mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Mchungaji Msigwa leo Ijumaa Septemba 06, 2024 kupitia Jukwaa la Sauti ya Watanzania katika mtandao wa Clubhouse akijibu barua ya Mawakili wa Freeman Mbowe ambayo imemtaka kuomba radhi au ajiandae kulipa faini ya Tsh bilioni 5, amesema haya
“Naichukulia hii kama kushuka kisiasa kulikopitiliza kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, kwa sababu kunidai bilioni 5 ninapofanya shughuli za kisiasa kwanza ni kuiua demokrasia yenyewe ya nchi ambayo pamoja na mapungufu yaliyokuwepo kwenye demokrasia ya nchi lakini bado wanasiasa wengi hasa wa upinzani wametumia uhuru wao wa kuipa changamoto serikali iliyopo madarakani kwa kuishutumu shutuma ambazo kimsingi nyingi hazina uthibitisho, kwamba serikali hii ni ya kifisadi, serikali hii ni ya wezi, serikali hii haileti maendeleo na hivi karibuni hata yeye mwenyewe amediriki kumuambia Mheshimiwa Rais kuwa yeye ni Mzanzibari, ameiuza bandari, hizi ndizo changamoto za kisiasa"
"Sasa mimi niliuliza maswali ya msingi kwa CHADEMA na maswali niliyouliza ni kwamba CHADEMA Digital siyo mali ya CHADEMA, nilitegemea mtu ambaye ana weledi, mtu ambaye anaongoza chama anataka kuchukua nchi ni jambo dogo tu la kusema Msigwa ni muongo, CHADEMA Digital ni mali ya CHADEMA, ikajulikana hadharani. Nilihoji kuwa Mbowe amekuwa akitumia msafara wa magari mengi, mwenzake anaenda na gari moja, alitakiwa aseme tu ni muongo Msigwa, mwenzangu anatumia magari matano au saba, ingelikuwa yameisha. Kwa hiyo masuala yote ambayo ameyaeleza ya kwamba mimi nimemvunjia heshima ni masuala ya kisiasa kwa hiyo nimesikitika kwamba anawezaje kuwa chini kwa kiwango hicho"
Pia soma