Peter Msigwa avamiwa na vibaka maeneo ya Ikulu

Peter Msigwa avamiwa na vibaka maeneo ya Ikulu

huyu hapa anafunguka facebook
""Niliharibikiwa na gari maeneo ya kutokea ikulu mda
sio mrefu,nikavamiwa na vibaka Saba Mimi pamoja
na Dereva wangu ambaye alikuwa anafungua tairi
nimepigwa vizuri ,na nimenyang'wa simu zote na
pesa pamoja na waleti ,hii Ndio bongo , ....watu
wengi nitakuwa nimepoteza namba zenu""

My take.: askari wapo bussy na Sheikh ponda na Faridi?? Its a big joke

Tafadhali mjulishe mbunge Peter Msigwa kwa facebook kwamba hayo ni madhara ya watoto wa mitaani walioongezeka sana, wakishakuwa wakubwa wanahamia beach na kukaba watu. Bunge letu likianza awasilishe hoja binafsi kuhusiana na ongezeko la watoto wa mitaani, hatua gani za kudumu zichukuliwe.
 
Kwani kuna ikulu sita hapa Tanzania!??

Kunawakati mwandishi anaweza kupitiwa

kuna ikulu ndogo mikowani na ile kuu ya magogoni

Inaweza kuwa na maana ya ikulu ndogo lakini kwa bahati mbaya neno ndogo au vingivo lisiwepo, ndiyo sabab ya swali hilo.

Isitoshe maeneo ya ikulu - magogoni kunaulinzi mzuri na hii kuongeza wasiwasi kwamba labda ilikuwa ikulu za mikowani.
 
Alipigwa na kuibiwa tu, au labda Maskaut jenta walinanihii, yaani labda walimkaba pia?
 
Mbunge unatembea kirahisi hivyo. Hata mguu wa kuku huna tena wakati huu ambao kuna siasa za uhasama mpaka wabuge wanapigwa na Mapanga.Nawashauri wajiweke fiti kimazoezi na watembee na miguu ya kuku
I was thinking about the same thing,mguu wa kuku muhimu sana kwenye jamii ya sasa bongo.
 
Mimi huwa mara chache sana nafika Dar.. Novemba nitakuwa Dar naamini shemeji Mwita Maranya atanisaidia.

Kama utakua na shemeji yako MWITA hakika usalama wako hautakua shakani...
 
MBUNGE wa Iringa Mjini, (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, ameeleza namna alivyovamiwa, kupigwa na kuporwa na vibaka maeneo ya Daraja la Salenda, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akisimulia mkasa huo jana, Mchungaji Msigwa alisema, alikabwa na vibaka juzi, saa moja usiku wakati akitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Siku hiyo Kamati yetu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, tulikuwa tumekwenda kutembelea Msitu wa Ruvu Kusini na wakati narudi nilipitia ile Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

“Nilipofika maeneo ya Daraja la Salenda Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ghafla gari yangu ilipata hitilafu katika upande wa tairi, ndipo nikashuka pamoja na dereva wangu ili kukagua.

“Kabla ya kushuka, nilimwambia dereva wangu anayeitwa Baraka, apaki pembeni kidogo ili asisababishe foleni. Tulipolikagua gari, tukakuta kuna kasoro zilizosababisha tairi zisiweze kuzunguka vizuri.

“Dereva wangu alichukua jeki na kuanza kutengeneza gari, wakati huo mimi nikawa nazungumza na mtu kwenye simu yangu, pembeni ya ukuta wa daraja. Ghafla mbele yangu wakatokea vijana kama nane hivi, wakawa wananisogelea, mimi nikaamini wale labda wamekuja kunisaidia kumbe sio.

“Waliponikaribia, nikawauliza wanataka nini, wakaniambia kaa kimya, kwa kuwa mimi ni mbishi, nikaendelea kuzungumza na simu, lakini mmoja wao akaanza kuninyang’anya ile simu nikawa naing’ang’ania, kwa sababu najua ina namba nyingi za watu.

“Nilipozidi kuonyesha ubishi walizidi kunikaba, wakati huo baadhi yao waliendelea kumminya dereva wangu ambaye tayari alikuwa kule chini ya gari akilitengeneza.

“Lakini mimi nikapambana na wawili niliokuwa nao nikawa nakaribia kuwashinda, hata hivyo wakaongezeka tena, ndipo wakafanikiwa kunidhibiti na kuninyang’anya simu yangu na nyingine zilikuwa kwenye gari, wakachukua pia na fedha taslimu Sh 400,000 na baadhi ya vitu vidogo vidogo vilivyokuwa kwenye gari, isipokuwa Ipad hawakufanikiwa kuiona kwa sababu ilikuwa kwenye kioo cha mbele cha gari.

“Kusema kweli walinipiga kisawasawa, wakaniumiza mguu kidogo na jicho, wakaniharibia na meno yangu mawili ya bandia.

“Wakati wananikaba, wengine walimkamata dereva wangu na kumtupa baharini, lakini nashukuru hakudhurika. Baadaye tukapata msaada kwa askari polisi waliofika eneo la tukio, ingawa walichelewa kufika.

“Hata hivyo, sasa hali yangu inaendelea vizuri kwa sababu hapo awali nilikuwa na tatizo la mguu, ambao mwezi uliopita nilikwenda Ujerumani nikaanguka na kufanyiwa uchunguzi, lakini niliporudi nchini Oktoba tisa, nilifanyiwa upasuaji na sasa naendelea vizuri kwa sababu nategemea kutoa hili hogo kesho,” alisema Mchungaji Msigwa.

Akizungumzia eneo hilo jinsi lilivyo, alisema limekuwa na historia ya watu kukabwa na kuibiwa fedha na vitu mbalimbali.

“Kwanza ni aibu sana kwa sababu ni eneo ambalo lipo karibu na Kituo cha Polisi, lakini ukiwauliza askari wanadai eti wakitaka kuwakamata hao vibaka huwa wanakimbilia baharini.

“Wapo pia wabunge mbalimbali nimesikia walishawahi kukabwa hapo na kuibiwa Sh milioni moja, ingawa hawakutaka kusema, mimi ni msema kweli nimesema kwamba walinikaba.

“Vivyo hivyo, nilishawahi kusikia huyu Kigogo wa JWTZ anayeitwa Shimbo, naye alishawahi kukabwa baada ya kufika eneo hilo baada ya kushuka kwenye gari na kuanza kujisadia haja ndogo,” alisema.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na gazeti moja linalochapishwa kila siku toleo la jana (siyo MTANZANIA), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba, alisema vibaka wawili wameshakamatwa na leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.
 
Msigwa bwana kumbe alishawahi kusikie eneo ilo ni hatarishi sasa kwanini asingetafuta sehemu nyngne salama.
Fikra hizi.
 
Lakini kuna thread humu iliyodai kuwa amekabwa karibu na Ikulu. Which is which
 
MBUNGE wa Iringa Mjini, (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, ameeleza namna alivyovamiwa, kupigwa na kuporwa na vibaka maeneo ya Daraja la Salenda, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akisimulia mkasa huo jana, Mchungaji Msigwa alisema, alikabwa na vibaka juzi, saa moja usiku wakati akitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

"Siku hiyo Kamati yetu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, tulikuwa tumekwenda kutembelea Msitu wa Ruvu Kusini na wakati narudi nilipitia ile Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

"Nilipofika maeneo ya Daraja la Salenda Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ghafla gari yangu ilipata hitilafu katika upande wa tairi, ndipo nikashuka pamoja na dereva wangu ili kukagua.

"Kabla ya kushuka, nilimwambia dereva wangu anayeitwa Baraka, apaki pembeni kidogo ili asisababishe foleni. Tulipolikagua gari, tukakuta kuna kasoro zilizosababisha tairi zisiweze kuzunguka vizuri.

"Dereva wangu alichukua jeki na kuanza kutengeneza gari, wakati huo mimi nikawa nazungumza na mtu kwenye simu yangu, pembeni ya ukuta wa daraja. Ghafla mbele yangu wakatokea vijana kama nane hivi, wakawa wananisogelea, mimi nikaamini wale labda wamekuja kunisaidia kumbe sio.

"Waliponikaribia, nikawauliza wanataka nini, wakaniambia kaa kimya, kwa kuwa mimi ni mbishi, nikaendelea kuzungumza na simu, lakini mmoja wao akaanza kuninyang'anya ile simu nikawa naing'ang'ania, kwa sababu najua ina namba nyingi za watu.

"Nilipozidi kuonyesha ubishi walizidi kunikaba, wakati huo baadhi yao waliendelea kumminya dereva wangu ambaye tayari alikuwa kule chini ya gari akilitengeneza.

"Lakini mimi nikapambana na wawili niliokuwa nao nikawa nakaribia kuwashinda, hata hivyo wakaongezeka tena, ndipo wakafanikiwa kunidhibiti na kuninyang'anya simu yangu na nyingine zilikuwa kwenye gari, wakachukua pia na fedha taslimu Sh 400,000 na baadhi ya vitu vidogo vidogo vilivyokuwa kwenye gari, isipokuwa Ipad hawakufanikiwa kuiona kwa sababu ilikuwa kwenye kioo cha mbele cha gari.

"Kusema kweli walinipiga kisawasawa, wakaniumiza mguu kidogo na jicho, wakaniharibia na meno yangu mawili ya bandia.

"Wakati wananikaba, wengine walimkamata dereva wangu na kumtupa baharini, lakini nashukuru hakudhurika. Baadaye tukapata msaada kwa askari polisi waliofika eneo la tukio, ingawa walichelewa kufika.

"Hata hivyo, sasa hali yangu inaendelea vizuri kwa sababu hapo awali nilikuwa na tatizo la mguu, ambao mwezi uliopita nilikwenda Ujerumani nikaanguka na kufanyiwa uchunguzi, lakini niliporudi nchini Oktoba tisa, nilifanyiwa upasuaji na sasa naendelea vizuri kwa sababu nategemea kutoa hili hogo kesho," alisema Mchungaji Msigwa.

Akizungumzia eneo hilo jinsi lilivyo, alisema limekuwa na historia ya watu kukabwa na kuibiwa fedha na vitu mbalimbali.

"Kwanza ni aibu sana kwa sababu ni eneo ambalo lipo karibu na Kituo cha Polisi, lakini ukiwauliza askari wanadai eti wakitaka kuwakamata hao vibaka huwa wanakimbilia baharini.

"Wapo pia wabunge mbalimbali nimesikia walishawahi kukabwa hapo na kuibiwa Sh milioni moja, ingawa hawakutaka kusema, mimi ni msema kweli nimesema kwamba walinikaba.

"Vivyo hivyo, nilishawahi kusikia huyu Kigogo wa JWTZ anayeitwa Shimbo, naye alishawahi kukabwa baada ya kufika eneo hilo baada ya kushuka kwenye gari na kuanza kujisadia haja ndogo," alisema.

Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na gazeti moja linalochapishwa kila siku toleo la jana (siyo MTANZANIA), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba, alisema vibaka wawili wameshakamatwa na leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Get a point, hapo kwenye red. uone jinsi hatuna wanasiasa bali wabishi, busara kidogo sana na ulalamishi. Hawajui kujenga hoja, eti polisi walichelewa , kwani walijua Msigwa atavamiwa na vibaka wajiweke tayari? Kulikuwa na haja yoyote ya kutumia maneno kama akijisaidia haja ndogo? Hivi umaarufu wa kisiasa unaweza kutafutwa hata chooni kumbe.
 
Msigwa bwana kumbe alishawahi kusikie eneo ilo ni hatarishi sasa kwanini asingetafuta sehemu nyngne salama.
Fikra hizi.

Ameshasema mwenye ni mbishi so alikwenda kibishi, bahati yake ingependeza kama wangemnanihi kabisa ili akome. Unaleta uheshimiwa hadi kwa vibaka.
 
huyu hapa anafunguka facebook
""Niliharibikiwa na gari maeneo ya kutokea ikulu mda
sio mrefu,nikavamiwa na vibaka Saba Mimi pamoja
na Dereva wangu ambaye alikuwa anafungua tairi
nimepigwa vizuri ,na nimenyang'wa simu zote na
pesa pamoja na waleti ,hii Ndio bongo , ....watu
wengi nitakuwa nimepoteza namba zenu""

.. (ni ikulu ya magogoni)

My take.: askari wapo bussy na Sheikh ponda na Faridi?? Its a big joke

Nashauri iundwe tume/kamati kuchunguza tukio hilo!
 
Get a point, hapo kwenye red. uone jinsi hatuna wanasiasa bali wabishi, busara kidogo sana na ulalamishi. Hawajui kujenga hoja, eti polisi walichelewa , kwani walijua Msigwa atavamiwa na vibaka wajiweke tayari? Kulikuwa na haja yoyote ya kutumia maneno kama akijisaidia haja ndogo? Hivi umaarufu wa kisiasa unaweza kutafutwa hata chooni kumbe.

Hivi we unaliona dogo hilo la mtu 'mkubwa' kama Shimbo kukojoa barabarani! Mita 20 tu kuna kituo cha Polisi chenye choo. aliweza kwensda hapo!...Na mkazi gani wa Dar es salaam hajui eneo lile kuna wezi? Polisi wanashindwaje kuweka doria kwa eneo wanalojua ni korofi? Tukihisi wanachukua hesabu toka kwa hao vibaka watabisha? Wanachoma mafuta wakitangatanga na defender/hardtop usiku kucha huko mbaali wakati watu wanakabwa mita 20 toka kituo kikubwa cha Polisi kama Salender!
 
huyu hapa anafunguka facebook
""Niliharibikiwa na gari maeneo ya kutokea ikulu mda
sio mrefu,nikavamiwa na vibaka Saba Mimi pamoja
na Dereva wangu ambaye alikuwa anafungua tairi
nimepigwa vizuri ,na nimenyang'wa simu zote na
pesa pamoja na waleti ,hii Ndio bongo , ....watu
wengi nitakuwa nimepoteza namba zenu""

.. (ni ikulu ya magogoni)

My take.: askari wapo bussy na Sheikh ponda na Faridi?? Its a big joke

Hawa ndo aina ya viongozi waongo, wachonganishi na wanaotafuta ujiko kwa nguvu. Mbona kuna umbali mkubwa tu, kati ya Salender Bridge na Ikulu. Kwa nini aitaje Ikulu hata kama alikuwa huko? Kwa nn tusiamini kuwa alikusudia kuhusisha uporwaji wake na Ikulu? By the way Kwa kuwa huyu jamaa alishajitangaza kuwa ni mkorofi na ndo maana aling'olewa meno mawili' ni dhahiri kuwa kila mara anatamani vurugu itokee.
 
Pole sana Mheshiwa, hata ulaya vibaka wapo na mbaya zaidi hawajuagi huyu ni Mbunge au mama ntilie au chinga wote ni twende kazi
 
Back
Top Bottom