Pre GE2025 Peter Msigwa amwandikia Mbowe barua akidai fidia ya Tsh. Bilioni 10

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kumtaka Mchungaji Peter Msigwa kuomba radhi na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu, Mchungaji Msigwa kupitia mawakili wake kutoka Mwamgiga Law Chambers ametoa majibu rasmi.

Katika barua ya majibu ya Msigwa iliyotolewa Septemba 5, 2024 na ambayo inaonesha kupokelewa upande wa Mbowe siku ya Jumatatu Septemba 9, 2024, mawakili wa Msigwa wamekanusha vikali madai hayo wakieleza kuwa sehemu kubwa ya malalamiko ya Mbowe yanakosa msingi wa kisheria.

Mchungaji Msigwa, ambaye alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa kabla ya kuhamia CCM, amekanusha kuwa matamshi yake yalikuwa na nia ya kumharibia sifa Mbowe. Katika majibu yake, Msigwa ameonesha kutoridhishwa na lugha iliyotumika katika notisi ya Mbowe, akiitaja kuwa "ya kejeli" na yenye lengo la kumchafua hadharani.

Mawakili wa Msigwa wamesema, "Mteja wetu anakataa kwa nguvu maneno yaliyotajwa kwenye barua yako, akisisitiza kwamba madai yote ni ya uongo na hayana msingi wowote wa ukweli."

Pia wametangaza kuwa iwapo Mbowe ataendelea na vitisho na tuhuma hizo, Msigwa atachukua hatua za kisheria kumlinda dhidi ya kile walichokiita "mashambulizi ya tabia" yanayoendelea.

Kwa kuongezea, mawakili wa Msigwa wameweka sharti kwamba Mbowe aombe radhi kwa matamshi yake ndani ya siku tano, na alipe fidia ya Shilingi bilioni 10 kwa uharibifu wa jina na sifa ya Msigwa.

Wamesema pia kuwa Msigwa yuko tayari kwa mazungumzo ya kutatua suala hili kwa njia ya amani, lakini ikiwa Mbowe ataendelea na madai yake, watafungua kesi ya kisheria ili kujitetea.

Barua hiyo imehitimishwa kwa kuashiria kuwa Msigwa ana nia ya kutafuta suluhu nje ya mahakama, lakini yuko tayari kupambana kisheria iwapo haitapatikana njia mbadala.
View attachment 3091693

Pia soma: Kuelekea 2025 - Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina
Heheh wanamdanganya huyu fake pastor hapa naona amemwagia mafuta kwenye moto. Anaomba kukaa mezani yazungumzwe halafu anatishia blalifaken tukutane mahakamani tutajua nani anapaswa kumlipa mwenzake .
 
Msigwa hajaua na kamwe siyo muuaji

Tuache upuuzi wa kusingizia

Tubaki kwenye ramani ya mbowe na msigwa
Tuachie mamlaka yatabainisha ukweli. Alisikika kwenye maswali aliyokuwa akijibu kwenye mtandao wa sauti ya watanzania akimtaja ally kama kiongozi hatari wa kikundi cha hamasa cha chadema na siku chache baadae mzee ally kauwawa kikatili.
 
Msigwa hajaua na kamwe siyo muuaji

Tuache upuuzi wa kusingizia

Tubaki kwenye ramani ya mbowe na msigwa
Inawezekana hajaua ila comments zake zimetoa suggestion, unapomtag as a threat what else do you expect zaidi ya mashambulizi?
 
Mbowe amemwambia msigwa kuwa amefanya defamation sasa anapoleta ujinga na hao wajinga wenzio atapata anachokitafuta.
Mawakili wa Msigwa wanaosema Mbowe kafanya character assassination (mashambulizi ya tabia). Huu mtifuano unaweza ukaamuliwa na ICC huu.
 
Baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kumtaka Mchungaji Peter Msigwa kuomba radhi na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu, Mchungaji Msigwa kupitia mawakili wake kutoka Mwamgiga Law Chambers ametoa majibu rasmi.

Katika barua ya majibu ya Msigwa iliyotolewa Septemba 5, 2024 na ambayo inaonesha kupokelewa upande wa Mbowe siku ya Jumatatu Septemba 9, 2024, mawakili wa Msigwa wamekanusha vikali madai hayo wakieleza kuwa sehemu kubwa ya malalamiko ya Mbowe yanakosa msingi wa kisheria.

Mchungaji Msigwa, ambaye alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa kabla ya kuhamia CCM, amekanusha kuwa matamshi yake yalikuwa na nia ya kumharibia sifa Mbowe. Katika majibu yake, Msigwa ameonesha kutoridhishwa na lugha iliyotumika katika notisi ya Mbowe, akiitaja kuwa "ya kejeli" na yenye lengo la kumchafua hadharani.

Mawakili wa Msigwa wamesema, "Mteja wetu anakataa kwa nguvu maneno yaliyotajwa kwenye barua yako, akisisitiza kwamba madai yote ni ya uongo na hayana msingi wowote wa ukweli."

Pia wametangaza kuwa iwapo Mbowe ataendelea na vitisho na tuhuma hizo, Msigwa atachukua hatua za kisheria kumlinda dhidi ya kile walichokiita "mashambulizi ya tabia" yanayoendelea.

Kwa kuongezea, mawakili wa Msigwa wameweka sharti kwamba Mbowe aombe radhi kwa matamshi yake ndani ya siku tano, na alipe fidia ya Shilingi bilioni 10 kwa uharibifu wa jina na sifa ya Msigwa.

Wamesema pia kuwa Msigwa yuko tayari kwa mazungumzo ya kutatua suala hili kwa njia ya amani, lakini ikiwa Mbowe ataendelea na madai yake, watafungua kesi ya kisheria ili kujitetea.

Barua hiyo imehitimishwa kwa kuashiria kuwa Msigwa ana nia ya kutafuta suluhu nje ya mahakama, lakini yuko tayari kupambana kisheria iwapo haitapatikana njia mbadala.
View attachment 3091693

Pia soma: Kuelekea 2025 - Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina
Huu sii muda wa maigizo ni muda muhimu wa mambo muhimu yanayo lihusu taifa letu.Tuacheni na yaliyo muhimu zaidi.
 
Jina la Msigwa na wala yy Msigwa hana hadhi ya hiyo hela, hadhi yake ni ya buku 2 au buku jero finito!! Kina Makalla wanamdanganywa mwisho wa siku kesi ni individual!
Kwani baba ndubwi ndiyo Ana hadhi ya 5bn?

Ali’ye wauza in 2015 kwa pesa chache? Na kuua rasmi chakademus and pliers?

Come on
 
Mch. Msigwa ni mental case, anadhani kwa huo utoto wake hapo ndio case imeisha na ushindi amechukua.

Hajui hapo sasa ndio kesi inaenda rasmi mahakamani, ule ujinga wake aliokuwa anaropoka kila siku kwenye majukwaa ya siasa upo kila mahali.

Hao mawakili wajanja waachwe wajilie pesa za mjinga.
Mbowe yupo kimya anamsubiri ambane mahakamani
 
"...Msigwa yuko tayari kwa mazungumzo ya kutatua suala hili kwa njia ya amani..." ukisikia poooooooo ndiyo yenyewe hiyo ya kunyanua mikono juu kabla ya kwenda kwa pilato... Tangu lini mtu anamtishia mshitaki wake kwa kutoa vitisho vya yeye pia kufungua kesi? Human nature inaonesha ni nani mkosaji kwa kauli kama hizi...
Ngoja anyooshwe
 
Hawa mawakili akili zao ni sawa na za Msigwa. Njaa mbaya sana
 
Na mimi nawashitaki kwa kutusumbua waniombe radhi au watoe 15B kama fidia 😂
 
Back
Top Bottom