Pre GE2025 Peter Msigwa: Kuna tofauti kubwa kati ya kulinda chama na kumlinda mtu

Pre GE2025 Peter Msigwa: Kuna tofauti kubwa kati ya kulinda chama na kumlinda mtu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Shida ya Msigwa ni nini?
Yeye angesubiri Ubunge apendekezwe kuwakilisha jimbo la Iringa tena.
 
CHADEMA Mali ya nani?
Katiba inasemaje kuhusu michakato ya kupata viongozi?
Nani anastahili kuwa kiongozi?
Kukitumikia chama lazima kuwa kiongozi?
Kwa nini Zengwe kipindi hiki?
 
Mchungaji Peter Msigwa ameendelea kurusha jiwe gizani.

Safari hii anawapa somo vijana walioingia juzi kwenye siasa wajue tofauti ya chama na mtu.

Siku si nyingi chama cha familia kitamrushia virago.

--
“Kuna tofouti kubwa kati ya kukilinda chama na kumlinda mtu, Kukipinga chama na kumpinga mtu Chama kina misingi na malengo ya kuanzishwa . Mtu yeyote anayejaribu kwenda kinyume na misingi na malengo ya chama atapingwa kwa nguvu zote tena hadharani.” Kuanzia msingi Mpaka Taifa”

Msingwa kama ana amini Chadema imepoteza msingi na malengo ya kuanzishwa kwake,

na ikiwa ni mwanasiasa makini mwenye nguvu, hapaswi kubabaiki na kuhamishia vita ya hiyo na kupambana na mtu.

ni ma anang'atuke kwenda chama kingine ama anajitokeze hadharini bila mafumbo wala kificho kuhubiri misingi na malengo ya chama hicho ilivyo vurugwa na kumtaja alieiivuruga na kuidhoofisha misingi hiyo na aseme na yeye alikua wap wakati huo 🐒

kubwekabweka pembeni kwa vijembe na nahau ni mihemko na ghadhabu za kushindwa uchaguzi zenye sura na dalili za hofu na woga wa kupambana 🐒
 
Msingwa; huwezi kushindana na CDM cha msingi tunakushauri achana na hii kitu, upumzike kwa sasa.

Mawe gizani hayatakisaidia kitu, kira hazikutosha ndugu.
Kati ya watu nilikuwa naona hawana akili vizuri ni huyu Msigwa kwa sababu aliwai lidanganya taifa na baadae akasema na yeye alidanganywa na mpenyeza taharifa kuhusu ishu Ya kinana Kuua Tembo(aliingiwa na Uoga)....Ila swala la Chadema kutumia Pesa kuwaonga wanachama wampigie Sugu kura ashinde dhidi ya Msigwa nimeshangaa sana...Sugu alishasaliti chama akata Hamia ccm hawamu ile ya JPM,so tuunganishe dot hapo wadau.
 
Ni haki ya Msigwa kutofautiana na uongozi wa chama chake. Hakuanza leo. Wakati wenzake wanawatetea wamasai wa Ngorongoro yeye aliunga mkono bila kificho uamuzi wa serikali wa kuwatoa katika hifadhi. Kwenye hili la uchaguzi ameishasema kuwa amekata rufaa sasa haya mashambulizi binafsi sijui yanasababishwa na nini! Kama anaona kuna kiongozi haendani na miongozo ya chama chake alipaswa kumalizana nae kwenye vikao vya chama chake. Huko akiona hatendewi haki basi atakuwa na haki ya kujitoa au kushindania nafasi ya juu ya uongozi. Anachokifanya sasa hakina afya kwa chama ambacho anasema anakitetea. Pamoja na hayo, sidhani kama atafukuzwa ila atajitoa kama walivyofanya wengine na kumwaga shutuma kuwa Mwenyekiti alikuwa hamtaki! Kwa kweli anajiharibia. Amuige mwenzake Heche ambae alikosa Uenyekiti lakini akaendelea kuwa mwanachama mtiifu. Kama hakuridhika alimalizana na wenzie ndani ya chama.

Amandla...
 
Amalizane kwenye vikao gani na yeye kwa sasa ni mwanachama wa kawaida Hana uongozi wowote?
Anaweza kuongea tu hadharani Hana uongozi tena na anasema alituma barua hazijibiwi afanyaje?
 
Amalizane kwenye vikao gani na yeye kwa sasa ni mwanachama wa kawaida Hana uongozi wowote?
Anaweza kuongea tu hadharani Hana uongozi tena na anasema alituma barua hazijibiwi afanyaje?
Huyu si mjumbe wa Kamati Kuu? Au huo ujumbe ulitokana na cheo chake cha uenyekiti wa Kanda? Kwa mantik yako ni kuwa mwanachama wa kawaida hana nafasi ya kupeleka hoja zake kwa viongozi wa chama? Mimi ningetegemea ajenge hoja zake katika vikao vya chama ambavyo anahudhuria kama mwanachama. Ana nafasi pia ya kushawishi wanachama wenzake wamsaidie katika kudai haki yake. Suala lake ni la kichama na watu pekee wanaoweza kumsaidia ni wanachama wenzake. Wanachama wa CCM hata wamuunge mkono vipi hawana impact yeyote katika chama. Yeye awahamasishe wanachama wenzake wamuunge mkono. Kutafuta sympathy katika kadamnasi hakutamsaidia kitu.

Amandla...
 
Back
Top Bottom