Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mchungaji Peter Msigwa akihojiwa kupitia kituo cha Redio cha Nuru FM, amesema;
"Mimi ni mtu wa kusema haki, mimi ni mtu wa kunyosha maelezo, mtu wa kusema ukweli. Sasa kuna vitu ambavyo naona nikiwa upande huu, ile umimi nashindwa. Naanza kuwa bata wakati natakiwa niwe tai. Sasa hii dunia tunaishi mara moja, kwa nini uishi kwa kusuffocate?
Lakini cha pili kikubwa, hayo mambo mengine yanaweza yakavumilika lakini kikubwa hasa mauaji ya tarehe 29 Oktoba. Nilivyoona wale vijana wanauawa wanapigwa risasi, vijana wetu... ile ilitesa sana. Na ndio maana baada ya uchaguzi sikuzungumza chochote, ilichukua muda mrefu sana. Lakini kikubwa zaidi, siku moja nimekaa na mtoto wangu wa miaka 18, anasema 'baba, hivi na mimi ningekuwa nimeuawa kama hawa watoto, ungeendelea kusema kidumu chama cha mapinduzi?'
Mimi niki kiongozi, naamini kwamba viongozi lazima tutoe majibu. Watu wakiuliza, unapokuwa kiongozi umebeba dhamana ya kuongoza watu. Watu wanayo vitu ambavyo ndani ya mioyo yao vinawaumiza, leadership lazima tuprovide majibu. Sasa vijana hawa ni kweli kuna changamoto nyingi; wanatakiwa waelekezwe, wafundishwe, waonywe, lakini hatuwezi kuwaonya kwa risasi. We cannot kill our own people.
Kwa hiyo hii imenitesa, nikaona hapana. Utu na ubinadamu ambao baba wa taifa alitufundisha, lazima tusimame kwenye haki. Na kibaya zaidi, haya mambo sikuona wanasiasa wenzangu waliosimama kidete kuyakemea, ukiacha Jaji Sinde Warioba. Lakini wengine wanaona kama ni mambo ya kawaida tu. Binadamu hawezi kuwa kama kuku. Kumekuwa na... achilia mbali mauaji, kuna yale mambo ya utekaji, watu kupotea. Sasa watu hawezi kupotea kama kokoto alafu tukakaa kimya.
Na mimi ni muumini wa mchungaji mmoja alikuwa anaitwa Bonhoeffer kule Ujerumani wakati wa utawala wa Hitler. Alisema kuka kimya mbele ya uovu, ni kushiriki uovu. Silence in the face of evil is itself evil. Sasa lazima tuseme, hii ni taifa la wote. Yale mambo sikukubaliana nayo hata kidogo."