Peter Msigwa: Hayati Magufuli alikuwa shujaa wa kizamani

Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Peter Msigwa - National interest, economic diplomacy, geopolitics
 
Mungu mkubwa, kweli Msigwa wewe umesahau ulivyolipiwa faini na JPM na leo hii unaanza kumdhihaki inshaallah Mungu atatenda.
Mchungaji Peter Simon Msigwa,
Asilimia mia moja nakubaliana nawe. Miaka 60 ya uhuru (Umri wa mzee), bado unasema mabeberu wanahangaika na nchi yetu, basi na huo UHURU tulioupata hauna maana. Kwa lugha rahisi, huo ni kutafuta visingizio kwa kushindwa kabisa kutumia akili alizotujalia Mwenyezi Mungu. Uhuru wa nini kama bado unaishi kwa mashaka. Uhuru ukuweke huru na kujiamini. Maendeleo ya nchi zetu yanadumazwa na viongozi wengi waliodumaa. Tuna kila kitu, tusiendelee kumkufuru Mungu kwa wema, upendo, upendeleo na huruma yake. Ulaya hawana rasilimali za maana lakini bado matajiri tunaomba misaada kwao huku sisi tukibaki kukandamizana kama tuko katika himaya za manyani (mwenye misuli ndiyo atakayeishi). Waafrika tuhame kutoka ukale kwenda dunia ya leo. Utilize the brains of our abundant resource-HUMAN BRAINS, we can easily see the bright light.
 
bwawa la nyerere viongozi wote walishindwa kujenga yeye ameweza kwa pesa za ndani uchaguzi ulifanyika kwa mara ya kwanza kwa pesa za ndani kajenga miundo mbinu nyingi daraja ka busisi kigongo usafiri w ndege vituo vya afya na mambo mwngi na jema zaidi kawakomoa wapinzani kuingia bungeni hilo ndilo msingwa linakuuma maana huna pesa sasa hivi umechakarika ile mbaya nenda kawe nabii wa kuponyesha watu uwadanganye kama wenzio wanapiga pesa
Bwawa lipi limejengwa kwa hela ya ndani, Yan mtu ameikuta nchi inadaiwa trillion 36 miaka 60 toka ipate uhuru, yeye peke yake ndani ya miaka 5 amekopa trillion 23.. amekufa ameacha deni limefika trillion 59! halaf anawadanganya wajinga kama wewe kuwa ametumia kwa pesa za ndani. Idiot! Mbaya zaidi kwa taarifa yako bwawa lenyewe hata nusu halijakamilika.
 
siku zote wanasiasa si watu wa kuwaamini hata kama itatokea mmeoa kwao!
ni watu wa fursa! kibaya zaidi wataalamu wetu wameshindwa kujenga mazingira ya wao kutegemewa na wanasiasa bali wao ndio wanaowategemea wanasiasa na matokeo yake wanatuchezesha nyimbo wanazotaka wao. na kwasababu wameshatujua kuwa sisi ni watu wa malalamiko wa tawala zilizopita basi wataanza na kuzipinga zilizopita ili watulazimishe tuimbe nyimbo tuzizojua na wanazozitaka wao!
lakini zaidi ya yote MUDA sikuzote amekuwa mwalimu mzuri japo anaowafundisha hawaelewi lakini nawasihi tujaribu kutunza maneno yetu kwa kuwa baada ya MUDA si mrefu tutaelewana tu
 
KATIKATI YA MAJONZI:
Ndiyo Nagutuka kuwa Tuliyempoteza ni Shujaa Aliyepitwa na Wakati!

Anaandika Peter Simon Msigwa

Sitaki kuwabishia wale wanaomwita Shujaa. Tofauti yangu na wao ni fikra tu. Kuna fikra za kisasa na fikra za kizamani!

Ukweli ni kwamba Mpendwa wetu JPM alikuwa ni mtawala wa zamani sana aliyejikuta amepata fursa ya kutawala nchi katika zama za sasa. Hakuwa "compatible" na ulimwengu wa leo hata kidogo!

Kwanini nimsingizie? Mifano ipo mingi sana. Nigusie machache:

1. Kwanza, lugha zake za kuita wazungu mabeberu ni lugha za miaka ya hamsini na miaka ya sitini. Ni lugha zilizotumiwa na vijana wa zamani wa kiafrika, akina Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba na wengine wakati wakipigania uhuru wa nchi zao kwenye miaka ile ya 1950's na 1960's.

Kusingizia wazungu kuwa ndio wanaokwamisha uchumi na maendeleo ya Tanzania hasa katika kipindi hichi cha takribani miaka 60 baada ya uhuru ni kukosa maono na kushindwa kujua mahitaji ya sasa, vikwazo vya sasa na namna sahihi ya kukabiliana navyo!

Kutokujua kwake ajenda za kimataifa zinazohusu uchumi na changamoto za dunia, kuliifanya Tanzania ionekane kama kisiwa na kituko duniani!

Kwa hiyo, kwa watu wote ambao walidhani na bado wanadhani tupo kwenye zama hizo, basi JPM ni Shujaa wao! Shida ni moja tu, ni Shujaa aliyepitwa na wakati! Mashujaa wa leo hawapambani tena na Wazungu kwa kususa kupanda ndege za kwenda Ulaya au Marekani kwenye Mikutano ya wakuu wa nchi, wala hawapambani kwa kufokafoka na kutumia lugha mbaya mbaya za kizamani! Mashujaa wa leo huvutia, husukuma na kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi zao kwa kutumia maarifa na weledi wa "diplomasia ya kiuchumi" (economic diplomacy). Kwa uelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi, tafadhali soma hotuba yangu niliyoitoa katika Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 nikiwa Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

2. Pili, uamuzi wake wa kuhimiza matumizi ya "kupiga nyungu" kuliko njia za kisayansi za kupambana na Corona, nao pia ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa kabisa. Shida ni moja tu, ulikuwa ni ushujaa uliopitwa na wakati. Historia inatukumbusha kuwa ushujaa kama huo alishafanyika miaka mingi sana nyuma, enzi zile Mzee wetu Kinjekitile Ngwale alipohamasisha wapiganaji watumie maji katika kukabiliana na risasi za wazungu kwa Imani kuwa risasi zao zingegeuka maji na kutowadhuru. Matokeo ya ushujaa wa Kinjekitile kwenye vita vya maji maji na matokeo ya ushujaa wa JPM kwenye vita ya Corona yote tumeyaona.

3. Tatu, alikuwa ni mtawala aliyekuwa na mamlaka na uhuru wote wa kiserikali ikiwemo kukusanya kodi, kuandaa dira, sera, mipango, bajeti na kutekeleza miradi ya maendeleo. Ajabu, bado eti aliamini wapinzani ndio wanaozuia na kukwamisha maendeleo ya Tanzania! Alipata kusema mbunge anayepinga bajeti ya serikali yake sio mzalendo, jambo ambalo Spika, Naibu Spika na aliyekuwa Waziri wa Fedha walikubaliana naye. Kwake yeye uzalendo ulikuwa na maana moja tu - nayo ni kuunga mkono fikra na maamuzi yote ya Rais! Kila aliyekwenda kinyume naye alishughulikiwa.

Wakati wa utawala wake mambo mengi yaligeuka kichwa chini miguu juu. Kwa mfano, baadhi ya majaji na mahakimu walishindwa kutoa hukumu za haki!

Polisi walitekeleza amri zisizo halali!

Baadhi ya viongozi wa dini walifurahia kuitwa kwenye dhifa za kitaifa na matukio ya kuipigia debe serikali wakisahau wito wao Mkuu wa Kitume!

Wandishi wa habari waliweka kalamu zao chini au walijikuta wakiandika vitu ambavyo nafsi zao ziliwasuta!

Baadhi ya wasanii walikuwa wasanii kweli kweli kwa maana halisi ya neno usanii! Walijua nini Shujaa anataka (sifa). Nao hawakufanya ajizi. Walitumia usanii wao kikamilifu kumpatia kile alichotaka hata kama hakikuwa cha kweli!

Hakika, hichi kilikuwa ni kipindi ambacho ujinga na unafiki vilipewa hadhi kubwa na kuketishwa kwenye kiti cha enzi, huku ukweli na akili vikifukiwa ardhini!

Haikuwa kazi rahisi kuibadili nchi kichwa chini miguu juu kiasi hicho! Kwa hiyo, sitaki kuwa mbishi. Ni kweli alikuwa Shujaa. Shida ni moja tu, alikuwa ni Shujaa aliyepitwa na wakati!

Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Kinyume chake, Mashujaa wa leo hawaongozi tena nchi kwa kulazimisha fikra zao pekee, bali kwa kupokea ukosoaji na ushauri wa kutosha.

Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.

JPM alichelewa sana kuboresha fikra na mitazamo yake ili kuendana na mahitaji ya dunia sasa. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hadi umauti unamfika bado hakuwa amefanikiwa ku- upgrade software yake. Aliendelea kutawala nyuma ya wakati katika kipindi chote cha utawala wake. Kwa maneno mengine alikuwa "the most incompatible and irrelevant ruler of our contemporary world".

Wengine wanamwita Shujaa wa Afrika. Wengine Mtakatifu lakini ukweli usiokufuru ni kwamba JPM alijulikana sana duniani sio kwa umahiri wake, bali kwa kutokujua nini kinaendelea duniani! Matokeo yake akawa kituko, "the world laughing stock"

Utawala wa JPM umetufunza jambo moja kubwa na la msingi sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwamba bado wapo watu wanaofikiri na kuenenda nyuma ya wakati. Tena miongoni mwao bado wapo wanaoweza kupata nafasi kubwa za uongozi hata kwa bahati tu kama alivyopata JPM. Wakipata nafasi hizo basi wanaweza kuirudisha nchi yetu nyuma ya wakati uliopo. Wakatenda mambo yaliyo kinyume na yasiyoendana kabisa na mahitaji ya sasa. Kwa hiyo, tunahitaji Katiba mpya kabisa na iliyo imara sana itakayoweka tunu, mifumo na misingi ya kumdhibiti kiongozi yeyote yule ili asiende nje sana ya matakwa na matarajio ya Taifa.

Tuache uvyama, tuna nchi ya kujenga. Tuandike Katiba Mpya ya kulilinda Taifa letu leo na kesho. Mashujaa wa zamani (kina JPM) bado tunao wengi huku mitaani.Tukifanya mchezo, ipo siku mmoja wa Mashujaa wa aina hii ataukwaa tena urais halafu tutaanza kujuta tena. Walisema Wahenga "Majuto ni Mjukuu mwishowe huja kinyume".

Hakika, tuliyempoteza ni Shujaa aliyepitwa na wakati. Nilipenda aendelee kuwa nasi duniani. Nilipenda abadilike na kuendana na dunia ya sasa. Lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Namshukuru sana kwa kutunyoosha. Namshukuru kwa funzo kubwa alilotuachia, ametupa fursa na namna ya kuimarisha mifumo na misingi ya nchi yetu vizuri. Kabla yake hatukuwahi kuona nyufa zilizopo katika Katiba yetu kiasi hichi! Ametusaidia kuonesha jinsi Taifa letu lilivyo legelege. Ahsante sana. Pumnzika kwa amani John Pombe Magufuli, ewe Shujaa wa Wakati Wako, Mwanahalisi wa Tanzania na Mpiganaji hodari wa Afrika kwa kadri ya fikra za wakati wako.

Ameandika Peter Msigw

Ameandika Peter Msigwa
Yes alikuwa shujaa aliyepitwa na wakati tunahitaji Katiba mpya ili asije jitokeza mwingine akaturudisha nyuma
 
Dunia imejaa Mashujaa wengi waliokufa.!
Hivyo usijaribu kuwa shujaa..!
 
bwawa la nyerere viongozi wote walishindwa kujenga yeye ameweza kwa pesa za ndani uchaguzi ulifanyika kwa mara ya kwanza kwa pesa za ndani kajenga miundo mbinu nyingi daraja ka busisi kigongo usafiri w ndege vituo vya afya na mambo mwngi na jema zaidi kawakomoa wapinzani kuingia bungeni hilo ndilo msingwa linakuuma maana huna pesa sasa hivi umechakarika ile mbaya nenda kawe nabii wa kuponyesha watu uwadanganye kama wenzio wanapiga pesa
Acha ujinga,Miundombinu hakuanza kujenga JPM,Wala hakuna alichofanya cha ajabu,alianzisha miradi mikubwa inayokula pesa nyingi kuriko uwezo wa nchi,mwisho wake akaishia kukopa,Wala sio pesa ya ndani.Deni la Taifa kwa kipindi chake limeongezeka kwa asilimia kubwa kuriko miaka 10 ya Kikwete.
Ameua,amepora,Ili kupata pesa.kila mtu anaweza kukopa na kujenga,sio rocket sayansi.
Tangu amekufa Ndege ngapi zimetua Chato airport?jibu Hili swali ndio utajua jinsi JpM alivyokuwa mtu wa ovyo.
 
Nimeamini Duniani Kuna Wanafiki Wengi , Mchungaji Msigwa Na Hayati Magufuli Walikuwa Na Ka Undugu Kwa Mbali (Mpwa Wa Mchungaji Msigwa Kamuoa Mtoto Wa Hayati Magufuli) Lakini Bado Ana Mponda
 
KATIKATI YA MAJONZI:
Ndiyo Nagutuka kuwa Tuliyempoteza ni Shujaa Aliyepitwa na Wakati!

Anaandika Peter Simon Msigwa

Sitaki kuwabishia wale wanaomwita Shujaa. Tofauti yangu na wao ni fikra tu. Kuna fikra za kisasa na fikra za kizamani!

Ukweli ni kwamba Mpendwa wetu JPM alikuwa ni mtawala wa zamani sana aliyejikuta amepata fursa ya kutawala nchi katika zama za sasa. Hakuwa "compatible" na ulimwengu wa leo hata kidogo!

Kwanini nimsingizie? Mifano ipo mingi sana. Nigusie machache:

1. Kwanza, lugha zake za kuita wazungu mabeberu ni lugha za miaka ya hamsini na miaka ya sitini. Ni lugha zilizotumiwa na vijana wa zamani wa kiafrika, akina Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba na wengine wakati wakipigania uhuru wa nchi zao kwenye miaka ile ya 1950's na 1960's.

Kusingizia wazungu kuwa ndio wanaokwamisha uchumi na maendeleo ya Tanzania hasa katika kipindi hichi cha takribani miaka 60 baada ya uhuru ni kukosa maono na kushindwa kujua mahitaji ya sasa, vikwazo vya sasa na namna sahihi ya kukabiliana navyo!

Kutokujua kwake ajenda za kimataifa zinazohusu uchumi na changamoto za dunia, kuliifanya Tanzania ionekane kama kisiwa na kituko duniani!

Kwa hiyo, kwa watu wote ambao walidhani na bado wanadhani tupo kwenye zama hizo, basi JPM ni Shujaa wao! Shida ni moja tu, ni Shujaa aliyepitwa na wakati! Mashujaa wa leo hawapambani tena na Wazungu kwa kususa kupanda ndege za kwenda Ulaya au Marekani kwenye Mikutano ya wakuu wa nchi, wala hawapambani kwa kufokafoka na kutumia lugha mbaya mbaya za kizamani! Mashujaa wa leo huvutia, husukuma na kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi zao kwa kutumia maarifa na weledi wa "diplomasia ya kiuchumi" (economic diplomacy). Kwa uelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi, tafadhali soma hotuba yangu niliyoitoa katika Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 nikiwa Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

2. Pili, uamuzi wake wa kuhimiza matumizi ya "kupiga nyungu" kuliko njia za kisayansi za kupambana na Corona, nao pia ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa kabisa. Shida ni moja tu, ulikuwa ni ushujaa uliopitwa na wakati. Historia inatukumbusha kuwa ushujaa kama huo alishafanyika miaka mingi sana nyuma, enzi zile Mzee wetu Kinjekitile Ngwale alipohamasisha wapiganaji watumie maji katika kukabiliana na risasi za wazungu kwa Imani kuwa risasi zao zingegeuka maji na kutowadhuru. Matokeo ya ushujaa wa Kinjekitile kwenye vita vya maji maji na matokeo ya ushujaa wa JPM kwenye vita ya Corona yote tumeyaona.

3. Tatu, alikuwa ni mtawala aliyekuwa na mamlaka na uhuru wote wa kiserikali ikiwemo kukusanya kodi, kuandaa dira, sera, mipango, bajeti na kutekeleza miradi ya maendeleo. Ajabu, bado eti aliamini wapinzani ndio wanaozuia na kukwamisha maendeleo ya Tanzania! Alipata kusema mbunge anayepinga bajeti ya serikali yake sio mzalendo, jambo ambalo Spika, Naibu Spika na aliyekuwa Waziri wa Fedha walikubaliana naye. Kwake yeye uzalendo ulikuwa na maana moja tu - nayo ni kuunga mkono fikra na maamuzi yote ya Rais! Kila aliyekwenda kinyume naye alishughulikiwa.

Wakati wa utawala wake mambo mengi yaligeuka kichwa chini miguu juu. Kwa mfano, baadhi ya majaji na mahakimu walishindwa kutoa hukumu za haki!

Polisi walitekeleza amri zisizo halali!

Baadhi ya viongozi wa dini walifurahia kuitwa kwenye dhifa za kitaifa na matukio ya kuipigia debe serikali wakisahau wito wao Mkuu wa Kitume!

Wandishi wa habari waliweka kalamu zao chini au walijikuta wakiandika vitu ambavyo nafsi zao ziliwasuta!

Baadhi ya wasanii walikuwa wasanii kweli kweli kwa maana halisi ya neno usanii! Walijua nini Shujaa anataka (sifa). Nao hawakufanya ajizi. Walitumia usanii wao kikamilifu kumpatia kile alichotaka hata kama hakikuwa cha kweli!

Hakika, hichi kilikuwa ni kipindi ambacho ujinga na unafiki vilipewa hadhi kubwa na kuketishwa kwenye kiti cha enzi, huku ukweli na akili vikifukiwa ardhini!

Haikuwa kazi rahisi kuibadili nchi kichwa chini miguu juu kiasi hicho! Kwa hiyo, sitaki kuwa mbishi. Ni kweli alikuwa Shujaa. Shida ni moja tu, alikuwa ni Shujaa aliyepitwa na wakati!

Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Kinyume chake, Mashujaa wa leo hawaongozi tena nchi kwa kulazimisha fikra zao pekee, bali kwa kupokea ukosoaji na ushauri wa kutosha.

Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.

JPM alichelewa sana kuboresha fikra na mitazamo yake ili kuendana na mahitaji ya dunia sasa. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hadi umauti unamfika bado hakuwa amefanikiwa ku- upgrade software yake. Aliendelea kutawala nyuma ya wakati katika kipindi chote cha utawala wake. Kwa maneno mengine alikuwa "the most incompatible and irrelevant ruler of our contemporary world".

Wengine wanamwita Shujaa wa Afrika. Wengine Mtakatifu lakini ukweli usiokufuru ni kwamba JPM alijulikana sana duniani sio kwa umahiri wake, bali kwa kutokujua nini kinaendelea duniani! Matokeo yake akawa kituko, "the world laughing stock"

Utawala wa JPM umetufunza jambo moja kubwa na la msingi sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwamba bado wapo watu wanaofikiri na kuenenda nyuma ya wakati. Tena miongoni mwao bado wapo wanaoweza kupata nafasi kubwa za uongozi hata kwa bahati tu kama alivyopata JPM. Wakipata nafasi hizo basi wanaweza kuirudisha nchi yetu nyuma ya wakati uliopo. Wakatenda mambo yaliyo kinyume na yasiyoendana kabisa na mahitaji ya sasa. Kwa hiyo, tunahitaji Katiba mpya kabisa na iliyo imara sana itakayoweka tunu, mifumo na misingi ya kumdhibiti kiongozi yeyote yule ili asiende nje sana ya matakwa na matarajio ya Taifa.

Tuache uvyama, tuna nchi ya kujenga. Tuandike Katiba Mpya ya kulilinda Taifa letu leo na kesho. Mashujaa wa zamani (kina JPM) bado tunao wengi huku mitaani.Tukifanya mchezo, ipo siku mmoja wa Mashujaa wa aina hii ataukwaa tena urais halafu tutaanza kujuta tena. Walisema Wahenga "Majuto ni Mjukuu mwishowe huja kinyume".

Hakika, tuliyempoteza ni Shujaa aliyepitwa na wakati. Nilipenda aendelee kuwa nasi duniani. Nilipenda abadilike na kuendana na dunia ya sasa. Lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Namshukuru sana kwa kutunyoosha. Namshukuru kwa funzo kubwa alilotuachia, ametupa fursa na namna ya kuimarisha mifumo na misingi ya nchi yetu vizuri. Kabla yake hatukuwahi kuona nyufa zilizopo katika Katiba yetu kiasi hichi! Ametusaidia kuonesha jinsi Taifa letu lilivyo legelege. Ahsante sana. Pumnzika kwa amani John Pombe Magufuli, ewe Shujaa wa Wakati Wako, Mwanahalisi wa Tanzania na Mpiganaji hodari wa Afrika kwa kadri ya fikra za wakati wako.

Ameandika Peter Msigwa
🤣🤣🤣🤣kwa lugha nyingine ni shujaa mshamba.
 
Acha ujinga,Miundombinu hakuanza kujenga JPM,Wala hakuna alichofanya cha ajabu,alianzisha miradi mikubwa inayokula pesa nyingi kuriko uwezo wa nchi,mwisho wake akaishia kukopa,Wala sio pesa ya ndani.Deni la Taifa kwa kipindi chake limeongezeka kwa asilimia kubwa kuriko miaka 10 ya Kikwete.
Ameua,amepora,Ili kupata pesa.kila mtu anaweza kukopa na kujenga,sio rocket sayansi.
Tangu amekufa Ndege ngapi zimetua Chato airport?jibu Hili swali ndio utajua jinsi JpM alivyokuwa mtu wa ovyo.
Na hakuna hat mradi mmoja uliofikia hatu ya 50% na pesa zimeshaisha.
 
Wewe ndio umesahau. JPM alioeleka faini wakati wananchi walishamlipia, all in all Msigwa kasema ukweli mtupu bila kumung'unya maneno kwa mifano hai. Shujaa wa aliyepitwa na wakati
Yaani wafungwe kwa amri yake then awalipie faini. Magu zilikuwa hazimtoshi.
 
Siasa bwana, juzi tu hapa siku ya mazishi maneno ya Msigwa yalikuwa kinyume na haya yapo kwa hii makala...
 
Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Kinyume chake, Mashujaa wa leo hawaongozi tena nchi kwa kulazimisha fikra zao pekee, bali kwa kupokea ukosoaji na ushauri wa kutosha.

Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.
Shujaa wa CCM wa Afrika mnamnanga sana. Muoneeni huruma basi khaa!
 
Back
Top Bottom