Peter Msigwa: Hayati Magufuli alikuwa shujaa wa kizamani

KATIKATI YA MAJONZI:
Ndiyo Nagutuka kuwa Tuliyempoteza ni Shujaa Aliyepitwa na Wakati!

Anaandika Peter Simon Msigwa

Sitaki kuwabishia wale wanaomwita Shujaa. Tofauti yangu na wao ni fikra tu. Kuna fikra za kisasa na fikra za kizamani!

Ukweli ni kwamba Mpendwa wetu JPM alikuwa ni mtawala wa zamani sana aliyejikuta amepata fursa ya kutawala nchi katika zama za sasa. Hakuwa "compatible" na ulimwengu wa leo hata kidogo!

Kwanini nimsingizie? Mifano ipo mingi sana. Nigusie machache:

1. Kwanza, lugha zake za kuita wazungu mabeberu ni lugha za miaka ya hamsini na miaka ya sitini. Ni lugha zilizotumiwa na vijana wa zamani wa kiafrika, akina Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba na wengine wakati wakipigania uhuru wa nchi zao kwenye miaka ile ya 1950's na 1960's.

Kusingizia wazungu kuwa ndio wanaokwamisha uchumi na maendeleo ya Tanzania hasa katika kipindi hichi cha takribani miaka 60 baada ya uhuru ni kukosa maono na kushindwa kujua mahitaji ya sasa, vikwazo vya sasa na namna sahihi ya kukabiliana navyo!

Kutokujua kwake ajenda za kimataifa zinazohusu uchumi na changamoto za dunia, kuliifanya Tanzania ionekane kama kisiwa na kituko duniani!

Kwa hiyo, kwa watu wote ambao walidhani na bado wanadhani tupo kwenye zama hizo, basi JPM ni Shujaa wao! Shida ni moja tu, ni Shujaa aliyepitwa na wakati! Mashujaa wa leo hawapambani tena na Wazungu kwa kususa kupanda ndege za kwenda Ulaya au Marekani kwenye Mikutano ya wakuu wa nchi, wala hawapambani kwa kufokafoka na kutumia lugha mbaya mbaya za kizamani! Mashujaa wa leo huvutia, husukuma na kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi zao kwa kutumia maarifa na weledi wa "diplomasia ya kiuchumi" (economic diplomacy). Kwa uelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi, tafadhali soma hotuba yangu niliyoitoa katika Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 nikiwa Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

2. Pili, uamuzi wake wa kuhimiza matumizi ya "kupiga nyungu" kuliko njia za kisayansi za kupambana na Corona, nao pia ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa kabisa. Shida ni moja tu, ulikuwa ni ushujaa uliopitwa na wakati. Historia inatukumbusha kuwa ushujaa kama huo alishafanyika miaka mingi sana nyuma, enzi zile Mzee wetu Kinjekitile Ngwale alipohamasisha wapiganaji watumie maji katika kukabiliana na risasi za wazungu kwa Imani kuwa risasi zao zingegeuka maji na kutowadhuru. Matokeo ya ushujaa wa Kinjekitile kwenye vita vya maji maji na matokeo ya ushujaa wa JPM kwenye vita ya Corona yote tumeyaona.

3. Tatu, alikuwa ni mtawala aliyekuwa na mamlaka na uhuru wote wa kiserikali ikiwemo kukusanya kodi, kuandaa dira, sera, mipango, bajeti na kutekeleza miradi ya maendeleo. Ajabu, bado eti aliamini wapinzani ndio wanaozuia na kukwamisha maendeleo ya Tanzania! Alipata kusema mbunge anayepinga bajeti ya serikali yake sio mzalendo, jambo ambalo Spika, Naibu Spika na aliyekuwa Waziri wa Fedha walikubaliana naye. Kwake yeye uzalendo ulikuwa na maana moja tu - nayo ni kuunga mkono fikra na maamuzi yote ya Rais! Kila aliyekwenda kinyume naye alishughulikiwa.

Wakati wa utawala wake mambo mengi yaligeuka kichwa chini miguu juu. Kwa mfano, baadhi ya majaji na mahakimu walishindwa kutoa hukumu za haki!

Polisi walitekeleza amri zisizo halali!

Baadhi ya viongozi wa dini walifurahia kuitwa kwenye dhifa za kitaifa na matukio ya kuipigia debe serikali wakisahau wito wao Mkuu wa Kitume!

Wandishi wa habari waliweka kalamu zao chini au walijikuta wakiandika vitu ambavyo nafsi zao ziliwasuta!

Baadhi ya wasanii walikuwa wasanii kweli kweli kwa maana halisi ya neno usanii! Walijua nini Shujaa anataka (sifa). Nao hawakufanya ajizi. Walitumia usanii wao kikamilifu kumpatia kile alichotaka hata kama hakikuwa cha kweli!

Hakika, hichi kilikuwa ni kipindi ambacho ujinga na unafiki vilipewa hadhi kubwa na kuketishwa kwenye kiti cha enzi, huku ukweli na akili vikifukiwa ardhini!

Haikuwa kazi rahisi kuibadili nchi kichwa chini miguu juu kiasi hicho! Kwa hiyo, sitaki kuwa mbishi. Ni kweli alikuwa Shujaa. Shida ni moja tu, alikuwa ni Shujaa aliyepitwa na wakati!

Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Kinyume chake, Mashujaa wa leo hawaongozi tena nchi kwa kulazimisha fikra zao pekee, bali kwa kupokea ukosoaji na ushauri wa kutosha.

Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.

JPM alichelewa sana kuboresha fikra na mitazamo yake ili kuendana na mahitaji ya dunia sasa. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hadi umauti unamfika bado hakuwa amefanikiwa ku- upgrade software yake. Aliendelea kutawala nyuma ya wakati katika kipindi chote cha utawala wake. Kwa maneno mengine alikuwa "the most incompatible and irrelevant ruler of our contemporary world".

Wengine wanamwita Shujaa wa Afrika. Wengine Mtakatifu lakini ukweli usiokufuru ni kwamba JPM alijulikana sana duniani sio kwa umahiri wake, bali kwa kutokujua nini kinaendelea duniani! Matokeo yake akawa kituko, "the world laughing stock"

Utawala wa JPM umetufunza jambo moja kubwa na la msingi sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwamba bado wapo watu wanaofikiri na kuenenda nyuma ya wakati. Tena miongoni mwao bado wapo wanaoweza kupata nafasi kubwa za uongozi hata kwa bahati tu kama alivyopata JPM. Wakipata nafasi hizo basi wanaweza kuirudisha nchi yetu nyuma ya wakati uliopo. Wakatenda mambo yaliyo kinyume na yasiyoendana kabisa na mahitaji ya sasa. Kwa hiyo, tunahitaji Katiba mpya kabisa na iliyo imara sana itakayoweka tunu, mifumo na misingi ya kumdhibiti kiongozi yeyote yule ili asiende nje sana ya matakwa na matarajio ya Taifa.

Tuache uvyama, tuna nchi ya kujenga. Tuandike Katiba Mpya ya kulilinda Taifa letu leo na kesho. Mashujaa wa zamani (kina JPM) bado tunao wengi huku mitaani.Tukifanya mchezo, ipo siku mmoja wa Mashujaa wa aina hii ataukwaa tena urais halafu tutaanza kujuta tena. Walisema Wahenga "Majuto ni Mjukuu mwishowe huja kinyume".

Hakika, tuliyempoteza ni Shujaa aliyepitwa na wakati. Nilipenda aendelee kuwa nasi duniani. Nilipenda abadilike na kuendana na dunia ya sasa. Lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Namshukuru sana kwa kutunyoosha. Namshukuru kwa funzo kubwa alilotuachia, ametupa fursa na namna ya kuimarisha mifumo na misingi ya nchi yetu vizuri. Kabla yake hatukuwahi kuona nyufa zilizopo katika Katiba yetu kiasi hichi! Ametusaidia kuonesha jinsi Taifa letu lilivyo legelege. Ahsante sana. Pumnzika kwa amani John Pombe Magufuli, ewe Shujaa wa Wakati Wako, Mwanahalisi wa Tanzania na Mpiganaji hodari wa Afrika kwa kadri ya fikra za wakati wako.

Ameandika Peter Msigwa
Msigwa hivi ukinyamaza utakuwa umepungukiwa nini. Eti bwana Msigwa, jaribu kujiheshimu mkuu hata kama siasa ni mihemko sasa hiyo imepitiliza. Hivi watanzania wanaweza kukuelewa hayo unayoyasema. Wewe umesaidia lipi katika Taifa hili zaidi ya porojo tu. Mwenzako kafanya kazi kwa bidii katika awamu yake kajenga madaraja kibao, kanunua ndege ninyi kazi kupiga porojo tu hapo bungeni.
 
Mungu mkubwa, kweli Msigwa wewe umesahau ulivyolipiwa faini na JPM na leo hii unaanza kumdhihaki inshaallah Mungu atatenda.
Kulipiwa faini kuna husikaje na mada,hata hivyo kesi za kipuuzi ambazo chanzo chake ni ukinzani wa mawazo ya mtu aliyeamini zama za kale
 
Msigwa hivi ukinyamaza utakuwa umepungukiwa nini. Eti bwana Msigwa, jaribu kujiheshimu mkuu hata kama siasa ni mihemko sasa hiyo imepitiliza. Hivi watanzania wanaweza kukuelewa hayo unayoyasema. Wewe umesaidia lipi katika Taifa hili zaidi ya porojo tu. Mwenzako kafanya kazi kwa bidii katika awamu yake kajenga madaraja kibao, kanunua ndege ninyi kazi kupiga porojo tu hapo bungeni.
Ushapata taarifa juu ya hasara iliyosababishwa na ndege hizo?.
 
John mbatizaji acha kuzingua, ila kama unataka u DC endelea, mama anasoma mitandao ya kijamii mpaka usiku ila usisahau kuweka namba za simu na email address . sasa hivi akili za watu zinarudi taraaaaatibu, mpaka mwaka huu ukiisha wale ambao ubongo wao ulitolewa watakuwa wamerudishiwa mfano kuna mmoja sasa hivi yuko operation theatre anarudishiwa kidogo na ameanza kupata nafuu mpaka ametamka nyungu hazifai. halafu wengine hatumjui asas ni nani mtu huyo?
Pasco Mayala ameshapona asante mungu
 
kama tukianza kuhesabu matendo ya wema ambayo madikteta jamii ya jiwe waliyafanya kwa raia mmoja mmoja, basi mobutu seseko na iddi amini walitenda mema zaidi kuliko huyo mtukufu wenu. na bado mpaka leo dunia inawapiga spana.

ukweli ni kwamba, mabaya mengi waliyoyafanya yanafuta mema yote waliyoyafanya kwa mtu mmoja mmoja. hivyo basi usimlaumu msigwa kwa kumuelezea jiwe licha ya kwamba alimlipia faini.

NB: tukumbushe kuhusu hilo tukio zima la faini na nani alisababisha.
Msigwa anaulilia ubunge wake. Ulivyomchoropoka hakuamini macho yake. Mchungaji gani anakosa maadili ya kidini mpaka kufikia kumsema marehemu.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
KATIKATI YA MAJONZI:
Ndiyo Nagutuka kuwa Tuliyempoteza ni Shujaa Aliyepitwa na Wakati!

Anaandika Peter Simon Msigwa

Sitaki kuwabishia wale wanaomwita Shujaa. Tofauti yangu na wao ni fikra tu. Kuna fikra za kisasa na fikra za kizamani!

Ukweli ni kwamba Mpendwa wetu JPM alikuwa ni mtawala wa zamani sana aliyejikuta amepata fursa ya kutawala nchi katika zama za sasa. Hakuwa "compatible" na ulimwengu wa leo hata kidogo!

Kwanini nimsingizie? Mifano ipo mingi sana. Nigusie machache:

1. Kwanza, lugha zake za kuita wazungu mabeberu ni lugha za miaka ya hamsini na miaka ya sitini. Ni lugha zilizotumiwa na vijana wa zamani wa kiafrika, akina Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba na wengine wakati wakipigania uhuru wa nchi zao kwenye miaka ile ya 1950's na 1960's.

Kusingizia wazungu kuwa ndio wanaokwamisha uchumi na maendeleo ya Tanzania hasa katika kipindi hichi cha takribani miaka 60 baada ya uhuru ni kukosa maono na kushindwa kujua mahitaji ya sasa, vikwazo vya sasa na namna sahihi ya kukabiliana navyo!

Kutokujua kwake ajenda za kimataifa zinazohusu uchumi na changamoto za dunia, kuliifanya Tanzania ionekane kama kisiwa na kituko duniani!

Kwa hiyo, kwa watu wote ambao walidhani na bado wanadhani tupo kwenye zama hizo, basi JPM ni Shujaa wao! Shida ni moja tu, ni Shujaa aliyepitwa na wakati! Mashujaa wa leo hawapambani tena na Wazungu kwa kususa kupanda ndege za kwenda Ulaya au Marekani kwenye Mikutano ya wakuu wa nchi, wala hawapambani kwa kufokafoka na kutumia lugha mbaya mbaya za kizamani! Mashujaa wa leo huvutia, husukuma na kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi zao kwa kutumia maarifa na weledi wa "diplomasia ya kiuchumi" (economic diplomacy). Kwa uelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi, tafadhali soma hotuba yangu niliyoitoa katika Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 nikiwa Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

2. Pili, uamuzi wake wa kuhimiza matumizi ya "kupiga nyungu" kuliko njia za kisayansi za kupambana na Corona, nao pia ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa kabisa. Shida ni moja tu, ulikuwa ni ushujaa uliopitwa na wakati. Historia inatukumbusha kuwa ushujaa kama huo alishafanyika miaka mingi sana nyuma, enzi zile Mzee wetu Kinjekitile Ngwale alipohamasisha wapiganaji watumie maji katika kukabiliana na risasi za wazungu kwa Imani kuwa risasi zao zingegeuka maji na kutowadhuru. Matokeo ya ushujaa wa Kinjekitile kwenye vita vya maji maji na matokeo ya ushujaa wa JPM kwenye vita ya Corona yote tumeyaona.

3. Tatu, alikuwa ni mtawala aliyekuwa na mamlaka na uhuru wote wa kiserikali ikiwemo kukusanya kodi, kuandaa dira, sera, mipango, bajeti na kutekeleza miradi ya maendeleo. Ajabu, bado eti aliamini wapinzani ndio wanaozuia na kukwamisha maendeleo ya Tanzania! Alipata kusema mbunge anayepinga bajeti ya serikali yake sio mzalendo, jambo ambalo Spika, Naibu Spika na aliyekuwa Waziri wa Fedha walikubaliana naye. Kwake yeye uzalendo ulikuwa na maana moja tu - nayo ni kuunga mkono fikra na maamuzi yote ya Rais! Kila aliyekwenda kinyume naye alishughulikiwa.

Wakati wa utawala wake mambo mengi yaligeuka kichwa chini miguu juu. Kwa mfano, baadhi ya majaji na mahakimu walishindwa kutoa hukumu za haki!

Polisi walitekeleza amri zisizo halali!

Baadhi ya viongozi wa dini walifurahia kuitwa kwenye dhifa za kitaifa na matukio ya kuipigia debe serikali wakisahau wito wao Mkuu wa Kitume!

Wandishi wa habari waliweka kalamu zao chini au walijikuta wakiandika vitu ambavyo nafsi zao ziliwasuta!

Baadhi ya wasanii walikuwa wasanii kweli kweli kwa maana halisi ya neno usanii! Walijua nini Shujaa anataka (sifa). Nao hawakufanya ajizi. Walitumia usanii wao kikamilifu kumpatia kile alichotaka hata kama hakikuwa cha kweli!

Hakika, hichi kilikuwa ni kipindi ambacho ujinga na unafiki vilipewa hadhi kubwa na kuketishwa kwenye kiti cha enzi, huku ukweli na akili vikifukiwa ardhini!

Haikuwa kazi rahisi kuibadili nchi kichwa chini miguu juu kiasi hicho! Kwa hiyo, sitaki kuwa mbishi. Ni kweli alikuwa Shujaa. Shida ni moja tu, alikuwa ni Shujaa aliyepitwa na wakati!

Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Kinyume chake, Mashujaa wa leo hawaongozi tena nchi kwa kulazimisha fikra zao pekee, bali kwa kupokea ukosoaji na ushauri wa kutosha.

Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.

JPM alichelewa sana kuboresha fikra na mitazamo yake ili kuendana na mahitaji ya dunia sasa. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hadi umauti unamfika bado hakuwa amefanikiwa ku- upgrade software yake. Aliendelea kutawala nyuma ya wakati katika kipindi chote cha utawala wake. Kwa maneno mengine alikuwa "the most incompatible and irrelevant ruler of our contemporary world".

Wengine wanamwita Shujaa wa Afrika. Wengine Mtakatifu lakini ukweli usiokufuru ni kwamba JPM alijulikana sana duniani sio kwa umahiri wake, bali kwa kutokujua nini kinaendelea duniani! Matokeo yake akawa kituko, "the world laughing stock"

Utawala wa JPM umetufunza jambo moja kubwa na la msingi sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwamba bado wapo watu wanaofikiri na kuenenda nyuma ya wakati. Tena miongoni mwao bado wapo wanaoweza kupata nafasi kubwa za uongozi hata kwa bahati tu kama alivyopata JPM. Wakipata nafasi hizo basi wanaweza kuirudisha nchi yetu nyuma ya wakati uliopo. Wakatenda mambo yaliyo kinyume na yasiyoendana kabisa na mahitaji ya sasa. Kwa hiyo, tunahitaji Katiba mpya kabisa na iliyo imara sana itakayoweka tunu, mifumo na misingi ya kumdhibiti kiongozi yeyote yule ili asiende nje sana ya matakwa na matarajio ya Taifa.

Tuache uvyama, tuna nchi ya kujenga. Tuandike Katiba Mpya ya kulilinda Taifa letu leo na kesho. Mashujaa wa zamani (kina JPM) bado tunao wengi huku mitaani.Tukifanya mchezo, ipo siku mmoja wa Mashujaa wa aina hii ataukwaa tena urais halafu tutaanza kujuta tena. Walisema Wahenga "Majuto ni Mjukuu mwishowe huja kinyume".

Hakika, tuliyempoteza ni Shujaa aliyepitwa na wakati. Nilipenda aendelee kuwa nasi duniani. Nilipenda abadilike na kuendana na dunia ya sasa. Lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Namshukuru sana kwa kutunyoosha. Namshukuru kwa funzo kubwa alilotuachia, ametupa fursa na namna ya kuimarisha mifumo na misingi ya nchi yetu vizuri. Kabla yake hatukuwahi kuona nyufa zilizopo katika Katiba yetu kiasi hichi! Ametusaidia kuonesha jinsi Taifa letu lilivyo legelege. Ahsante sana. Pumnzika kwa amani John Pombe Magufuli, ewe Shujaa wa Wakati Wako, Mwanahalisi wa Tanzania na Mpiganaji hodari wa Afrika kwa kadri ya fikra za wakati wako.

Ameandika Peter Msigwa
Arobain bado

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Huyu naye atuambie ushujaa wake wa kidigitali na kisasa Chadema iko wapi leo? Aendelee na utumishi wake wa Mbwamwitu aliye vaa ngozi ya kondoo atuondokee hapa!
Ndiyo Chama kilichoibua maovu mengi ya Serikali ya maCCM. Halafu jiulize aliyesababisha kiwe hapa kilipo ni nani na sasa hivi yuko wapi?

Mbweha jike usiye na uzazi wewe!
 
Mtifuano wa kambi ya Lowassa na Membe.
Huwa najiuliza, hivi JPM aliwezaje kupita mchuujo wa 2015?? je kulikuwa na proper vetting ya kumpata mgombea Uraisi??

Je Ccm hawakuona mgombea mwingine anayeijua nchi vizuri tofauti na JPM??

Na je JPM aliwezaje kuwafunga midono Wana ccm wote, viongozi wastafu , na taasisi zote zikatii na kufuata mawazo yake??

Huyu kweli alikuwa ni shujaaa wa karne ya zamani, aliyetawala katika kipindi Cha karne ya Sasa
 
See mwambieni msigwa na wapinzani woote kwa sasa tunahitaji mikakati ya kuing'oa ccm madarakani na sio kumsifia aliyepo na kumponda mwenda zake

Msisahau hata huyu naye ni ccm hivyo hawezi kukaa hapo kwa maslahi ya upinzani
CCM inatawala milele Tanzania. Kila wakati wanakuja strategy ya ku counter analysis ya utawala uliopita then zile changamoto wanazifanya ndo vipaumbele vyao. Matokeo yake wanakomba wafuasi unakua mtaji wao wa kura. Kikwete alikuja na swaga zake, wakati anaondoka hakuna aliemtaka na CCM ilipata shida sana kwenye uchaguzi. Ikabidi wampe JPM the game changer. Alisahihisha makosa yote ya Kikwete. Lakini ndo hivyo changamoto huwa hazikosekani kwa binadamu. Sasa mama Samia anadeal na changamoto za magu. Upinzani hawajui watoke na swaga gani? Zaidi ya kucheza ngoma wasioijua.
 
KATIKATI YA MAJONZI:
Ndiyo Nagutuka kuwa Tuliyempoteza ni Shujaa Aliyepitwa na Wakati!

Anaandika Peter Simon Msigwa

Sitaki kuwabishia wale wanaomwita Shujaa. Tofauti yangu na wao ni fikra tu. Kuna fikra za kisasa na fikra za kizamani!

Ukweli ni kwamba Mpendwa wetu JPM alikuwa ni mtawala wa zamani sana aliyejikuta amepata fursa ya kutawala nchi katika zama za sasa. Hakuwa "compatible" na ulimwengu wa leo hata kidogo!

Kwanini nimsingizie? Mifano ipo mingi sana. Nigusie machache:

1. Kwanza, lugha zake za kuita wazungu mabeberu ni lugha za miaka ya hamsini na miaka ya sitini. Ni lugha zilizotumiwa na vijana wa zamani wa kiafrika, akina Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba na wengine wakati wakipigania uhuru wa nchi zao kwenye miaka ile ya 1950's na 1960's.

Kusingizia wazungu kuwa ndio wanaokwamisha uchumi na maendeleo ya Tanzania hasa katika kipindi hichi cha takribani miaka 60 baada ya uhuru ni kukosa maono na kushindwa kujua mahitaji ya sasa, vikwazo vya sasa na namna sahihi ya kukabiliana navyo!

Kutokujua kwake ajenda za kimataifa zinazohusu uchumi na changamoto za dunia, kuliifanya Tanzania ionekane kama kisiwa na kituko duniani!

Kwa hiyo, kwa watu wote ambao walidhani na bado wanadhani tupo kwenye zama hizo, basi JPM ni Shujaa wao! Shida ni moja tu, ni Shujaa aliyepitwa na wakati! Mashujaa wa leo hawapambani tena na Wazungu kwa kususa kupanda ndege za kwenda Ulaya au Marekani kwenye Mikutano ya wakuu wa nchi, wala hawapambani kwa kufokafoka na kutumia lugha mbaya mbaya za kizamani! Mashujaa wa leo huvutia, husukuma na kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi zao kwa kutumia maarifa na weledi wa "diplomasia ya kiuchumi" (economic diplomacy). Kwa uelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi, tafadhali soma hotuba yangu niliyoitoa katika Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 nikiwa Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

2. Pili, uamuzi wake wa kuhimiza matumizi ya "kupiga nyungu" kuliko njia za kisayansi za kupambana na Corona, nao pia ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa kabisa. Shida ni moja tu, ulikuwa ni ushujaa uliopitwa na wakati. Historia inatukumbusha kuwa ushujaa kama huo alishafanyika miaka mingi sana nyuma, enzi zile Mzee wetu Kinjekitile Ngwale alipohamasisha wapiganaji watumie maji katika kukabiliana na risasi za wazungu kwa Imani kuwa risasi zao zingegeuka maji na kutowadhuru. Matokeo ya ushujaa wa Kinjekitile kwenye vita vya maji maji na matokeo ya ushujaa wa JPM kwenye vita ya Corona yote tumeyaona.

3. Tatu, alikuwa ni mtawala aliyekuwa na mamlaka na uhuru wote wa kiserikali ikiwemo kukusanya kodi, kuandaa dira, sera, mipango, bajeti na kutekeleza miradi ya maendeleo. Ajabu, bado eti aliamini wapinzani ndio wanaozuia na kukwamisha maendeleo ya Tanzania! Alipata kusema mbunge anayepinga bajeti ya serikali yake sio mzalendo, jambo ambalo Spika, Naibu Spika na aliyekuwa Waziri wa Fedha walikubaliana naye. Kwake yeye uzalendo ulikuwa na maana moja tu - nayo ni kuunga mkono fikra na maamuzi yote ya Rais! Kila aliyekwenda kinyume naye alishughulikiwa.

Wakati wa utawala wake mambo mengi yaligeuka kichwa chini miguu juu. Kwa mfano, baadhi ya majaji na mahakimu walishindwa kutoa hukumu za haki!

Polisi walitekeleza amri zisizo halali!

Baadhi ya viongozi wa dini walifurahia kuitwa kwenye dhifa za kitaifa na matukio ya kuipigia debe serikali wakisahau wito wao Mkuu wa Kitume!

Wandishi wa habari waliweka kalamu zao chini au walijikuta wakiandika vitu ambavyo nafsi zao ziliwasuta!

Baadhi ya wasanii walikuwa wasanii kweli kweli kwa maana halisi ya neno usanii! Walijua nini Shujaa anataka (sifa). Nao hawakufanya ajizi. Walitumia usanii wao kikamilifu kumpatia kile alichotaka hata kama hakikuwa cha kweli!

Hakika, hichi kilikuwa ni kipindi ambacho ujinga na unafiki vilipewa hadhi kubwa na kuketishwa kwenye kiti cha enzi, huku ukweli na akili vikifukiwa ardhini!

Haikuwa kazi rahisi kuibadili nchi kichwa chini miguu juu kiasi hicho! Kwa hiyo, sitaki kuwa mbishi. Ni kweli alikuwa Shujaa. Shida ni moja tu, alikuwa ni Shujaa aliyepitwa na wakati!

Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Kinyume chake, Mashujaa wa leo hawaongozi tena nchi kwa kulazimisha fikra zao pekee, bali kwa kupokea ukosoaji na ushauri wa kutosha.

Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.

JPM alichelewa sana kuboresha fikra na mitazamo yake ili kuendana na mahitaji ya dunia sasa. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hadi umauti unamfika bado hakuwa amefanikiwa ku- upgrade software yake. Aliendelea kutawala nyuma ya wakati katika kipindi chote cha utawala wake. Kwa maneno mengine alikuwa "the most incompatible and irrelevant ruler of our contemporary world".

Wengine wanamwita Shujaa wa Afrika. Wengine Mtakatifu lakini ukweli usiokufuru ni kwamba JPM alijulikana sana duniani sio kwa umahiri wake, bali kwa kutokujua nini kinaendelea duniani! Matokeo yake akawa kituko, "the world laughing stock"

Utawala wa JPM umetufunza jambo moja kubwa na la msingi sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwamba bado wapo watu wanaofikiri na kuenenda nyuma ya wakati. Tena miongoni mwao bado wapo wanaoweza kupata nafasi kubwa za uongozi hata kwa bahati tu kama alivyopata JPM. Wakipata nafasi hizo basi wanaweza kuirudisha nchi yetu nyuma ya wakati uliopo. Wakatenda mambo yaliyo kinyume na yasiyoendana kabisa na mahitaji ya sasa. Kwa hiyo, tunahitaji Katiba mpya kabisa na iliyo imara sana itakayoweka tunu, mifumo na misingi ya kumdhibiti kiongozi yeyote yule ili asiende nje sana ya matakwa na matarajio ya Taifa.

Tuache uvyama, tuna nchi ya kujenga. Tuandike Katiba Mpya ya kulilinda Taifa letu leo na kesho. Mashujaa wa zamani (kina JPM) bado tunao wengi huku mitaani.Tukifanya mchezo, ipo siku mmoja wa Mashujaa wa aina hii ataukwaa tena urais halafu tutaanza kujuta tena. Walisema Wahenga "Majuto ni Mjukuu mwishowe huja kinyume".

Hakika, tuliyempoteza ni Shujaa aliyepitwa na wakati. Nilipenda aendelee kuwa nasi duniani. Nilipenda abadilike na kuendana na dunia ya sasa. Lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Namshukuru sana kwa kutunyoosha. Namshukuru kwa funzo kubwa alilotuachia, ametupa fursa na namna ya kuimarisha mifumo na misingi ya nchi yetu vizuri. Kabla yake hatukuwahi kuona nyufa zilizopo katika Katiba yetu kiasi hichi! Ametusaidia kuonesha jinsi Taifa letu lilivyo legelege. Ahsante sana. Pumnzika kwa amani John Pombe Magufuli, ewe Shujaa wa Wakati Wako, Mwanahalisi wa Tanzania na Mpiganaji hodari wa Afrika kwa kadri ya fikra za wakati wako.

Ameandika Peter Msigwa
Mbona kumsema hivyo baba mkwe wa mpwa wako...kulikoni[emoji848]
 
Mungu mkubwa, kweli Msigwa wewe umesahau ulivyolipiwa faini na JPM na leo hii unaanza kumdhihaki inshaallah Mungu atatenda.
Weka kumbukumbu zako sawa alilipiwa ili baadae ahamie ccm lkn akagoma, atakuja kujitetea mwenyewe
 
Mungu mkubwa, kweli Msigwa wewe umesahau ulivyolipiwa faini na JPM na leo hii unaanza kumdhihaki inshaallah Mungu atatenda.
Alimlipia faini kwa sababu ni family member....mtoto wa magu kamuoa mtoto wa dadake msigwa
 
Namshukuru kwa funzo kubwa alilotuachia, ametupa fursa na namna ya kuimarisha mifumo na misingi ya nchi yetu vizuri. Kabla yake hatukuwahi kuona nyufa zilizopo katika Katiba yetu kiasi hichi! Ametusaidia kuonesha jinsi Taifa letu lilivyo legelege.

Maneno haya yanaonyesha jinsi Mchungaji Peter Msigwa alivyokuwa juha, anamkandia Magu na huku anamsifia!!!
 
Back
Top Bottom