii" utagundua kuna maneno makuu matatu:-
1. Watu
2. Muingiliano (Kuchangamana)
3. Eneo

So tuna-share na kujadili nini? (what contents?) - hapo ndipo panapo-matter zaidi.
Kwa maana "Akili kubwa hujadili mawazo; Akili za wastani hujadili matukio; Akili ndogo hujadili watu."

Ni matumaini yangu, umejiona una angukia katika kundi gani?
Usipojifunza na hapa hicho ni kiburi, unatakiwa ubadili mwenendo wako juu ya akili yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…