Pre GE2025 Peter Msigwa: Kuna tofauti kubwa kati ya kulinda chama na kumlinda mtu

Pre GE2025 Peter Msigwa: Kuna tofauti kubwa kati ya kulinda chama na kumlinda mtu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Erythrocyte huyu vipi? mbona anatia kinyaaa? Ataivuruga chadema. Nimeandika humu kuwa muda huu si wa kupambana wenyewe kwa wenyewe. Haya mambo yawe internal politics na si kadamnasi. Mdhibitini


Muache aongee huu uoga ndo unafanya CDM na CCM kiwe chama kimoja
 
Mbowe analinda chama cha baba mkwe, hicho chama ni Mali ya familia. Mbowe hawezi kukubali chama kitoke nje ya misingi ya kifamilia.
 
Mchungaji Peter Msigwa ameendelea kurusha jiwe gizani.

Safari hii anawapa somo vijana walioingia juzi kwenye siasa wajue tofauti ya chama na mtu.

Siku si nyingi chama cha familia kitamrushia virago.

--
“Kuna tofouti kubwa kati ya kukilinda chama na kumlinda mtu, Kukipinga chama na kumpinga mtu Chama kina misingi na malengo ya kuanzishwa . Mtu yeyote anayejaribu kwenda kinyume na misingi na malengo ya chama atapingwa kwa nguvu zote tena hadharani.” Kuanzia msingi Mpaka Taifa”

Sugu kakubwaga unakimbilia kumlaumu Mbowe,uliposhinda hapakuwa na lawama.
 
Kiongozi hubeba maono

Kiranja hubeba maagizo

Mbowe ndiye mgombea Urais wa JMT kupitia Chadema aliyepata kura chache
1. Samia anabeba maono gani?
2. Kura chache ni relative, at what time and the like!
3. Unadhani kwenye fair election samia atamzidi Mbowe?
 
CDM ni chama cha Mbowe ukienda kinyume nae utaondoshwa tu na utaitwa msaliti.
Oooh .. Kumbe wanatumia Mode ya Kenya...ODM-Odinga+ Luos , Jubilee - Kenyatta+ Kikuyus, Wiper - Kalonzo+Kambas and UDA -Ruto+ Kalenjins
 
1. Samia anabeba maono gani?
2. Kura chache ni relative, at what time and the like!
3. Unadhani kwenye fair election samia atamzidi Mbowe?
Mbowe hamuwezi Samia katika angle zote

Kwa sababu una akili kiduchu hujui kwamba kwa sasa Freeman ni sawa na Kuku aliyefungwa kamba mguuni 😂😂

Wanaotaka kumpumzisha Mangi hapo Ufipa st wameona mbali
 
Mbowe awe na hekima awaachie wengine chama. Demokrasia gani mtu yupo mwenyekiti miaka nenda rudi.
 
Kuliko kuwa kenge kwenye msafara wa mamba ,so Bora ungeanzisha chama chako na utaungwa mkono na wenye moyo was kukuunga mkono!!?

Mbona zito anapeta tu kule na anamoango wa kuwa Rais 2030!
Msigwa ameongea vizuri. Lakini angeweza kuboresha vizuri kauli yake:

Kuna tofauti kubwa ya kukipinga chama na kumpinga mtu.

Na kuna tofauti kubwa ya kumpinga mtu na kuyapinga mawazo au matakwa ya mtu.

Mawazo kinzani ndani ya taasisi yoyote, ni afya ya hiyo taasisi, na ndiyo faida ya kuwa wengi katika taasisi husika.

Na kutofautiana mawazo ndani ya vyama haimaanishi ni ugomvi, wala kuondoka katika chama. Mtu anaweza kuondoka kwenye chama endapo falsafa ya chama imebadilika, na mhusika hakubaliani na hiyo falsafa mpya.
 
Back
Top Bottom