Peter Msigwa: Hayati Magufuli alikuwa shujaa wa kizamani


Kinjekitile alidharau sayansi huku akijua ana malukanga+Pacer.
 
Alikopa mpaka bank za biashara halafu taga kama wewe unatuambia alitumia pesa za ndani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wetu Kinjekitile Ngwale alipohamasisha wapiganaji watumie maji katika kukabiliana na risasi za wazungu kwa Imani kuwa risasi zao zingegeuka maji na kutowadhuru. Matokeo ya ushujaa wa Kinjekitile kwenye vita vya maji maji na matokeo ya ushujaa wa JPM kwenye vita ya Corona yote tumeyaona.

Mtupoli wa zamani sana.. 😂
 
Mungu mkubwa, kweli Msigwa wewe umesahau ulivyolipiwa faini na JPM na leo hii unaanza kumdhihaki inshaallah Mungu atatenda.
kama tukianza kuhesabu matendo ya wema ambayo madikteta jamii ya jiwe waliyafanya kwa raia mmoja mmoja, basi mobutu seseko na iddi amini walitenda mema zaidi kuliko huyo mtukufu wenu. na bado mpaka leo dunia inawapiga spana.

ukweli ni kwamba, mabaya mengi waliyoyafanya yanafuta mema yote waliyoyafanya kwa mtu mmoja mmoja. hivyo basi usimlaumu msigwa kwa kumuelezea jiwe licha ya kwamba alimlipia faini.

NB: tukumbushe kuhusu hilo tukio zima la faini na nani alisababisha.
 
Hilo bichwa lako ishia kufugia nywele tu, hata kubebea mizigo halifai.
 
Shujaa ni shujaa, awe wa zamani au wa sasa.

Ni sawasawa na kusema Pele alikuwa mchezaji mpira bora wa zamani na si wa sasa.

Au huyu ni mrembo wa zama za kale lakini si wa sasa.

Vipo vitu humu duniani ni timeless. Talanta ya ushujaa (bravery) ni miongoni mwa vitu visivyopitwa na wakati.

Kuna sababu kwanini JPM akawa rais wa Tanzania nyakati za sasa. Ni kwa sababu talanta ya ushujaa alikuwa nayo, na kwa vile ushujaa haufichiki, aliaminiwa ndani ya chama chake (pamoja na figisu zote) na akaaminiwa na watanzania.

Na kinyume cha ushujaa ni undondocha. Na undondocha si sifa ya maana -- iwe kwa zamani au kwa sasa.
 
Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.
Msigwa hakika umeutendea haki muda uliotumia kuandika hii tanzia


Kabisa. JPM alikuwa kituko kabisa katika ulimwengu wa leo wa kidigital

Hapa kina Elitwege watapinga ila huu ndiyo ukweli mchungu

Na mm nasema pumzika kwa amani Ewe Shujaa uliyetawala nyakati zilizokuwa mbele yako kwa muda. JPM Ulitakiwa uwe rais 1954
 

Maneno mazito hayo na ndiyo maana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ameanza kivingine ilhali ni CCM . Sababu ni hiyo wanaLumumba mchungaji Peter S. Msigwa anaifafanua na muielewe.

 
Ndiyo hivyo Msigwa anasema huyu Shujaa hana tofauti na Kinjekitile.
 
Mungu mkubwa, kweli Msigwa wewe umesahau ulivyolipiwa faini na JPM na leo hii unaanza kumdhihaki inshaallah Mungu atatenda.
Dhihaka iko wapi hapo sasa! Aliyo yasema Mchungaji Msigwa ni mambo ya kweli na ya msingi sana. Na hata sisi tulishawahi kuyasema humu, tena wakati marehemu akiwa hai! Ya kwamba anaturudisha miaka ya 1970's!

Tukubali tu ukweli! Hayati aliiviruga sana hii nchi kwa misimamo yake mingi ya hovyo na iliyopitwa na wakati. Kuna umuhimu wa Kuurejesha Mchakato wa Katiba Mpya ili tuwe na Katiba inayo endana na maisha halisi ya sasa. Katiba inayotoa usawa kwa vyama vyote, Katiba inayo tambua uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, Katiba itakayo punguza mamlaka ya Rais katika uteuzi, nk.
 
Mashujaa wa leo huvutia, husukuma na kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi zao kwa kutumia maarifa na weledi wa "diplomasia ya kiuchumi" (economic diplomacy)
Mzaha wa diplomasia ya uchumi chini ya utawala wa shujaa mwendazake ulifafanuliwa mapema , wanaLumumba sikia hiyo..
 
Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 09.12.1961.
Zanzibar ilifanya mapinduzi 12.01.1964.
Tanzania ilipata Uhuru tarehe 17.03.2021.
 
NImemsoma mchungaji Msigwa vizuri sana kwenye haya maandishi yake; sina hakika kama mleta uzi ni Msigwa mwenyewe au somebody kanakiri maandishi ya Msigwa na kuyaleta humu; kuna baadi ya maandishi yake nakubaliana nae but kuna mengine sikubaliani nae; nasikitika wachangiaji wenzangu baadhi baada ya kuwasoma, badala ya kujikita kwenye HOJA za Msigwa, wamejikita kwenye kumjadiri Msigwa. Tunakua masikini sana kwa kujadiri msemaji badala ya alichokisema. Tujikite kwenye HOJA badala ya MTOA hoja.
 
Mungu mkubwa, kweli Msigwa wewe umesahau ulivyolipiwa faini na JPM na leo hii unaanza kumdhihaki inshaallah Mungu atatenda.
Kwani alimuomba? Au alifanya kujitafutia sifa. Yan unanishitaki kwa mkono wa kulia halaf unanilipia kwa mkono wa kushoto halaf unataka nikusifu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…