Peter Msechu adai kupungua kilo 7 baada kuwekewa puto Tumboni

Mbona ghafla sana? Rate ya upunguaji ni kubwa sana ,kwa siku kilo moja siyo mchezo,atakuja kuleta matatizo mengine.
ntashangaa sana kama Muhimbili watasema hii ni sawa.
Kwamba hii rate ya ushukaji wa hizi kilo ndo lengo pekee haijalishi mwili unapitia mchakato mwingine upi unaohusisha na kuathiri viungo vipi?
Kazi ipo!
 
Nilishawahi kumwambia mtu humu ndani,kuwa unene wa watu wengine huwa unatokana na kula sana akabisha,sasa ilivyo ni kuwa tumbo likishatanuka na kuwa kubwa huwezi kukaa tena muda mrefu bila ya kutia kitu tumboni,na mwishowe kupunguza unene inakuwa ni mtihani kwake,kwahiyo kwa kuwekewa puto,food intake yake inakuwa imepunguzwa sana.Naona sasa hivi atakuwa ananielewa...
 
Shida gani tena kwa Msechu mpaka anafikia kilo 143?! Mzee ulimeza mtu au nini?Mmhh?! Eeeh, watu wakishafanikiwa huku Africa wanaishia kula kama simba na kupelekea kuharibu maisha yao. Au ni nini kilimpata huyu bwana? Mtu unashindwa kujizuia kula mpaka uwekewe puto tumboni?!
 
Msechu Mwenye Enzi Mungu akubariki sana na akupe haja ya moyo wako walahi!
 
Bado ana kilo 136.5, kwani haiwezekani kumeza maputo matatu apunguze kilo tatu kwa siku?
 
Nimeondika mpaka nimekosa cha kuandika.
Dah! Watu waelejezwe kubugia vyakula hai kutuna kama mdudu ni ishara ya maadili duni.
Sawa Lakini upande siyo hivyo, kuna watu wameumbwa na mili minenetu hata ale mawe yeye atakuwa mnenetu.
 
Kupungua kilo moja ndani ya siku moja, hilo siyo jambo la kufurahia.

Kitu umekiweka kwa miaka kadhaa ukiondoe kwa siku moja. Ni hatari.
Mabondia hupunguza hadi 3kg kwa siku
 
Angemuuliza dada Wema sepetu.. ..alikoenda.. mbona angerudi na kilo 25 tu!
Ya sepetu ni mbaya maana hakuna kurudi nyuma, hii unaweza tolewa puto ukarudi kuwa mnene
 
Pita(Petero) kama unapitia JF kuwa makini na hilo puto aiseee kusoma nyuzi za Tanzia sio poa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…